Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe 26 Jan 2022. Shahidi wa 12 Luteni Denis Urio kuendelea kutoa ushahidi wake

🤣🤣🤣,we jamaa Huwa unanichekesha unavyokomaa na hivyo vimisemo ila Huwa unaingia mitini mazima!
Yule shahidi wa ethical hacking ulichukua kaneno "Cellebrite" Ukaenda google ukacopy maana basi ndio ukawa unatamba nayo kwenye ule Uzi,hapo Ilikuwa kabla ya spana za kina Kibatala!
Baada ya mawakili wa utetezi ukaingia mitini na maana Yako kutoka google!
Naona Leo uko na tactical appreciation na ushacopy maana kutoka google!
Endelea kukapaste kila mahala ila usije ukaingia mitini Kibatala akisimama!
🤣🤣
comte ni kituko humu jukwaani Chief! Kituko kweli kweli.
 
What is a tactical appreciation?

The appreciation is essentially the process whereby operational information is collected and then used to produce outline plans. The references cover the appreciation as it relates to strategic, tactical, and administrative problems at formation level.
Kama kamondoo mwenye cheo Cha Luten anafanya utoto huu nchi yetu haipo salama, yaani mtu unaambiwa Jambo kubwa Kama hili la kuvuruga Amani, unaamua kucheza mchezo wa kua undercover kwenye kikundi kinachopanga kuleta vurugu, then wewe unaenda kufanya recruitment ya watu ambao wameachichwa jeshi kwa utovu wa nidhamu ili wakawe sehemu ya kundi, then kabla ya ushahidi wa kutosha kuhusu hizo habari unaenda kuwakamatisha watu ambao wewe ndo umewashawishi kujiunga. Je, alishindwa vipi kutafuta askari ambao bado ni waadilifu wakawa undercover ili wakaendelee kuufuatilia mtandao mkubwa wa Mbowe ambayo hata yeye alihisi kua anaweza kua ana backup ndio maana akaamua kumkubalia. That is nonsense! Kama kweli hizi njama zilikuwepo hafai kua Luten wa jeshi, Ila Kama game yao unaendelea kuchezwa tuendelee kufuatilia
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 24/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

Kujua kesi ilipoishia soma: Yaliyojiri kesi ya Mbowe 24/01/2022: Shahidi wa 11, H4347 Goodluck amaliza ushahidi wake. Shahidi wa 12 kuendelea tarehe 26/01/2022

UPDATES

- Jaji ameingia Mahakamani

- Kesi inatajwa


Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili Wa Serikali Robert Kidando nipo pamoja na wakili
  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Tulimanywa Majige
  • Ignasi Mwinuka
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na wakili
  • Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Maria Mushi
  • Khadija Aron
  • Seleman Matauka
  • Idd Msawanga
  • Michael Lugina
- Jaji anaita Washitakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja Wakili Peter

Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kuendelea.

Jaji: Anakuwa Shahidi namba Ngapi?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Anakuwa Shahidi namba 12 Shahidi anakwenda kuitwa Shahidi anaingia Mahakamani, Mrefu Mwembamba, Mweupe Kidogo

Jaji: Majina yako

Shahidi: Naitwa Luteni Denis Urio

Jaji: Umri

Shahidi: Miaka 42

Jaji: Kabila

Shahidi: Mchaga

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Jaji: Kazi yako

Shahidi: Askari Wa Jeshi la Wananchi Tanzania.

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama, kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa wa kweli, kweli tupu, Mungu Nisaidie Wakili wa Serikali.

Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili Abdallah Chavula

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anqsimama na Kwenda Kwa Shahidi
Wakili wa Serikali: Shahidi nitakuwa nakuuliza Maswali, Ukijibu utakuwa unamjibu Mheshimiwa Jaji, Naomba Uongee kwa Sauti Ya Juu

Shahidi: Sawa

Wakili wa Serikali: Tukumbushe Majina yako

Shahidi: Naitwa Luteni Denis Leo Urio

Wakili wa Serikali: Mkazi wa Wapi?

Shahidi: Mkazi wa Ngerengere Morogoro

Wakili wa Serikali: Unafanya Shughuli gani

Shahidi: Ni Mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi Tanzania

Wakili wa Serikali: Kituo Chako Cha Kazi ni wapi

Shahidi: Ni Ngerengere Morogoro

Wakili wa Serikali: Kituo Chako Kinafahamika kwa Jina gani?

