Wizara ya Afya yamtafuta mtaalamu aliyefumua jeraha la mgonjwa baada ya kushindwa kulipa hela

Wizara ya Afya yamtafuta mtaalamu aliyefumua jeraha la mgonjwa baada ya kushindwa kulipa hela

Wanaroho mbaya sana km walivyotufanyia kwenye miamala.
Leo km upo kigamboni na unataka kumtumia mtu laki 4 yupo kariakoo. Ni bora upande gari umpelekee au umtumie mtu.
Hahahaaaa........ Ndio maana anawafanyia ubaya akina meku!
 
Ndivyo walivyo...kwan kumnyima mtu maiti si kitu hiki hiki...vyote kutanguliza pesa na sio utu
WEWE UMEONA MBALI. WIZARA INAWACHONGANISHA WAHUDUMU WA AFYA NA WANANCHI. MFANO SUALA LA KUZUIA MAITI NA HILI LA MALIPO SIO RAIS WALA WIZARA WALIOLISEMEA.

HUYO MGONJWA ANGEONDOKA BILA KULIPA HUYU MUUGUZI ANGEKATWA MSHAHARA.

USHAURI: WIZARA ITOE WARAKA WA KUELEWEKA KUHUSU KUZUIA MAITI NA GHARAMA ZA MATIBABU KWA WAGONJWA WASIO NA UWEZO.

HELA ZA TOZO NA MAFUTA ZIKATOE HUDUMA BURE ZA AFYA NA ELIMU.
 
Hivi ukipigwa chini na hali ngumu hii, jamani, huku mtaani ni kugumu sana kama huna chanzo chochote cha mapato. Unaitamani jero lakini huioni.
 
Bila kulipa hiyo hela, daktari angekatwa mshahara au posho yake, kinachoendelea kwenye vituo vya afya kuhusu ukusanyaji wa mapato, audits za fedha, dawa na huduma kimewafanya watumishi waone hakuna haja tena ya kuheshimu utu na kuwa na huruma wala busara maana ukifanya hivyo unaitwa mwizi wa dawa au fedha za umma, taratibu za kupata msamaha wa matibabu kwa mtu asiye na uwezo zimekuwa ngumu mno sawa na kusema tu misamaha hakuna maana mpaka unakamilisha kupata msamaha kama ni mgonjwa sana ndugu yako atakuwa mbele za haki, mtumishi akijaribu kupindisha taratibu akatoa msamaha haraka ataitwa mwizi na atalipa mwenyewe fedha hizo. Roho mbaya ya watumishi wa afya inayosemwa siyo ya kuzaliwa nayo, imetengenezwa na mfumo wenye negative attitude na watumishi wa afya nchini, hivyo system hiyohiyo inao uwezo wa kuiondoa kwa kubadili attitude hiyo, ni lini jambo zuri lililofanywa na watumishi wa afya limeongelewa? Wao hufanya mabaya kila siku? Ukiyatukana Maji kwenye glass yakikukwama usilalamike, hii ni nature, ndivyo ilivyo, inakupa unachotia. Kusema haya sio kwamba naunga mkono tendo baya alilofanya huyo ndugu au matendo mengine maovu, hapana, najaribu kuonesha wapi tulipojikwaa badala ya kulaumu tulikoangukia.
 
Wizara ya Afya imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hii inayozunguka mitandaoni kuwa, mtaalamu wa Afya katika kituo ambacho bado hakijatambuliwa amemshona mgonjwa jeraha kisha akalifumua kwa madai kuwa mgonjwa huyo hakuweza kulipia gharama. Ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu. Hivyo, wizara inaomba wenye taarifa za wapi huku au kituo gani wawasilishe mara moja kwa namba ya huduma kea mteja 199 ya wizara ya afya au watume ujumbe mfupi kwenye namba ya waziri wa Afya ya 0734124191.

View attachment 1923425
Tangu nione sijazaliwa
 
Lakini serikali si ilijenga vituo 4000 si angechagua kimoja akapewa huduma ya mkopo. Ukienda hospital binafsi ujue ni biashara ya mtu na kulipa ni muhimu, ndio maana hakuna jeneza la bure kisa huruma ya kufiwa.
 
Back
Top Bottom