Wizi wa mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ndiyo sababu kubwa ya DP World kukabidhiwa

Wizi wa mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam ndiyo sababu kubwa ya DP World kukabidhiwa

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kwa bandari ya Dar es Salaam kukabidhiwa kwa DP World, lakini sababu kubwa zaidi ni wizi wa mapato ya Serikali uliokithiri pamoja na dhuluma kubwa kwa wateja wanaoagiza mizigo bandarini.

Mizigo inayopita bandarini ni mingi sana lakini Serikali imekuwa haipati mapato sahihi ya bandari hiyo kwani fedha hizo zimekuwa zikidhulumiwa tangu kipindi cha Mwl Nyerere na hata alipokuja Dr Magufuli wizi huu ulimkera sana na kujaribu kuchukua hatua ambazo hazikuzaa matunda.

Watanzania tujitoe boliti kwenye macho yetu ndipo tumnyooshee kidole raisi Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali kwa uamuzi waliochukua.

Watanzania tujiulize je tumekuwa tukipeleka mapato sahihi serikalini kama tulivyopaswa kufanya? Je hatukuwa tukidhulumu wateja wanaoagiza mizigo kupitia bandari hiyo? Lengo la Serikali kuleta wawekezaji DP World ni kupata mapato makubwa kwasababu ya uendeshaji wao mzuri wa bandari usiokuwa na hujuma.

Kama kusingekuwa na wizi na ubadhilifu unaofanyika bandarini basi Serikali isingewakumbuka wawekezaji wa nje ya nchi.

Watanzania tujifunze kuacha hujuma kupitia uamuzi huu wa DP World kwenye mali za Serikali kwasababu kadiri itakavyozidi kukosa mapato sahihi ndipo itazidi kualika wawekezaji kutoka nje ya nchi yetu ili wasimamie kwa haki.

Reference:
Mkataba wa DP ni mzuri kiutekelezaji. Lkn ni mbaya kwenye vipengele vyake. Hapa duniani hakuna mkataba wenye umilele.
 
Ha ha mmepata sehemu ya kuendeleza kufanya ugaidi wa mtandaoni na matusi yenu tu. Na kama ulikuwa hujui, hawa Waarabu wote wanajisifia kuwa ni Waswahili, wanajisifia kuwa ni Wazanzibari! Sasa kama nilivyosema huko juu.....Haya ni matusi dhidi ya Mtu mweusi, hayana tofauti yeyote ile na matusi ya Mwarabu, Mzungu dhidi ya Mtu mweusi. Lakini, Ukumbuke pia, Madhalimu ya Dunia hii ni kina nani. Usijiondoe ufahamu!

Hakuna sehemu yeyote ile katika mkataba ule, hakuna sehemu yeyote ile katika bunge la Jamhuri , hakuna sehemu yeyote ile katika ripoti za Kitaalamu iliyosema, Iliyotoa sababu kuwa ni "Wizi" ndio uliowafanya DPW wagaiwe Bandari, As a matter of fact hakuna sababu zezote zile za msingi zinazowapa Serikali kugawa bandari Bure kwa Maharamia wakiarabu zaidi ya Ukaribu na Rushwa iliyotamalaki....itoshe kusema nyuma ya pazia hili ni bakuli kubwa-Nimeliita robota sehemu nyingine- ya kuja kununua Uchaguzi wa 2025.

Ninasimama kidete na maneno yangu. Nikuhakukishie, kwenye makorido ya Ofisi kuna watu hawaonani nyuso kwa nyuso na kwa muendelezo huu wa kejeli, na unyanyasaji ni suala la muda tu kuwa wale mnaowatetea watakuja kuumbuka.

2025 sio mbali. Tutachagua kwa Umakini mkubwa sana.....Majambazi nje!
DP World ni jinamizi ktk zama hizi.
 
Back
Top Bottom