Shahidi: 92 KJ Ngerengere

Wakili wa Serikali: Cheo Chako ni Kipi

Shahidi: Luteni wa Jeshi

Wakili wa Serikali: Majukumu yako ni Yapi

Shahidi: Ni Platoon Commander Kuongoza Askari Walio Chini yangu

Wakili wa Serikali: Unaongoza Askari Wangapi

Shahidi: Afisa Mmoja na Askari 30

Wakili wa Serikali: Ni Askari gani wanayofanya kazi Katika Kikosi cha KJ 92

Shahidi: Ni Wanajeshi Waliopata Mafunzo Maalum, Komando

Wakili wa Serikali: tuambie Wewe Umetumikia Jeshi Kwa Miaka Mingapi

Shahidi: Miaka 18

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama ulijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania Mwaka gani

Shahidi: Tarehe 16,June 2003

Wakili wa Serikali: Jeshi la Wananchi Tanzania lina Majukumu yepi

Shahidi: Lina Majukumu ya Ulinzi wa Mipaka dhidi ya Uvamizi Wa Ndani na Nje

Wakili wa Serikali: Jukumu lingine ni lipi

Shahidi: Kwenye Operation ya Ulinzi Wa Amani Kwenye Mataifa yenye Mgogoro

Wakili wa Serikali: Umesema Wewe ni Luteni wa Jeshi, Je Umekuwa Kwenye Nafasi hiyo kwa Miaka Mingapi

Shahidi: Kwa Miaka 6

Wakili wa Serikali: Umeeleza Mahakama Kwamba Miongoni Mwa Majukumu ya Jeshi ni Kuleta Amani Kwenye Mataifa Mengine, Ushiriki wako ni Vipi

Shahidi: Nimeshirriki Kulinda Amani 2011 Nchini Sudani, Na 2019 ni Sudan hiyo hiyo Jimbo la Darfur

Wakili wa Serikali: Tueleze Mahakama Kule Darfur ulipo enda Majukumu yako yalikuwa yepi

Shahidi: Kuhakikisha Wale Staff Officer (Wapatanishi) Ku Ensure Usalama wao Kwa Sababu Wao ni Unarmed Personnel

Wakili wa Serikali: Kuna Mtu anafahamika Kwa Jina la Khalfani Bwire Unamfahamu Vipi

Shahidi: Nina Mfahamu Kwa Muda Mrefu, Nili Mtrain, Nikifanya naye Kazi Kituo Kimoja cha 92 KJ

Wakili wa Serikali: Umemfahamu Kuanzia Mwaka gani

Shahidi: Kuanzia 2006 Mpaka 2009

Wakili wa Serikali: Wakati Unamfahamu, yeye alikuwa ana Jukumu gani

Shahidi: alikuwa Kiongozi Mdogo, anaongoza,Ni Section Commander, alikuwa anaongoza Watu 9

Wakili wa Serikali: Cheo Chake Kilikuwa ni Kipi

Shahidi: Rank ya koplo

Wakili wa Serikali: Unaposema Ulifahamiana naye kuanzia 2006 Mpaka 2009 umamaam gani

Shahidi: Ukomo wake Ulikuwa Mwaka 2019

Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mpaka I kafika Ukomo wake

Shahidi: alifukuzwa Kazi Jeshini

Wakili wa Serikali: Kwa sababu Zipi afukuzwe Kazi

Shahidi: Kwa Utovu wa Nidhamu

Wakili wa Serikali: Wakati Mwaka 2019 anafukuzwa + kazi Wewe Ulikuwa wapi

Shahidi: Kwenye Operation Ya Peace Keeping, Sudan Jimbo la Darfur

Wakili wa Serikali: Ni wakati gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Khalfani Bwire alifukuzwa Kazi kwa Utovu wa Nidhamu

Shahidi: Ni 2020 Mwezi March Baada ya Kutoka Darfur

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ni Mazingira Yapi Ulifahamu Kwa Yeye Kufukuzwa Kazi Jeshini

Shahidi: Nilipata Taarifa hizo kutoka Kwa Administration Officer of the Unit

Wakili wa Serikali: Administration Officer ndiyo nani?

