Salaam Wakuu,
Leo tarehe 24/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
Kujua kesi ilipoishia soma: Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022
UPDATES
- Jaji ameingia Mahakamani
- Kesi inatajwa
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili Wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na wakili
- Pius Hilla
- Abdallah Chavula
- Jenitreza Kitali
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Tulimanywa Majige
- Ignasi Mwinuka
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
- Nashon Nkungu
- John Mallya
- Dickson Matata
- Maria Mushi
- Khadija Aron
- Seleman Matauka
- Idd Msawanga
- Michael Lugina
- Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja Wakili Peter
Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea.
Jaji: Anakuwa Shahidi namba Ngapi?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Anakuwa Shahidi namba 12 Shahidi anakwenda kuitwa Shahidi anaingia Mahakamani, Mrefu Mwembamba, Mweupe Kidogo
Jaji: Majina yako
Shahidi: Naitwa Luteni Denis Urio
Jaji: Umri
Shahidi: Miaka 42
Jaji: Kabila
Shahidi: Mchaga
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkristo
Jaji: Kazi yako
Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi Tanzania.
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama, kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu, Mungu Nisaidie Wakili wa Serikali.
Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili Abdallah Chavula
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anqsimama na Kwenda Kwa Shahidi
Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuwa nakuuliza Maswali, Ukijibu utakuwa unamjibu Mheshimiwa Jaji, Naomba Uongee kwa Sauti Ya Juu
Shahidi: Sawa
Wakili wa Serikali: Tukumbushe Majina yako
Shahidi: Naitwa Luteni Denis Leo Urio
Wakili wa Serikali: Mkazi wa Wapi?
Shahidi: Mkazi wa Ngerengere Morogoro
Wakili wa Serikali: Unafanya Shughuli gani
Shahidi: Ni Mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi ni wapi
Shahidi: Ni Ngerengere Morogoro
Wakili wa Serikali: Kituo Chako Kinafahamika kwa Jina gani?
Shahidi: 92 KJ Ngerengere
Wakili wa Serikali: Cheo Chako ni Kipi
Shahidi: Luteni wa Jeshi
Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni Yapi
Shahidi: Ni Platoon Commander Kuongoza Askari Walio Chini yangu
Wakili wa Serikali: Unaongoza Askari Wangapi
Shahidi: Afisa Mmoja na Askari 30
Wakili wa Serikali: Ni Askari gani wanayofanya kazi Katika Kikosi cha KJ 92
Shahidi: Ni Wanajeshi Waliopata Mafunzo Maalum, Komando
Wakili wa Serikali: tuambie Wewe Umetumikia Jeshi Kwa Miaka Mingapi
Shahidi: Miaka 18
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania Mwaka gani
Shahidi: Tarehe 16,June 2003
Wakili wa Serikali: Jeshi la Wananchi Tanzania lina Majukumu yepi
Shahidi: Lina Majukumu ya Ulinzi wa Mipaka dhidi ya Uvamizi Wa Ndani na Nje
Wakili wa Serikali: Jukumu lingine ni lipi
Shahidi: Kwenye Operation ya Ulinzi Wa Amani Kwenye Mataifa yenye Mgogoro
Wakili wa Serikali: Umesema Wewe ni Luteni wa Jeshi, Je Umekuwa Kwenye Nafasi hiyo kwa Miaka Mingapi
Shahidi: Kwa Miaka 6
Wakili wa Serikali: Umeeleza Mahakama Kwamba Miongoni Mwa Majukumu ya Jeshi ni Kuleta Amani Kwenye Mataifa Mengine, Ushiriki wako ni Vipi
Shahidi: Nimeshirriki Kulinda Amani 2011 Nchini Sudani, Na 2019 ni Sudan hiyo hiyo Jimbo la Darfur
Wakili wa Serikali: Tueleze Mahakama Kule Darfur ulipo enda Majukumu yako yalikuwa yepi
Shahidi: Kuhakikisha Wale Staff Officer (Wapatanishi) Ku Ensure Usalama wao Kwa Sababu Wao ni Unarmed Personnel
Wakili wa Serikali: Kuna Mtu anafahamika Kwa Jina la Khalfani Bwire Unamfahamu Vipi
Shahidi: Nina Mfahamu Kwa Muda Mrefu, Nili Mtrain, Nikifanya naye Kazi Kituo Kimoja cha 92 KJ
Wakili wa Serikali: Umemfahamu Kuanzia Mwaka gani
Shahidi: Kuanzia 2006 Mpaka 2009
Wakili wa Serikali: Wakati Unamfahamu, yeye alikuwa ana Jukumu gani
Shahidi: alikuwa Kiongozi Mdogo, anaongoza,Ni Section Commander, alikuwa anaongoza Watu 9
Wakili wa Serikali: Cheo Chake Kilikuwa ni Kipi
Shahidi: Rank ya koplo
Wakili wa Serikali: Unaposema Ulifahamiana naye kuanzia 2006 Mpaka 2009 umamaam gani
Shahidi: Ukomo wake Ulikuwa Mwaka 2019
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mpaka I kafika Ukomo wake
Shahidi: alifukuzwa Kazi Jeshini
Wakili wa Serikali: Kwa sababu Zipi afukuzwe Kazi
Shahidi: Kwa Utovu wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Wakati Mwaka 2019 anafukuzwa + kazi Wewe Ulikuwa wapi
Shahidi: Kwenye Operation Ya Peace Keeping, Sudan Jimbo la Darfur
Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kazi kwa Utovu wa Nidhamu
Shahidi: Ni 2020 Mwezi March Baada ya Kutoka Darfur
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ni Mazingira Yapi Ulifahamu Kwa Yeye Kufukuzwa Kazi Jeshini
Shahidi: Nilipata Taarifa hizo kutoka Kwa Administration Officer of the Unit
Wakili wa Serikali: Administration Officer ndiyo nani?
