WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

THREAT TO THE WORLD PEACE kama umesoma hii kitu inafahamika ....big up..
Kuna insight ndogo nilizisoma kwenye kakitabu kadogo kanaitwa the enemy unmasked.
Kinaelezea mipango tajwa hapo juu, pia Kinaelezea undercover wa mipango hii ni modern illuminati ambayo iliasisiwa na jamaa anaitwa Adam weishaupt huyu akiwa financed na Rothschild alianzisha chama hiki may mosi 1776 huko bavaria German.

Na huyuhuyu Adam kinaelezea ndie aliyempa mjerumani mwenzake mwenye Asili ya uyahudi Karl Marx document iliyoitwa communist manifesto na dunia inamuona Karl Marx badala ya walionyuma yake.
Na mambo mengine mengi kama haya ni kweli yanakuwa matured na kuleta hiyo barua tajwa. Hawa ni watu halisi na sio manefili wala machotara wakishetani. Mambo haya yanaweza kuwa kweli, sio kweli au changamoto kwa wakazi wa dunia kulink uhalisia wa matukio na hizi conspiracy zilizotungwa zamani lkn zinamap matukio mengi halisi Sasa.
 
Wakuu EIYER na MSEZA MKULU,binafsi naona nyote mna hoja tena zina mashiko mazuri ila inaonekana sources zenu ndio zinatofautiana na hapo kupelekea ninyi kubishana. Napendekeza kila mtu amwage madini kulingana na anavyojua ili sisi tupate mwanga pia. Kuna mengi ya kujifunza hapa na lengo la wote ni kutuelimisha
Wakibishana kwa hoja tunafaidika sana, ila hawajui tu. Yaani mim kila nikikaa dakika chache naufungua tena Uzi huu kuona madini mapya toka kwao.
 
Wakuu EIYER na MSEZA MKULU,binafsi naona nyote mna hoja tena zina mashiko mazuri ila inaonekana sources zenu ndio zinatofautiana na hapo kupelekea ninyi kubishana. Napendekeza kila mtu amwage madini kulingana na anavyojua ili sisi tupate mwanga pia. Kuna mengi ya kujifunza hapa na lengo la wote ni kutuelimisha
Kweli mtazamo wa huyu ndugu ni haya mambo yanafanywa na machotara au hybrid wa Shatani na mwanadamu, yaani viumbe wasio pure human being Bali ni nusu mwanadamu nusu Shatani. Hoja hii inatia hofu isiyo ya lazima kuwa Kuna advanced being between human being and Satan ambaye anainfluence maisha hapa duniani kitu ambacho ni non biblical and unscientific. Ila kwa sababu Mungu aliumba planet earth na kwenye universe Kuna billions of plannets sio hajabu kukawa na uumbaji wa viumbe wengine huko maana bibilia iko bound na uhusiano wa Mungu dunia na Mbingu na Shatani.
Dunia hii ni vita Kati ya Shatani na Malaika zake, Mungu na Malaika zake na Mwanadamu aliyeanguka. Hakuna advanced human being hao ufo kama wapo kweli uwezekano ni kuwa intelligent being from other planets ambao hawana nafasi wala ushawishi wowote na kinachoendelea Sasa duniani.
 
Kwa mujibu wa watafiti mbali mbali na vitabu na makala mbali mbali na utafiti wangu mwenyewe na ushahidi wa maandiko matakatifu ni kwamba hakuna tena muingiliano ule kwakuwa wale malaika wapo kifungoni lakini kuna kitu sijaweza kukielewa ni kwa namna ipi hii blood line ipo hadi leo baada ya gharika maana hata Biblia inasema kwamba Wanefili walikuwepo kabla ya gharioka na baadaye....

Waisraeli,wakati wanawaona Wakanaan walijiona ni kama panzi mbele yao,hii inaonesha walikutana na Wanefili,Goliathi alikuwa ni Mnefili n.k na hii ni baada ya gharika....

