Wizara ya Afya yamtafuta mtaalamu aliyefumua jeraha la mgonjwa baada ya kushindwa kulipa hela

Kilichonishangaza zaidi ni huyo mgonjwa kuachwa kajilaza chini na huku wakubwa wanamjadili utafikiri kama ni ng’ombe na sio binadamu

Najua wengi hawalioni hili kwa sababu wamezoeshwa udhalilishaji
Yaani badala ya huyo anaejinasibu zaidi ya mara 10 kuwa wao ndio wakubwa
Ameshindwa kutumia busara na kusema aondolewe hapo na awekwe hata sehemu safi
Au mimi ndio mkorofi
 
Ndio muone ccm walipotufikisha kutwa kujigamba tumerejesha nidhamu kwa watumishi hyo nidhamu ndo Hadi kukosa utu? Ccm mtayalipa haya yote ikiwemo ugaidi was Jada wenu Hamza.
 
Hili limeanza limeanza baada huyu waziri wa afya wa sasa kuwa katibu mkuu tamisemi akishughulikia afya.
 

 

AMEKIUKA MIIKO YA UDAKTARI Tukio hili lilitokea Mwezi Julai, 2021 na mtumishi aliyekiuka miiko ya Udaktari anaitwa Jackson Meli ni Clinical Officer wa Kituo cha Afya Kerenge Tarafa ya Magoma, Halmashauri ya Wilaya ya korogwe Mkoani Tanga. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa Hati ya Mashtaka na pia ameshafikishwa kwenye Baraza la Taaluma ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda Kinyume na Miiko ya Taaluma ya Udakrari. Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais - TAMISEMI 04.09.2022
 
SubhanAllah, daa hata kiofu kidogo kabis hakikua ndani mwake?
 
Tozo na kukaa na maiti watu hawana hela kuna tofauti gani wanatafuta video wakati wenyewe ni video tosha...
 
Watanzania na frustrations ni sawa na uji na mgonjwa..

Maisha yamekuwa magumu sana chini ya CCM..
 
hio wizara ya Afya kama wangekuwa wanawalipa hao watumishi vizuri yasingetokea hayo, lazima ijitathmini....kuna mambo ya kipuuzi mengi yana go unreported..
 
Aise kumbe ni korogwe tu hapo kwa watani zangu, wapare nyie ndo maana mnanunua uchawi kumbe roho zenu ni mbaya hivyo, aibu
 
Watu ni wengi ila binadamu ni wachache, aliyefanya huo unyama ana cheti cha kuchonga, hakusomea hiyo fani. Angejua maadili hangefanya hivyo. Namlaani kwa nguvu zote.
 
Muache mihemko

Msikilize na madai ya muhusika


Asipolipa mgonjwa muhudumu atalipia yeye
Mbona majeneza mnanunua? Yani mtu akuhudumie halafu ghalama azilipe yeye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…