Hii point ilishakuwa debunked mara nyingi tuu labda wewe sio mfuatiliaji, hata mimi nilishawahi kuwaelekeza watu flani humu ndani na wakanielewa vizur tuu.
Siku ya saba ya juma ni Jmosi, and this is a fact, wanahistoria wote wanakubaliana na hii point hata RC inajua kwamba siku ya saba ya juma ni Jmosi.
Mabadiliko yaliyofanyika kweny calendar are very well documented na hakuna kilichobadilika, Mungu kaziumba siku za wiki in a way that hata ufanyaje zitabaki kuwa vilevile, na hii ni moja kati ya sifa kuu za wiki ni kwamba huwez kucheza nayo kwa vyovyote, kutoka tarehe moja kwenda tarehe nyingine (kutokana na mabadiliko waliyofanya kweny calendar) hayabadilisha normal flow ya wiki, waliweza kubadilisha tarehe but the days are still the same, mfano wewe leo ubadilishe calendar useme leo ni tarehe 29 Sept kesho itakuwa tarehe 12 June, sawa utacheza na tarehe ila watu watahesabu normally kwamba leo ni J'pili kesho J'tatu, week days huwez cheza nazo kwasababu zimekuwa designed in a way that huwez kuzivuruga.
Siku ya Sabato ni ipi ndani ya Juma?
Jibu: Jumamosi! Ushahidi wa Biblia.
Ndani ya Biblia hakuna majina ya siku ya Jumatatu, Jumanne, n.k. isipokuwa kwa Biblia ya Kiswahili cha Kisasa. Ndani ya Biblia Mungu aliziita siku ya kwanza, pili, tatu, n.k (Mwanzo 1…).
Kibiblia Yesu alifufuka siku ya Kwanza ya Juma, yaani Jumapili. Fanya hesabu rahisi! Siku ya Saba itakuwa ni lini? Daima ni Jumamosi.
Majina haya yalitokea wapi?
Mf: Kiingereza
1. Sunday , siku ya jua, siku ya mungu mume wa Roma ya kale ya kipagani.
2. Monday, siku ya mwezi, mungu mke wa Roma ya kale ya kipagani.
3. Tuesday, siku ya mungu tuis wa Roma ya kale ya kipagani.
4. Wednesday, siku ya mungu wenes wa Roma ya kale ya kipagani.
5. Thursday, siku ya mungu thrus wa Roma ya kale ya kipagani.
6. Friday, siku ya mungu frigus wa Roma ya kale ya kipagani.
7. Saturday, siku ya mungu satun wa Roma ya kale ya kipagani.
Kiswahili:
Waswahili wao walifuata utaratibu wa waarabu katika kuita siku majina. Lengo la waarabu, ni kuifanya siku ya ijumaa kuwa siku ya saba(siku ya kusanyiko la ibaada). Lakini pamoja na jitihada zao hizo, walichemka mahali. Fuatilia uone!!
1. Jumamosi, siku ya kwanza ya juma
2. Jumapili, siku ya pili ya juma
3. Jumatatu, siku ya tatu ya juma
4. Jumanne, siku ya nne ya juma
5. Jumatano, siku ya tano ya juma
6. Alhamisi, (neno la kiarabu lenye maana ya –a tano=alhamsa) ya sita ya juma
7. Ijumaa, siku ya saba ya juma(sabato ya waarabu/waislamu)
Jiulize, utatokaje ya tano(Jumatano) uende ya tano(alhamisi) tena??
Msaada zaidi, angalia kamusi zozote za Kiingereza za zamani, zitakupatia maana halisi za majina ya siku. Mf. Collins English Dictionary, 1979 reprited on 1984.
Uthibitisho wa kibiblia unaonesha kuwa, siku ya Sabato ni Jumamosi kama leo inavyojulikana. Angalia!
Mathayo 28:1 Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.
Marko 16:2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza;
Marko 16:9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba
Luka 24:1 Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.
Yohana 20:1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.
Yohana 20:19 Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Yesu alifufuka siku ya jumapili ambayo Biblia inaiita kuwa ni siku ya kwanza ya juma. Kama Yesu alifufufuka siku ya kwanza ya juma(jumapili), Sabato itakuwa lini??
Jibu: Jumamosi