Hili ngoja niendelee kufanya utafiti ili nijue ilikuwaje....
Hao Malaika kufungwa kifungoni ili wasiendelee kuzini na wanadamu na kuzaa hao machotara wa kishetani ambao kwa maelezo yako ni advanced being ambao wako nyuma ya uovu na mipango hasi ya dunia hii haihitaji utafiti ni vitu ambayo vitapatikana kwenye first book of Enoch japo umekanusha na kusema hizo ni quotes from distorted book of Enoch Bila kuweka your current truth kutoka kwa hicho pure. Pili vitu hivyo haviko supported na bibilia, bibilia I nazungumzia kifungo cha Shatani na maraika zake wote miaka elfu baada ya Mungu kuja kuchukua wa teule wake.
 
Dunia haijawahi kuendelea kwa utabiri.

Ni ujinga tu umewaita. Sisi huwa tunayasoma sana hayo na mwishowe tunaelewa kuwa huu ni upuuzi.

Kwa ajili ya kukujuza tu kuwa huo ni ujinga, tuchukulie huo ni ukweli, ingawa siyo. Jee, unakusaidia / utakusaidia nini? Au wengine unawasaidia nini?

Ukijibu hayo honestly, utajielewa kuwa kufata hayo ni ujinga tu.

Hakika wajinga ndiyo waliwao.
Hakuna kitu kinachotokea bila sababu
Labda nikuulize we ulizaliwa kwa sababu gani?
Mi tangu mwanzo nipo mdogo wakati najifunza,
Somo kuhusu kwa nini kuna majanga yanatokea na yanaua watu wengi sana..!
Niligundua kila kitu kinatokea kwa sababu?

Mwisho wa siku niligundua kuna matukio yaliopangwa tangu zamani sana
Ni sawa na picha ya utawala wa NAZI iliyopigwa zamani sana
Lakini katika ile picha alionekana jamaa mmoja akiwa modern camera
Ambayo kwa wakati huo ilikuwa bado haijatengenezwa,!

Kwa hiyo amini usiami mambo mengi ni ya kutengeneza.
Na kuhusu elimu ya hizi taarifa za namna hii sijaanza kujifunzi juzi au jana,
Ni muda mrefu kwa kuwa huwa natumia kauli ya.....
Kile unachokiona na kukifikiria hakiwezi kuwa hivyo amini ndivyo kilivyo ila wewe tu umeziweka fahamu zako kifungoni kuto ziacha ziwe huru..

Kwa kuwa tayari ulishapandikiziwa taarifa ya kwamba...
Sababu ya WW1 ni hii na ukafundishwa darasani basi tayari walishafunga
Uwezo wako wa kufikiri na kudadisi.
 
Mungu ndiyo anazuia hili mkuu....

Yesu alikuja kufifisha kabisa nguvu ya huyu kiumbe muovu kabisa kupata kuwepo....

Kazi aliyopifanya Yesu pale msalabani ni kazi kubwa kabisa kupata kufanyika na ni pigo kubwa kabisa kwa kiumbe huyu muovu kabisa...

Alijua hili na ndiyo maana alitaka kuzuia hili mara kadhaa na akafeli.....
Mkuu hapa mbona kama unachanganya au unajichanganya. Yesu alikuja kuhafifisha kazi ya Shatani. Wewe huyohuyo unasema watoto waliozaliwa na Shatani na watu, hao machotara ndio wanarun dunia kwa background na sio free human being. Huoni kama unawainua hao viumbe wako zaidi ya kazi ya yesu msalabani. Kwa mfano hili chotara likamkubali yesu yesu analifanyaje kulinganisha na mabadiliko ya mwanadamu mdhambi aliyemkubali yesu/Mungu.
 
Je hawa wanefili ndio ile "13 bloodline family" inayotawala dunia?

Kuna mahala nilisoma kuwa watawala wa mataifa makubwa yaani maraisi na wafalme wote wametokana na hizi familia 13. Humo zimezungumziwa familia kama Rothchilds, Bush family, Rockafela, familia ya ufalme wa uingereza na zengine kuwa hawa wote ni ndugu. Wanaoana wenyewe kwa wenyewe wakalink na kifo cha Princess Diana kisa ilikua ni kutembea na kutaka kufunga ndoa na yule jamaa wa kimisri hivyo angetoka ktk bloodline.

Wenye ujuzi tunaomba ufafanuzi hapa
 
Tangu niliposoma na kujua alichokuwa anakimaanisha Plato kwenye kitabu chake cha Republic hasa kwenye story yake ya Allegory of the Cave ndiyo nilianza kuelewa kabisa hasa tunaishi kwenye dunia ya namna ipi....

