Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Kuhusu jambo hilo linaleta utata pindi unapopeleka shauri/shtaka mahakamani. Naenda kutambua sheria anasemaje iwapo mtu au taasisi itakukuwa imekutendea vibaya iwe negligence au general damage mana inamlazimu mtu approve cost wakati kuna wakati damage zinazotokea huwezi prove. Hili linatokea nchi za wenzetu endapo mtu au taasisi imekuharibia taswira yako ama imekusumbua kwenye kupata huduma unaweza peleka shauri mahakamani na mahakama ikailazimu taasisi husika kukulipa general damages pai na kuprove specific damages?
Kulitolea ufafanuzi kwa maslahi ya Emma.
Ni kwamba kuna general damages Amazon's hutokana na kupotezewa mda, usumbufu, msongo wa mawazo na kadhalika na kuna specific damages Ambazo ni hasara za moja kwa moja ambazo mtu hupata kwenye kipato chake. Sasa specific damages kwa mtu ambae hana kazi rasmi (hana paperwork/document/mkataba wa kazi) anashindwa kuziprove au ni chache anafanyaje? Haki ya kuomba general damages anakosa?

1. Mfano mtumishi aliechapwa viboko?
2. Mtu aliekwa zaidi ya masaa 24 mahabusu anawezaje pats fidia kama hana kazi rasmi?
3. Benki imefanya negligence? Maelezo : mm ni signatory ya kampeni fulani, sasa signatory mwenzangu akaongea na benki ili waniblock nisiweze tanya miamala bila kupewa notice au kufata sheria. Bank ikanitoa usignatory. Wakileta anasema lazima improve specific damages kwanza kwa hiyo ikakwamisha kufungua shauri mahakamani mpaka nitakapo pata ruling mahakamani ya kesi na kampuni mana waligoma kulipa(kufanya kazi bila mikataba,kindugundugu). Sasa kuna damages kama kuniharibia Jina na kuweka mahusiano na wadau vibaya mana nimeifanya malipo yakabounce na kuhangaika huku na huku kutafuta tatizo. Hapo natakiwa nifanyeje au ndo km siwezi kuprove specific damage ndo nimepokea haki zote pamoja na general damage?
Naomba msaada. Ila kama inamlazimu mtu kuprove specific damages kwanza ndio apate general damages basi utakuwa na tatizo ambalo wizara inahitaji kukaa na kuondoa hugo masomo mana watu ambao hawana kazi rasmi napambana vp na polisi au bank na taasisi pindipo hawamtandea haki?
Nawasilisha
 
Swala jengine, mahakamani kesi zinachukua mda mrefu. Mda mwengine inaahirishwa kesi zaidi ya mara tatu sababu jaji hayupo. Hiki kitu hakiwezekani kwani yy yuko kazini na marurupu yake wanapata ila wananchi wanapeleka kesi pengine ndo inategemea hapo mambo yake yaende. Kesi inachukua miaka 2 na kuendelea kiholela. Majani wanakuwaje na kiburi. Tunaomba muliangalie hili kwa umakini, jaji analipwa kutuhudumikia na sio kumnyenyekewa, jaji ni wajibu wake kisheria na kikatiba hivyo wanahitaji kuwajibika.kama anashughuli nyengine aache kazi ya ujaji na sio kusumbua watu mpaka wanakata tamaa na kuchukua sheria mikono kwao?!!na holi swala la kuwa kesi inasikilizwa mwezi hadi mwezi haliko sawa (mtu nasubiri mwezi af umefika jaji hayupo unakuja mwezi mwengine hayupo, mnataka tuuwane mana maisha hayamngojei mtu, bili tanesco dawasa na shule ,kodi ya nyumba hawajui kuwa unachangamoto mahakamani) mda ni mali naomba wizara iwajibike na hilo. Kama jaji hawatoshi ongezeni ili mutatue Keroa za wananchi kwa haraka!!
Wizara wajibikieni, mambo ya serekali yachukue muda ila sio uhai wa mtu, mda ni mali. Naomba mlifafanue hili
 
Kesi za madai zinatutesa xnaa.unakuta umetapeliwa unaenda polisi wanasema hio ni kesi ya madai hawahusiki nazo .mahamakan ukifanikiwa kufungua kesi..aisee izo tarehe utazokua unapewa mwenyewe utaona usamehe deni..mwisho wa siku tunaona tuchukue sheria mkononi na tukifanya ivo tuh polisi hao hapo na ukipelekwa mahakamani hukumu yatoka chap
 
Katiba ipi tunayoongelea ile iliyowekewa viraka au ile iliyotumia mapesa mengi (ya Warioba) ikaja badilishwa na Bunge ?

