DOKEZO Wizara ya elimu fuatilieni shule binafsi za msingi zinazokiuka maagizo ya Serikali

DOKEZO Wizara ya elimu fuatilieni shule binafsi za msingi zinazokiuka maagizo ya Serikali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wanakimbizana na module

Kwa sababu inatakiwa mpaka kufika mwezi WA tatu pale wanapoanza kufanya mitihani ya kujipima ya nje na ndani ya shule wawe washamaliza topic hii ni kwa Sababu mitihani ya nje hu include topic zote, haijalishi mwanafunzi kafundishwa au hajafundishwa.
Katika kitu kinachoua uelewa ni hili suala la kulazimisha ndani ya miezi mi3 au 4 muhtasari (syllabus) iwe imekamilika ili mtoto apate kujibu vizuri mitihani ya utamirifu (mock) au kumaliza tu ili ifanyike marudio. Elimu imekuwa kama vita. Ni banking education tupu.
 
Upo sahihi mkuu. Kimsingi, unapofuata huduma ya kulipia, wewe ndio unakua mfalme, unaelekeza namna gani unataka ufanyiwe hiyo huduma ingawa utaalamu utafanywa na huyo mtoa huduma.

Sasa hizo shule za kulipia, zimejigeuza zenyewe ndio wateja. Watoto wanasoma kwa nguvu sio kwa faida yao bali kwa faida ya wenye shule kujenga reputation.

Ila shule za mitaala ya Cambridge nafikiri hawana hizo mbanga. Mtoto likizo anapumzika na shule anasoma masaa yaliyopendekezwa na sio kukaa kaa tu shule siku nzima
Na hiyo ndio elimu inapaswa kusomwa kwa namna hiyo. Kuna wakati wa kusoma na wakati wa kupumzisha akili. Shule binafsi zinashindana sana kutafuta 'A' za kwenye karatasi bila kujua kuwa wanaua uelewa wa mtoto.
 
Back
Top Bottom