Kwa ufupi tu leo CNN wameonyesha picha na kuwahoji madaktari nchini Uganda.
Watu wanateketea na picha zinaonyeshwa. Jamani inahuzunisha sana.
Wizara ya Afya ichukue tahadhari. Mikusanyiko ya watu mipirani, kwenye misiba, harusi, mikusanyiko ya watu kwenye mihadhara ya kidini kama ya makanisa, misikiti n.k ipigwe marufuku.
Ilinibidi nizime TV kwa huzuni ya majirani zetu Waganda. Hiyo imewapata yaani wanaiita second wave na tayari WHO washatangaza leo kuwa wimbi la pili la corona litazikumba nchi za kusini mwa jangwa la sahara yaani Sub saharan countries ambapo Tanzania imo.
Tuache mzaha jamani. Asiyeamini afungue saa hizi CNN ataona Live.
Wizara lazima ikubali kuchukua hatua za dharura. Its now or Never.
Leo tunamuuguza ndugu yetu ambaye amedhibitika kuwa na covid-19. Naye alipata hospitalini alipokuwa anauguza mgonjwa aliyelazwa wodini. Je tuseme nini? Tujifunze kusema kweli ili kweli ituweke huru!
Nimeona Museveni ametangaza kufunga shule na vyuo, sisi hapa kwetu tuliunda kamati ambayo mapendekezo yake bado tunatafakari kama yafuatwe au yaachwe, tukija kuamka usingizini tayari Corona iko vyumbani mwetu tuanze kukimbizana kama kawaida yetu.
Barakoa zimeshasahaulika ukiongezea na yale mawazo ya wajinga Mungu anatupenda sisi zaidi ya wengine ndio kabisa hatuna habari.
Taratibu ndugu, hata hivyo Waganda ni asilimia ndogo sana waliochanjwa hadi sasa na chanjo huwa haizuii mtu kuambukiza mwingine asie na korona ,na nyie mlioko mpakani sijui wale wa Kagera, kaeni chonjo! Kila mtu apambane na hali yake!
Hofu..mbaya Sana aisee..kunywa malimao ,,jikinge na chukua tahadhari mwenyewe..hao WHO wenyewe sa hivi wanajiandaa kuja na tamko la kuwataka watu wajifunze kuishi na COvid ..so achane kujipa hofu Kama kufa tutakufa tu..
Nimeona Museveni ametangaza kufunga shule na vyuo, sisi hapa kwetu tuliunda kamati ambayo mapendekezo yake bado tunatafakari kama yafuatwe au yaachwe, tukija kuamka usingizini tayari Corona iko vyumbani mwetu tuanze kukimbizana kama kawaida yetu.
Barakoa zimeshasahaulika ukiongezea na yale mawazo ya wajinga Mungu anatupenda sisi zaidi ya wengine ndio kabisa hatuna habari.
Nimeongea na dada yangu Kyotera leo amesema strain ya Corona waliyonayo sasa ni mbaya kwa vile inasambaa haraka na haichagui umri. Watoto na vijana nao wameambukizwa sana na kufa pia. Mashule yamefungwa. Dalili ni mafua na homa kali, kukohoa na pneumonia. Yeye ameshapata chanjo yuko safe mpaka sasa.
Bahati mbaya dalili kama hizo zimesahaanza kusambaa sasa vijijini Bukoba. Mama mkwe barely survived recently yupo kijijini. Tumemweka lockdown sasa maana kijana wake anayemsaidi anaumwa sasa na dalili ni zile zile.
Leo nimeongea naye anasema ugonjwa umeshasambaa sana kijiji hapo Kangabusharo
Nimeandika haya mjue kuwa hali si shwari nyumbani na kwa vile mobility ya watu kutoka huko ni kubwa tunahitaji kuanza kuwa careful zaidi.
Taratibu ndugu, hata hivyo Waganda ni asilimia ndogo sana waliochanjwa hadi sasa na chanjo huwa haizuii mtu kuambukiza mwingine asie na korona ,na nyie mlioko mpakani sijui wale wa Kagera, kaeni chonjo! Kila mtu apambane na hali yake!
Basi elewa ndugu yangu, kwamba aliyechanjwa huwa anabaki tu kuwa na uwezo wa kuwa 'carrier',kwa hiyo tatizo akikutana na mtu mwingine ambaye hajachukua tahadhari au hajachanjwa, basi inakuwa ni rahisi kumwambukiza.....