In short hata tukitoa maoni ya kubadilisha sio kwamba tunapoteza muda iwapo hata Warioba mwenyewe na Tume pamoja na yote waliyofanya kilichotoka kilikuwa tofauti ?

Kwa ufupi swali langu ni hili...., Are we Serious Kweli ?
 
Nawashukuru kwa majibu yenu. Kwa mtazamo wangu, karibia maswali yote yamejibiwa kwa tahadhari na umakini mkubwa. Hilo sina shaka nalo. Nyinyi ni Serikali na pia mnatekeleza ilani ya CCM pasipo na shaka yoyote ile.
Safari hii nimekuja tu kwa ajili ya kutoa ushauri kwa manufaa ya Taifa letu.

Mkiwa kama Serikali iliyopewa dhamana ya kuwaongoza/kuwatawala Watanzania zaidi ya milioni 50, mnatakiwa KUBADILIKA! Punguzeni au ikiwezekana acheni kabisa kitu kinachoitwa UHAFIDHINA!

Mimi ni mmoja kati ya watanzania wengi walioshiriki kwenye zoezi la mchakato wa Katiba Mpya kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Nilibahatika kulifuatilia Bunge la Katiba kupitia luninga, na pia sarakasi zilizokuja kujitokeza kati ya pande mbili; CCM vs UKAWA kuhusu aina ya Serikali za kuiunda Tanzania Mpya!

Hakuna shaka yoyote ile kusema, mchakato ule ulivurugwa na Wanasiasa! Na mpaka leo sijapata jibu ni kwa nini Rais wa wakati ule aliamua kujaza Wanasiasa wengi (huku akitambua fika WANASIASA WOTE ni WABINAFSI na wengi wao wapo kwa ajili ya maslahi yao na ya vyama vyao) kuliko wataalamu wa makundi mbalimbali, huku hao wanasiasa wakibakia kuwa wachache.

Turudi kwenye mjadala:

1.) Naomba mfanyie kazi niliyo waeleza. Mkiwa kama Wizara, mna uwezo wa kumshauri Mh. Rais kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya. Mwambieni Watanzania tulio wengi tunahitaji Katiba Mpya. Ikiendelea kutumika hii Katiba ya Chama Kimoja ya 1977, inaweza kuja kusababisha machafuko siku za usoni. Na hilo siliombei. Kisingizio cha kufanya maendeleo, hakina mashiko sana! Maendeleo bila Katiba Bora/mfumo imara wa kiutawala na mgawanyo mzuri wa madaraka, ni kazi bure!

By the way, hii ni awamu yake ya mwisho kutawala! hivyo hana cha kupoteza iwapo atatuachia Watanzania zawadi bora kabisa ya Katiba Mpya kama alivyojaribu Mtangulizi wake na mwisho kuishia kushindwa hatua za mwisho! Hayo madaraja mnayojenga, ndege mnazo nunua, flyovers, treni ya umeme, vitaishia tu kubomolewa na kuharibiwa vibaya! iwapo tu vitatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu tu ya uwepo wa Katiba isiyo kidhi mahitaji ya wengi. Tujifunze kutoka LIBYA!

2.) Suala la Uraia Pacha, naomba nalo mlitafakari kwa kina. Mnaweza mkawapa haki zote hao Diaspora katika nyanja za uchumi na masuala ya kijamii na kuwabana sana kwenye masuala ya kisiasa kama mnaogopa hao kama watakuja kuwanyang'anya vyeo vyenu. Leo hii wenzetu wa Algeria, Morocco, Afrika Magharibi, nk. Wananufaika na Uraia Pacha kupitia michezo, uwekezaji, nk. Sisi tumekaza tu shingo huku tukiwa hatuna hata sababu zenye mashiko za kuzuia huo Uraia Pacha.