Kimsingi,watu wote ambao leo tunawachukulia kama "majiniaz" walipata ujuzi waliokuwa nao kutoka mahali fulani,Mesopotamia huko.Pythagoras,Socrates,Galileo,Alexander the Great,Plato na hadi hawa akina Sir Francis Beacon na John Dee ni watu ambao walipata elimu hizi tofauti kabisa na wanafunzi wengine waliikuwa kwenye madarasa ya watu hawa....

Socrates aliwahi kumueleza mwanafunzi wake mmoja aitwaye Plato kwenye madarasa yao kwamba,elimu anayowapa ni elimu iliyoko kwenye makundi mawili.Kunsi la kwanza ni lile la kawaida ambalo wanapewa elimu ya kawaida kuhusu mafuzo waliyokuwa wanapewa na kundi la pili ni lile ambalo linapewa elimu maalum na nyeti ambayo hakupaswa kupewa mtu yoyote na ni elimu maalum ambayo ndiyo lengo kuu la wao kufundishwa....

Kwenye darasa maalum ambalo walipewa elimu maalum ambayo Socrates alimueleza Plato,miongopni mwa wanafunzi waliokuwemo ni Plato mwenyewe.Utaratiobu huu ambao Plato alielezwa na mwalimu wake ulikuwepo tangu Socrates mwenyewe alipopata ujuzi huo kutoka kwa Pythagoras na Plato aliendelea kuwa nao na hata wanafunzi wake waliofuatioa kama akina Alexander The Great waliendelea nao....

Hapa sasa dipo tunakuja kupata maana mbili za hadithi ya Allegory of the Cave inayopatikana kwenye kitabu cha Plato kiitwacho The Republic.....

Hadithi ile inazungumzia watu waliokuwa kwenye pango ambao walikuwa wamefungwa kwa minyororo kwenye miguu yao wakati huo huo nyuma yao kukiwa kuna mto unaowaka.Watu hawa waliishi kwenye pango hili kwa miaka mingi sana,wakiwa wameelekezea nyuso zao kwenye ukuta wa pango lile wakitazama vivuli vyao ukutani na waliamini ule ndiyo ulikuwa uhalisia [the dancing shadow became their reality]....

Kwao maisha na dunia ilikuwa ni ile waliyokuwa wakiiona kwenye pango lile.vivuli ndiyo mazingira yaliyowazunguka na huo ulikuwa ni ukweli mkubwa sana kwao....

Uhalisia ule ambao ulikuwa wazi kabisa kwenye macho yao ndiyo ulikuwa ukweli.Haikuwa rahisi kabisa kuja kumueleza mmoja wao au wote kwamba ule hukuwa uhalisia kwakuwa walikuwa wakiona kwa macho yao.Waliamini kila walichokuwa wakikiangalia kilikuwa ndicho halisi...

Bahati mbaya kabisa ni kwamba hawakujua kwamba uhalisia ule ulikuwa umetengenezwa tu,haukuwa halisi.Waliamini kila walichokuwa wanakiona ni halisi.Waliamini hakuna anayeweza kutengeneza kitu halafu kikaonekana kuwa halisi hadi siku mmoja wao alipokata mnyororo na kutoka nje na kuuona uhalisia halisi na kurudi ndani kuwafungua wenzake minyororo ile na wao kuja kuuona uhalisia ambao hata kwa bunduki wasingekubali kuwa upo kama mtu angeenda kuwaeleza hili.....

Ukiangalia au ukitaka kujua maana ya hadithihii ndipo utakuja kuona kile ambacho kinaendelea duniani.Plato aliwaeleza maana halisi ya hadithi hii watu wachache sana wanaitwa "the elect ones",watu ambao walikuwa wakielezwa haya kwa sababu maalaum ili waje kutawala dunia....

