Tunatambua umuhimu wa wanafunzi wa darasa la 4 na darasa la 7 kusoma na kujiandaa kwa ajili ya mitihani yao ya kitaifa baadae mwaka huu. Lakini imekuwa ni kawaida kwa shule za binafsi kukiuka utaratibu wa mapumziko(likizo)pindi shule zinapofungwa kwa kulazimisha wanafunzi kupumzika Kwa wiki moja tu ya mwanzo kisha kuendelea na masomo wkt wanafunzi wa madarasa mengine wakiwa likizo.
Isitoshe pia, shule nyingi za binafsi kwa siku ambazo shule hazijafungwa, zimepanga ratiba tofauti kwa darasa la 4 na 7 kuwahi shuleni saa 12 asubuhi na kutoka saa12 jioni. Ndio! Tunahitaji watoto wafaulu mitihani lakini sio kwa dose hii kubwa kiasi hiki kwa watoto ambao wengi ni miaka 11, 12 na 13.
Na sio kweli kwamba kuwa overload kusoma wanafunzi hawa ndio kufaulu kwao mitihani. Kuna shule nyingine ambazo kwa kukiuka agizo la serikali zimeamua kuwafundishia wanafunzi kwenye hostel zao wanapolala.
Hii sio sawa. Tunaomba wanafunzi hawa wapate muda wa kupumzisha akili zao. Hivyo serikali fuatilieni shule hizo.