Yajue mambo mazuri ya wakurya ambayo ulikuwa huyafahamu

Duh uu ni uongo wa karne
 
Mghaka oghambele bhuya mbane.
 
wakurya bana hawaeleweki au labda wanajielewa zaidi wao wenyewe maana mnaweza kuwa mnapiga stori za kawaida tu tena katika hali ya utulivu kabisa mara ghafla hali ikabadilika kabisa ukashangaa watu wazima wanatupiana migumi ya maana kabisa au hata kupigana visu vya hatari yani ukikaa kizembe unaondoka iviivi. kuna wakati unaweza kuhisi jamaa ni kama bado wapo zama za mawe ivi😆
 
1. Mkurya akiwa rafiki yako ni rafiki wa kweli. Mnachanjana damu. 2. Mwanamke wa Kikurya kama hakubahatika kuzaa basi mila inamruhusu kuoa msichana kwa mali yake na kumchagulia mwanamme atakayemzalisha huyu msichana aliyeolewa naye. Watoto wote watakaozaliwa wanakuwa watoto wa yule mama aliyoa na majina yote yataitwa kwa ukoo wake. 3. Mkurya ni mtu wa ahadi ya kweli. Mfano mkikibaliana utamsaidia kwenye kesi yake na kukubaliana kitu fulani na akakupa basi tekeleza ahadi mliyokubaliana vinginevyo yatakayokutokea usimlaumu. 4. Mkurya wakati wa uchaguzi hapendi rushwa kuwa akuchague. Akikupenda anakuchagua bila rushwa. Ndiyo mara nyingi majimbo ya Tarime muda mrefu yamekuwa na Wabunge wapinzani. 5. Vijana wa Kikurya ni wajasiri sana. Wale wanaotahiriwa hawaendi kutahiriwa mahospitalini. Unapigwa kisu umesimama bila kupepesa macho na bila kupiga yowe. Ukitahiriwa hospitalini vijana wenzako (rika) watakudharau sana.
 
Kama walikuwa wanafanya "Mazoezi" ulitakiwa kuwakemea kuwa zoezi lao lilikuwa hatarishi sio kulalamika humu JF😅
 
🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Nikuongezee kidogo. Binti wa kikurya akifiwa na mume huwa ndoa yake "haifi". Kimila anachagua/anachaguliwa mwanaukoo wa kuisimamia nyumba yake na kuwajali yatima waliobaki. Huyu mjane halazimishwi kujamiana na huyo mwangalizi, ila anaendelea kujulikana kama ni mke wa marehemu fulani. Mara nyingi huyu mjane huwa yuko huria na maisha yake. Ukijichanga kutembea nae pengine kuzaa nae, huwa hao watoto wote wanachukua nasaba ya marehemu mume wake. Kama wale wenzao walioachwa na marehemu mume. Wewe uliyezaa nae kimchepuko unachulikuliwa kama dume lililopanda mitamba ya wengine kukidhi haja ya ngono kwa hiyo hao watoto hawarithi chochote chako na wala wewe hurithi chochote chao labda wakupe wenyewe ukiwa hai. Kiufupi Wakurya hawawezi kukuachia uvune/ujenge nasaba kutokana na uzinzi wako. Labda urejeshe mahari aliyotoa marehemu ili uozeshwe rasmi. Kwa sababu hii ni familia nyingi sana za jamii za Kikurya utasikia hawa wote ni kina "Wambura" lakini ni wao tuu ndio wanajua kiundani baba asilia wa fulani wao ni yulee (yule mpita njia) Hii ni tofauti sana na makabila mengi. Kuna makabila humu Bongo utakuta jamaa kazaa kijibinti kiharamu bila hata kumuoa mama mtu kisha kaingia mitini, halafu hiki kitoto kikija kukomaa eti kwenye harusi jamaa aliyekizaa anatafutwa kuja kukaa high table. Kama mama mtu aliolewa kirasmi na mkuria na yeye ndie alilea huyo binti kindly kaa mbali, unaweza kuibukia ICU ya jirani😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…