Kinachoendelea duniani leo sicho kilichopo kwenye uhalisia,siyo uhalisia bali ni uhalisia uliotengenezwa tu.Wengi na nadhani hata wewe unaamini kuna ugonjwa unaosababishwa na kirusi fulani kinachoitwa HIV,unaamini kuna ugonjwa unoitwa EBOLA unaoua kikatili kabisa,unaamini kuna mafua ya ndege,unaamini kuna watu wanaotishia maisha ya watu wanaoitwa magaidi,unaamini rais wa Marekani anachaguliwa na wapiga kura kidemokrasia,unaamini kuna uadui kati ya Marekani,China na Urusi,unaamini dunia ina watu wengi sana hivyo inaweza kuja kuleta matatizo hapo baadaye hivyo tunapaswa kutumia uzazi wa mpango.Unaamini kuwa dunia ina mabilioni ya miaka,Unaamini kuwa viwanda vinaharibu hali ya hewa na kuzababisha mvua kutonyesha na kuongeza joto duniani,fake relity ziko nyingi sana....

Tunaishi kwenye pango,vivuli vilivyotengenezwa na moto ndiyo uhalisia wetu,giza lililoko ndani ya pango ndiyo ukweli wetu.Minyoror inatufanya tuamini hivyo kwakuwa hatuwezi kutoka humo....

Sasa basi pango ni nini,minyororo ni nini?Moto na vivuli ni nini? Maana za haya yote utaweza kupata angalau clue kama utanisoma hapo juu kwa makini.Hapa ndipo tunapokuja kuamini kwamba vita vinasababishwa kwasababu tunazoambiwa,lakini kuna sababu za kweli ambazo hatuambiwi....

Tunaishi kwenye dunia ambayo ukipata hata nukta kidogo ya ukweli utaogopa....

Nimesema haya ili kukufanya mkuu MSEZA MKULU uangalie tena mara mbili sababu za vita ulivyovisema hapo kwenye mada yako ili uone kama hazina chumvi au uongo.....

Ashante......
nmeizingatia sana hii comment.

kuna vitu vingi nikiviona huwa napata maswali ambayo majibu nnayopewa ni ya ukweli lakini akili yangu huwa hairidhiki kabisa.

kwenye hii dunia kuna namna
 
Niupo hapa JF tangu mwaka 2011,tumejadili mengi sana.Kuna mtu anaitwa juve2012 huyu jamaa namheshimu sana tena sana na anajua mengi sana na wala sihitaji kulegeza kamba za viatu vyake maana ni hatari....

Kuna mwingine anaitwa Deception huyu naye ni kiboko na ni hatari maana ana vitu adimu sana.Hawa ni watu ambao wapo hapa JF na ni watu ambao wanafabnya utafiti sana wa haya mambo.....

Kuna ukweli wa kutisha ambao wengi hawaujui au wanaujua lakini hawataki kabisa kuukubali,ukweli huu ni kwamba mambo yote haya yanahusiana na mambo ya kiroho,ni vita ya kiroho.Sasa wengine wakiona hivi wanakimbia au kudharau wakidhani mambo yakishaingia kwenye mambo ya kiroho basi ni mambo ya watu wasiojielewa.....

Kwao mambo ya kiroho ni mambo ya wajinga,wanashindwa tu kujua kuwa waliowafanya waamini hivyo wamefanya hivyo kwasababu tu wanataka wasijue mambo mazuri na yenye manufaa kwao.Watu hawajui tu kuwa watu wanaodhania hawafuati imani hao ndio watu wa imani hatari....

Huwezi kuamini,lakini ukweli ni kwamba sayansi na wanasayansi ni watu wa imani sana tu.Ni wafuasi wa dini tena dini za ajabu kabisa.Jiulize sababu ya wanasayansi kuwa watu wa imani wakati wao ni watu wa evidence....

Ukweli utakuweka huru,soma kuna bango hapo juu huenda ukapata mwanga kidogo....
Mkuu umenikumbusha mbaali sana enzi hizo ni kweli hawa watu ulowasema wako vizuri mnoo juve2012 Deception @Mgalanjuka na kuna mmoja naona kama kapotea kabisa humu anaitwa Barcelona
 
Hii dunia ina mambo mengi yamejificha, huwa najiuliza kwanini Rothschild family na Rockefeller families hawamo kwenye Forbes au kwa sababu wao ni trillionaires?

2b38bc01fa0ac4d8366381a2ed359ee3.jpg
Katika vita vyote hivi vitatu ilitafutwa sababu ya kuwashawishi raia wa marekani kuona ni Sawa nchi yao kuingia isipokuwa Vietnam War ambayo hadi kesho wengi hawajui kwa nini wapeleka kuua vijana wao huko.

