Yajue haya majani ni dawa ya vidonda vya tumbo

Umenikumbusha home, Mbeya tunayaita matatila ni kweli. Japo ili uyatumie kama tiba huchemshi. Unatwanga hayo majani ya aina mbili, kila aina ya majani ijae kiganja kimoja, kisha chukua maji robo lita kisha chuja mchanganyiko huo wa rojo ya majani kisha kunywa kwa siku 4,
Nashauri dozi iwe fresh daily ili kupata matokeo mazuri, sio kuhifadhi kwenye friji, ili utumie siku nne.
 
Mimi ni shuhuda wa hilo Jani la pili,,, sinywi dawa za vidonda vya tumbo siku hizi,imekuwa Kama utaratibu wangu nakunywa kila baada ya miezi miwili kwa siku tano . Na hata wakati wa covid tumelitumia Sana home kwa ajili ya covid.
Hili huwa linaota wapi mkuu
 
Hapo hayo yote ni majani ya chai,,wa kwanza ni mchomachoma unatibu vidonda vya nje,vya tumbo,kuongeza damu mwilini na wa pili sijui kaz yake ila naweka tu kama majan ya chai
 
Nimepata tabu kweli kuujua huu mmea..ila kutokana na maelekezo nimeujua[emoji1317][emoji1317]
Wahaya wanayaita "obukurula"...
 
Nashukuru kwa maelekezo mkuu, nasumbuka sana na vidonda vya tumbo. Kwa bahati nzuri mkoa niliopo sasa haya majani yapo kwa wingi sana nitayatumia na nitakupa mrejesho.
Upo mkoa gani jmn
Nateseka na vidonda aisee!
Naomba msaada wako
Mrejesho pia
 
Asante
Kiasi gani hayo maji yake unayotakiwa kunywa?,kikombe au
 
Kama kuna anayepata taabu na vidonda vya tumbo nitafte inbox nikupe no. kwa dawa hii usipopona basi wewe utakuwa na tatizo jingine.Kama mimi nimepona kwa nini wewe usipone.
Kwann inbox na usiwe hapa km wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…