Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Wanasheria wa JF mmeingia mitini, njooni huku mjadili mambo ya kisheria na mwakilishi wa wizara juu sisi tunaamini ninyi mnafahamu vingi kuliko sisi tusio wana sheria.

Swali kwa Wizara: Ni lini wizara itashirikiana na Social workers kutoa elimu kwa umma juu ya haki za raia wa Tanzania? sababu ni ukweli ulio wazi kuwa raia wengi wa Tanzania hawafahamu haki zao, hata wakionewa hawafahamu wafuate mchakato gani ili kupata haki zao, mimi nashauri zifanyike kampeni (advocacy) juu ya elimu kwa raia kuhusiana na haki zao za msingi kama binadamu na kama raia wa nchi hii.

Swali namba mbili: Wizara inamchukuliaje mfungwa wa Tanzania aliyeko gerezani? Ninyi mnaona wafungwa wanatendewa haki huko gerezani? Hali ya magereza yetu ikoje kuweza kumu-accomodate mfungwa ambaye anatambulika kuwa na haki kama binadamu wengine? Je, Magereza yetu yameundwa ili yarekebishe tabia au yanachochea kuharibu tabia ya wale wanaopelekwa kule? Kisheria nini kinafanyika ili wafungwa wahakikishiwe wanakingwa katika mwamvuli wa haki za binadamu. Ahsante.
 
Wanasheria wa JF mmeingia mitini, njooni huku mjadili mambo ya kisheria na mwakilishi wa wizara. Juu sisi tunaamini ninyi mnafahamu vingi kuliko sisi tusio wana sheria.

Swali kwa wizara, Ni lini wizara itashirikiana na Social workers kutoa elimu kwa umma juu ya haki za raia wa Tanzania? sababu ni ukweli ulio wazi kuwa raia wengi wa Tanzania hawafahamu haki zao, hata wakionewa hawafahamu wafuate mchakato gani ili kupata haki zao, mimi nashauri zifanyike kampeni (advocacy) juu ya elimu kwa raia kuhusiana na haki zao za msingi kama binadamu na kama raia wa nchi hii.

Swali namba mbili, Wizara inamchukuliaje mfungwa wa Tanzania aliyeko gerezani? Ninyi mnaona wafungwa wanatendewa haki huko gerezani? hali ya magereza yetu ikoje kuweza kumuaccomodate mfungwa ambaye anatambulika kuwa na haki kama binadamu wengine? Je magereza yetu yameundwa ili yarekebishe tabia au yanachochea kuharibu tabia ya wale wanaopelekwa kule? kisheria nini kinafanyika ili wafungwa wahakikishiwe wanakingwa katika mwamvuli wa haki za binadamu, Ahsante.

Asante kwa mawazo mazuri. Tayari wizara imeanza kuchukua hatua za kimkakati kuhakikisha inatoa elimu kwa umma kuhusu haki za kiraia na sheria mbalimbali.

Hata sisi kuja hapa JamiiForums ni sehemu ya mkakati huo. Hayo mengine tutayachukua na kuangalia namna ya kuyafanyia kazi ikiwemo kushirikiana na makundi ya kijamii na kiharakati.

Suala la haki za wafungwa, kupitia tume ya haki za binadamu, tunajitahidi kuboresha mazingira yao ndani ya magereza ikiwemo kuhakikisha wanapatiwa haki zao kwa mujibu wa sheria. Pia kupunguza msongamano kupitia mahakama kuendesha na kuamua mashauri kwa haraka na adhabu za faini au vifungo vya nje kwa makosa madogo madogo.

Asante.
 
Pongezi nyingi sana ziende kwenu Wizara ya Katiba na Sheria.

Natumai mutatatua vizuri kero za wananchi. Tunaomba na Wizara zingine zijifunze hiki mulichofanya kuwa karibu na jamii ya waTanzania.
Hongereni sana, nawatakia kazi njema.
 
Hongereni sana.

