Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Kulitolea ufafanuzi kwa maslahi ya Emma.
Ni kwamba kuna general damages Amazon's hutokana na kupotezewa mda, usumbufu, msongo wa mawazo na kadhalika na kuna specific damages Ambazo ni hasara za moja kwa moja ambazo mtu hupata kwenye kipato chake. Sasa specific damages kwa mtu ambae hana kazi rasmi (hana paperwork/document/mkataba wa kazi) anashindwa kuziprove au ni chache anafanyaje? Haki ya kuomba general damages anakosa?

1. Mfano mtumishi aliechapwa viboko?
2. Mtu aliekwa zaidi ya masaa 24 mahabusu anawezaje pats fidia kama hana kazi rasmi?
3. Benki imefanya negligence? Maelezo : mm ni signatory ya kampeni fulani, sasa signatory mwenzangu akaongea na benki ili waniblock nisiweze tanya miamala bila kupewa notice au kufata sheria. Bank ikanitoa usignatory. Wakileta anasema lazima improve specific damages kwanza kwa hiyo ikakwamisha kufungua shauri mahakamani mpaka nitakapo pata ruling mahakamani ya kesi na kampuni mana waligoma kulipa(kufanya kazi bila mikataba,kindugundugu). Sasa kuna damages kama kuniharibia Jina na kuweka mahusiano na wadau vibaya mana nimeifanya malipo yakabounce na kuhangaika huku na huku kutafuta tatizo. Hapo natakiwa nifanyeje au ndo km siwezi kuprove specific damage ndo nimepokea haki zote pamoja na general damage?
Naomba msaada. Ila kama inamlazimu mtu kuprove specific damages kwanza ndio apate general damages basi utakuwa na tatizo ambalo wizara inahitaji kukaa na kuondoa hugo masomo mana watu ambao hawana kazi rasmi napambana vp na polisi au bank na taasisi pindipo hawamtandea haki?
Nawasilisha
 
Swala jengine, mahakamani kesi zinachukua mda mrefu. Mda mwengine inaahirishwa kesi zaidi ya mara tatu sababu jaji hayupo. Hiki kitu hakiwezekani kwani yy yuko kazini na marurupu yake wanapata ila wananchi wanapeleka kesi pengine ndo inategemea hapo mambo yake yaende. Kesi inachukua miaka 2 na kuendelea kiholela. Majani wanakuwaje na kiburi. Tunaomba muliangalie hili kwa umakini, jaji analipwa kutuhudumikia na sio kumnyenyekewa, jaji ni wajibu wake kisheria na kikatiba hivyo wanahitaji kuwajibika.kama anashughuli nyengine aache kazi ya ujaji na sio kusumbua watu mpaka wanakata tamaa na kuchukua sheria mikono kwao?!!na holi swala la kuwa kesi inasikilizwa mwezi hadi mwezi haliko sawa (mtu nasubiri mwezi af umefika jaji hayupo unakuja mwezi mwengine hayupo, mnataka tuuwane mana maisha hayamngojei mtu, bili tanesco dawasa na shule ,kodi ya nyumba hawajui kuwa unachangamoto mahakamani) mda ni mali naomba wizara iwajibike na hilo. Kama jaji hawatoshi ongezeni ili mutatue Keroa za wananchi kwa haraka!!
Wizara wajibikieni, mambo ya serekali yachukue muda ila sio uhai wa mtu, mda ni mali. Naomba mlifafanue hili
 
Kesi za madai zinatutesa xnaa.unakuta umetapeliwa unaenda polisi wanasema hio ni kesi ya madai hawahusiki nazo .mahamakan ukifanikiwa kufungua kesi..aisee izo tarehe utazokua unapewa mwenyewe utaona usamehe deni..mwisho wa siku tunaona tuchukue sheria mkononi na tukifanya ivo tuh polisi hao hapo na ukipelekwa mahakamani hukumu yatoka chap
 
Katiba ipi tunayoongelea ile iliyowekewa viraka au ile iliyotumia mapesa mengi (ya Warioba) ikaja badilishwa na Bunge ?

In short hata tukitoa maoni ya kubadilisha sio kwamba tunapoteza muda iwapo hata Warioba mwenyewe na Tume pamoja na yote waliyofanya kilichotoka kilikuwa tofauti ?

Kwa ufupi swali langu ni hili...., Are we Serious Kweli ?
 
Asante sana kwa ushauri na maoni mazuri ndugu Tate Mkuu
 
Tumeshalifafanua suala hili. Asante sana kwa maoni.
 
Swali linalofanana na hili tumeshalifafanua katika majibu yetu yaliyopita.

Zipo hatua za kinidhamu huchukuliwa katika ngazi husika dhidi ya watendaji au watumishi wa umma wanaoenda kinyume na sheria za nchi au maadili ya kazi zao.