1:WW1 meli kubwa lililojaa wamarekani lililipuliwa ( LUSITANIA attack) rais Wilson akaingia vitani.
2:WW2 Pearl Harbour Attack, Pamoja na kiongozi wa Japan kubembeleza wakae wayamalize Rais Roosevelt akaiingiza US vitani
3: War on Terror, September 11 attack Bush kuiingiza dunia nzima vitani.
Matukio yote hayo ya kigaidi yanasemekana kuPangwa ili kuhalalisha us kaingia vitani ili angalau hidden agenda ifanikiwe na mwisho unaosubiriwa na wanaimani wengi ufike. Hapo hakuna cha ufo wala allien wala semishetani being ni hawahawa wanadamu wanaokula Wali maharage.
 
Kuhusu Wanefili ni kwamba nina vyanzo tofauti tofauti ikiwemo Biblia.Kuna findings nyingi zana za kiutafiti ambazo zimepatikana na zinazoendelea kupatikana ambazo zinaonesha kwamba ni kweli wanefili walikuwepo.Vyanzo ambavyo ni baadhi ni The Book of Enock,The book of Giants,The book of the Dead n.k....

Ni kweli na nina uhakika kuwa Wanefili na masuala yote ya interbreed ni matokeo ya malaika waasi kukutana na wanadamu kimwili.Hili limeelezwa kwa upana wa ajabu kabisa na Henoko [Enoch] kwenye kitabu chake,ngoja nikuambie kitu....

Wakati wa kihistoria wa kule Qumran wa vitabu vya kale kabisa kugunduliwa karne ya 20,miongoni mwa vitabu vilivyogunduliwa huko ni The Book of Enoch,baada ya ugunduzi huu kutokea taarifa zilipofika UN,haraka sana jeshi la umoja huo lilifika eneo lile na kuzuia kile kilichokuwa kikiendelea eneo lile na baadaye eneo lile lilikabidhiwa kwa Vatican na baadaye hakuna kilichosikika tena kuhusu kitabu cha Enoch lakini ikasikika kuhusu mambo mengine ambayo yanaendana sawia kabisa na historia yetu.....

The book of Enoch ni kitabu ambacho kinaelezea mengi yasiyotakiwa kujulikana katika ulimwengu huu ikiwemo na rangi halisi ya Yesu,Waisraeli na ukweli juu ya yote haya ambayo yanaendelea leo.Yesu alikuwa mweusi kama wewe pamoja na Waisraeli,pia kwa namna ya ajabu ya ambayo unaweza kuona ni kama kichaa hivi ni kwamba kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa Wabantu ni Waisraeli,hili tuliache kwa sasa maana unaweza kuniona kichaa,lakini hayo ndiyo ambayo yalisababisha kitabu cha Enock kupigwa ban....

Kwa bahati mbaya sana copy ya kitabu hiki ilikuja kugunduliwa tena Ethiopia na walishindwa kuthibiti kusambaa kwake.kwa maana hii kitabu hiki kinatoa details za kutisha juu ya haya mambo....

Kinawataja malaika hao kwa majina,kazi walizofanya kudanganya wanadamu na chanzo cha yote haya.Kitabu cha ufunuo nacho kilitakiwa kisiwepo kwenye maandiko matakatifu ya Biblia lakini kilisalimika kutokana na lugha yake kuwa ngumu na kushindwa kueleweka na watu wengi.Lakini pamoja na hayo Shetani ameleta walimu wa uongo ili kupotosha kile ambacho kimeandikwa humo japokuwa kwa lugha ngumu kabisa,tuwe makini sana na hawa watu.....

Uwezekano wa jambo hili upo na linawezekana kabisa malaika hao waasi kuingiliana na binadamu.Kuna watu wanapinga hili lakini ushahidi uliopo unaonesha kinyuime na madai yao.Mfano kwenye Biblia agano la kale,waana wa Mungu wamekuwa wakisemwa kuwa ni malaika,ushahidi wa hili ni kwenye kitabu cha Ayubu nimesahau kidogo ni mstari upi lakini ipo na siyo mara moja,nikikumbuka nitakueleza maana hapa sipo kwenye utulivu mzuri kiasi,pia ushahidi kutoka kwenye vitabu vingine nilivyovitaja hapo juu....

Naomba niweke wazi kuwa,vitabu hivi,ukiacha kitabu cha Enoch,vingine vinbazungumzia mambo mengine ambayo siyo ya kweli.Kitabu cha Enech ni kitabu ambacho kwangu ni muhimu sana kwasababu ni kitabu ambacho hata baadhi ya wanafunzi wa Yesu walikirejea hasa Yuda aliyeandika barua ambayo ni miongoni mwa barua zilizopo kwenye Biblia,hivyo watu wanapovitafuta vitabu hivyo na kuvisoma wawe makini kweli kweli.....

Kuna kitabu ambacho wanaweza wasikipate,kitabu hicho ni The book of Jasher,hiki ni kitabu kilichosemekana kilitoweka na kilichopo ni copy ambayo siyo halisi hivyo pia wawe makini.Vitabu hivi ni source nzuri ya mambo haya pamoja na kutafuta makala ambazo watafiti wamefanya na kupata ushahidi wa uwepo wa viumbe hawa....

Kwa maana rahisi kabisa ni kwamba inawezekana na ilifanyika na inafanyika hadi leo kwamba kuna binadamu tunawaona kuwa ni binadamu lakini kiuhalisia siyo binadamu kwa silimia 100 na hawa ni matokeo ya wanadamu kukutana kimwili na wale malaika waovu....

Fuatilia kitu kinachoendelea kule Geneva kwenye mitambo ya baraza la Nyuklia la Ulaya lijulikanalo kama CERN kwenye mitambo ya LHC kisha uanzie hapo.Kama ni mchunguzi kuna mengi utayajua kupitia project hiyo.....
Kuhusu hayo ya Vatcan ndo maana ni vigumu na haitotokea Papa mweusi kutawala Vatcan,msinipige mawe nawaza tu japo kwa sauti!
 
Inahitaji jicho la tatu kuona haya mambo yanayoendelea kwenye hii dunia kama MKUU EIYER alivyojaribu kutumia jicho lake la tatu,,,,,,ukweli ni kwamba the world is far from perfect
Unachokitenda na kukiamini sasa ni matunda ya lucifer...... na huu ukweli vatican wanaujua na kamwe hawawezi kuufichua
 
Napenda kuungana na mkuu EIYER ya kwamba shetani anahusika kwenye udanganyifu huu kwa kadri anavyoona inafaa. Tukianzia eden kwa kutumia reference ya biblia shetani alimshawishi Hawa akiwa katika umbo la nyoka,Yesu alishawishiwa na shetani akiwa katika umbo la nyoka vile vile.
Uwezo huu wa shetani kujibadili na kuwa katika maumbo na tabia mbalimbali inaweza kusapoti wazo kwamba hata yanayotukia yanaweza kuwa yanatekelezwa naye mwenyewe au roho waasi wenzie. Mfano,Adam weishupt angefaidikaje na uandaaji wa plani ya miaka zaidi ya mia 3 na zaidi wakati anafahamu hata kuwepo kwa kipindi hicho? Inawezekana kabisa bloodline inayoongelewa hapa ndio inayotekeleza haya maana tunaambia katika biblia ya kwamba roho zao hazifi hadi siku ya mwisho ama shetani katika umbo la kibinadamu anayatekeleza haya.
Point yangu ya pili ni kwamba,references za mijadala yetu sote inatokana na kitabu biblia ambacho binafsi naamini hawa jamaa wanaweza kuwa wameisha distort ukweli kwa kiwango cha kutosha ndio maana mijadala yetu inakuwa haiishi kama duara. Mungu aliposema ya kwamba tutafute maarifa,alijua kutakuwa na hidden truth kuhusu yeye na uumbaji.
 
Katika vita vyote hivi vitatu ilitafutwa sababu ya kuwashawishi raia wa marekani kuona ni Sawa nchi yao kuingia isipokuwa Vietnam War ambayo hadi kesho wengi hawajui kwa nini wapeleka kuua vijana wao huko.