3.) Kuhusu suala la Mgombea Binafsi, Matokeo ya Rais kupingwa Mahakamani, nk. Ni vitu ambavyo havizuiliki kwa sasa! Haya mambo ya kumlazimisha mtu kudhaminiwa na Chama cha Kisiasa kugombea nafasi ya Uongozi, kunadumaza Demokrasia na pia kunaongeza kiwango cha UNAFIKI na kujipendekeza nchini.

4.) Kuhusu ishu ya baadhi ya watu mfano POLISI kuwa juu ya sheria, nalo mlitazame kwa kina. Kwa sasa POLISI wetu wamejigeuza kuwa MAHAKAMA! (Kwenye kuua watuhumiwa wanao dhaniwa kuwa ni majambazi, kupokea rushwa na pia kwenye utozaji wa faini ya makisa ya barabarani) Jambo hili halikubaliki! Maana hao polisi ni binadamu! Kuna ushahidi mwingi tu wa kukengeuka kwao. Na mfano mdogo tu ni huo wa Wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge.

Naomba kuwasilisha.
Asante sana kwa ushauri na maoni mazuri ndugu Tate Mkuu
 
Umejitahidi sana kufafanua kwa uzuri,
Jibu namba 3 unasema kipaumbele cha serikali sasa ni kushughulikia kero zinazogusa wananchi moja kwa moja.

Swali langu ni kwamba, kwani ishu ya katiba Mpya sio kero ya wananchi? Unyanyasaji na uvunjifu wa haki unaoendelea hauwagusi wananchi moja kwa moja? Ninanachoona viongozi wa sasa hamuwezi kumshauri Rais afanye nini mpaka yeye mwenyewe atakapoamua.

Kama Wizara Katiba Na Sheria, hili ni jukumu lenu kuhakikisha mnamshauri Rais kuhusu katiba Mpya. Hii iliyopo imepitwa na wakati vitu vya 77 ni tofauti sana na sasa hivi.
Tumeshalifafanua suala hili. Asante sana kwa maoni.
 
Naomba ufafanuzi kuhusu kauli ya Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama, ambae amesikika akisema kuwa wanafunzi watakaopata daraja la nne na sifuri (Division 4 & 0) katika shule ya sekondari ya Wavulana ya Umbwe iliyopo wilaya ya Moshi wajiandae kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
(Angalia video kwenye link hii, akiyasema hayo https://t.co/iEA6roeyzw)
Je, kama wizara yenye dhamana ya kusimamia sheria nchini mnasemaje juu ya hili? Kupata four na zero ni punishable offence in Tanzania as economic sabotage? Kama jibu ni hapana kama ambavyo uelewa wangu finyu unaniambia, je wizara ina mpango gani kuchukua hatua stahiki za kinidhamu/kisheria/kiutawala kwa kiongozi huyu na wengine ambao wamekua wakitoa matamko mbalimbali ambayo yanaleta taharuki na pia kupotosha sheria mbalimbali za nchi yetu?
Wizara Katiba Na Sheria
Swali linalofanana na hili tumeshalifafanua katika majibu yetu yaliyopita.

Zipo hatua za kinidhamu huchukuliwa katika ngazi husika dhidi ya watendaji au watumishi wa umma wanaoenda kinyume na sheria za nchi au maadili ya kazi zao.

Asante.
 
Swala jengine, mahakamani kesi zinachukua mda mrefu. Mda mwengine inaahirishwa kesi zaidi ya mara tatu sababu jaji hayupo. Hiki kitu hakiwezekani kwani yy yuko kazini na marurupu yake wanapata ila wananchi wanapeleka kesi pengine ndo inategemea hapo mambo yake yaende. Kesi inachukua miaka 2 na kuendelea kiholela. Majani wanakuwaje na kiburi. Tunaomba muliangalie hili kwa umakini, jaji analipwa kutuhudumikia na sio kumnyenyekewa, jaji ni wajibu wake kisheria na kikatiba hivyo wanahitaji kuwajibika.kama anashughuli nyengine aache kazi ya ujaji na sio kusumbua watu mpaka wanakata tamaa na kuchukua sheria mikono kwao?!!na holi swala la kuwa kesi inasikilizwa mwezi hadi mwezi haliko sawa (mtu nasubiri mwezi af umefika jaji hayupo unakuja mwezi mwengine hayupo, mnataka tuuwane mana maisha hayamngojei mtu, bili tanesco dawasa na shule ,kodi ya nyumba hawajui kuwa unachangamoto mahakamani) mda ni mali naomba wizara iwajibike na hilo. Kama jaji hawatoshi ongezeni ili mutatue Keroa za wananchi kwa haraka!!
Wizara wajibikieni, mambo ya serekali yachukue muda ila sio uhai wa mtu, mda ni mali. Naomba mlifafanue hili
Asante kwa maoni na ushauri.

