Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Magufuli the best president haitatokea tupate rais mzuri kama magufuli mungu amlinde
 
JF bana yani hotuba yote ya rais wameona wa quote ka kipisi tu cha hotuba nzima

Rais Magufuli: Kwa CAG mpya nakutakia kazi njema. Usiende huko ukajifanya Muhimili. Mihimili ni mitatu tu na umeiona hapa Mahakama, Bunge na Sisi wa Serikali

Katika Kiapo chako ni Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, kwa hiyo mwenye Serikali yupo


nikisemaga JF imekaa kichochezi chochezi kuna watu watabisha....
 
Kwahiyo Assad naye alikuwa fisadi?

Alafu mbona dingi anaongea kibabe sana
Rais Magufuli ampa maagizo haya CAG mpya.

''Ukipewa maagizo kutoka kwenye mihimili fanya''

''Wewe ni mtumishi kama wengine''

''Pale ofisi za CAG ni pachafu sana, kapasafishe''

''Una elimu nzuri una Division one O Level na A Level, wewe sio kilaza ni kipanga''

''Una nidhamu sana nilivyokushusha ulikubali kwa moyo mweupe''

''Nakuonya, unaweza ukakaa hata mwaka mmoja na sio lazima ukae hadi 60 yrs''

''Nina mamlaka ya kuteua na kutengua, mimi ndiyo Rais''

''Assad leo saa sita usiku anamaliza muda wake, kesho nenda ofisini''

''Kaisafishe ile ofisi, Wizara ya Fedha itakupa taarifa zingine''


State agent
 
Kukisia watu wanaotoka kabila fulani ni wezi mafisadi,matepeli,au hawasitahili uwongozi ,tungeachana na hisia za aina hizo.Hakuna mtu anayezaliwa akiwa ana mapungufu hayo.Vile vile hakuna kabila fulani ndio wanaostahili kutawala wengine kila mtanzania ana haki hiyo hili mradi anatimiza vigezo vya uongozi
 
Kicheere anaenda kukagua madudu yake TRA.

Wakati akitumbuliwa TRA tuliambiwa ali 'under perform'.

Sasa hivi kapewa kazi ya kukagua taasisi ambayo mwaka wa fedha uliopita yeye ndie alikuwa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.

Siye Team TANROAD tunamtakia kila la kheri.
Polisi anajifanyia upelelezi na uchunguzi dhidi ya kesi

Hapo TRA namshauri awe MUHIMILI mwingine.
 
Kwa sababu Serikali zetu kote duniani zinaongozwa Na binadamu ambao kiasili ni dhaifu,(Kwa sisi wakatoliki wakati wa Kwaresma huwa tunafundishwa kuwa Yesu alianguka Mara tatu msalabani, hiyo ni ishara kuwa katika ubinadamu wetu tu dhaifu na tunaweza anguka dhambini),tukakubaliana tuwe na Vyombo,sheria,kanuni Na taratibu za kuhakikisha katika ubinadamu watu tutasimamiwa na kudhibitiwa .

Katika udhaifu wetu huu uwezekano wa kwenda kinyume ni mkubwa kwani sisi ni binadam na ni dhaifu,tukakubaliana iwepo taasisi huru ambayo Kazi yake ni kukagua na kudhibiti utendaji kazi wetu hasa matumizi ya umma.

Uongozi bora ni pamoja kujenga taasisi huru ambazo zitakagua na kudhibiti hesabu za Serikali na namna pekee ya kuuthibitisha ubinadamu wako ni kukubali kuwa tupo dhaifu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mbali na udhaifu wa kibinadamu unapokuwa Kiongozi utazungukwa na Presha nyingi kama familia,rafiki,Ndugu,jamaa ambao wanaweza sababisha ukashindwa kutimiza wajibu wako vizuri,hivyo lazima kuwe na vyombo huru vitakavyokusimamia katika Kazi zako ili usianguke na umalize salama.
 
Huyu jamaa kuna vitu anaongea unabaki unashangaa... Hivi anaficha nini hasa??
 
I quote, "
Rais Magufuli: Nakumbuka Jaji, aliyekuwa kwenye Fair Competation (si ni wewe?), huyu wakati akifanya kazi alishaamuliwa kufukuzwa kwasababu alisimamia haki - Walikuwa wanamshangaa kuona Mchaga asiyependa rushwa. Kwasababu pale kwenye Fair Competation kuna kazi"

Kumbe kwenye rushwa vipo vi-factors vya ukabila pia? Punguza hawa kabila lile na unapunguza rushwa! Ona sasa, WAPENDA rushwa walishaamua kumtimua. Hakuna hiyo!!!
Kwa hiyo: rushwa na ukabila wapi na wapi. Judge not a book by the cover.
 
Back
Top Bottom