Shahidi: Mtu anaye fuatilia Maisha ya Askari Wote Kikosini na Maafisa ya Jeshi, Pia ni Kiongozi

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu na Khalfani Bwire tangu 2006 Mpaka 2019 yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa ni Mahusiano Mazuri tu, Ya Kiongozi na afisa wake.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mahusiano yenu baada ya Ajira Kukoma yalikuwaje

Shahidi: Bado nilikuwa naendelea Kuwasiliana naye, Mawasiliano ya Kawaida tu

Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu anaitwa Adam Hassan Kasekwa ama Jina Lingine anaitwa Adamoo.

Shahidi: Nafahamiana naye toka Mwaka 2012 ndipo alipofika Kwenye Unit ya 92KJ alifika Kwenye Mafunzo, Nikam' train, aka' pass Maana nilimpokea Mimi.

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama, Huyu Adam Kasekwa ama Adamoo alifanya kazi Jeshini Kwenye 92 KJ alifanya kazi Mpaka Lini

Shahidi: Mpaka Mwaka 2018

Wakili wa Serikali: Nini Kilimsibu Mwaka huo 2018

Shahidi: Alifukuzwa Kazi Jeshini.

Wakili wa Serikali: Alifukuzwa Kazi Jeshini Kwa Sababu zipi

Shahidi: Kwa Utovu Wa Nidhamu

Wakili wa Serikali: Mpaka anafukuzwa Kazi Jeshini Kwa Utovu, Je alikuwa na Cheo gani

Shahidi: alikuwa Private Soldier.

Wakili wa Serikali: Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini

Shahidi: Ni Askari ambaye hana Rank inayo kuwa Displayed, Ni Askari anayekuwa Chini ya Kiongozi Wake

Wakili wa Serikali: Wakati Adam Kasekwa anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa upo wapi

Shahidi: Nilikuwa Nipo Arusha.

Wakili wa Serikali: Ni wakati Gani Ulikuja Kufahamu Kwamba Adam Kasekwa kafukuzwa Kazi Jeshini

Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi Kutoka Arusha Kwenye Kozi

Wakili wa Serikali: Taarifa za Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu Wewe Ulizipata Wapi?

Shahidi: Administration Officer

Wakili wa Serikali: alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira gani

Shahidi: Ofisini Kwake

Wakili wa Serikali: Mazingira ya Mahusiano Baina ya Wewe na Adam Kasekwa yalikuwa Je Kipindi Kile Kabla ajafukuzwa Jeshi.

Shahidi: Yalikuwa Mazuri tu

Wakili wa Serikali: VIpi Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi na Kuondoka Jeshini yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa Mazuri

Wakili wa Serikali: Shahidi Kuna Mtu Naitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya Unamfahamu Vipi

Shahidi: Namfahamu Nilifanya naye Kazi Kituo Kimoja

Wakili wa Serikali: Kituo Gani hicho

Shahidi: 92 KJ

Wakili wa Serikali: umeanza Kufanya naye Kazi huyo Mohammed Ling'wenya kuanzia Mwaka gani Mpka Mwaka gani

Shahidi: Kuanzia Mwaka 2010 Mpaka Mwaka 2017

Wakili wa Serikali: Nini Kilitokea Mwaka 2017

Shahidi: alifukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mpaka anafukuzwa Kazi, alikuwa ana Cheo gani Katika Jeshi

Shahidi: Alikuwa ni Private Soldier

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Unaposema Private Soldier Unamaanisha nini

Shahidi: Ni Askari Mwenye Cheo Cha Mwisho chini

Wakili wa Serikali: VIpi Kuhusiana na Mahusiano yenu

Shahidi: Tulikuwa na Mahusiano Mazuri

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Baada ya Yeye Kufukuzwa Kazi Kwa Utovu Wa Nidhamu, Mahusiano yenu yalikuwaje

Shahidi: Yaliendelea Kuwa Kama alipokuwa Kazini

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati Mohammed Ling'wenya anafukuzwa kazi Wewe Ulikuwa Wapi

Shahidi: Nilikuwa Kwenye Kazi Maalum

Wakili wa Serikali: Ni Wakati Gani Ulikuja Kupata Ufahamu, kuwa Mohammed Ling'wenya amefukuzwa kazi

Shahidi: Baada ya Kurudi Kwenye Kituo Changu Cha Kazi, kutoka kwa Administration Officer