Masuala yote uliyoyaainisha yapo kwenye vipaumbele vya wizara na serikali kwa ujumla.

Tutatoa mrejesho wa hatua zinazochukuliwa katika taarifa zetu rasmi.

Asante.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na mijadala inayoendelea hapa kila siku kuhusu masuala ya Katiba na Sheria za nchi yetu. Aidha kuhusu haki za binadamu, rushwa, utawala wa sheria na mengineyo.

Kupitia thread hii maalum; tutapokea maoni, ushauri na hata malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message (PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurasa rasmi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapa JamiiForums kupata taarifa mbalimbali kuhusu utoaji wa huduma za Katiba na Sheria nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram: @katibasheria_
Twitter: @sheria_katiba
Facebook: Wizara ya Katiba na Sheria

ANUANI ZETU NI:
Wizara ya Katiba na Sheria
Mji wa Serikali, Mtumba
S.L.P. 315,
Dodoma.

Masijala: barua@sheria.go.tz
Simu: +255 26 2310021
Nukushi: 255 26 2321679
Barua pepe: km@sheria.go.tz
Tovuti: www.sheria.go.tz
Wizara hiyo ipo tu kwa mazoea kuwa ipo na itaendelea kuwepo kama wizara,lakini inapokuja kwenye ukweli wa Wizara na sifa zake hii wizara ni jipu kuliko wizara nyingine kwa ustawi wa nchi kwani wanachokifanya wanakielewa wenyewe,tatizo kubwa ni kusimamia na kuilinda pamoja na kuitetea sheria kama mwongozo wa nchi.
 
pongezi kwa wizara kwa maamuzi ya kutunga sheria zote kwa lugha yetu ya kiswahili pia hukumu na maamuzi mbalimbali kuanzia mahakama za mwanzo mpaka mahakama za Rufaa kutolewa kwa Lugha yetu ya kiswahili.
Jambo lilobakia ni usimamizi kwa kuhakikisha dhamira na nia iliyo kusudiwa inatekelezeka.
 
Wizara Katiba Na Sheria mimi nina mengi sana kuhusu sheria zetu nyingi. Lakini naomba nilifikishe kwenu hili kama maoni, juu ya sheria mbalimbali haswa zinazohusu matumizi ya Teknolojia. Sote tunakubaliana kuwa matumizi ya mitandao yanakuja na matumizi mabaya, lakini sheria zetu nyingi ni blanket kwa maana zinawakumba wote bila kuwa na speciation. Nitatoa mfano mmoja japo ipo mingi.

Sheria ya maudhui na kanuni zake zinataka Mtanzania yeyote asirushe maudhui bila Leseni ya TCRA. Sasa hii ni sawa kwa mfano mtu anayefanya Online TV kwa sababu anashindana na Television. Lakini pale mtu anaporusha maudhui ya kufundisha, kuelimisha, au zinazofanana na hizo, hamuoni kama haijakaa sawa?

Sera yetu ya taifa ya Tehama inasisitiza kuongeza local contents ambazo kwa kweli ni haba. Je, hii sheria kwa umbali iliokwenda hamuoni kama inaua lengo la Sera ya taifa ya Tehama?

Lakini pia wakati freelancer wa Kitanzania hawezi kutumia YouTube au mitandao mingine bila hiz constraints, mwenzake wa Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi et al anaitumia bila kizuizi. Kwa hiyo sheria zetu wenyewe zinaturudisha nyuma.

Maoni yangu ni kuwa Wizara ipitie sheria zote ambazo ni blanket na kupeleka marekebisho Bungeni ili sheria zetu zifanye kilichokusudiwa bila kuumiza ambao hawahusiki.

Mfano katika sheria hii, contents zote educational, religious, na zingine ambazo zafaa kwa maslahi mapana ya taifa ziwe bure na bila leseni. Wale wanaoanzisha biashara ambazo ni regulated tayari kama TV, Radio, et al ambazo kimsingi zinahama tu kiteknolojia ndio ziwe covered.

