Wizara ya Nishati umeshindwa kutatua kero za kuunga umeme kwa wananchi na badala yake imezidisha ugumu wa kupata huduma ya umeme hasa kwa wateja Wanahitaji nguzo 1,2,3,4,5,6,7,8,9, Hadi kumi.
Wizara ilitoa sharti gumu kwa TANESCO inayojiendesha kihasara kupunguza gharama za umeme wa nguzo na kufanya zote ziwe 27,000/= yaani mtu atalipia nguzo moja 27000 badala ya 177000/= nguzo mbili atalipia 27000/= badala ya 385000 na hata mtu akitaka nguzo 10 atalipia 27000/=
Maelekezo hayo ni hatua nzuri kwa machoni kwa wengi lakini kiukweli watu Wana zaidi ya mwaka mmoja hawajaungiwa umeme na wamelipia nguzo 27000. Kiuhalisia TANESCO hawana bajeti ya kulipia hizo nguzo, hivyo wananchi wengi kukosa umeme.
Ukitaka kulipia gharama halisi tanesco hawataki wanaogopa kufukuzwa kazi lakini hapo hapo mteja hapati huduma.
TANESCO wanadai walilazimishwa na serikali kuwalipisha watu 27000, Ila wao hawakuridhia, hivyo kwao ni sawa wananchi kuendelea kukosa umeme. Naamini serikali itatatua shida hii na kuacha kuitwika tanesco mizigo na lawama
Umetoa dukuduku lako, japo linajibika kirahisi sana kwa kujibu maswali yafuatayo...;
1. Huduma ya kusambaza nishati ya umeme ni jukumu la nani?
JIBU: Obviously, ni la serikali na TANESCO ni wakala wa serikali tu ktk kutoa huduma hiyo..
2. Ni nani katoa agizo la kila mwananchi mwenye kuhitaji kuunganishwa na huduma ya nishati ya umeme alipie Tshs. 27,000 bila kujali anahitaji nguzo 1,2,3,4 nk au la?
JIBU: Mtoa huduma ambaye ni SERIKALI na kumtaka wakala wake atii na kufuata maelekezo hayo...
3. Kama haya mambo yako hivyo, shida ya TANESCO na msingi wa malalamiko yao ni nini hasa?
JIBU: Kwa maoni yangu, msingi wa malalamiko ya TANESCO uko ktk hoja hizi:
å MOSI, TANESCO kupitia watumishi wake walikuwa wananufaika na gharama hizi kwa njia moja au nyingine. Biashara yao hii ya faida kubwa kwao binafsi imekuwa "shaken", sasa wanalia na kutafuta sympathy kwa umma tuone kuwa serikali inakurupuka ktk kutoa muelekeo wa utendaji kazi wa TANESCO...
Swali kubwa linabaki kuwa hili;
Kwamba, serikali ambayo ndiyo mtoa huduma ya nishati hii kwa wananchi wake inawezaje kutoa maagizo ya kujichanganya na kujipinga yenyewe..?
å PILI, kama nilivyosema kuwa kuwa TANESCO ni shirika la umma (serikali) lenye jukumu la kutoa huduma ya nishati ya umeme kwa wananchi wote. Kwa 100% linaitegemea serikali kujiendesha ili litoe huduma hii. Hoja ya fidia ya gharama ya nguzo inatoka wapi? Kwani mwenye TANESCO hakujua kuwa kwa kushusha gharama ya uunganishaji umeme kutahitajika fedha zaidi kwa TANESCO..??
Kama tatizo ni "UHABA WA NGUZO" ndiyo unawapelekea mshindwe kutoa huduma hii kwa wananchi kwa gharama ya Tshs. 27,000 kwa kila mteja, kwanini TANESCO isitoe taarifa kwa mwenye fedha na shirika ambayo ni serikali yenyewe ili iongeze/ifidie bajeti hii kama kweli mnachokilalamikia ni cha kweli..?
Kama TANESCO mmeshaiambia serikali juu kufidia gharama hizi ambazo kabla zilikuwa zinalipwa/zinabebwa na mteja na imekataa (kitu ambacho mimi siamini), basi leteni kama hoja ili tuijadili kupitia platforms mbalimbali...
Kumbukeni sauti ya umma (wananchi) ndizo zenye nguvu kuliko serikali maana serikali tumeiweka sisi wananchi...!!