Kuna mdau kaulizia kuhusu uraia pacha huko juu nasubiri pia.

Kweli diaspora wanachangia sana kwa kutuma hela nyumbani na kuwasaidia ila wanashindwa kuwa na mali zozote au hata kufungua bishara kwa kupata vigezo vingi serikalini.

Naona ni bora sheria ingeainisha zaidi kuhusu uwekezaji hata ununuzi wa nyumba. Nchi nyingi zinaruhusu kununua nyumba hata kama una pasi ya nchi zingine.

Sheria inasemaje kuhusu ununuzi wa nyumba?

Asanteni sana
 
Wizara Katiba Na Sheria mimi nina mengi sana kuhusu sheria zetu nyingi. Lakini naomba nilifikishe kwenu hili kama maoni, juu ya sheria mbalimbali haswa zinazohusu matumizi ya Teknolojia. Sote tunakubaliana kuwa matumizi ya mitandao yanakuja na matumizi mabaya, lakini sheria zetu nyingi ni blanket kwa maana zinawakumba wote bila kuwa na speciation. Nitatoa mfano mmoja japo ipo mingi.

Sheria ya maudhui na kanuni zake zinataka Mtanzania yeyote asirushe maudhui bila Leseni ya TCRA. Sasa hii ni sawa kwa mfano mtu anayefanya Online TV kwa sababu anashindana na Television. Lakini pale mtu anaporusha maudhui ya kufundisha, kuelimisha, au zinazofanana na hizo, hamuoni kama haijakaa sawa?

Sera yetu ya taifa ya Tehama inasisitiza kuongeza local contents ambazo kwa kweli ni haba. Je, hii sheria kwa umbali iliokwenda hamuoni kama inaua lengo la Sera ya taifa ya Tehama?

Lakini pia wakati freelancer wa Kitanzania hawezi kutumia YouTube au mitandao mingine bila hiz constraints, mwenzake wa Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi et al anaitumia bila kizuizi. Kwa hiyo sheria zetu wenyewe zinaturudisha nyuma.

Maoni yangu ni kuwa Wizara ipitie sheria zote ambazo ni blanket na kupeleka marekebisho Bungeni ili sheria zetu zifanye kilichokusudiwa bila kuumiza ambao hawahusiki.

Mfano katika sheria hii, contents zote educational, religious, na zingine ambazo zafaa kwa maslahi mapana ya taifa ziwe bure na bila leseni. Wale wanaoanzisha biashara ambazo ni regulated tayari kama TV, Radio, et al ambazo kimsingi zinahama tu kiteknolojia ndio ziwe covered.

Ahsanteni!
 
Tumeshuhudia madaktari kushitakiwa pindi watendapo mabaya kwenye taaluma yao, wahandisi kushitakiwa pindi majengo yanapodondoka.... SHERIA INASEMAJE PALE ALIYEHUKUMIWA NA MAHAKAMA, THEN AKAKATA RUFAA NA KUSHINDA..!? Inasemaje kuhusu mahakama iliyotoa hukumu ya mwanzo!?
 
Karibuni sana janvini but mtuvulikie msichoke manake mnaweza mkaandikiwa jambo hapa mkajiuliza hv huyu alimaliza hata elimu ya msingi?

Ombi langu kwenu tuvumilieni kama swali mliloulizwa halijaeleweka basi msisite kutuuliza ili tuweze ku-frem upya.
 
Sasa kama hairuhusiwi kwanini hao wahusika wasiadhibiwe kwa kukiuka sheria za Serikali?
Hili jambo lilishatolewa ufafanuzi na serikali.

Hakuna sheria inayoruhusu watendaji wa serikali kutoa adabu ya viboko kwa mtu yeyote. Aliyefanyiwa hivyo, ana haki ya kwenda kufungua kesi dhidi ya viongozi hao.

Sisi kama wizara tunatoa wito kwa viongozi na watumishi wote wa umma, kufuata sheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
 
Asante kwa swali MEXICANA.

