Hongereni sana kwa hatua hii nzuri, ombi langu tu pamoja na hongera hizo ni kwamba muutendee haki uzi huu, kwa kujibu maswali yote, kuyafanyia kazi yale ambayo inabidi muyafanyie kazi, na pia kwa KUTOA MREJESHO kuhusu yale ambayo mmeyafanyia kazi kutoka kwenye uzi huu (mnaweza kuwa na utaratibu, kwa mfano kila baada ya mwezi mmoja mnatoa mrejesho ya yale ambayo mmeyafanyia kazi kutoka uzi huu, na yamefikia wapi)-Hii ni muhimu sana, maana kusema tu kwamba, "tutalifanyia kazi" halafu imeishia hapo, inaweza isiwe inatusaidia sana sisi wananchi na wala nyie wenyewe.
Swali langu:
Mkoani Mbeya, wilaya ya Mbeya Mjini, kata ya Mwakibete, mtaa wa Shewa viongozi wa mtaa wamekua wakilazimisha wananchi wa mtaa huu kuchangia "kwa lazima" michango ya ujenzi wa shule. Hii imekua kero kubwa kiasi cha kufikia viongozi hawa kutishia wananchi ambao wameshindwa kuchangia mchango huo kuwa watawafunga.
Hii imekua ni kero kubwa sana, kwani wananchi wanakua harrased sana, na viongozi wanasisitiza kuwa ni MCHANGO WA LAZIMA KWA KILA MWANA-MTAA.
Nimeona kuwa watu wengine kadhaa kutoka mikoa mingine kwenye uzi huu huu wakilalamika pia kuhusu suala hili, na nimeona pia response yenu kuwa hamna taarifa juu ya hili. Ushauri wangu ni kwamba kwa sababu hili suala lipo, na wananchi wamelilalamikia sana, je kwa nini wizara isichukue hatua ya kulifanyia uchunguzi kidogo, kisha kutoa tamko kulaani vitisho hivyo na kutamka wazi kuwa hilo suala ni kinyume cha sheria? Hii itasaidia sana kuwakinga wananchi na uonevu unaoendelea huku mitaani na vijijini kuhusiana na hili la michango ya lazima ya shule?
Ahsante sana.
Wizara Katiba Na Sheria