Wizara ya Ulinzi na Usalama inahitaji mtu mahsusi, Bashungwa bado hajakomaa

Zungu mbona hapewi Wizara pamoja na kujipendekeza kote Kule!!!!! Kapambana saba kuleta zigo la tozo kwa watanzania lakini mama hajampa hata u naibu waziri? Zungu afikiriwe jamani nadhani akipewa unaibu waziri wa fedha atafaa sana maana anaweza kubuni tozo zingine ili uchumi wa nchi uendelee kukua na viongozi wetu waweze kununuliwa walau V8 tano tano, na kuongezewa posho .na Tanzania ikiwa ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa zaidi Africa
 
Inno kawekwa tu hapo.

Huyo alie chini ndie mtendaji lakini wapo watu maalum waendesha wizara.

Kuna mengi pale, mikataba, zabuni na kadhalika ni vitu ambavyo wapo watu wafanya mambo yao.
 
Mtaka afaa kuwa RC ili aweke mawazo yake ya maendeleo katika mikoa ya kimkakati.

Hivyo angeachwa pale Simiyu na kisha apelekwe mkoa mwingine.

Kumwondoa mtu hajamaliza mradi (project) sio sahihi.
 
Kwani siyo mwenyekiti wa bunge yule mzee
 
Ilishawahi kuongozwa na kijana mdogo enzi za Nyerere, umri sio tija jambo la msingi ni kutokuwa mjuaji kule kuna watu wanaojitambua na wenye nidhamu ya hali ya juu na wasiopenda siamba nyingi.
 
hahahaha
 
Napongeza uteuzi wa Tax.

Ila bashungwa bado hajakomaa Kwa hiyo wizara, sijajua kwanini awamu hii ya sita inaogopa kufanya kazi na wakongwe, inawaondoa kwenye system watu mahsusi.

Hizi ndio zilikuwa nafasi za watu aina ya kabudi ni wakomavu.
kwa Kabudi hapo umechemsha!

ungesena hata mashimba ndaki au Pindi chana! au angemrudisha Nchimbi
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🏃🏃
 
Hii nafasi angepewa Simbachawene ila nadhani system imeona ana Uyangachawene kidogo!
 
Waziri wa ulinzi ni kiongozi wa kisiasa tu, wenye kazi yao wapo - Magenerali, Waziri Bashungwa bado kijana na ataweza kumudu huo mchakamchaka hapo wizarani. Hii imani kwamba kuna watu fulani fulani tu ndio wanaweza kuwa Viongozi inabidii tuifute akilini mwetu. Binadamu wengi wana uwezo wa kuongoza wakipatiwa nafasi. Unaweza kuona uongozi unawarudia watu wale wale wakati kuna zaidi ya watu millioni moja wanaweza kuziba hizo nafasi.
 
Napongeza uteuzi wa Tax.

Ila bashungwa bado hajakomaa Kwa hiyo wizara, sijajua kwanini awamu hii ya sita inaogopa kufanya kazi na wakongwe, inawaondoa kwenye system watu mahsusi.

Hizi ndio zilikuwa nafasi za watu aina ya kabudi ni wakomavu.
Bashungwa ni bomu. Kaenda kusalimia tu hiyo wizara, atatoka hivi punde. Tena ataomba mwenyewe...

Du hapa Rais kakosea sana, au ni mtego kwake Bashungwa..... Yetu macho.
 
Napongeza uteuzi wa Tax.

Ila bashungwa bado hajakomaa Kwa hiyo wizara, sijajua kwanini awamu hii ya sita inaogopa kufanya kazi na wakongwe, inawaondoa kwenye system watu mahsusi.

Hizi ndio zilikuwa nafasi za watu aina ya kabudi ni wakomavu.
kazi ya wazir wa ulinzi ni zipi?
kazi za mkuu wa majeshi ni zipi
kazi za mnadhimu mkuu wa jeshi ninini?
 
Hivi ni kweli za korido Inno ilibidi aende fedha na uchumi mwigulu apelekwe Tamisemi maza akabadilisha?
 
Ilishawahi kuongozwa na kijana mdogo enzi za Nyerere, umri sio tija jambo la msingi ni kutokuwa mjuaji kule kuna watu wanaojitambua na wenye nidhamu ya hali ya juu na wasiopenda siamba nyingi.
Iyo wizara tangu tupate uhuru aliyoiweza, kuidhibit na kuimudu siyo mwengine bali profesa Juma Kapuya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…