Sweet16
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 5,314
- 9,215
Mbona uyo mkoa katoka lakini yuko jijini tuseme tu ni wa dar mc pilipiliWanaume wa mikoani wameumia sana nyie wanaume wa mikoani ni dhaifu na washamba...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona uyo mkoa katoka lakini yuko jijini tuseme tu ni wa dar mc pilipiliWanaume wa mikoani wameumia sana nyie wanaume wa mikoani ni dhaifu na washamba...
Mmh hapanaKulia ni normal reaction,tendo lilikua emotionally significant...
ameojiwa nimeona clip anasema alikuwa anapigiwa sana simu na majamaa wanalalamika wamepokonywa demu wao ambaye walikuwa naye toka chuo,hivyo wakati anamvalimisha pete akakumbuka milima na mabonde yote hakuamini kama wamefika hatua hiyo akalia kwa furaha
Mmh hapana
OkeeIko subjective,Kama unaona hapana kwake ilikua Ndio,hakuna safari ya mapenzi inayolingana na mtu mwingine,kila mtu ana experiences zake
[emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16]ah ah ah daah,siamini km kitu km hiki kimetokea,ah ah ahHuyu jamaa hii clip yake nimeshindwa kuirudia hadi najisikia aibu kuitazama tena,kafanya kitendo cha kilofa nahisi ana chembechembe za mwanaume wa Dar.
Eti mwanaume rijali unamvish pete mpenzi wako huku unajiliza huo ni udada,yaani ni balaa sitamani kijana mwingine aje afanye kitu kama hiki.
ILA LABDA HUENDA JAMAA KAMKUTA MWANAMKE NA BIKRA[emoji23] [emoji23] [emoji23]
MGOGO KADATA
Beautiful ones are not yet born
Nakubali mwanaume analia lkn pale hakukuwa na hisia zozote.Kasumba ya wachangiaji jf bhana ni kufuata mkumbo wa wachangiaji wa kwanza kwenye uzi, kama wachangiaji wa mwanzo wakiwa na mtazamo hasi basi hata wanaofuatia huendelezea mkumbo uleule na iwapo wachangiaji wa mwanzo wakiwa chanya wengi wa wanaofuata huwa hivyo hivyo.
Nina hakika wapo waliochangia bila hata kuiona video husika kwa kuwa hawana MB za kutosha ila mkumbo tu...
Wapo ambao ni wanaume na wapo dar ila huji-position mikoani kwa muda tu hasa pale mada inapohusu udhaifu wa kinachoitwa "wanaume wa dar" na kisha hujirudisha Dar wakati wa kuelezea "ushamba wa watu wa mikoani (nje ya dar)". Hawa ni kama popo-watu.
Mimi nakataa kabisa, Mc Pilipili hakulia bali machozi ndiyo yalimtoka machoni kutokana na hisia kali anazozijua yeye mwenyewe! Ni machozi yanayobemba ujumbe mkubwa kuliko kile kinachooneka mbele ya macho ya watazamaji... Machozi ya namna hiyo hayatawaliki, na kila unapojaribu kuyatawala, nayo huongezeka mara dufu.
Sio kweli kwamba wanaume hawatokwi na machozi, hayo ya hisia huwatoka wanaume wengi tu hata kama kwa kujificha ili kuficha 'aibu'... Ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko uwezo wa kibabe wa kiume. Nina uhakika, Mc Pilipili anaweza kupigwa fimbo 20 au zaidi na asilie... Lakini machozi yatokanayo na nguvu ya hisia hayazuiliki.
Kitu ambacho siungi mkono, ni suala la kumpigia magoti mwanamke wakati upo katika hatua muhimu ya kuchukua uongozi wa familia yako kama baba, ni kuigaiga tu.
Kama hujanielewa unaongozwa na ushabiki ama wivu kumuhukumu Mc Pilipili.
Siyo li mtu la shinyanga kweli? Kama ningekuwa baba yake lingekula kofi moja matata sana