Ahsanteni!
Tanzania ni nchi fukara yenye viongozi wenye mitizamo ya kifukara, watendaji wabinafsi na itaendelea kuwa ya kifukara tu jua liwake ama lisiwake.

Hii sheria ni ya kipuuzi sana.
Baada ya miaka miwili ijayo Kenya itakuwa thousands miles away from us kwenye hizi issue za freelancing na zinginezo sasa hivi tu hatuwakamati hata wakisimama.
 
Wizara hiyo ipo tu kwa mazoea kuwa ipo na itaendelea kuwepo kama wizara,lakini inapokuja kwenye ukweli wa Wizara na sifa zake hii wizara ni jipu kuliko wizara nyingine kwa ustawi wa nchi kwani wanachokifanya wanakielewa wenyewe,tatizo kubwa ni kusimamia na kuilinda pamoja na kuitetea sheria kama mwongozo wa nchi.
Sioni hata maana ya uwepo wake.
Wanakula mishahara ya bure tu pale Mtumba wizarani kwao saa 10 ukiwakuta wanavyojazana kwenye mabasi kurudi majumbani mwao as if walikuwa wanafanya cha maana.

Watu mtaani wanapigika, wanaonewa wenyewe wapo tu na matumbo yao
 
pongezi kwa wizara kwa maamuzi ya kutunga sheria zote kwa lugha yetu ya kiswahili pia hukumu na maamuzi mbalimbali kuanzia mahakama za mwanzo mpaka mahakama za Rufaa kutolewa kwa Lugha yetu ya kiswahili.
Jambo lilobakia ni usimamizi kwa kuhakikisha dhamira na nia iliyo kusudiwa inatekelezeka.
Shukrani sana.
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na mijadala inayoendelea hapa kila siku kuhusu masuala ya Katiba na Sheria za nchi yetu. Aidha kuhusu haki za binadamu, rushwa, utawala wa sheria na mengineyo.

Kupitia thread hii maalum; tutapokea maoni, ushauri na hata malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message (PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurasa rasmi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapa JamiiForums kupata taarifa mbalimbali kuhusu utoaji wa huduma za Katiba na Sheria nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram: @katibasheria_
Twitter: @sheria_katiba
Facebook: Wizara ya Katiba na Sheria

ANUANI ZETU NI:
Wizara ya Katiba na Sheria
Mji wa Serikali, Mtumba
S.L.P. 315,
Dodoma.

Masijala: barua@sheria.go.tz
Simu: +255 26 2310021
Nukushi: 255 26 2321679
Barua pepe: km@sheria.go.tz
Tovuti: www.sheria.go.tz

Pongezi kwenu kwa kuwa tayari kusikiliza kero zinazowakabili wananchi bila wao kujua wapate wapi ufafanuzi.

Inawakuta watu wengi. Mtu una gari. Kwa ubovu wa barabara au pia hata barabara zinapokuwa zinatengenezwa kunakuwa na changarawe au hata mawe (loose gravel) ambazo zinarushwa na magari yanayopita.

Hizi hupelekea kusababisha cracks kwenye vioo au hata taa za magari mengine yanayotumia njia hizi kwa viwango tofauti.

Kiwango kipi cha crack kwenye kioo au taa kinafuzu kuwa ni kosa kuwepo kwenye gari? Unakuta mtu anasumbuliwa kwa mambo kama haya wakati polisi wenyewe wanaosumbua vioo vyao vina cracks hata nyingi na mbaya zaidi kuliko ya wanazowasumbua nazo wengine.

Kama watumia barabara kwa mujibu wa sheria mtu umelipa kodi zote na serikali iliwajibika kupitia tanroads na tarura kuhakikisha barabara zilizo chini yao hazituathiri sisi watumiaji kwa namna yoyote ile na hasa iliyohasi.

Uhalali wa kuadhibiwa na mamlaka za serikali kwa kosa linalo sababishwa na mapungufu ya utendaji wa serikali yenyewe uko wapi?

Haki zetu kama watumia miundo mbinu mibovu zinalindwa vipi?
 