Shahidi: Mtu anaye fuatilia Maisha ya Askari Wote Kikosini na Maafisa ya Jeshi, Pia ni Kiongozi
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu na Khalfani Bwire tangu 2006 Mpaka 2019 yalikuwaje
Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri tu, Ya Kiongozi na afisa wake.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu baada ya Ajira Kukoma yalikuwaje
Shahidi: Bado nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye, Mawasiliano ya Kawaida tu
Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu anaitwa Adam Hassan Kasekwa ama Jina Lingine anaitwa Adamoo.
Shahidi: Nafahamiana naye toka Mwaka 2012 ndipo alipofika Kwenye Unit ya 92KJ alifika Kwenye Mafunzo, Nikam' train, aka' pass Maana nilimpokea Mimi.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama, Huyu Adam Kasekwa ama Adamoo alifanya kazi Jeshini Kwenye 92 KJ alifanya kazi Mpaka Lini
Shahidi: Mpaka Mwaka 2018
Wakili wa Serikali: Nini Kilimsibu Mwaka huo 2018
Shahidi: Alifukuzwa Kazi Jeshini.
Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Kazi Jeshini Kwa Sababu zipi
Shahidi: Kwa Utovu Wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Mpaka anafukuzwa Kazi Jeshini Kwa Utovu, Je alikuwa na Cheo gani
Shahidi: alikuwa Private Soldier.
Wakili wa Serikali: Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini
Shahidi: Ni Askari ambaye hana Rank inayo kuwa Displayed, Ni Askari anayekuwa Chini ya Kiongozi Wake
Wakili wa Serikali: Wakati Adam Kasekwa anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa upo wapi
Shahidi: Nilikuwa Nipo Arusha.
Wakili wa Serikali: Ni wakati Gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Adam Kasekwa kafukuzwa Kazi Jeshini
Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi Kutoka Arusha Kwenye Kozi
Wakili wa Serikali: Taarifa za Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu Wewe Ulizipata Wapi?
Shahidi: Administration Officer
Wakili wa Serikali: alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira gani
Shahidi: Ofisini Kwake
Wakili wa Serikali: Mazingira ya Mahusiano Baina ya Wewe na Adam Kasekwa yalikuwa Je Kipindi Kile Kabla ajafukuzwa Jeshi.
Shahidi: Yalikuwa Mazuri tu
Wakili wa Serikali: VIpi Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi na Kuondoka Jeshini yalikuwaje
S
hahidi: Yalikuwa Mazuri
Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu Naitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya Unamfahamu Vipi
Shahidi: Namfahamu Nilifanya naye Kazi Kituo Kimoja
Wakili wa Serikali: Kituo Gani hicho
Shahidi: 92 KJ
Wakili wa Serikali: umeanza Kufanya naye Kazi huyo Mohammed Ling'wenya kuanzia Mwaka gani Mpka Mwaka gani
Shahidi: Kuanzia Mwaka 2010 Mpaka Mwaka 2017
Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mwaka 2017
Shahidi: alifukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mpaka anafukuzwa Kazi, alikuwa ana Cheo gani Katika Jeshi
Shahidi: Alikuwa ni Private Soldier
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini
Shahidi: Ni Askari Mwenye Cheo Cha Mwisho chini
Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Mahusiano yenu
Shahidi: Tulikuwa na Mahusiano Mazuri
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu, Mahusiano yenu yalikuwaje
Shahidi: Yaliendelea Kuwa Kama alipokuwa Kazini
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati Mohammed Ling'wenya anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa Wapi
Shahidi: Nilikuwa Kwenye Kazi Maalum
Wakili wa Serikali: Ni Wakati Gani Ulikuja Kupata Ufahamu, kuwa Mohammed Ling'wenya amefukuzwa kazi
Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi, kutoka kwa Administration Officer
Wakili wa Serikali: Huyo Administration Officer alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira Yepi
Shahidi: Tukiwa Ofisini
Wakili wa Serikali: Unasema Unamfahamu Khalfani Bwire Je akiwa Miongoni Mwetu unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakufanya Umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 10, lakini pia Body Morphology
Wakili wa Serikali: Mtu huyo Yupo wapi
Shahidi: aliyepo Mbele yangu, Tunatizamana, Yupo Jirani na Magereza
Wakili wa Serikali: Pia Umemtaja Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo, Je Unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Ni sababu Zipi hasa zitafanya Umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5 lakini pia na Body Morphology Yake
Wakili wa Serikali: Hebu tuonyeshe Mtu huyo Yupo wapi
Shahidi: Ni Wapili Kutoka Kulia Mwa Khalfani Bwire
Wakili wa Serikali: tuambie Mwingine unaye Msema ni Mohammed Abdilah Ling'wenya, na Yeye Vipi Unaweza Kumtambua
Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua
Wakili wa Serikali: Sababu Ipi Itakufanya umtambue
Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5, pia Body Morphology yake, Tatu ana Makovu Usoni na Mkononi.