Asante.
 
Asante kwa maoni na ushauri.

Masuala yote uliyoyaainisha yapo kwenye vipaumbele vya wizara na serikali kwa ujumla.

Tutatoa mrejesho wa hatua zinazochukuliwa katika taarifa zetu rasmi.

Asante.
 
Wizara hiyo ipo tu kwa mazoea kuwa ipo na itaendelea kuwepo kama wizara,lakini inapokuja kwenye ukweli wa Wizara na sifa zake hii wizara ni jipu kuliko wizara nyingine kwa ustawi wa nchi kwani wanachokifanya wanakielewa wenyewe,tatizo kubwa ni kusimamia na kuilinda pamoja na kuitetea sheria kama mwongozo wa nchi.
 
pongezi kwa wizara kwa maamuzi ya kutunga sheria zote kwa lugha yetu ya kiswahili pia hukumu na maamuzi mbalimbali kuanzia mahakama za mwanzo mpaka mahakama za Rufaa kutolewa kwa Lugha yetu ya kiswahili.
Jambo lilobakia ni usimamizi kwa kuhakikisha dhamira na nia iliyo kusudiwa inatekelezeka.
 
Tanzania ni nchi fukara yenye viongozi wenye mitizamo ya kifukara, watendaji wabinafsi na itaendelea kuwa ya kifukara tu jua liwake ama lisiwake.

Hii sheria ni ya kipuuzi sana.
Baada ya miaka miwili ijayo Kenya itakuwa thousands miles away from us kwenye hizi issue za freelancing na zinginezo sasa hivi tu hatuwakamati hata wakisimama.
 
Sioni hata maana ya uwepo wake.
Wanakula mishahara ya bure tu pale Mtumba wizarani kwao saa 10 ukiwakuta wanavyojazana kwenye mabasi kurudi majumbani mwao as if walikuwa wanafanya cha maana.

Watu mtaani wanapigika, wanaonewa wenyewe wapo tu na matumbo yao
 
Shukrani sana.
 

Pongezi kwenu kwa kuwa tayari kusikiliza kero zinazowakabili wananchi bila wao kujua wapate wapi ufafanuzi.

Inawakuta watu wengi. Mtu una gari. Kwa ubovu wa barabara au pia hata barabara zinapokuwa zinatengenezwa kunakuwa na changarawe au hata mawe (loose gravel) ambazo zinarushwa na magari yanayopita.

Hizi hupelekea kusababisha cracks kwenye vioo au hata taa za magari mengine yanayotumia njia hizi kwa viwango tofauti.

Kiwango kipi cha crack kwenye kioo au taa kinafuzu kuwa ni kosa kuwepo kwenye gari? Unakuta mtu anasumbuliwa kwa mambo kama haya wakati polisi wenyewe wanaosumbua vioo vyao vina cracks hata nyingi na mbaya zaidi kuliko ya wanazowasumbua nazo wengine.

Kama watumia barabara kwa mujibu wa sheria mtu umelipa kodi zote na serikali iliwajibika kupitia tanroads na tarura kuhakikisha barabara zilizo chini yao hazituathiri sisi watumiaji kwa namna yoyote ile na hasa iliyohasi.

Uhalali wa kuadhibiwa na mamlaka za serikali kwa kosa linalo sababishwa na mapungufu ya utendaji wa serikali yenyewe uko wapi?

Haki zetu kama watumia miundo mbinu mibovu zinalindwa vipi?
 
Wakikujibu mimi najisaidia ndani ya suruali
 
Reactions: JMF
Siyo kwamba haya mambo hawayajui wanayajua vzr sema mfumo ndiyo unawabana haswa, ukute unayemlalamikia hapa ni mtu wa field kapewa kazi ya kujifunza namna ya kujibu maswali
 
Kuna baadhi ya kesi huwa zina ngazi ya kimahakama kusikilizwa.
Mfano kesi ya mauaji na uhujumu uchumi haiwezi kusikilizwa mahakama ya mwanzo,lakini wahalifu wamekuwa wakipelekwa katika mahakama hizo ,kesi inapotajwa mtuhumiwa anaambiwa haruhusiwi kuzungumza kwa vile mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi ya namna hiyo

Ushauri wangu
Kwa nini wasiwepo mahakama wenye hadhi ya kusikiliza kesi kama hizo ili aipandishe hadhi mahakama ile kwa muda au wahalifu wawe wanapelekwa moja kwa moja kwenye mahakama ambazo zina mamlaka ya kusilikiza kesi hizo kuliko kupoteza muda na fedha katika mahakama ambayo haina mamlala kisheria kusikiliza kesi hizo.?
 
Suala hilo limeanza kufanyiwa kazi na wenzetu kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Wameanza na kuelekeza kushushwa kwa gharama za usajili na tozo. Ni hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…