Wizi wa kwenye mabasi wanaswa na kamera ya bus la ABC

Kwa hesabu za kawaida tu, tuseme laptop ya laki 3, Mwizi katumia angalau elfu 30 ya nauli ili akaibe. Atapata faida akiiba.
 
Vijana muda wote anaasikiliza

Honeyyyy honeyyyyy honeyyyy

Kavaa earphones

Ova
 
Yani atajutia sana jamani..ukute lecturer kuna mtihani ya UE humo hahahh
 
Nakumbuka siku moja nimepanda basi la kampuni X nimeweka kibegi changu kwenye keria hizo. Safari ikawa inaendelea tulikuwa tunatoka dar kwenda arusha. Kufika hedaru gari likaharibika bana, abiria wote tukashuka kusubiri litengamae, lilivyokaa sawa kuja kufika moshi ishafika saa mbili usiku mi nikaona nisiendelee na safari nitalala moshi. Katika harakati za kuondoka nikabeba begi kumbe sio langu. Nikalibeba na kusepa mpaka pale kindoroko. Lakwangu lilikuwa na nguo na viatu tuu. Kufika room nakagua nakuta nguo ambazo sio zangu, kukagua kagua naona mfuko wa rambo mweusi, nikaufungua na kupekenyua nakutana na maburungutu ya pesa na kipistol. Jaribu kutafta vitambulisho hamna. Nikahesabu ile hela ilikuwa milioni 25 cash. Kesho yake nikaenda ofisini kwenye hio kampuni nikakuta tayari ripoti zipo za mtu kupotelewa na begi. Lile lakwangu lishaletwa pale na jamaa yupo ana wenge balaa ila uzuri hakusema kilichopo ndani. Nikaongea naye akaniambia alikuwa na haraka hivyo akachanganya mabegi. Nikamuhoji ndani kulikuwa na nini mule kwa bag yake. Akasema vyote, tukaongozana mpaka pale kindoroko. Ile kufika tuu naona mtu anatoka chumbani kwangu, na sa hio nliomba nisifanyiwe usafi ndani kwangu. Aiseeh to cut short hii story nlimkabidhi vitu vyake, ila yule mwamba mpaka leo yupo karanga ananyea debe.
 
Good. Na kuchunga mzigo wako ndani ya basi hakikisha kwamfano siti yako iko upande wa kushoto, basi pachika mzigo wako kwenye keria iliyo mbele ya siti yako upande wa kulia, ni rahisi kuuchunga mzigo wako na kubaini movement za abiria kwa urahisi muda wote na kwa nafasi.

Hili la kuweka juu ya siti uliyokaa, ni rahisi sana kutaimiwa bila kumbaini mwizi kwa urahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…