Wakili wa Serikali: Hapa Yupo wapi
Shahidi: Ni watatu Kutoka Upande Wa Kulia wa Bwire
Wakili wa Serikali: Shahidi isaidie Mahakama, Unasema Adam Kasekwa Na Mohamed Ling'wenya Walikuwa ni Private Soldier, Je pale Jeshini Walikuwa na Majukumu Yapi
Shahidi: Wao Ni watendaji wa Shughuli za Kijeshi
Wakili wa Serikali: Huyu Khalfani Hassan Bwire, Adam Hassan Kasekwa, Mohammed Abdilah Ling'wenya wakati wa Utumishi wao Wa Jeshi Pale 92 KJ Makazi yao yalikuwa wapi?
Shahidi: Walikuwa Wa naishi huko, Khalfani Bwire Ngerengere, Adam Kasekwa alikuwa Anaishi Chalinze katika Utaratibu Wa Misbehave
Wakili wa Serikali: Hapana Usiende Huko
Shahidi: Na Mohamed Ling'wenya na Yeye Chalinze
Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Mwaka 2011 ulikuwa Darfur, Je katika Wenye Cheo Cha Private Soldier nani Uliyekuwa naye
Shahidi: Sikumbuki
Wakili wa Serikali: Unaposema Ukumbuki unamaanisha nini
Shahidi: Sina Kumbukumbu Ka Nilikuwa na Mmoja wapo.
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama pale Darfur Ulipokuwa Unaishi Kwenye ile Nyumba yako Ulikuwa Unaishi na Nani
Shahidi: Tulikuwa tunaishi Viongozi Watupu
Wakili wa Serikali: Na Mwaka 2012 pale Darfur Pia Mwenye Cheo Cha Private, nani ulikuwa naye
Shahidi: Sikumbuki.
Wakili wa Serikali: Mtu anaitwa Freeman Mbowe Wewe Unahusiana naye Vipi
Shahidi: Tulifahamiana naye Mwaka 2008 Mpaka 2020
Wakili wa Serikali: Unaweza Kusema ni Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kufahamiana.
Shahidi: Mwaka 2008 Freeman Mbowe anilipigia Simu akaniita Kwa Majina yangu
Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi
Shahidi: Siwezi Kukumbuka hiyo Tarehe
Wakili wa Serikali: Shahidi Irejee Mahakama tena, Unasema alikupigia Simu lini
Shahidi: Mwaka 2008
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi na Mwezi gani
Shahidi: Sikumbuki Tarehe Wala Mwezi
Wakili wa Serikali: alikupigia Simu, wewe si yako ilikuwa ya Namba gani
Shahidi: ilikuwa 0754612518
Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka na Yeye namba yake iliyokupogoa ilikuwa namba gani
Shahidi: Ilikuwa Mtandao Wa Airtel, ila namba Sikumbuki
Wakili wa Serikali: alikueleza nini
Shahidi: alipiga Simu akauliza Wewe ni Denis Urio, Nikamwambia Yes ndiyo Mimi, akasema ni Askari wa Jeshi la Wananchi, Nikamwambia Ndiyo, akajitambulisha, Kwa Sababu Namfahamu Nikamuamkia.
Wakili wa Serikali: Kwa Sababu Unamfahamu Ukamuamkia, Ulikuwa Unamfahamu Vipi
Shahidi: Alikuwa anaonekana Kwenye Vyombo Vya Habari, Haikuwa Jina geni, I Amana anafahamika
Wakili wa Serikali: Baada ya wewe Kumpa Salamu nini Ulifanya
Shahidi: alikuwa ana confirm Profile Yangu.
