Yajue mafao ya viongozi wa kisiasa

Mada kama hizi ndizo haswa zinatakiwa hapa JF,ilikujua nchi inafirimbwa kiasi gani,sio zile mada zakina nani wale vichwa maji,kutwa mapambio..

Kwa mfano sioni haja ya Mstaafu kulipwa 80% ya mshahara wa aliyeopo madarakani..30% ingetosha sana..80% ni kama vile wana majukumu sawa,wakati huyu tayari ni Mstaafu..ni kutumwa tu hapa na pale
 
Mkuu pambana kijana wako awe mwanasiasa. Au la, pambana nawe uingie siasani kama umri haujakutupa mkono[emoji23][emoji23]
Mkuu, siwezi kutamani wanangu waingie kwenye siasa. Namimi sitamani kuingia kwenye siasa kabisa kwasababu naamini mafanikio yangu yatatokana na bidii zangu.
 
Wabunge wakimaliza miaka 5 hulipwa 400M
 
Na hii ndo maana tunataka katiba mpya na wao hawataki wanajua kitakachofata baadae
 
Na hapo ni mafao ya miaka 10 kwa awamu mbili....
Ila kuna mtumishi kafanya kazi zaidi ya miaka 30 mafao yake kupata ni sarakasi, na hicho kidogo anachostahili bado eti apewe kidogo kidogo😢
Tena wanampa Mil 50, 70 au 90 halafu anaambiwa zingine atapewa baadae 🤣🤣🤣
 
Hii ndiyo CCM niijuayo mimi.
 
Duh! Kwa hakika inashangaza sana..
 
Kwa kifupi, mfumo mzima wa serikali haupo kwa manufaa ya raia walio wengi. Sheri wanazotunga ni zile ambazo haziwagusi wao kabisa. Jeshi la polisi lipo kuwalinda walio wachache na si kulinda mali na usalama wa raia.
Kuzaliwa mtu mwesi imekua kamalaana by default. Wananchi hawana maji, hawana umeme, hawana madawa mahospitalini. Mbaya sana viongozi tukisha wachagua wanaenda kuukaa kwenye nyumba zilizoandaliwa kwa ajili yao ambapo umeme haukatiki, maji hayakati barabara zipo saafi na mazingira yanayovutia. Viongozi hawa hawawezi kamwe kujua wananchi wao wanaishije ishije kwa sababu hawapo tena pamoja nao.
Pia matumizi makubwa yanayofanywa na serikali ni kwa sababu haijui hiyo pesa inapatikana vipi. Ni kama mtu anaesubiri kupewa pesa tu. Matumizi yake lazma yawe mabaya kwasababu hajui watu wanavyotoili kwa ground kuzitafuta hizo pesa.
Tuendelee kuangalia tu yanayoendelea.
 
Reactions: Ame
Mbunge wetu huku kajenga madarasa mawili na kuipa shule jina lake. Watu wanamsifia kinoma yani.
Kuna mwalimu wangu anamsifia sana huko mitandaoni.
Nimemdharau sana aisee. Nikajisemea if an educated person think like this,hali ipoje kwa maelfu ya watu ambao hawajapata fursa ya kupata elimu katika nchi hii kutokana na kutowajibika kwa viongozi wetu???
Bado tuna safari ndefu sanaaa.
 
Reactions: Ame
Ama Salma Kikwete atanufaka sana...

Atakula mafao ya ustaafu wa mumewe huku akipokea mshahara na marupurupu ya ubunge. Akistaafu Ubunge anazoa mafao ya kustaafu ubunge huku akiendelea kula pensheni ya ustaafu wa mumewe...

Mbinguni kuna watu watapewa kazi ya kudeki vyoo na watakuwa wanalala stoo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…