Uchaguzi 2020 World Bank yapitisha Mkopo wa Zaidi ya Trillion 1 Uliopingwa na Wanasiasa pamoja na Wanaharakati

Ukiwa tegemezi au Omba Omba huwezi kuwa muweka masharti. Na huna jeuri ya kukataa msaada kwa vile wewe Tanzania bado ni nchi maskini.
Ww acha hizo, Tz ni donor country, siyo maskini, ofcourse ww huwezi elewa sasa ila baadae kama Mungu atakujalia maisha utaelewa in near future! Tunaweza kuukataa kama tulivyoikataa misaada mingi mingine...soma historia rafiki uelewe!
 
Tuache unaa inabidi tuwashukuru wapinzani kwa kiasi chake kwa kuwapigania ndugu zetu watoto wetu ili waendelee na masomo. Unajua kwa akili za kawaida huweziona umuhimu wa mtoto wa kike mwenye ujauzito kuendelea na shule ila nimuhimu sana. Kama ni kodi tunalipa wote bila kubaguliwa kwanini inapofikia kwenye matumizi yanayofanyika kutoka na kodi zetu tuanze kubaguana? Hiyo haikubaliki hata kidogo ndo maana hata wazungu huwa wanatucheka sn kwa ujinga wetu. Ulishawahi kufikiri kwanini mtu anajua mwanae anamtindio wa ubongo yaani tunasemaa zezeta lkn bado atapelekwa shule akasome . Lkn kwa mtu ambaye ana uwezo mzuri lkn kutoka na nature ya maumbile yao na mpango wa Mungu anaujauzito akose shule hii haiingii akilini. Naishukuru pia serikali kwa kubadili msimamo wake na kuwasupport hawa watoto wakike.

DUMU KUBWA
 
Hero , wewe mwenyewe ni zao la mwanamke aliyepata mimba akiwa shule, shika adabu yako. Mama yako aangekatizwa kuendelea kusoma na wewe usingesoma
😂😂😂😂😂😂😂😂😂! Hapana, mie sio zao ya mimba dropout! Bado nasimamia palepale, tukiruhusu wazazi waendelee kusoma elimu rasmi ni sawa na kuwaambia mabinti zetu sasa ni ruhusa ngono nzembe, msisubiri kumaliza shule! Ninauhakika zaidi ya nusu watakuwa na mimba na kuwa wazazi wanafunzi!
 
Zaidi ya kupigia debe la kuwataka watoto wetu wa kike kuzalia mashuleni, na kupigia debe mimba za utotoni bila kujali madhara ya kiafya ya uzazi kwa watoto hawa kuna nini cha ziada? Hebu nieleweshe ndugu!
 
Jamani wengine kusoma document ya
@WorldBank
changamoto, ni hivi: 96% ya fedha itatolewa tu pale Benki itakaporidhika na matokeo yatakayoidhinishwa na Agent anayejitegemea na Serikali ikiwa imetumia pesa zake zenyewe sawa na kiasi kinachoombwa Malipo yanaanza 2021 #ArudiShule
 
Hivi unaongea ukiwa unaifahamu Tz au unasikiaaika tu kuhusu Tz! Ni utamaduni wa kitz mtoto akipaxhikwa mimba anatimuliwa shule na antafita njia mbadala za elimu ya watu wazima!
FYI, huwa siandiki mambo kwa hisia kama mfanyavyo wengine especially watetezi wa mfumo! Kwamba ni "utamaduni wa Kitanzania" maana yake nini?! Taifa haliendeshwi kwa tamaduni bali kwa misingi iliyojiwekea!!