Wakili wa Serikali: Huyo Administration Officer alikupatia Taarifa Hizo Mkiwa katika Mazingira Yepi

Shahidi: Tukiwa Ofisini

Wakili wa Serikali: Unasema Unamfahamu Khalfani Bwire Je akiwa Miongoni Mwetu unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Sababu ipi itakufanya Umtambue

Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 10, lakini pia Body Morphology

Wakili wa Serikali: Mtu huyo Yupo wapi

Shahidi: aliyepo Mbele yangu, Tunatizamana, Yupo Jirani na Magereza

Wakili wa Serikali: Pia Umemtaja Adam Kasekwa Maarufu Kama Adamoo, Je Unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Ni sababu Zipi hasa zitafanya Umtambue

Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5 lakini pia na Body Morphology Yake

Wakili wa Serikali: Hebu tuonyeshe Mtu huyo Yupo wapi

Shahidi: Ni Wapili Kutoka Kulia Mwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: tuambie Mwingine unaye Msema ni Mohammed Abdilah Ling'wenya, na Yeye Vipi Unaweza Kumtambua

Shahidi: Ndiyo naweza Kumtambua

Wakili wa Serikali: Sababu Ipi Itakufanya umtambue

Shahidi: Nimefanya naye Kazi zaidi Ya Miaka 5, pia Body Morphology yake, Tatu ana Makovu Usoni na Mkononi.

Wakili wa Serikali: Hapa Yupo wapi

Shahidi: Ni watatu Kutoka Upande Wa Kulia wa Bwire

Wakili wa Serikali: Shahidi isaidie Mahakama, Unasema Adam Kasekwa Na Mohamed Ling'wenya Walikuwa ni Private Soldier, Je pale Jeshini Walikuwa na Majukumu Yapi

Shahidi: Wao Ni watendaji wa Shughuli za Kijeshi

Wakili wa Serikali: Huyu Khalfani Hassan Bwire, Adam Hassan Kasekwa, Mohammed Abdilah Ling'wenya wakati wa Utumishi wao Wa Jeshi Pale 92 KJ Makazi yao yalikuwa wapi?

Shahidi: Walikuwa Wa naishi huko, Khalfani Bwire Ngerengere, Adam Kasekwa alikuwa Anaishi Chalinze katika Utaratibu Wa Misbehave

Wakili wa Serikali: Hapana Usiende Huko

Shahidi: Na Mohamed Ling'wenya na Yeye Chalinze

Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Mwaka 2011 ulikuwa Darfur, Je katika Wenye Cheo Cha Private Soldier nani Uliyekuwa naye

Shahidi: Sikumbuki

Wakili wa Serikali: Unaposema Ukumbuki unamaanisha nini

Shahidi: Sina Kumbukumbu Ka Nilikuwa na Mmoja wapo.

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama pale Darfur Ulipokuwa Unaishi Kwenye ile Nyumba yako Ulikuwa Unaishi na Nani

Shahidi: Tulikuwa tunaishi Viongozi Watupu

Wakili wa Serikali: Na Mwaka 2012 pale Darfur Pia Mwenye Cheo Cha Private, nani ulikuwa naye

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili wa Serikali: Mtu anaitwa Freeman Mbowe Wewe Unahusiana naye Vipi

Shahidi: Tulifahamiana naye Mwaka 2008 Mpaka 2020

Wakili wa Serikali: Unaweza Kusema ni Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kufahamiana.

Shahidi: Mwaka 2008 Freeman Mbowe anilipigia Simu akaniita Kwa Majina yangu

Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Siwezi Kukumbuka hiyo Tarehe

Wakili wa Serikali: Shahidi Irejee Mahakama tena, Unasema alikupigia Simu lini

Shahidi: Mwaka 2008

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Ilikuwa Tarehe Ngapi na Mwezi gani

Shahidi: Sikumbuki Tarehe Wala Mwezi

Wakili wa Serikali: alikupigia Simu, wewe si yako ilikuwa ya Namba gani

Shahidi: ilikuwa 0754612518

Wakili wa Serikali: Unaweza Kukumbuka na Yeye namba yake iliyokupogoa ilikuwa namba gani

Shahidi: Ilikuwa Mtandao Wa Airtel, ila namba Sikumbuki

Wakili wa Serikali: alikueleza nini

Shahidi: alipiga Simu akauliza Wewe ni Denis Urio, Nikamwambia Yes ndiyo Mimi, akasema ni Askari wa Jeshi la Wananchi, Nikamwambia Ndiyo, akajitambulisha, Kwa Sababu Namfahamu Nikamuamkia.