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini
Shahidi: alikuwa nauliza wewe si Denis Urio Nikasema Ndiyo, ni Mtu wa Kilimanjaro basi Mimi Ndugu yako, Ndipo Uhusiano Ulianza
Wakili wa Serikali: Hebu Iambie Mahakama Namba yako ya Simu alitoa Wapi
Shahidi: Sifahamu alipoitoa.
Wakili wa Serikali: Yeye alikueleza, Ni wapi ametoa Namba yako
Shahidi: aliniambia Kuwa Mbona Unafahamu, Kwa Mtu Kupata Namba ya Simu Siyo Tatizo, Usiwe na Wasiwasi
Wakili wa Serikali: Ni Kitu gani kilipelekea Mpaka Yeye Kusema Kuwa Mbona Unafahamika Sana.
Shahidi: Ni pale Nilipo taka Kujua amepata wapi Namba Yangu
Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hayo Maneno ni Wakati gani alikutamkia
Shahidi: Mara ile ya Kwanza Kuwasiliana, Nikiwa natumia Mtandao Wa Voda yeye akitumia Mtandao Wa Airtel.
Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Baada ya Siku hiyo kuwasiliana Mawasiliano yenu yalikuwaje
Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana, Iwe Kwa Kunisalimia alikuwa ananitumia Ujumbe wa Kuni wish hata Kama Kuna Sikukuu au Event Yoyote
Wakili wa Serikali: Mlimkuta ana kwa ana Lini
Shahidi: Tukikutana Ana Kwa Ana Mwaka 2012
Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Mwaka huo 2012 Ilikuwa ni Tarehe Ngapi na Mwezi Gani
Shahidi: Siwezi Kukumbuka Tarehe Wala Mwezi
Wakili wa Serikali: Shahidi nikirudishe Nyuma, Umeeleza Awali Kwamba 2011 ulikuwa Darfur Nchi Sudan, Je Ulirejea Nchi Mwaka Gani
Shahidi: Nili rejea Mwaka 2011 Mwezi wa 10
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe Ngapi
Shahidi: Siwezi Kukumbuka Siku wala Tarehe.
Wakili wa Serikali: Ni Mazingira Yepi Yalipelekea Ninyi Mwaka 2012 Kukutana
Shahidi: Mwaka 2012 nikiwa Maeneo Ya Mgulani (Saba Saba) Nilipokea Simu ya Mheshimiwa Mbowe Kama Ilivyo Kawaida yake akaniambia Upo wapi, Nikamwambia Nipo Maeneo Ya Mgulani (sabasaba).
Wakili wa Serikali: alikueleza nini
Shahidi: Alini uliza nipo Wapi, Nikamuelekeza Location nilipo
Wakili wa Serikali: Location Maana yake ni nini
Shahidi: Eneo nilipo
Wakili wa Serikali: Endelea
Shahidi: aliniambia Kuwa Kuna Kitu anataka Tuongee, Je tunaweza Kuonana? Nikamuuliza Wewe Upo wapi akasema Yupo Mikocheni Cassa Motel
Jaji: Unaweza Kutaja Spelling zake
Shahidi: CASA Sikumbuki Vizuri
Wakili wa Serikali: Wewe Ukamwambia Nini
Shahidi: Sijui Mikocheni Vizuri, Wala Mahala Ilipo
Wakili wa Serikali: Ulifanya Nini sasa
Shahidi: Baada ya kumwambia Siyo Mwenyeji aliambiwa niende Kituo Cha Tax Ni Mwambie Dereva Yoyote yule anipeleke CASA Motel
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupewa hayo Maelekezo, Maamuzi yako yalikuwa ni nini
Shahidi: Nilienda Kwa Dereva Tax, Nikamwambia Anipeleke CASA Motel, nikaweza Kufika CASA Motel
Wakili wa Serikali: Hicho Kituo Cha Tax Ulicho enda Kutafuta Tax ni Kituo Cha Wapi
Shahidi: Ni Saba Saba Mbele Kidogo Kama Unaenda Kwa Aziz Ally Wilaya Ya Temeke.
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Hiyo Safari yako ya CASA hotel Ilikuwaje
Shahidi: Nili weza Kufika, Nikampigia Simu akapokea, akauliza nimefika Wapi, Nikamwambia Nimeshafika
Wakili wa Serikali: Taratibu Jaji anaandika..
Wakili wa Serikali: endeleaaaa
Shahidi: akanielkeza Pale CASA Motel Kuna Vitu Kama Vimepangwa Kuna watu walikuwa wamekaa Mbali Mbali Ka Wanne hivi, Baada ya Kufika akaniuliza huyu anadai TSh ngapi Nikamwambia TSh 20
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumwambia Ikawaje
Shahidi: Alilipa hiyo Tsh 20.
