Yajue Maisha yalivyo jela

Yajue Maisha yalivyo jela

Hakika ukifanya hivyo uta balikiwa Sana Tena kabla hauja wapelekea tembelea kwanza

Utawaona wanao hitaji msaada hata hata kwa kuwa angalia tu

waulize majina yao Kisha wapelekee mkuu uta barikiwa
Hivi inawezekana kwa mtu binafsi kwenda tu pale gerezani ukasema nahitaji kuonana na wafungwa na ukaruhusiwa???
 
Utaratibu wa kutembelea upoje?
Mimi nilienda bila kujua utaratibu
Lakin bahati nzur nilimkuta kamanda mkuu msangi mwisilam ambaye ni mkuu wa gereza kabisa butimba

Kwahiyo akanihoji maswali akanambia nimpe kibali au barua ya mwenyekiti wa mtaa nikawa sina akaniuliuza umeleta vifaa vya kidini wewe ni padre au mchungaji nikawambia hapana mimi ni muumini tu na huu ni mwezi wa rozari kwahiyo nimeletea wakristo wezangu rozari wasali
Jamaa nikazidi kumchanganya zaid ikabidi amuite kamanda ambaye anahusika na dini ya kikristo akaja dada mmoja kavaa kikamanda akapiga salute kubwa sana mbele ya kamanda msangi

Kamanda msangi akamuuliza unavijua hivi vitu yule dada afande akafufuhi sana akasema wewe kijana umefanya vizur sana wafungwa hawana rozari humu ndan ohoo umeleta na vitabu vya sala ubalikiwe sana kaka

Akaanza kumuuleza yule kamanda hivi ni vitabu vya novena tegemea wafungwa wataanza kuachiwa mmoja baada ya mwingine na hizi ni rozari ambazo nyie waislam mnaita tasibih

Kwa kifupi hata wao hawapendi kabisa mtu kufungwa na walifurahi sana hata huyo kamanda msangi akabaki mdomo wazi maana hajawahi ona mtu kupeleka rozari sasa imekuwaje

Kwa kifupi walipenda na walifurahi sana hata makamanda wengine walinipongeza sana

Kidogo tu nipate mchumba kamanda dada mmoja hivi mzuri sana

Kwahiyo utaratibu wao nenda kwa mwenyekiti wa mtaa akuandikie barua na muhuri uolozeshe vifaa unavyopeleka

Asanten
 
Amini mkuu,mfungwa akiwa kwenye kazi za nje kukutana na raia wa kawaida ni kitu simple na mara nyingi huwa hawana cha kukuomba zaidi ya kama hivyo hela au kama unakula kitu umpe etc.

August nilihudhuria msiba kijijini kwetu nikawakuta wanafanya tree pruning kwenye hospital moja ya serikali mmoja akanigongea kitu kidogo nikammwachia buku aliniona mtu sana,jamaa ni wa kusaidiwa kwa chochote kama mtu ukipata wasaa wa kufanya hivyo.
 
Kwanini mashirika yanayotoa misaada ya kisheria yasiende kuwasaisldia hao waliosingiziwa? Waliokaa mahabusu miaka mitano anaona Bora ningefanya hayo ninayotuhumiwa niwe hapa kihalali. Kuna mashirika, mpk mawakili wa serikali, na legal aids mbalimbali ikiwemo na ya Mhe Rais hebu wawe wakiwakumbuka na hao kama Kijana aliyeokota risasi
Hakuna wa kufanya hivyo nchi hii cha kufanya ni wewe kwa nafasi yako kuwasisitiza nduguzo na yeyote mtaani kwako kukaa mbali na kiumbe kinachoitwa polisi.

Hata akiona tukio limetokea sijui mtu katupa bunduki machakani akakimbia na yeye akimbie hivyo hivyo tena kumzidi mwenye bunduki yake askari bongo hawasaidiki akijipendekeza ushahidi watampoteza maisha.
 
