Wizara ya Afya yamtafuta mtaalamu aliyefumua jeraha la mgonjwa baada ya kushindwa kulipa hela

Mkuu umetufumbua Sana kumbe ndio Hali halisi ilivyo huko kwenye sekta ya afya

Nadhan mwamba amefanya vile Kama kufikisha meseji huenda ashawah kukatwa fefha kwa wema wake huko nyuma

HAKIKA USILOLIJUA N SAWA NA USIKU WA GIZA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nimemsikiliza huyo kiongozi kaongea kwa utu na busara sana kwamba huyo mama kupata hio ajali ni dharura,je kuna mtu huwa anajiandaa na ajali au dharura?

Hivi huyo daktari unawezaje kufanya unyama kama huu?

Na alivyo na roho Chafu,Huyu hata akipewa dili la kuiba vitovu vya watoto hapo kituoni anafanya huyu
 
Hata mabandama atanyofoa.
 
Sasa kule kufumua ndio hatadaiwa pesa?!

Au nyuzi na dawa alizotumia zinaweza

kutumika tena?!

Angezuia hata simu basi..
 
Aisee
 
Umeongea vizuri sana hatuna budi kujiuliza pia,huenda kuna shida huko kwenye hayo maeneo ya kutoa huduma za afya. Pasi na shaka yanayozungumzwa huku kwetu wananchi ni tofauti na maelekezo wanayokutana nayo watendaji katika maeneo yao ya kazi. Nalaani kwa nguvu zote hilo tukio lililokosa utu na uungwana lakini Wizara na wadau wote tujitafakari kwanini limetokea tukio la namna hiyo!?
 
Si ndio hapo et leo wanajifanya sio..'money oriented'..kifupi hospitalini hakuna utu
Kama huna pesa unafia kitandani wanakupita kama vile hawakuoni kabisa. Kwa sasa hali hii imetamalaki katika sehemu nyingi hapa nchini. Je umepata kusikia wajawazito wakifanyiwa Caesar hata pasipo kuwa na tatizo linalohitaji operation hiyo? Ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni.
 
Wengi tunamlaumu muuguzi. Lakini tujiulize kuna mtu kati yetu anaweza kutoa huduma bure?..Watanzania tunapenda sana vitu vya bure. Huyo muuguzi atakua naye amewachoka!
 
huyu jamaa ana akili ndogo sana,
hata uwezo wa kujieleza unaonesha alivyo mpumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…