Wakili wa Serikali: Wakati yoye Haya Unayosema Kuanzia Kupigana Simu Mpaka Unafika CASA Hotel Ilikuwa ni Majira yapi
Shahidi: Ilikuwa Kuanzia Saa Saba Mchana Mpaka Alasiri
Wakili wa Serikali: Pale Mlipoliwa Mmekaa na Kukutana naye, Mwingine nani Mliye kuwa Mmekaa naye
Shahidi: Hapakuwa na Mtu Mwingine zaidi yangu Mimi na Yeye
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa, Nini Mlichozungumza Wakati Mmekutana
Shahidi: Mambo Makubwa matatu, Kutaka Kujua Mimi ni Nani, nafanya kazi gani, Nina Cheo gani?
Wakili wa Serikali: Kwenye Hayo Madodoso wewe Ulimjibu nini
Shahidi: Mimi ni +Rank gami Majibu niliyompa, Nilimwambia Mimi Sina Rank
Wakili wa Serikali: Ulipomueleza Wewe huna Rank Ulikuwa Unamanisha Nini
Shahidi: Nilimwambia Mimi Sina Cheo Chochote.
Wakili wa Serikali: Kwanini Ulimueleza hayo
Shahidi: Kwa sababu aliniuliza Swali
Wakili wa Serikali: Lingine lipi ulilomjibu
Shahidi: Nilimjibu nafanya kazi Mkoani Morogoro, na Nyumbani ni wapi nilimwambia Mimi Nyumbani ni Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Vijijini.
Wakili wa Serikali: Kingine Kipi
Shahidi: Akitaka Kujua Msimamo Wangu dhidi ya Vyama Vya Upinzani
Wakili wa Serikali: Kwenye hilo la Msimamo Wako Majibu yako Yalikuwa ni Yepi
Shahidi: Nilimwambia Kwa Mujibu wa Kazi yangu Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote.
Wakili wa serikali: ukamueleza nini?
Shahidi: Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote, Ila Kwa Kiongozi aliyepo Madarakani
Wakili wa Serikali: Lingine lipi mililozungumza
Shahidi: Alini uliza Juu ya Makampuni ambayo yangeweza Kufunga Mfumo Wa Mawasiliano Kwenye Ofisi zao, na Kama Jeshini Kuna Makampuni yaliyofunga Mawasiliano Jeshini. Nilipo Muuliza Kwanini anataka Kufanya kazi na Makampuni Yaliyofunga Mawasiliano Jeshini, Akajibu Kuwa anataka Kufuatilia Mawasiliano ya Viongozi Wenzie Wanaotoa Siri Nje ya Chama.
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kuku uliza Juu ya Swala hilo, Majibu yako Yalikuwa ni nini
Shahidi: Nilimshauri aende Kwenye Taasisi za Elimu ya Juu ndiyo atapata Suluhu ya Tatizo lake Wakili wa Serikali Nini Kiliendelea Sasa Baada ya Hapo.
Shahidi: Baada ya Hapo tuliachana, Akaita Tax akamlipa nikaondoka zangu
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Fedha kiasi gani aliyolipwa
Shahidi: Sijui ni fedha Kiasi gani
Wakili wa Serikali: Baada ya akiwa mmeachana, Mliachana Majira gani.
Shahidi: Majira ya Jioni kati ya Saa 9 Mpaka Saa 11 Jioni
Wakili wa Serikali: Baada ya Wewe Kuachana naye Ulieleka Wapi
Shahidi: Nilirudi Nyumbani
Wakili wa Serikali: Baada ya Kikao Chenu Mawasiliano Yalikuwaje
Shahidi: Yalikuwa Ka Kawaida, anipigia Simu, ananitumia Meseji na anani' Wish Kama ni Sikukuu
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya Mwaka 2012, Je ni wakati gani Mwingine Mlikutana ana kwa ana
Shahidi: Ilikuwa ni Mwaka 2020 Mwezi Saba Tarehe za Katikati
Wakili wa Serikali: Hebu elezea Mahakama ni. Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kukutana.
Shahidi: Ilikuwa Kwenye Tarehe 26 Mpaka 30 June Mwaka 2020, Niliacha Simu Kwenye Gari, Nipo rudi Nilikutana Missed Calls Nyingi. Missed Calls zaidi ya Tano Katika Simu
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Unaposema Missed Call zaidi ya Tano.
Shahidi: Ni simu ambazo hazikupokelewa
Wakili wa Serikali: Zilikuwa ni Namba za akina nani?
Shahidi: Hazikuwa Saved, Zilikuwa ni Namba Ngeni Katika Simu yangu
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukuta namba Ngeni na Huku pokea, Ulihisi nini
Shahidi: Nili Fikiri ni Familia Yangu, Nilipiga Mwanzo Haku pokea, Nilipiga tena akapokea akasema alikuwa anakutafuta Mwenyekiti Baadae Nilipiga Simu Nyingine, ikapokelewa akasema alikuwa anakutafuta Chairman. Basi sikupiga tena namba Nyingine
Wakili wa Serikali: Hebu elezea Mahakama ni nini Kilitokea
Shahidi: Baadae Ikipigwa Simu na namba Ngeni akasema ni Kaka Yangu wa Dodoma, Nikamwambia Mbona sina Kaka Dodoma, akasema Sikia Mimi ni Freeman Mbowe, Nikamsalimia Shikamoo Mzee.
