Wizara Katiba Na Sheria
Member
- Feb 28, 2021
- 42
- 84
- Thread starter
-
- #21
Swali zuri.Sheria ya mafao kwa mtu aliyeachishwa kazi ni sheria inayobagua..
Hongereni wakuu kwa kuja huku.
This is good thing, ubaya tu ninaouona ni kwamba mtaukimbia huu uzi kama taasisi nyengine zinavyofanya. Let's hope kwamba nyinyi mpo serious !
Taarifa ndio hiyo sasa, mahakama za mwanzo wakishirikiana na watendaji wa kata na vijiji wanatesa watu kisa hawana fedha za kuchangia ujenzi wa madarasa,wazazi wetu wameanza kuiona nchi hii ni chungu kweli kama alivyotabiri mgombea mmoja hivi wakati wa uchaguzi 2020.
Chaajabu,mzee wa miaka 70 bado mnakurupushana nae achangie maendeleo!!!
Hili jambo lilishatolewa ufafanuzi na serikali.Tumeshuhudia watendaji wa serikali wakitoa adhabu za viboko kwa watu waliowaona ni wakosaji(mwenye mamlaka ya kusema mtu amekosea ni mahakama tu)...
Hongera sana Wizara ya Katiba na Sheria
Nimependa ujasiri wenu kaaribu sana hapa
Jitahidi kutoa Ufafanuzi wa kila jambo
Pia Msiwe na Jazba maana humu ndani kuna watu wa Elimu zote mnazozijua!
Karibuni Sana
Kwanini bado nyie kama wizara hamu wachukuliii hatua zangu kisheria.?.wanao endelea na utamaduni huuuHili jambo lilishatolewa ufafanuzi na serikali.
Hakuna sheria inayoruhusu watendaji wa serikali kutoa adabu ya viboko kwa mtu yeyote. Aliyefanyiwa hivyo, ana haki ya kwenda kufungua kesi dhidi ya viongozi hao.
Sisi kama wizara tunatoa wito kwa viongozi na watumishi wote wa umma, kufuata sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
Samahani naomba kuongezea nyama hapo kidogo hivi hapo unakuwa unamshitaki nani hasa aliyekukamata au jamhuri?Ni maoni mazuri. Hata hivyo, sheria inampa nafasi ya kufungua kesi ya madai ili kulipwa fidia. Ni haki yake kisheria na atapatiwa stahiki zake akifuata utaratibu huo.
Ndugu Mwanadome, asante kwa maswali mazuri.Ni kwanini hadi leo swala la dhamana kwenye makosa ya dhamana imebaki kua ni hisani kutoka kwa polisi/hakimu?...
Kwamba kosa lina dhaminika kisheria lakini polisi/mahakama hawatoi dhamana.Ndugu Mwanadome, asante kwa maswali mazuri.
Unaweza kufafanua zaidi swali lako kuhusu dhamana kuwa hisani?
Kuhusu watumishi wa umma kutoa adhabu ambazo zipo kinyume na sheria na maadili ya utumishi wa umma, tumeshafafanua katika majibu yetu yaliyopita.
Asante.
Kwamba kosa lina dhaminika kisheria lakini polisi/mahakama hawatoi dhamana.
Tena bila sababu yoyote.
Sasa nyie kama wizara mnayajua haya mpooo kimyaaa, mnafanya jitihada gani kukomesha haya? Kama wizara mnashindwa kulisimamia hili mimi mwananchi wa huku kaliua ndani ndani nawezaje katika hili?Kama kosa linadhaminika kisheria, basi huo ni utovu wa nidhamu wa baadhi ya watumishi na sio utaratibu wa kimahakama/kipolisi.
Unaweza kuripoti kwa ngazi husika ili hatua zichukuliwe kwa watumishi hao.
Asante.
Hongereni sana kwa hatua hii nzuri, ombi langu tu pamoja na hongera hizo ni kwamba muutendee haki uzi huu, kwa kujibu maswali yote, kuyafanyia kazi yale ambayo inabidi muyafanyie kazi, na pia kwa KUTOA MREJESHO kuhusu yale ambayo mmeyafanyia kazi kutoka kwenye uzi huu (mnaweza kuwa na utaratibu, kwa mfano kila baada ya mwezi mmoja mnatoa mrejesho ya yale ambayo mmeyafanyia kazi kutoka uzi huu, na yamefikia wapi)-Hii ni muhimu sana, maana kusema tu kwamba, "tutalifanyia kazi" halafu imeishia hapo, inaweza isiwe inatusaidia sana sisi wananchi na wala nyie wenyewe.
Swali langu:
Mkoani Mbeya, wilaya ya Mbeya Mjini, kata ya Mwakibete, mtaa wa Shewa viongozi wa mtaa wamekua wakilazimisha wananchi wa mtaa huu kuchangia "kwa lazima" michango ya ujenzi wa shule. Hii imekua kero kubwa kiasi cha kufikia viongozi hawa kutishia wananchi ambao wameshindwa kuchangia mchango huo kuwa watawafunga.
Hii imekua ni kero kubwa sana, kwani wananchi wanakua harrased sana, na viongozi wanasisitiza kuwa ni MCHANGO WA LAZIMA KWA KILA MWANA-MTAA.
Nimeona kuwa watu wengine kadhaa kutoka mikoa mingine kwenye uzi huu huu wakilalamika pia kuhusu suala hili, na nimeona pia response yenu kuwa hamna taarifa juu ya hili. Ushauri wangu ni kwamba kwa sababu hili suala lipo, na wananchi wamelilalamikia sana, je kwa nini wizara isichukue hatua ya kulifanyia uchunguzi kidogo, kisha kutoa tamko kulaani vitisho hivyo na kutamka wazi kuwa hilo suala ni kinyume cha sheria? Hii itasaidia sana kuwakinga wananchi na uonevu unaoendelea huku mitaani na vijijini kuhusiana na hili la michango ya lazima ya shule?
Ahsante sana.
Wizara Katiba Na Sheria
Hii sheria ya Wizara ya Ardhi kutaka kila kiwanja kisome namba ya Nida ya mhusika mnaizunguziaje?
Hamuoni kama kuna wananchi watapoteza haki zao as asilimia kubwa ya wa-tz hawana Nida?
Inakuwaje kwa watu wa vijijini wasio na hati?