Wizara ya Afya chukueni tahadhari kuhusu COVID-19, Waganda wanateketea

Wizara ya Afya chukueni tahadhari kuhusu COVID-19, Waganda wanateketea

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Kwa ufupi tu leo CNN wameonyesha picha na kuwahoji madaktari nchini Uganda.

Watu wanateketea na picha zinaonyeshwa. Jamani inahuzunisha sana.

Wizara ya Afya ichukue tahadhari. Mikusanyiko ya watu mipirani, kwenye misiba, harusi, mikusanyiko ya watu kwenye mihadhara ya kidini kama ya makanisa, misikiti n.k ipigwe marufuku.

Ilinibidi nizime TV kwa huzuni ya majirani zetu Waganda. Hiyo imewapata yaani wanaiita second wave na tayari WHO washatangaza leo kuwa wimbi la pili la corona litazikumba nchi za kusini mwa jangwa la sahara yaani Sub saharan countries ambapo Tanzania imo.

Tuache mzaha jamani. Asiyeamini afungue saa hizi CNN ataona Live.

Wizara lazima ikubali kuchukua hatua za dharura. Its now or Never.
 
Wa TZ sijui nani katuloga? Hakuna taadhari yeyote sasa hivi vitakasa mikoni maji tiririka vyote wametupa mbali

Heri kipindi cha Mwendazake
Nilidhani uhai at some point lazima kila mmoja ajisimamie

Ulinzi wa roho ni suala la nafsi
 
Nimeona Museveni ametangaza kufunga shule na vyuo, sisi hapa kwetu tuliunda kamati ambayo mapendekezo yake bado tunatafakari kama yafuatwe au yaachwe, tukija kuamka usingizini tayari Corona iko vyumbani mwetu tuanze kukimbizana kama kawaida yetu.

Barakoa zimeshasahaulika ukiongezea na yale mawazo ya wajinga Mungu anatupenda sisi zaidi ya wengine ndio kabisa hatuna habari.
 
Pumbavu hao waganda wameshadungwa mpaka chanjo! leo unataka kusema wanateketea kwa kushindwa kuchukua tahadhari?
Taratibu ndugu, hata hivyo Waganda ni asilimia ndogo sana waliochanjwa hadi sasa na chanjo huwa haizuii mtu kuambukiza mwingine asie na korona ,na nyie mlioko mpakani sijui wale wa Kagera, kaeni chonjo! Kila mtu apambane na hali yake!
 
Hofu..mbaya Sana aisee..kunywa malimao ,,jikinge na chukua tahadhari mwenyewe..hao WHO wenyewe sa hivi wanajiandaa kuja na tamko la kuwataka watu wajifunze kuishi na COvid ..so achane kujipa hofu Kama kufa tutakufa tu..
 
Nimeona Museveni ametangaza kufunga shule na vyuo, sisi hapa kwetu tuliunda kamati ambayo mapendekezo yake bado tunatafakari kama yafuatwe au yaachwe, tukija kuamka usingizini tayari Corona iko vyumbani mwetu tuanze kukimbizana kama kawaida yetu.

Barakoa zimeshasahaulika ukiongezea na yale mawazo ya wajinga Mungu anatupenda sisi zaidi ya wengine ndio kabisa hatuna habari.
Mama utaona leo kavaa barakoa mara kesho hana!

Nashangaa mkusanyiko wa akina mama pale Dodoma watu hawakuwa na habari ya Hutu tujidudu!
 
Ndugu zangu nategemea mnafahamu lockdown iliyoanza UG.

Nimeongea na dada yangu Kyotera leo amesema strain ya Corona waliyonayo sasa ni mbaya kwa vile inasambaa haraka na haichagui umri. Watoto na vijana nao wameambukizwa sana na kufa pia. Mashule yamefungwa. Dalili ni mafua na homa kali, kukohoa na pneumonia. Yeye ameshapata chanjo yuko safe mpaka sasa.

Bahati mbaya dalili kama hizo zimesahaanza kusambaa sasa vijijini Bukoba. Mama mkwe barely survived recently yupo kijijini. Tumemweka lockdown sasa maana kijana wake anayemsaidi anaumwa sasa na dalili ni zile zile.

Leo nimeongea naye anasema ugonjwa umeshasambaa sana kijiji hapo Kangabusharo

Nimeandika haya mjue kuwa hali si shwari nyumbani na kwa vile mobility ya watu kutoka huko ni kubwa tunahitaji kuanza kuwa careful zaidi.

C&P
 
Hawa si walisha chanjwa? Au walichanjwa ile dawa ya akina Putin ya buku saba?

Dah! Namkumbuka mzee wa ma pawpaw!
 
Taratibu ndugu, hata hivyo Waganda ni asilimia ndogo sana waliochanjwa hadi sasa na chanjo huwa haizuii mtu kuambukiza mwingine asie na korona ,na nyie mlioko mpakani sijui wale wa Kagera, kaeni chonjo! Kila mtu apambane na hali yake!
Sasa kazi ya chanjo ni nini ikiwa haizuii maambukizi?
 
Back
Top Bottom