JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Serikali iweke wazi korona ipo,watu wajikinge,tunajua Ukimwi upo,na Serikali inatoa pesa za ARV,Polio ipo na Serikali inasisitiza watoto kupewa chanjo,Kansa ya shingo ya uzazi ipo,na Serikali inasisitiza watoto wakike wapate chanjo,Muulize Mnyika alitaka Magufuli amfanyie nini ambacho kimefanyika kwingineko kilichoondoa corona?
Yani anataka Magufuli afanye nini ili watu wasife?
Inapokuja Swala la corona,serikali inataka tupige dua na maombi!unafiki kiasi gani!?
Viongozi waaandamizi wanashambulia watu waliovaa barakoa,na Serikali inakaa kimya,?
Hizi story kwamba Mungu anaipenda TZ kuriko anavyoipenda SA,UK,USA,ni upuuzi mtupu,sisi ni maskini wakutupwa ukijiringanisha na hizo nchi za magharibi,hayo mapenzi ya Mungu kwanini hakuyaonyesha wakati wa majanga ya ebora,Ukimwi,ukame,vita,utumwa,ukoloni!
Huyu Mungu ametupenda leo wakati wa corona????
Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app