Tuombeane jela sio kabisa....haswa ukiwa kesi haina dhamana....mbaya mnoooo....kuna jamaa Bank moja alizingua pesa za ATM tangu 2008 hafi leo yuko ndani.....sijui ile kesi itaisha lini...amesota sana mali zoote kwisha skitoka masikini wa kuanza upya
Inasikitisha sana.
 
Hakuna wa kufanya hivyo nchi hii cha kufanya ni wewe kwa nafasi yako kuwasisitiza nduguzo na yeyote mtaani kwako kukaa mbali na kiumbe kinachoitwa polisi.

Hata akiona tukio limetokea sijui mtu katupa bunduki machakani akakimbia na yeye akimbie hivyo hivyo tena kumzidi mwenye bunduki yake askari bongo hawasaidiki akijipendekeza ushahidi watampoteza maisha.
Baraka nyingi zikufikie popote pale ulipo
 
Hao viongozi wa dini wakati wa ibada hawakemei ushoga?
Wakemee ushoga wakiitwa wakiambiwa wawataje mashoga wanaowakemea na moja wapo ya sheria za wafungwa ni kum-point mtu ushoga watajibu nini?

Ni mtihani sana na nimekosa logic kwamba kwanini mfungwa asipeleke malalamiko yake kwa askari jela moja kwa moja hadi apite kwa nyapala?
 
Habari gani wakuu

Maisha changa Moto na Katika kuzitatua nikajikuta nimevuka mstari mwekundu na kujikuta nipo police station

Baada ya kushindana na wale bwana wazee wa nguo za kaki kwenye maswala ya pasu wakaapa kuni fanyia siyo

Nakumbuka mmoja wao akasema Sasa kwasababu wewe ni mtata kwenye maswala ya mpalaso

Basi Sasa movie ndiyo Lina anza.. akaendelea unalijua lile picha la commando la anord Schwarzenegger?

Nika muuliza lipi ilo?

Akaniambia lile Lina anzia polini. Jamaa ame beba gogo begani,anasogea mbele kidogo analitua chini,

Anapiga shoka la kwanza,shoka la pili, analinyenyua

Analitazama lile shoka,Kisha anamwona Jean/binti yake ndani ya shoka jeupeee

Anageuka anankumbatiwa lakini hawaja kaa sawa Kuna chopa zinaingia pale.,. Unalijua Hilo picha

Nikamjibu Hilo nalijua nipicha la kitambo sana.,,

Akacheka kicheko Cha husda na hasira Kisha akasema Sasa ndiyo linaanza..

Baada ya mda nikatinga kituoni siku mbili baadae nikatinga mahakamani baada ya kusomewa kesi na kulikana shtaka

Nawengine kufanyiwa hivyo hivyo tukaingizwa kwenye kalandinga na hatukuludishwa kituoni Tena Bari tulielekea upande mwingine

Baada ya safari ya mda wa saa moja na nusu tukashushwa mbele ya mjengo mkuubwa na wenye geti na maaskali nje
Nyuma yangu lika skika jamaa moja likiwa limepigwa pingu likasema kwa sauti oyaaa afande mudi

fungua chapu geti Nina njaa nataka nikale ugaliii""

nikamuuliza jamaa aliyekuwa amekaa upande wangu wa kulia kwani hapa wapi

jamaa akaniuliza hujawaikuja huku? nikamwambia ndiyo akaniambia hapa bwana ni jera Kama ume wai kuliskia jina la jera x ndiyo hapa"

Kisha ikaskika sauti nje ya gali/kalandinga ikisema tokeni nje na ukishuka unaluka kichula mpaka kwenye ngazi zile pale getini Ila usiingie getini.

