Yajue haya majani ni dawa ya vidonda vya tumbo

Kama kuna anayepata taabu na vidonda vya tumbo nitafte inbox nikupe no. kwa dawa hii usipopona basi wewe utakuwa na tatizo jingine.Kama mimi nimepona kwa nini wewe usipone.
mkuu naomba nikuone
 
Mimi ni shuhuda wa hilo Jani la pili,,, sinywi dawa za vidonda vya tumbo siku hizi,imekuwa Kama utaratibu wangu nakunywa kila baada ya miezi miwili kwa siku tano . Na hata wakati wa covid tumelitumia Sana home kwa ajili ya covid.
Kwaiyo unatwanga au unachemsha ndugu
 
Akunamaelezo ya matumizi kuwa unachuma una twanga au unachemsha swara unasema dawa ya tumbo na kunywa basi apo ujasaidia kwakweli toa maelezo na mtu apate kuelewa
 
Kama kuna anayepata taabu na vidonda vya tumbo nitafte inbox nikupe no. kwa dawa hii usipopona basi wewe utakuwa na tatizo jingine.Kama mimi nimepona kwa nini wewe usipone.

Wakuu achaneni na Inbox...Au unafanya Biashara?
Weka wazi ili na wengine wafaidike na Utabarikiwa...
Sasa kila Mtu unataka Aje inbox duu....wewe hakuna Vitu ambavyo umefaidika kwa Kusoma haoa JF au kwingine?
Je wangesema na wao kwa wao watumiane inbox wewe 3part ungejuaje?
Jifunze mkuu
 
Wewe sio mgonjwa na haujawahi kuumwa, mshukuru Mungu kwa hilo. Inbox sio mbali ( na dawa sitoi bure nakuuzia)
 
Kama kuna anayepata taabu na vidonda vya tumbo nitafte inbox nikupe no. kwa dawa hii usipopona basi wewe utakuwa na tatizo jingine.Kama mimi nimepona kwa nini wewe usipone.
Boss Pm umefunga
 
hayo mashona nguo kwenye picha ya kwanza moshi tunayaita "mambara" sema pronounciation yake sio kama inavyosomeka hapo. ni tiba hata kwa wale wajawazito walio na upungufu wa damu hata ukienda clinic huwa wanashauri kutumia majani haya kwani yanaongeza damu. yakikomaa yanakuwa na vimiiba flani hivi vyeusi vidogo dogoo lakini havichomi. vimiiba hivyo vinakuwa kwenye vi bunch bunch na sio scattered ila ukipita na nguo zako ndefu huwa yanakamata na kubakia kwenye nguo.

picha ya pili ki moshi moshi hayo majani tunayaita "ombo au wombo" ni yale waliyasema yanatibu corona. hata kama hayatibu vidonda bado ni majani mazuri. kwa wale tumbo hujaa gesi au kuunguruma wanapokula maharage au nyama basi huchemshiwa huko kuunguruma au kujaa gesi au kiungulia hutakusikia. wale wenzangu tunaochinjiaga mgombani na kupiga supu ya pale kitu cha mgombani mtakubaliana na mimi kuwa wakati mwingine huwa tunachemshia huko hayo majani. na nyama inakuwa na ladha na harufu nzuri sana, husema hata mtu awe na kijicho cha namna gani wakati mnakunywa supu hiyo hutodhurika kabisa

kwa wale wengine ambao kwenye sherehe habanduki mpaka ale chakula, kama utatoka hapo umeangaliwa na kijicho tumbo likakushika ghafla basi ''ombo" ndio kiboko kabisa. hata tumbo likiwa linakuuma, au umeamka umevimbiwa basi hii kitu ni dawa nzuri sana.

dawa nyingine nzuri kwa tumbo ni yale majani laini ya mapera.

niishie hapo....
 
Hii ya kwanza ikikuwa ikokomaa inakuwa na vitu vinashika nguo vyeusi?
 
Hili jani nimelielewa jana tu kuna mzee mmoja aliniambia hiyo dawa nzuri ya vidonda.ina harufu mbaya ila ni dawa kwetu ni aina ya magugu yanaota kwenye migomba.
 
Ahsante kwa kuonesha moyo wa kujali
 
Sidhani kama ina side effect maana kwetu mtu akijikata hiyo dawa ndo tunamfungia kwenye kidonda kuzuia damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…