1:WW1 meli kubwa lililojaa wamarekani lililipuliwa ( LUSITANIA attack) rais Wilson akaingia vitani.
2:WW2 Pearl Harbour Attack, Pamoja na kiongozi wa Japan kubembeleza wakae wayamalize Rais Roosevelt akaiingiza US vitani
3: War on Terror, September 11 attack Bush kuiingiza dunia nzima vitani.
Matukio yote hayo ya kigaidi yanasemekana kubangwa ili kuhalalisha us kaingia vitani ili angalau hidden agenda ifanikiwe na mwisho unaosubiriwa na wanaimani wengi ufike. Hapo hakuna cha ufo wala allien wala semishetani being ni hawahawa wanadamu wanaokula Wali maharage.
Asante sana kwa ufafanuzi wako, hebu niambie wanataka nini kwetu kama kupotosha na kuwaibia wamisri mambo mengi hawatuachi?

Watawezi kumaliza dunia kwa malengo yao hata kama wakileta maradhi kama HIV zika nk au WW3 will wipe the entire population?
 
Asante sana kwa ufafanuzi wako, hebu niambie wanataka nini kwetu kama kupotosha na kuwaibia wamisri mambo mengi hawatuachi?

Watawezi kumaliza dunia kwa malengo yao hata kama wakileta maradhi kama HIV zika nk au WW3 will wipe the entire population?
hapa kuna mambo mengi na mitazamo mingi ila kinachotarajiwa sio kumaliza wakazi wa dunia. Hapana ni kuwaandaa wakazi wadunia wote watakaokuwepo juu ya kile kinachoitwa MAISHA BORA KABISA KWA KILA MWANADUNIA. Yaani ONE WORLD GOVERNMENT. ukifuatilia miaka ya zamani wafalme walitawala Dunia nzima bila kuwepo na vita vyovyote kikanda. lakini leo ni vita kila kona(probably planned to still minds of people to accept the pre-planned grobal proporsal). Haya mambo bado yapo kinadharia lakini siku yatakapo tokea tukiwa hai tutafanya informed decision. WW3 au War on Terror sio kwa ajili ya KUFANYA DEPOPULATION ila kuwashawishi wakazi wa dunia nzima juu ya mpango wa kuiunganisha iwe kitu kimoja, Na hapo kila raia wa dunia atakuwa na Option Moja kukubali au Kukataa na kubaki katika dilema hasa kama hauna imani dhabiti ya Mungu. Ila Asilimia ya kupinga inategemewa iwe ndogo maana tayari tunaandaliw a kupitia TV,MOVIES, SOCIAL MEDIA,CHurches, International forums and organizations, Schools and university Curriculums, Theatre centres, Entertainments etc, Yaani popote alipo mwanadamu amezingirwa na ushawishi wa kuprogram Ubongo kuchagua vya kupenda na vya kuchukia automatically. Automatic Grobal Mental Reprogramming. Haya tunayasema hayana haja sana kuaminiwa sasa ila ikitokea tusishangae sana kana kwamba ni wageni. Watu wanafuatilia trend hizi kwa Ku decode vitabu vya Daniel na Ufunuo japo sio kazi rahisi na kutia tick kila kinachotimia. Mambo haya yanafanywa na wanadamu purely. Kwa waamini na wafuatiliaji wa Bibilia kwa kusoma na kutafakari kuna suluisho kubwa tu la kuexist katika mazingira haya yanaoyoonekana ni ya kufikirika lakn ni busara kuacha chumba cha uhakika wa uwepo wake katika Ubongo ili yakitokea isiwe kama Suprise.
 
Mkuu mseza mkulu,kwa maana hiyo haja ya kuiunganisha dunia haiishii kwenye maisha bora kwa kila mwanadunia bali kutakuwa na conditions zitakazoingilia imani zetu katika kuabudu? Msituchoke jamani
 
