Ya MC Pilipili hayapaswi kufanywa na mwanaume rijali

Ya MC Pilipili hayapaswi kufanywa na mwanaume rijali

Walikuwa wanamtosa sababu nasikia jamaa ni aina ya Wale Wanaume wenye viherehere. Wanaongea sana. Na Mwanaume unapaswa kuwa na Akiba ya Maneno. Sasa unaambiwa akiwa na Demu halafu akakutana na Marafiki wa huyo Demu ni yule Mwanaume asiyekuwa na Haiba. Anaongea anapitiliza. Aliwahi kudate na Rafiki yangu Mmoja hivi siwezi kumtaja hapa. Alimwacha kwa mambo yake hayohayo. Atofautishi Mahusiano na Comedy zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Oouh..sawa sawa.
 
Hivi mkuu hujaona vizuri hiyo clip au unajitoa ufahamu, jamaa kapiga kwikwi kama zote, domo limejikunja uso umejikusanya unasema hajalia, yani pale angepigwa busu kabla hajavika pete angegalagala chini au angezimia kabisa we angalia vizuri usipotoshe uma, kaanza taratiibu kafinya finya macho, then domo likajikunja, then huku anasikitika haamini anachokiona mbele yake baadae fulu mafuriko we huoni au unakataa kuona makusudi, au ulilia mzee baba na ww ulivyoona hiyo video clip

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha baba la baba
Unaonekana jinsi gani hufai kuwa KIONGOZI katika jamii yoyote ile duniani maana kwa kuendekeza hisia zako kila siku utakuwa unatamani Wake za wafanyakazi wenzako, na watakutafuta kwa mapanga na marungu hadi wakutoe marinda, wakuasi na kukuua kwa kushindwa ku-control hisia zako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Duh! Punguza stress mwana, hayo mambo ulofanyiwa unadhani yanafanyika kwa kila mmoja!! Pole sana, nikuhakikishie hukunielewa, waachie tu wenye uwezo huo.
 
hii thread itawafanya waliotaka kupiga magoti wawavishe pete wachumba wao wasifanye hivyo kwa kuhofia kuonekana 'dhaifu'...jamani kupiga magoti na kulia ni expression how you feel...kusema kweli anayeliliwa hujisikia vizuri na yule anayelia anajiskia vizuri kumuonyesha jinsi anavyompenda na jinsi hafichi hisia zake juu yake…kwa kimombo ni 'affection'..kwa kweli ni gesture tu..UANAUME WA MC PILI PILI ANAYEJUA NI HUYO MCHUMBA WAKE..msimpake kaka wa watu matope mpaka aanze yeye na mkewe mtarajiwa kujishtukia...MC POLE POLE KAMA UNAISOMA HII TOPIC JUA ULICHOFANYA NI PERFECT NORMAL...
Rebeca83, hakunaga kitu kama hicho. Ni muigo wa kipuuzi kweli kweli ni udhaifu upuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili jambo la mwanaume kupiga goti wakati wa kumvalisha pete mchumba naona linazidi kukomaa,si utamaduni wetu japo sio mbaya sana kwani ni effects za globalization kwenye muingiliano wa kiutamaduni na wazungu/waarabu/wachina na vile tunasema "strong culture absorbs weak culture" na hii inachangiwa sana na nguvu ya kiuchumi.

Tuyaache hayo,leo Mc wa taifa Pilipili kama anavyojiita mwenyewe kamvisha pete mdada mrembo sana huko Boko Dsm hongera kwake but concern yangu kubwa ni kitendo cha yeye Pilipili kama Mwanaume kulia sana wakati kapiga goti mbele ya binti halaf binti anaonekana hana hata chembe ya hofu na kuguswa na kilio cha pilipili,huu ni udhaifu ambao kama.

Mwanaume lijali hakika hupaswi kuuonyesha,that is a big point of weaknes,hata kama umewahi kuumizwa sana kwenye mapenzi jitahidi usitoe chozi mbele ya mwanamke ambaye si mama yako,hii itakusaidia sana hata ukiwa kwenye ndoa ukitoa maamuzi yanakua ya kiume kweli kweli but hii ya kulia lia si dalili njema sana,kwa anayewajua vizuri wanawake atakua amenielewa.

By the way hongera sana Pilipili kwa kupata mchumbaView attachment 987138View attachment 987135
Mchekeshaji maarufu Bongo, MC Pilipili jioni ya leo amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake (Mke mtarajiwa) Philomena Thadey, nyumbani kwa Wazazi wa mwanamke maeneo ya Boko (Tegeta) jijini DSM, sherehe hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wa Serikali na taasisi zisizo za kiserikali.
Wale wanaUME walokwisha fanyaga huo ukuda hivo watuambie ninini kiliwasukuma, sikuhizi naona wana wanalia michozi na kupiga goti kama sio magoti. Utamaduni mpya huu au uzuzu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo tumejijengea mwanaume hatakiwi kulia wakati wanaume wako sensitive and vulnerable Kama sisi tu,mie ningependa mwanaume wangu alie tena kwa yowe,yewoooomiiii
Yani halafu akishalia, uanze kumuona dhaifu na kumdharau!
 
Yani halafu akishalia, uanze kumuona dhaifu na kumdharau!

tuna mitazamo inayokinzana,siwezi kumuona mwanaume anayelia ni dhaifu,na siwezi kumdharau,sikushangai lakini kama umekuzwa ukiaminishwa mtoto wa kiume halii..utaendelea kuwa mkubwa ukiamini hivyo hivyo...
 
Nikupigie magoti? Are you doing me a favor? Kwani wewe hutaki kuolewa na mimi?

Don't you want this as much as I do? If not then nimekosea mahala. If you do, put the goddamn overpriced ring on.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tuna mitazamo inayokinzana,siwezi kumuona mwanaume anayelia ni dhaifu,na siwezi kumdharau,sikushangai lakini kama umekuzwa ukiaminishwa mtoto wa kiume halii..utaendelea kuwa mkubwa ukiamini hivyo hivyo...
Kuna wakati ninakuwa na huzuni, ila ni aghalabu kuonesha hisia zangu dhahiri, nikizidiwa ntalia nikiwa alone. Males must be nurtured to be strong otherwise tutakuza vizazi vya akina MC Pilipili ambao wataingia kwenye ndoa huku wakiwa hawawezi kusimama imara. Inatokea changamoto, mke analia baba anashindwa ku take charge nae anaungana na mkewe kulia. Ulishawahi kumuona baba yako anajiliza mbele za watu!
 
Back
Top Bottom