basi kijana wa kwanza akatoka na kufuata utaratibu nawengine woote hivyo hivyo

baada ya mda kidogo tukiwa tume chuchumaa akaskika afande wa ndani ya geti akisema

ukiitwa jina unaingia unaacha ulicho nacho hapa counter Kisha una vuka geti la pili una chuchu maa

basi utaratibu ukafwatwa tukawa wote sasa tume vuka geti la pili

basi bwana tukiwa tume chuchumaa pale tukaona watu kibao kwenye kwenye cells

gafra akatokea askali jela mwingine nakusema vueni nguo wekeni hapo Kisha geukieni ukuta mkiwa mmechuchu maa"

hapo ndipo nilipo ishiwa nguvu aiseeh"

basi nikanmwona mtu wakwanza kavua mpaka woote tukamaliza naku chuchumaa tukiwa tume ugeukia ukuta

kisha Yule askali jera akaanza kuikagua nguo Hadi nguo huku akipitia kiunoni mpaka mkunjo wa mguu

nakumbuka alisema Kama hamja kabidhi vyote pale counter Basi chochote nitakacho kikuta mmekiacha kwenye nguo nichakwangu"

aliendelea ku search nguo huku akitupigisha story hii ilionyesha wazi kabisa kwamba hata yeye alijiskia aibu kwa kile alichokuwa ana fanya

baada ya kujilidhisha akatuambia Sasa Ina meni Nione vinyeo vyenu Kama hamja ficha kitu huko""

basi yule wa kwanza akaanza bila kusita kufanya hivyo.

nakibaya zaidi kulikuwa na wazee Kama watatu watu wazima nawao wali fanya hivyo kiukweli lilikuwa Jambo baya Sana na lakuaibisha sana na lisilo sahaulika

baada ya hapo tuka vaa nguo na kuongozwa kwenye mess/sehemu ya chakula

hapo akaitwa mpishi aka tupakulia maharage ambayo yalionekana haya kuungwa Wala kuchambuliwa

Pamoja na ugari/dona chakula hicho kilikuwa kime pakuliwa kwenye bakuri za aluminium zilizo bondeka,bondeka na kutoboka

kwahiyo wakati mwingine zilimwaga mchuzi wa maharage

baada ya kupewa chakula hicho nilkata Yonge la ugali nilipo lisogeza karibu na mdomo nikaskia harufu ya mafuta ya taa japo skujua inatokea wapi

kati ya maharage au ugari?

Nilipo ona wengine/wenzangu wanaendelea kufakamia chakula hicho nami Nika amua kufanya hivyo
Lakini nilipo kata tonge la pili na kulinusa ndipo Nika gundua kwamba ule ugari/unga

ume changanywa na mafuta ya taa sjui kwa Nini ? Nikaona ntajua tu mda ukifika

baada ya chakula Kuna jamaa kilimshinda kabisa kile chakula.

lakini aliskika mfungwa mmoja akisema utazoea tu na utakula chakula hicho vizuli tu hata sisi tulikuwa Kama wewe

basi kwasababu tulikuwa tume fika mda ambao wafungwa walikuwa wameingia ndani/cells

afande magerez pale akawaita nyampala waote nje na kuanza kutu kabidhi kwao

Nyampara wao ndiyo walio amua kwamba huyu atakaa cell frani na huyu cell frani

baada ya hapo Mimi nilichaguliwa cell no 1 lakini cell yenyewe nikama bweni au darasa/godown

nilipo fika kwenye ule mlango wa cell Ile na kutazama ndani sikuamini na ilikuwa Kama naota...

itaendelea wakuu...
Mkuu je kuna matukio yoyote ya kikatili wafungwa hufanyiana?

Na vipi kuhusu nyembe za kunyolea huwa hazitumiki kama silaha?
 
Hakuna wa kufanya hivyo nchi hii cha kufanya ni wewe kwa nafasi yako kuwasisitiza nduguzo na yeyote mtaani kwako kukaa mbali na kiumbe kinachoitwa polisi.

Hata akiona tukio limetokea sijui mtu katupa bunduki machakani akakimbia na yeye akimbie hivyo hivyo tena kumzidi mwenye bunduki yake askari bongo hawasaidiki akijipendekeza ushahidi watampoteza maisha.
Wasiishie kuongea Kwenye matiivii tunatoa misaada ya kisheria na siku ya sheria kutoa msaada Kwa wananchi walio huru mitaani badala kuanzia na ndugu wanaoozea huko Kwa kesi za kusingiziwa.
 
Back
Top Bottom