Wakili wa Serikali: Kasema nini
Shahidi: Akaniambia Kuna Mambo ya Muhimu Sana nataka Tuongee, Nikamwambia Kuwa tunaweza Kuongea tuh kwenye Simu, akasema Ni Jambo Muhimu Sana ni Lazima tuonane, Nikamwambia Kwa sasa Sina Muda.
Wakili wa Serikali: Wakati hayo Yanatokea yalikuwa ni Majira gani
Shahidi: Yalikuwa Majira ya Saa 10 Jioni
Wakili wa Serikali: Wakati hayo Yanatokea wewe Ulikuwa wapi?
Shahidi: Nilikuwa nipo Likizo Morogoro
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kukupa Ombi lake la Kuonana, Nini Kiliendelea
Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana tu. Baada ya Hapo Nilikuja Dar es Salaam Mwezi wa Saba 2020 nilikuja kwa kazi Binafsi, nikafanya Shughuli zangu za Kijeshi, Majira ya Saa 10 nikakummbuka Nilikuwa na appointment, Nimampigia Simu yake Mara Kadhaa hazikupokelewa, Basi Nikawa naenda Station, Kupanda Magari ya Mgulani
Wakili wa Serikali: Nini kitokea
Shahidi: Wakati Nasubiri Gari Kituoni Majira ya Saa 12 alinipigia Simu Kwa namba Nyingine, akaniambia Alikuwa yupo Bussy alishindwa Kupokea simu yangu, Kaniuliza upo wapi? Nikawa Mwambia nipo Station Najiandaa Kwenda Mgulani akaniambia Homeboy hatuwezi Kuonana?
Wakili wa Serikali: Nimesikia Mara Kadhaa unatamla Homeboy, Je Tafsiri yake ni nini
Shahidi: Tafsiri yake Mimi siwezi Kujua, Ila mara Kadhaa alikuwa ananiita Homeboy.
Wakili wa Serikali: Wewe Sasa Ulimjibu nini Kuhusiana na Ombi lake
Shahidi: Alini taka kama naweza Kufika Mikocheni, Nakamwambia Kuwa Mikocheni sipajui Vizuri, naweza Kupotea Akaniambia huwezi Kupotea, akaniambia Cheki Dereva Tax au Bodaboda Karibu amuelekeze Mahali alipo. Nikampa Bodaboda Simu Pale Stand ya Station akamuelekeza, baada ya hapo nikaondoka na Bodaboda Kuelekea Mikocheni.
Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hapo Mikocheni Mlienda Hadi sehemu gani
Shahidi: Tulienda Mpaka Kwenye Mgahawa Sipafahamu, Kuna Parking ya Magari, I kabidhi nipigie simu Hakupokea, Wakati Napiga simu, akatokea Kijana Mmoja Nyuma Yangu. Akaniuliza wewe Ndiyo Denis Urio, Nikamwambia Ndiyo Mimi, akatoa Elfu 10 akamlipa Bodaboda akaniambia Mwenyekiti Yupo huku, Tukaenda kwa Nyuma kama VIP, Basi yeye akatoka Nje
Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tuambie wakati huo Unafika Pale sasa, Ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi.
Shahidi: Ilikuwa Majira ya Saa Moja Kasoro, Jua lilikuwa Leshazama lakini Bado Kuna Mwanga, Kwa hiyo Kama Saa Moja Kasoro
Wakili wa Serikali: Na Wakati una Mpigia Simu, Na Yeye akakupigia baadae, alikuwa anatumia namba gani?
Shahidi: alikuwa ana tumia namba ambayo siyo ya kwake ni Namba ambayo sihifahamu
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati wewe Umefika pale ulipokutana naye, Ulimpigia Simu Kwa namba ipi?
Shahidi: alikuwa na namba yake ya Airtel na Tigo, Nilipiga Airtel hakupokea na Nilipiga Tigo hakupokea pia
Wakili wa Serikali: Ukiondoa Pale Mlipokutana, Ni nani Mwingine alikuwa pale
Shahidi: Hapakuwa na mtu, Ni Mazingira ya starehe, Tulikuwa wawili tu Mimi na Yeye.
Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Sasa nini Kilichotokea Sasa Pale Mlipokutana
Shahidi: Nilimkuta yupo Pekee yake anakunywa Redbul anamuita Muhudumu anisikilize na mimi nikaagiza Malta
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Tuambie, Ieleze Mahakama Alikueleza au Kukwambia Kitu gani alichokuitia
Shahidi: Kitu cha Kwanza tulisalimiana Salamu za Muda Mrefu, Lakini Baada ya Salamu hizo akaniambia komredi mwaka huu wa 2020 Kuna Uchaguzi Mkuu, Hivyo Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola Kwa namna na Kwa Gharama Yoyote ile. Akaniambia Wewe si Unaona Watu wa wanyonge wa hali ya Chini wanavyoishi Maisha ya Shida Akanielekeza, komredi Tumefahamiana Muda Mrefu, Tunatoka Mkoa Mmoja, pia wewe ni Mchaga Mwenzangu, Tukichukua Dola Unafikiri Wewe Utakosa Cheo Cha Juu Jeshini?
Akaniambia hivyo Jeshini Kuna Watu Waliostaafu au Kufukuzwa Kazi ya Jeshi.. Wale ambao wamefanya Mafunzo Maalum ya Komandoo. Homeboy naomba unitafutie Vijana hao wenye Mafunzo Maalum ya Komando, ambao nitaambatana nao kwenye Harakati za Kuchukua Dola. Najua Watakuwa na Uwezo wa Kunisaidia Kufanya Nchi isitawalike, Kuleta Taharuki na Kusiwe na Amani.. Tutafanya hayo Kwa Kuzua Taharuki Mheshimiwa Freeman Mbowe Alisema yalikuwa ni Kulipua Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Moto Masoko na Mikusanyiko Mkubwa Ya watu.
Kukata Miti Mikubwa iliyoota pembezoni Mwa Barabara zote, Hasa Kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro hasa Mjinwa Moshi na Barabara Kuu ya Morogoro - Iringa, Kwa Kufanya Vitendo hivyo Vitatu Kutapelekea watu Kuwa na Taharuki na Kuandamana Nchi Nzima.
Mikoa Mingine Iliyobakia Itasapoti Mikoa hii niliyo highlight.. Point Nyingine ya Mwisho ni Kuwadhuru Viongozi Wengine Wa Serikali, Ni Viongozi ambao ni Vikwazo Kwa Vyama Vya Upinzani.. Hivyo Homeboy nisaidie Kuwapata hao watu Nina Haraka nao sana, MWISHO WA MAELEZO YAKE FREEMAN.
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama alipokueleza yeye Hayo Makusudi yake wewe Ulifanya Jambo Gani
Shahidi: Nilitafakari nikamkubalia
Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tueleze Wewe alipokueleza hayo Maneno, Ni Kipi kilikupelekea ukamkubalia
Shahidi: Kwa Experience yangu Kuna kitu kinaitwa Tactical appreciation
Wakili wa Serikali: Experience yako Kwenye Nini
Shahidi: Kwenye Ulinzi
Wakili wa Serikali: Tactical appreciation ni Kitu gani hicho
Shahidi: Kuna Binadamu, Kuna Mimi na Tanzania, lakini Mimi si kitu Kuliko Tanzania, Freeman Ni Ndugu yangu, Tayari Alishakuja na Ile Nia, Kwamba Unataka nimkatalie, lakini Mimi huenda ni Plan B au C. Je Nikimkatalia atachukua hatua gani? Je, nitakuwa ni solution matatizo yasitokee, Naweza Kumkatalia lakini kumbe ana Backup plan nitakuwa sija solve tatizo.
Wakili wa Serikali: Sasa hiyo Tactical Appreciation Uliyotumia Ulitumia Kufanya nini
Shahidi: Ikaniongoza Kwamba Nimkubalie, Kwamba Nipe Muda Nikutafute hao watu
Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Tuambie, yeye alikwambia anataka Wangapi
Shahidi: Hakuna Kikomo cha Watu, Ni wale Watakaopatikana.
Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Baada ya kukueleza Maneno yale nini Kilitokea
Shahidi: alimuita Kijana wake, Akaita Tax nikarudishwa nilipotolewa
Wakili wa Serikali: Wakati huo unamaliza na Wewe unarudi Mgulani ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi
Shahidi: Saa Mbili hadi Saa Tatu, Kwa sababu Taarifa ya Habari Ilikuwa imeshaanza
Wakili wa Serikali: Na Huyo Dereva Tax alikuwa amelipwa TSh ngapi
Shahidi: Sijui alikuwa amelipwa TSh ngapi
Wakili wa Serikali: Shahidi Umerudi Mgulani, Nini Sasa Ulichofanya au Hatua ulizo chukua Juu ya Ujumbe Uliopewa
Shahidi: Nilishindwa Kulimeza
Wakili wa Serikali: Kushindwa Kulimeza ndiyo nini
Shahidi: Nilishindwa kukaa nalo.