Mkuu mseza mkulu,kwa maana hiyo haja ya kuiunganisha dunia haiishii kwenye maisha bora kwa kila mwanadunia bali kutakuwa na conditions zitakazoingilia imani zetu katika kuabudu? Msituchoke jamani
Wakati dunia ilipokuwa chini ya Mtawala mmoja mfano, Mesopotamia au Babylonian empire Chini ya mfalme Super Genius NEBUCHADNEZZAR dunia nzima ya wakati huo ilikuwa chini ya Mungu mmoja, Taratibu moja za dini, Mfumo mmoja wa kiuchumi,hata kama unafanya taratibu zako zako basi ufanye sirini usionekane. Na ilionekana ni rahisi sana kutawala dunia.
Ndio maana Wale jamaa watatu walioelezewa kwenye kitabu cha daniel walipogomea taratibu za dini wakati watu wote wa kila rangi kabila itikadi wakipiga magoti na kukubaliana Walitupwa ndani ya Moto. Na Ikaonekana kuwa na taratibu tofauti ni kama kuhatarisha amani. Na sasa kwa Mujibu wa wafuatiliaji wa mambo yajayo Dunia Inarudishwa kulekule babeli kwa kasi nzuri tu. Watu wa imani wanaamini Dunia inaelekezwa kwenye Vita ya Mwisho ambao Shetani na wafuasi wake wanakwenda kutumia SIlaha zao za mwisho za maangamizi Ila Mungu nae anaingilia kati kwa kwa walio wanyenyekevu kwake. Kwa lugha ya picha hiyo hali imeelezewa Ufunuo 18:2,3 Ila haita dumu muda mrefu Mungu anaingilia Kati na Huo ndio Mwisho wa Historia ya Ulimwengu. Huu ni Mtazamo wa kidini japo kuna Mitazamo mingi maana dunia hii huru tunajadili mambo Kidini, Kiuchumi, Kisiasa, Kimaendeleo na kila Mtazamo Unapingika na unakubalika. Kwa mtazamo wa Kidini Dunia hii kama ni Meli imekalibia Bandarini hakuna kurudi nyuma. Ila kisiasa na kiuchumi ngoja tuendelee kutatua matatizo yetu ta kila siku maana haya Mambo lazima yamuathiri kila mkazi wa dunia kaika nyanja zote za maisha yake ikitokea yametokea.
 
Huwa najiuliza maswali kama haya haya je hii Dunia iko Miaka mingapi? Je ni kweli vita zile zilizotokea zilikua na sababu hiyo tu ya mtu kuuwawa basi ikawa balaa lile...lakini ukiangalia Duniani hapa Matajiri na watu wenye pesa wana nguvu kubwa hata kushawishi nani awe nani serikalini..hilo limetokea majuzi kule Afrika Kusini familia ya Gupta ikituhumiwa kuteua Mawaziri..
Lakini kule Brasil kuna mawaziri wa Rais Temer wana tuhumiwa kucheza deal na yeye Rais huyo ambae alijitenga na serikali ya Dilma Rousef...Mama huyu inasemekana kama ilivyokua kwa Chavez..kichner yule wa Argentina na wengine wengi waliokua na misimamo mikali kuanzia Saddam Hussein..Ghadafi..Ahmed Nejjad...na dogo wa korea ya kasikazini manake hawa ilitakiwa waondoke mmoja baada ya mwingine kwa njia zozote zile...ukiangalia Dunia hapa kwasasa mtu kabisa mwenye msimamo mkali na ushawishi mkubwa hayupo tena....na msisahau watu wale wapambanaji sio rahisi kupatokina....naamini kuna zimwi linaongoza Dunia kiimani..fikra na matendo
 
Nimejaribu kuwafuatilia wadau hapo juu ila naona mtanichanganya tu .Mkuu Eiyer hivi ni kitu gani kitanifanya niamini haya uyasemayo ni kweli na nisiamini hichi nilichokikuta na kukiamini ? Hapo kwa hawa jamaa Wanefil bado kuna majibu naona hayajakaa kushawishi kwamba ndio ukweli wenyewe

Kuna swali mdau kakuuliza hapo juu
Inakuwaje kwa malaika kuwaingilia kimwili wanadamu ? Je waliumbwa na jinsia tofauti ?
Au kwa sababu ni malaika basi wana uwezo wa kujibadilisha ?

Hicho kizazi cha Wanefil kilicho teketezwa na Gharika kuu ilikuwaje wakasalia ? Wakati safina ilibeba watu nane tu ? ..

Pia siwezi kukulaumu sana kwa sababu itahitaji miaka kama 30 kuanza kuamini huu ulimwengu wa pili tofauti na huu nilio zaliwa nikaukuta

Na maswali mawili hapa baada ya wewe kujua habari za ulimwengu wa pili umepata faida gani mpaka sasa ?

Kwamba kila tunachoambiwa ni uongo tu huku ukweli ukibaki kwa watu wachache
Ni kwanini wanadamu wachache wenye kujua hizo siri wazipiganie kwa hali na mali huku wakijua watakufa na hawaishi milele ?
 
Back
Top Bottom