Kasumba ya wachangiaji jf bhana ni kufuata mkumbo wa wachangiaji wa kwanza kwenye uzi, kama wachangiaji wa mwanzo wakiwa na mtazamo hasi basi hata wanaofuatia huendelezea mkumbo uleule na iwapo wachangiaji wa mwanzo wakiwa chanya wengi wa wanaofuata huwa hivyo hivyo.
Nina hakika wapo waliochangia bila hata kuiona video husika kwa kuwa hawana MB za kutosha ila mkumbo tu...
Wapo ambao ni wanaume na wapo dar ila huji-position mikoani kwa muda tu hasa pale mada inapohusu udhaifu wa kinachoitwa "wanaume wa dar" na kisha hujirudisha Dar wakati wa kuelezea "ushamba wa watu wa mikoani (nje ya dar)". Hawa ni kama popo-watu.
Mimi nakataa kabisa, Mc Pilipili hakulia bali machozi ndiyo yalimtoka machoni kutokana na hisia kali anazozijua yeye mwenyewe! Ni machozi yanayobemba ujumbe mkubwa kuliko kile kinachooneka mbele ya macho ya watazamaji... Machozi ya namna hiyo hayatawaliki, na kila unapojaribu kuyatawala, nayo huongezeka mara dufu.
Sio kweli kwamba wanaume hawatokwi na machozi, hayo ya hisia huwatoka wanaume wengi tu hata kama kwa kujificha ili kuficha 'aibu'... Ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko uwezo wa kibabe wa kiume. Nina uhakika, Mc Pilipili anaweza kupigwa fimbo 20 au zaidi na asilie... Lakini machozi yatokanayo na nguvu ya hisia hayazuiliki.
Kitu ambacho siungi mkono, ni suala la kumpigia magoti mwanamke wakati upo katika hatua muhimu ya kuchukua uongozi wa familia yako kama baba, ni kuigaiga tu.
Kama hujanielewa unaongozwa na ushabiki ama wivu kumuhukumu Mc Pilipili.