Wakili wa Serikali: Kwanini Ushindwe Kukaa na Taarifa Ya siri
Shahidi: Nature ya Taarifa
Wakili wa Serikali: Taarifa Ipi
Shahidi: Ya Kuleta Taharuki
Wakili wa Serikali: Baada ya Kushindwa Kueleza Ulifanya nini
Shahidi: Nilichukua Hatua Ya akimpigia DCI Afande Boazi Majura ya Saa 3 Usiku
Wakili wa Serikali: DCI ni Kitu gani?
Shahidi: Director of Criminal intelligence, Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai.
Wakili wa Serikali: ulipo Mpigia nini Kilitokea
Shahidi: Nilimpa Taarifa amilizopewa na Freeman Mbowe, Juu ya Uvunjifu wa Amani, Kwamba ameniambia nitafutie Watu wa Kukata Miti Barabarani na Kuchoma Masoko wakati naendelea Kusema hivyo akasema Subiri, Unaweza Kuja Kesho Ofisini Kwangu Asubuhi.
Wakili wa Serikali: alikwambia nini
Shahidi: Kama naweza Kufika Ofisini Kwake Kesho Asubuhi
Wakili wa Serikali: Na shahidi Unaweza Kukumbuka namba ya Simu ya Robert Boazi (DCI) Uliyompigia
Shahidi: Sijaikariri Kichwani.
Wakili wa Serikali: alikwambia Uende Ofisini Kwake wapi
Shahidi: Makao Makuu ya Polisi, Jijini Dar es Salaam Mtaa wa Ohio
Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Alikutaka Uende Ofisini Kwake Saa ngapi
Shahidi: Majira ya Asubuhi
Shahidi: Nilifika Makao Makuu ya Jeshi Polisi, nikajitambulisha Getini Kuwa Nina Appointment na Afande DCI, Nikaenda Pia nikamkuta Polisi nilajitambulisha Kuwa mimi ni Afande Mwenzao Nina appointment na Afande DCI, wakaniruhusu Nikaenda Ghorofa ya Saba
Wakili wa Serikali: Wewe Ulikuwa unapanda Juu Kuelekea Wapi
Shahidi: Nilikuwa napanda Juu Ofisi ya DCI Ghorofa Ya Saba
Wakili wa Serikali: kabla Ya Siku hiyo Kwemda Kwa DCI ni lini tena Ulienda Ofisi hiyo
Shahidi: Nilishafika Mara Mbili Mwaka 2017 na Mwaka 2014
Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Kipi kililufahamisha Ofisi za DCI zipo Ghorofa ya Saba
Shahidi: Nilishafika Awali, ila baada ya Kufika Reception Nili Confirm kwa wale askari
Wakili wa Serikali: Ulienda Vipi Ghorofa ya saba
Shahidi: Kuna Njia Mbili Kuna Lift na Kuna Ngazi, Lift ilikuwa haifanyi kazi, nikapanda ngazi.
Shahidi: Inapofika Ghorofa ya Saba Kwa Kupanda Ngazi, Pembeni yake Kuna Mlango, Nilipo Fungua Mlango Nikakuta Kuna Askari Mwanamke ambaye ni PS wake, Nikajitambulisha Kwamba Naitwa Luteni Denis Leo Urio Askari Wa Jeshi la Jeshi la Wananchi.
Wakili wa Serikali: Baada ya Kujitambulisha, Ulimwambia nini huyo PS
Shahidi: Nilimwambia Nina appointment na Afande DCI
Wakili wa Serikali: Baada Ya Kumueleza hayo
Shahidi: Palikuwa na Kochi pembeni akaniambia Nikae pale pembeni afanye Mawasiliano naye. Baada ya Kufanya Mawasiliano naye, Nikaambiwa Ingia, Nikakuta tena kuna Makochi na Kuna msaidizi Wake akasema Subiri utaitwa
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukaa hapo Nini Kiliendelea.
Shahidi: Baada ya Muda PS Wake akaja akaniambia Fungua Mlango Niingie Kwa DCI
Wakili wa Serikali: Ulikutana na Kitu gani
Shahidi: Nilimkuta Afande DCI yupo Pekee yake, Nikamsalimia, Nikajitambulisha, Nikamkumbusha
Wakili wa Serikali: Ukajitambulishaje
Shahidi: Mimi naitwa Luten Denis Urio, Miliyekupigia simu Jana Usiku
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani Sasa ni saa Saba Kasoro Dakika Nne, Na Mimi bado Nina Maswali mengi sana, Naomba Tupate Break Kidogo
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi
Jaji: Basi tunahairisha Kwa Muda Kupata Health Break, Kwa hiyo tutarudi Saa Saba na Dakika 45
- Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Jaji..
- Jaji anatoka
Jaji ametoa mapumziko ya dakika 45 itaendelea...
- Jaji ameingia Mahakamani
- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile kama awali tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia Upande wa Utetezi Quorum yetu haijabadirika Shahidi aliingia Mahakamani aliongozana Wakili Wa Serikali Ignasi Mwinuka