Yafuatayo ni mawazo mgando ya Wanaume wengi Mabwege na wenye Akili duni.

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
YAFUATAYO NI MAWAZO MGANDO YA WANAUME WENGI MABWEGE na WENYE AKILI DUNI.

Anaandika, Robert Heriel Mtibeli.
Yule Shujaa.

Moja ya mambo yaliyonifanya nisipende kukaa vijiweni na kuwaelewa wazazi na walezi wangu ni kutokana na mitazamo, fikara, na mawazo ya vijana na wanaume wengi wanaokaa vijiweni. Ambapo kimsingi, nikiri na niseme kwa kinywa kipana kwamba asilimia 90% ya wanaume wanaokaa vijiweni ni Wambea, wasengenyaji, na wana akili finyu au fikra potofu.

Ukifika vijiweni, stori kubwa utasikia ni kelele za mipira, udaku, stori za kina Diamond, kusengenya wapita njia,
Kuonea wivu waliofanikiwa kidogo, fikiria mwanaume mzima linalialia kwamba fulani alipita hasalimii. Unaweza ukaona akili yake inavyofanya kazi. Ni akili ndogo sana. Alafu ukiyakuta yanavyosengenya, jamaa anajiona sana, kagari kenyewe kamkopo, ni aibu tupu kwa kweli. Kimsingi mimi siwezi kukaa na watu wenye mitazamo duni kama hiyo.

Vijana lazima mjifunze ku-Mind businesses zenu. Kama ni mpira jadilini mpira bila matusi. Kuweni kama wanaume wenye Akili.
Sasa ukute huo ujanja wakujadili mpira yanavyojadili. Yaani kutukana na maneno ya kiupuuzi kwao ndio wanajiona wajanja fulani hivi au kwamba wanajua mambo ya kihuni. Kimsingi wanaume wajinga na wapumbavu huchukulia uchafu na matusi kama utambulisho wao wa kuonekana wa mjini. Kumbe ni majinga majinga tuu.

Sishangai CCM na serikali yake ikiwanyoosha. Huwezi kuyapa haki na mambo mazuri majitu majinga majinga yenye akili chafu. Inasemwa usiwape Nguruwe dhahabu wasije wakakurarua rarua.

Sisi Watibeli tunapenda HAKI, tunaijua na tunaiishi.
Tunajua kuwa ni haki watu wajinga watumiwe,
Tunajua ni haki watu wasiojitambua wanyooshwe.
Tunajua ni haki watu wachafu na wenye mitazamo michafu kuishi jalalani huko. Huko ndiko wanakoishi nzi, mende na funza.

Wanaume,naongea na wale wanaume ambao bado wanaakili na wanatamani kuwa wanaume wenye Akili ambao hao ndio watawala.
Uanaume unaanzia Akilini, jua hilo. Huwezi ukawa mwanaume kama unakichwa kibovu, kichafu.

Sasa nisiongee sana maana ni kama nime panic hivi. Au nimechukulia mambo personal.

Yafuatayo ni mawazo mgando ya wanaume mabwege na wenye akili Finyu;

a) Mwanaume kaumbwa Mateso.
Ukiwaza hivi wewe ni kichaa, unaakili chafu.
Mwanaume ni mtawala. Uliwahi kuona mtawala akiteseka. Msiwe majinga majinga.

Uteseke kwaajili ya nini na nani?
Uanaume sio kuteseka. Hiyo ni misemo na mitazamo ya wanaume mabwege, watumwa na misukule.
Ni lazima ufundishe mtoto wako wakiume hivi, yeye ni mwanaume. Yeye ni mtawala. Yeye ndiye anatakiwa kuyafanya mambo yaende.

Unaposema mwanaume kaumbiwa mateso unamfundisha pia mtoto kuwa na mtazamo wa kuteswa. Lakini pia kutesa wanaume wengine kwa kisingizio cha wewe mwanaume bhana. Jikaze.
Alafu wenye mitazamo kama hii ukifuatilia wanautumwa ndani yake. Huwezi sikia mtu mwenye kipato kikubwa ukamletea hizo stori. Hizo stori utapelekea wafanya kazi ngumu, watesekaji alafu unawalipa malipo kidogo. Unawaambia mwanaume ni mateso.

Huko kwenye mapenzi na ndoa. Unakuta mwanaume anateswa na mkewe, matoto yanamdharau, hayana adabu. Lenyewe unalikuta huko kibaruani linaimba aiseeh wanaume tumeumbwa mateso. Pumbavu wewe ndio mpuuzi uliyeumbwa kuteswa na huyo mwanamke wako aliyekutawala. Na matoto uliyoshindwa kuyaongoza.
Yaani Mimi mtibeli nitafutie pesa, nihudumie limwanamke na matoto yasiyo na adabu kwa jina la ndio uanaume. Labda sio Mimi.

Sisi Watibeli, wanaume hatuteseki. Bali tunatawala.

b) Mwanaume lazima uwe na kovu na usiwe msafi sana.
Haya ni mawazo wanaume maskini wa akili na wachafu.
Yaani ni yale mawazo ya wasela Mavi. Yaani kwao kuwa na Ngeu, machata, na makovu ya kipumbavu kwao ni sifa.
Wewe sio Askari wala mwanajeshi. Hufanyi kazi za kukupa majeraha kipi sasa kinakufanya mwili wako uwe na majeraha kama sio akili ndogo.