Tafuta online, au nenda pale Wizara ya Elimu waombe document titled:

Huo ni muongozo wa serikali kupitia Wizara ya Elimu ambao ulitolewa April 2009. Section 2.3 ya muongozo inatoa maelekezo kwa wazazi/walezi kwamba:-
  • Shall be counseled and guided by the school leadership on the pregnancy of the school girl;
  • Shall show empathy and accept to take care of the pregnant girl;
  • Shall be guided and counseled by the school leadership concerning maternal health of the pregnant schoolgirl;
  • Shall be informed and required to fulfill re-admittance requirements;
  • Shall be required to update the school leadership on the health condition during pregnancy and after birth; and
  • Shall be involved in deciding on which mode of education (Formal or informal) and school the pregnant girl would like to continue with, after giving birth.
Aidha, section 2.6 ya Muongozo unatoa maelekezo kwa serikali kwamba:-
  • Shall educate and sensitize the society/community on the importance of readmitting impregnated school girls;
  • Shall educate and sensitize the society/community on the process of readmitting impregnated school girls; and
  • Shall empower school leadership on the issue of readmission of pregnant school girls; and
  • Shall task the ward social welfare officers to monitor the health welfare of the impregnated school girls.
Huo ndio MWONGOZO halali ambao Magufuli anaukanyaga! Sasa wewe niwekee hapa huo utamaduni unaosema kwamba watoto wa kike wakipata ujauzito, ni marufu kuendelea na elimu rasmi kwa shule za serikali!!!
Maana hatakuwa tena kwenye kundi la watoto bali wazazi! Huu utamaduni kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwatisha wototo wa kike kuogopa kushiriki ngono za kizembe!
Kwanini uwatishe badala ya kuweka mikakati inayoeleweka kuhakikisha hakuna ujauzito?! Hivi unaweza kunieleza hapa serikali ina mkakati upi kuhakikisha watoto hawafanyi ngono za mapema au angalau hizo ngono salama?

Btw, kama kuwatisha mbona mimba bado zipo pale pale hata siku hizi ambapo watoto wanaanza shule mapema sana?
Haiingii akilini, mtu mwenye akili timamu aje kutaka wazazi nao waruhuaiwe kusoma na watoto wakati kuna elimu ya watu wazima!
Unamaanisha Wizara ya Elimu hawana akili timamu, au?!

Ukweli ni kwamba, kama nilivyowahi kusema kwenye post moja wapo hapa jamvini, Mh. JPM ni mkurupukaji, na wala hafahamu misingi ya serikali mwenyewe!!

Hapa JPM alikuwa kama wewe tu kwa kuamini "kutimua shule wanaopata ujauzito ni utamaduni wetu" bila kufahamu mwaka 2009 serikali kupitia wizara ilitengeneza utaratibu wa kuhakikisha watoto wanopata ujauzito hawafukuzwi, bali wanakuwa suspended na kurudi tena shuleni unless kama ataamu mwenyewe kuendelea kwenye mfumo usio rasmi ambao Magufuli na wafuasi wake wanadhani ndo sheria inavyosema!
Hoja ya huyo ziro wako huyo haikuwa na mashiko hata kidogo ndio maana wameidharau hata hao watoa mkopo!
Hoja ya Zitto kivipi?! Kwani Zitto anafanya kazi Wizara ya Elimu au alihusika kwenye kuandaa huo muongozo?

Btw, Wakopeshaji gani waliodharau hoja ya Zitto?! Hivi umesoma maelezo ya WB au unaongea tu?!

Kipengele kimoja cha taarifa ya World Bank kinasema:- Hiyo ndo kauli ya WB ambayo inaakisi sehemu ya mwongozo wa serikali nilioweka hapo juu!

Kwa maana nyingine, suala la wanafunzi kutimuliwa sio la kisera bali ni la JPM na watu wake!!!

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya WB inasema:- Sasa wewe habari kwamba WB wamempuuza Zitto umezitoa wapi?!

Na labda nikujuze lingine! WB hawatatoa fungu lote kwa pamoja bali watatoa kwa awamu baada ya kuhakikisha serikali inatekeleza masharti waliyopewa, including kuwaacha watoto wajawazito kuendelea na shule kama mwongozo wa wizara unavyosema:-
Of the project funds, 96 percent (US$480 million) are subject to (a) achievement of agreed results verified by an Independent Verification Agent subject to the World Bank’s approval; and (b) submission of evidence that the government has already spent an equivalent amount on eligible expenditures in the secondary education sector. Assuming that these conditions are met each year, the disbursement schedule, is as follows:
  • FY 2021 - US$72.47 million
  • FY 2022 - US$101.10 million
  • FY 2023 - US$114.73 million
  • FY 2024 - US$98.52 million
  • FY 2025 - US$85.37 million
  • FY 2026 - US$27.81 million
Na sio tu kwamba serikali watakuwa wanasema "tumetekeleza kwa kiwango fulani bali hadi pale Independent Verification Agent atakapothibitisha!!! Eti mmesikia wenyewe, achana na hao wengine; niambie wewe ulimsikia wapi kama sio unatumia nukuu za propaganda za Lumumba!!

Ambacho alisema Tundu Lissu, ni hiki hapa chini:-


Hiyo video ni ya dakika 3:43 lakini MATAGA kwa kujua Wa-TZ hamna utamaduni wa kutafuta ukweli, waka wanaongelea maeleo ya dakika 2 za mwanzo na wakawaficha zaidi ya dakika 1 unusu nyingine zilizobaki!

Sasa pamoja na kunitolea povu kwamba eti nimetumwa kuandika uzushi, kwa mwenye akili timamu hapa atajua ni nani aliyetumwa kuleta uzushi kati yangu na wewe! Yote niliyosema hapo kabla nimekuwekea ushahidi, weka hapa ushahidi wa maelezo yako!!!
 
Xaf
Xana rais wetu Na Mungu akuongoze katika uongoz wako
 
Aliyeaibika hapa ni nani ?! Yule aliyeapa kule simiyu kwamba hawezi kusomesha wazazi, au huyu aliyepigania wakubaliwe kuendelea na masomo baada ya kuzaa ??!!. .



Odhis *
Lakini msimamo wa serikali si upo pale pale? Ukipata mimba altenative program ni veta au kajifunze kijiweni charahani. Kwa mantiki hii aliyeabika ni yule aliyaekurupuka kupinga pesa za mkopo zisitolewe.
 
Tatizo lako unaongea tu hisia zako bila uhalisia!Uganda na Kenya hawawazuii watoto kirudi shule wanaopata ujauzito na kujifungua,lakini rate ya wanaopata mimba Tanzania inaizidi ya Kenya na Uganda!Unafikiri kwanini?Kwa mazingira hayo hoja yako ni mfu!
 
Msaada Wa Masharti.duh yaleyale yaliyopigiwa kelele ndo tumekubali
 
Upuuzi mtupu! Eti mzazi asome darasa hilohilo na mtoto! Haitawezekana abadani Tz! Wao walete hizo hela, after all ni mkopo tu! Mambo ya nyumbani na namna tunavyoendesha jamii yetu watuachie wenyewe! Otherwise waurudishe mkopo wao!
Ndio tushanywea hivyo!Kenya na Uganda hawawazuii watoto kurudi shule wanapojifungua,hakuna ushahidi wowote wa madhara wanayoleta kuchanganyika na wenzao wa umri wao!Zinabaki tu hisia za Jiwe!Team ya CCM ilikaa na kuandaa sera na ilani za CCM 2015,moja ya mambo waliyoahidi ni pamoja na hilo la watoto watakapata ujauzito watapewa fursa ya kurydi shule katika mfumo rasmi kumalizia masomo yao!Hata Mama Samia Suluhu wakati mmoja akihutubia alizungumza hayo kabla ya siku chache baadae JPM kuja na msimamo wake!So suala hilo la kuondoa kabisa watoto wa aina hiyo kwenye mfumo rasmi ni mawazo ya JPM na si CCM!Hapa ndio tunaona madhara ya Rais wa nchi kuwa kichwa ngumu na kutoshaurika au kusikiliza wengine!
 
Kwa utaratibu huu mfano nchi ingekuwa inapigana vita ya Kagera leo makada wa vyama vya siasa bado wangekuwa wanatafuta matukio ya kufanyia cheap politics; tunasiasa za kishamba kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…