Bado wizara haina taarifa rasmi kuhusu suala husika. Unaweza kutufahamisha zaidi?
Mheshimiwa Wizara,Je Hakuna namna ya kufuatilia na kupata taarifa kamili kwa kutumia vyanzo vyenu.Na je kwa kuwa mmepatiwa taarifa hapa hamuoni kwamba ni vyema mkalitolea tamku katika misingi ya kisheria.Kama lipo au halipo.Au mnakwepa nini kwa kusema mnataka taarifa zaidi.

Aliloulizwa ni swali General lenye specific example.Mngetoa General answer kisha mshughulikie hio specific example independently.Au mnaonaje ndugu zangu?
 
Ili kukuza mitandao yetu,inabidi taasisi na wizara zijiunge huku ili waone lawama za wananchi.

Polisi wamekuwa waonevu mno kwa raia.

Polisi wa barabarani wanasumbua na wanaenda kinyume na sheria, mf ukikutwa huna leseni hawakupi muda kama sheria inavyotaka wao wanaandika tu na ukiwasumbua wanakutukna na kukupiga, nyie hili swala mwalionaje maana hata ukimfungulia mashtaka hutawashinda kamwe
 
Kuna masuala matatu ninayoomba wizara iweze kuyafanyia kazi:

1. Law School. Vyuo vikuu vingi kwa sasa vina programmes ambazo zinawa'accomodate' wanafunzi wanaosoma asubuhi hadi mchana na pia masomo ya jioni. Ukichukulia kwamba kuna wanafanyakazi wanaosoma sheria na wangetaka kusoma law school, lakini kwa sababu ya utaratibu wa kazi, hawawezi kusoma law school. Je, haiwezekani kuwa na masomo ya jioni kama ilivyo kwa UDSM?

2. Mara nyingi tunasikia mtu kakamatwa kwa tuhuma fulani, lakini polisi hawana ushahidi au ushahidi wa kutosha na mtu huyo anawekwa lockup/rumande na upelelezi unaendelea na wakati mwingine inachukua miaka kadhaa na ushahidi unakuwa haujakamilika na baadaye serikali inaweza kusema haina interest ya kuendelea na kesi hiyo kwa sababu ya kukosa ushahidi. Je, kusingekuwa na sheria inayoelekeza kama mtu amewekwa ndani miaka kadhaa kwa kosa ambalo ushahidi wake umekosekana, lakini mtuhumiwa ameshapoteza kazi, familia yake imeshateseka kwa kutokuwepo ndani ya familia na yeye mwenyewe ameshaathirika kisaikolojia afidiwe kwa kuwekwa ndani bila kuwa na ushahidi wa kosa analotuhumiwa nalo na baadaye kuachiwa kwa kukosa ushahidi?

3. Kuna pia malalamiko kwamba baadhi ya raia wanabambikiwa makosa ya jinai, labda kwa sababu binafsi (zisizo za kisheria) na unakuta mtu anakaa jela miaka nenda rudi na wakati mwingine hata kufia huko wakati kumbe ni kosa la kupika. Je, haiwezikani kuweka sheria kwamba kama raia akibambikiwa kosa ambalo hajawahi kulitenda na ikatokea akafungwa au akashinda kesi, je tusingekuwa na sheria inayozuia hilo kwa kuweka masharti kwamba kama ikidhihirika mtu kabambikiwa kosa kwa sababu zisizo za kisheria, bali kosa hilo kulingana na adhabu yake liende kwa yule aliyelipika kosa lenyewe?

Kwa maoni yangu, hii ingeimarisha rule of law na uwajibikaji kwa watu wanaohusika na uchunguzi wa makosa ya jinai ili wasije wakamfanya mtu 'guilty awe innocent' na 'innocent awe guilty'.
 
Uhusika wenu upo wapi juu ya watu wanaochukua muda mrefu mahakamani bila ya kuanza kusomewa mashtaka? Mfaano mtu anakaa miaka miwili uchunguzi badohaujafanyika.
 
Back
Top Bottom