Naomba ufafanuzi kuhusu kauli ya Afisa Elimu Mkoa wa Kilimanjaro, Paulina Mkwama, ambae amesikika akisema kuwa wanafunzi watakaopata daraja la nne na sifuri (Division 4 & 0) katika shule ya sekondari ya Wavulana ya Umbwe iliyopo wilaya ya Moshi wajiandae kushtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi.
(Angalia video kwenye link hii, akiyasema hayo https://t.co/iEA6roeyzw)
Je, kama wizara yenye dhamana ya kusimamia sheria nchini mnasemaje juu ya hili? Kupata four na zero ni punishable offence in Tanzania as economic sabotage? Kama jibu ni hapana kama ambavyo uelewa wangu finyu unaniambia, je wizara ina mpango gani kuchukua hatua stahiki za kinidhamu/kisheria/kiutawala kwa kiongozi huyu na wengine ambao wamekua wakitoa matamko mbalimbali ambayo yanaleta taharuki na pia kupotosha sheria mbalimbali za nchi yetu?
Wizara Katiba Na Sheria
Wakikujibu mimi najisaidia ndani ya suruali
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Swala jengine, mahakamani kesi zinachukua mda mrefu. Mda mwengine inaahirishwa kesi zaidi ya mara tatu sababu jaji hayupo. Hiki kitu hakiwezekani kwani yy yuko kazini na marurupu yake wanapata ila wananchi wanapeleka kesi pengine ndo inategemea hapo mambo yake yaende. Kesi inachukua miaka 2 na kuendelea kiholela. Majani wanakuwaje na kiburi. Tunaomba muliangalie hili kwa umakini, jaji analipwa kutuhudumikia na sio kumnyenyekewa, jaji ni wajibu wake kisheria na kikatiba hivyo wanahitaji kuwajibika.kama anashughuli nyengine aache kazi ya ujaji na sio kusumbua watu mpaka wanakata tamaa na kuchukua sheria mikono kwao?!!na holi swala la kuwa kesi inasikilizwa mwezi hadi mwezi haliko sawa (mtu nasubiri mwezi af umefika jaji hayupo unakuja mwezi mwengine hayupo, mnataka tuuwane mana maisha hayamngojei mtu, bili tanesco dawasa na shule ,kodi ya nyumba hawajui kuwa unachangamoto mahakamani) mda ni mali naomba wizara iwajibike na hilo. Kama jaji hawatoshi ongezeni ili mutatue Keroa za wananchi kwa haraka!!
Wizara wajibikieni, mambo ya serekali yachukue muda ila sio uhai wa mtu, mda ni mali. Naomba mlifafanue hili
Siyo kwamba haya mambo hawayajui wanayajua vzr sema mfumo ndiyo unawabana haswa, ukute unayemlalamikia hapa ni mtu wa field kapewa kazi ya kujifunza namna ya kujibu maswali
 
Kuna baadhi ya kesi huwa zina ngazi ya kimahakama kusikilizwa.
Mfano kesi ya mauaji na uhujumu uchumi haiwezi kusikilizwa mahakama ya mwanzo,lakini wahalifu wamekuwa wakipelekwa katika mahakama hizo ,kesi inapotajwa mtuhumiwa anaambiwa haruhusiwi kuzungumza kwa vile mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi ya namna hiyo

Ushauri wangu
Kwa nini wasiwepo mahakama wenye hadhi ya kusikiliza kesi kama hizo ili aipandishe hadhi mahakama ile kwa muda au wahalifu wawe wanapelekwa moja kwa moja kwenye mahakama ambazo zina mamlaka ya kusilikiza kesi hizo kuliko kupoteza muda na fedha katika mahakama ambayo haina mamlala kisheria kusikiliza kesi hizo.?
 
Tanzania ni nchi fukara yenye viongozi wenye mitizamo ya kifukara, watendaji wabinafsi na itaendelea kuwa ya kifukara tu jua liwake ama lisiwake.

Hii sheria ni ya kipuuzi sana.
Baada ya miaka miwili ijayo Kenya itakuwa thousands miles away from us kwenye hizi issue za freelancing na zinginezo sasa hivi tu hatuwakamati hata wakisimama.
Suala hilo limeanza kufanyiwa kazi na wenzetu kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Wameanza na kuelekeza kushushwa kwa gharama za usajili na tozo. Ni hatua.
 
Back
Top Bottom