Kitu kidogo unataka kupigana pigana hovyo kama mwendawazimu. Kwamba kumpiga mtu ndio kumfanya akuheshimu.
Wewe uliwahi kuona mtu mpumbavu, maskini wa akili na kipato, asiye na maadili akaheshimika popote?

Fikiria mwanaume kutokuoga kwake ni sifa. Kuvaa boksa wiki nzima ni sifa. Anaita uanaume.
Kwamba anavyonuka, na boksa kuchita, kushika ukurutu ni sifa.

c) Mwanaume lazima akae Jela au mahabusu.
Sio lazima uende jela au mahabusu.
Jela sio sifa. Mahabusu sio sifa.
Mahabusu au jela uende kama kuna huo ulazima sana tena sana.
Mfano;
Ulazima labda umeiba pesa nyingi sana. Na wanaume wenye akili wanajua maana ya pesa nyingi. Sio uende jela kwa milioni mbili sijui kumi.
Uende jela kwa kutetea familia yako dhidi ya wavamizi kama majambazi.
Sio unaenda jela ati umeiba kuku sijui milioni 10. Au mmepigana.
Nenda Jela kama unapigania Haki za taifa lako. Kwamba unapenda nchi yako na upo tayari kuilinda.

d) Mwanaume lazima ahonge.
Ni majinga tuu na mashamba ya wanawake ndio huwa na misemo na mitazamo kama hii.
Sisi Watibeli, mwanaume lazima umpende Mungu kuliko unavyompenda mwanamke,
mwanaume lazima ujipende wewe kuliko unavyompenda mwanamke.
Lazima upende kazi yako kuliko mwanamke.
Lazima upende hela yako kuliko unavyompenda mwanamke.
Kisha utakapooa na kuwa na mke ndiye unayetakiwa umpende lakini upendo huo usizidi yale niliyoyataja kule juu.

Usitoe pesa kwa mwanamke zaidi ya unavyojihudumia wewe mwenyewe.
Kama utamnunulia mwanamke simu ya laki tano. Hakikisha wewe unasimu ya milioni moja na nusu.

Kama utampangia mwanamke nyumba ya laki Tatu. Hakikisha unaishi nyumba yenye thamani ya kupangishwa laki tisa kuendelea.
Yaani kila unachompa mwanamke hakikisha wewe ulishajipa mara Tatu yake.

Alafu uone kama hii Dunia utaiona ni mbaya. Alafu uone hii Dunia utawachukia wanawake.
Wanawake hawana matatizo. Matatizo unayo wewe na akili yako finyu.

Angalia watawala na serikali.
Mtumishi analipwa milioni moja. Kisha angalia mbunge au waziri au Rais wao wanajilipa ngapi.
Tumia kanuni hizo za kitawala.

Ukiitwa mbinafsi wewe usijali. Ubinafsi kwenye kitu chako ulichotafuta Kwa jasho na nguvu zako sio kosa.
Mbona kwenye kutafuta hakuiti mbinafsi, hataki nusu kwa nusu au zaidi kushiriki. Lakini kwenye mapato anataka nyingi.

Tumia akili. Usiwe kama Punda. Shenzi.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es sal
 
Mbona kama umepanic na hayo uliyoandika yoote ndo wewe😂😂😂😂😂
mwanaume mfikilivu hana muda wa kuandika ujinga kama huo

Kazi yangu ni kuandika.
Hilo sasa umelijua. Naamini ungekuwa unalijua hili ungetoa maoni mengine
 
Mwanaume hatatei ushoga, wala huwezi kuta mwanaume anakuambia Yesu alikuwa anakaa na mashoga.

Upo sahihi. Kwenye sentensi ya kwanza.

Ila kuhusu Yesu kukaa na Mashoga hilo haupo sahihi. Yesu alikaa pia na mashoga.

Kati ya kukaa na mashoga na kufia mashoga kipi kwako ni rahisi?
 
we bwege huna uanaume wowote, huna jambo lolote la maana

tangu nilipo ona mchangoo wako kufurahia TL kuteswa ndio nilipo gundia n bwege wewe

Hivi vibandiko vyako vinakufanya ujione we tofauti kumbe bwege tu

Mtazamo wako ni mali yako. Maoni yako ni uhuru wako.

Hayo ya Lisu huna ujualo.
 
Upo sahihi. Kwenye sentensi ya kwanza.

Ila kuhusu Yesu kukaa na Mashoga hilo haupo sahihi. Yesu alikaa pia na mashoga.

Kati ya kukaa na mashoga na kufia mashoga kipi kwako ni rahisi?
acha zako kijana, usiongeze maneno yako mahala ambapo yapo. Labda hiyo ni biblia ya version yako. Unashindwa elewa tofauti ya dhambi na shoga
 
acha zako kijana, usiongeze maneno yako mahala ambapo yapo. Labda hiyo ni biblia ya version yako

Wewe kipi kinakufanya ukatae?

Ukisikia Wenye dhambi waliokaa na Yesu, unakataaje Maashoga hawakukaa naye? Kwani mashoga sio wenye dhambi?
 
Bado vipo sana mkuu, kimsingi wanaume wakika kikundi ni mwendo wa kusengenya tu.
Habari za Jumapili mkuu?
Sawa kiongozi. Ndio umuhimu unakuja wa kuwa na watu mnaoongea mambo ya kufanana, hasa kama ni ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom