Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Wizara ya Katiba na Sheria Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Joined
Feb 28, 2021
Posts
42
Reaction score
84
IMG_20210308_070525_987.jpg

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na mijadala inayoendelea hapa kila siku kuhusu masuala ya Katiba na Sheria za nchi yetu. Aidha kuhusu haki za binadamu, rushwa, utawala wa sheria na mengineyo.

Kupitia thread hii maalum; tutapokea maoni, ushauri na hata malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message (PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurasa rasmi wa Wizara ya Katiba na Sheria hapa JamiiForums kupata taarifa mbalimbali kuhusu utoaji wa huduma za Katiba na Sheria nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram: @katibasheria_
Twitter: @sheria_katiba
Facebook: Wizara ya Katiba na Sheria

ANUANI ZETU NI:
Wizara ya Katiba na Sheria
Mji wa Serikali, Mtumba
S.L.P. 315,
Dodoma.

Masijala: barua@sheria.go.tz
Simu: +255 26 2310021
Nukushi: 255 26 2321679
Barua pepe: km@sheria.go.tz
Tovuti: www.sheria.go.tz
 
Mimi nataka kufahamu inakuwaje kuna adhabu zinazotoka kwa mujibu wa sheria lakini ukizitathimini unaona kabisa sheria inamapungufu lakini wizara ipo na haijali kabisa.

Mfano:
Mtu kakwapua mabilioni ya serikali halafu adhabu inakuja aende jela miaka mitatu au alipe faini ya milioni 50, sasa mtu kaiba bilioni faini milioni ndio nini sasa?

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Seth kulipa fidia ya Sh26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia Sh309 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
 
Tumeshuhudia watendaji wa Serikali wakitoa adhabu za viboko kwa watu waliowaona ni wakosaji(mwenye mamlaka ya kusema mtu amekosea ni mahakama tu).

Mfano, yule Naibu waziri wa walemavu, DC arusha na RC Mbeya.

Je, sheria inawaruhusu kufanya hivi?

Ninyi kama wizara yenye dhamana, wajibu wenu ni upi katika hili?
 
Ni kweli kuna baadhi ya Sheria zina mapungufu na Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inaendelea kuzifanyia kazi ikiwemo kuziboresha, kuzifuta na kutunga zinazoendana na wakati.

Kuhusu ubadhilifu wa mali za umma, kosa husika linaweza kuhesabika katika makosa ya uhujumu uchumi (inategemea), na sheria ya uhujumu uchumi ipo pamoja na adhabu zake.

Au unazungumzia sheria ipi mahsusi nguvu
 
Asanteni kwa kuja huku, Ombi langu majibu yenu yawe ya wazi na ya uhakika, msije na majibu ya kisiasa.

Kama hamna taarifa au uhakika au kama mnaona swali liko nje ya uwezo wenu ni vyema kuomba muda ili kutafuta majibu sahihi kuliko kujibu kama wale Wahudumu wa Mitandao ya simu.

Hongereni sana sana
 
Asanteni kwa kuja huku, Ombi langu majibu yenu yawe ya wazi na ya uhakika, msije na majibu ya kisiasa. Kama hamna taarifa au uhakika au kama mnaona swali liko nje ya uwezo wenu ni vyema kuomba muida ili kutafuta majibu sahihi kuliko kujibu kama wale Wahudumu wa Mitandao ya simu. Hongereni sana sana
Asante sana kwa ushauri Elli. Tumeupokea na tutazingatia.
 
Sheria ya mafao kwa mtu aliyeachishwa kazi ni sheria inayobagua.

Kama mtu alieachishwa kazi alikuwa anafanya kazi ya kisomi akidai mafao yake analipwa asilimia 33 ya mshahara wake kwa miezi sita tu na mfanyakazi kama hakuwa msomi analipwa mafao yake yote.

Simaanishi wasio wasomi wasilipwe mafao yao yote ila hii sheria ina manufaa gani kwa msomi alieachishwa kazi kutolipwa mafao yake yote ili akajiajiri kama inavyofanyika kwa wabunge wanapomaliza miaka mitano wanalipwa mafao yao yote?
 
Sheria unasemaje kuhusu kumuweka mtu ndani harafu, mwisho wa Siku anakutwa Hana hatia, humuoni mmepotezea muda,na anastahili kulipwa! Tena Bila kumpasa kufungua kesi ya madai, sheria inasemaje hapo

Ni maoni mazuri. Hata hivyo, sheria inampa nafasi ya kufungua kesi ya madai ili kulipwa fidia. Ni haki yake kisheria na atapatiwa stahiki zake akifuata utaratibu huo.
 
Asante kwa swali Mexicana. Bado wizara haina taarifa rasmi kuhusu suala husika. Unaweza kutufahamisha zaidi?
Taarifa ndio hiyo sasa.

Mahakama za mwanzo wakishirikiana na watendaji wa kata na vijiji wanatesa watu kisa hawana fedha za kuchangia ujenzi wa madarasa, wazazi wetu wameanza kuiona nchi hii ni chungu kweli kama alivyotabiri mgombea mmoja hivi wakati wa uchaguzi 2020.

Cha ajabu, mzee wa miaka 70 bado mnakurupushana nae achangie maendeleo.
 
1.) Ni kwanini Serikali ya Tanzania inapinga kwa nguvu zote uwepo wa Uraia Pacha huku Nchi nyingine zikinufaika kupitia Uraia Pacha huo huo katika nyanja mbalimbali mfano. Uwekezaji, biashara, michezo, nk?

2.) Ni lini Serikali itaruhusu uwepo wa Mgombea Binafsi katika Uchaguzi?

3.) Kama Wizara, hamuoni kuna umuhimu wa kumshawishi Mh. Rais kuurejesha na kuuamlizia kabisa ule Mchakato wa Katiba Mpya na ya Wananchi na hivyo kuondokana na hii Katiba ya Mwaka 1977, iliyojaa viraka vingi na pia iliyo andaliwa wakati huo kwa madhumuni ya mlengo wa Nchi ya chama kimoja?

4.) Mnaridhika kama Wizara na Matendo yafanywayo na Jeshi letu la Polisi kuendekeza vitendo vya rushwa (hasa polisi wa usalama barabarani), kuua watuhumiwa kwa visingizio vile vile kika siku? Maana hatujasahau bado yale mauaji yaliyofanywa na akina Zombe kwa wale Wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge Ulanga.

Natanguliza shukrani zangu za dhati iwapo haya maswali yangu yatajibiwa kwa usahihi. Na hongereni kwa kujiunga na sisi humu JamiiForums.
 
Back
Top Bottom