Wakili wa Serikali: Kwa Sababu Unamfahamu Ukamuamkia, Ulikuwa Unamfahamu Vipi

Shahidi: Alikuwa anaonekana Kwenye Vyombo Vya Habari, Haikuwa Jina geni, I Amana anafahamika

Wakili wa Serikali: Baada ya wewe Kumpa Salamu nini Ulifanya

Shahidi: alikuwa ana confirm Profile Yangu.

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini

Shahidi: alikuwa nauliza wewe si Denis Urio Nikasema Ndiyo, ni Mtu wa Kilimanjaro basi Mimi Ndugu yako, Ndipo Uhusiano Ulianza

Wakili wa Serikali: Hebu Iambie Mahakama Namba yako ya Simu alitoa Wapi

Shahidi: Sifahamu alipoitoa.

Wakili wa Serikali: Yeye alikueleza, Ni wapi ametoa Namba yako

Shahidi: aliniambia Kuwa Mbona Unafahamu, Kwa Mtu Kupata Namba ya Simu Siyo Tatizo, Usiwe na Wasiwasi

Wakili wa Serikali: Ni Kitu gani kilipelekea Mpaka Yeye Kusema Kuwa Mbona Unafahamika Sana.

Shahidi: Ni pale Nilipo taka Kujua amepata wapi Namba Yangu

Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hayo Maneno ni Wakati gani alikutamkia

Shahidi: Mara ile ya Kwanza Kuwasiliana, Nikiwa natumia Mtandao Wa Voda yeye akitumia Mtandao Wa Airtel.

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tuambie Baada ya Siku hiyo kuwasiliana Mawasiliano yenu yalikuwaje

Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana, Iwe Kwa Kunisalimia alikuwa ananitumia Ujumbe wa Kuni wish hata Kama Kuna Sikukuu au Event Yoyote

Wakili wa Serikali: Mlimkuta ana kwa ana Lini

Shahidi: Tukikutana Ana Kwa Ana Mwaka 2012

Wakili wa Serikali: Unaweza Kueleza Mahakama Mwaka huo 2012 Ilikuwa ni Tarehe Ngapi na Mwezi Gani

Shahidi: Siwezi Kukumbuka Tarehe Wala Mwezi

Wakili wa Serikali: Shahidi nikirudishe Nyuma, Umeeleza Awali Kwamba 2011 ulikuwa Darfur Nchi Sudan, Je Ulirejea Nchi Mwaka Gani

Shahidi: Nili rejea Mwaka 2011 Mwezi wa 10

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Siwezi Kukumbuka Siku wala Tarehe.

Wakili wa Serikali: Ni Mazingira Yepi Yalipelekea Ninyi Mwaka 2012 Kukutana

Shahidi: Mwaka 2012 nikiwa Maeneo Ya Mgulani (Saba Saba) Nilipokea Simu ya Mheshimiwa Mbowe Kama Ilivyo Kawaida yake akaniambia Upo wapi, Nikamwambia Nipo Maeneo Ya Mgulani (sabasaba).

Wakili wa Serikali: alikueleza nini

Shahidi: Alini uliza nipo Wapi, Nikamuelekeza Location nilipo

Wakili wa Serikali: Location Maana yake ni nini

Shahidi: Eneo nilipo

Wakili wa Serikali: Endelea

Shahidi: aliniambia Kuwa Kuna Kitu anataka Tuongee, Je tunaweza Kuonana? Nikamuuliza Wewe Upo wapi akasema Yupo Mikocheni Cassa Motel

Jaji: Unaweza Kutaja Spelling zake

Shahidi: CASA Sikumbuki Vizuri

Wakili wa Serikali: Wewe Ukamwambia Nini

Shahidi: Sijui Mikocheni Vizuri, Wala Mahala Ilipo

Wakili wa Serikali: Ulifanya Nini sasa

Shahidi: Baada ya kumwambia Siyo Mwenyeji aliambiwa niende Kituo Cha Tax Ni Mwambie Dereva Yoyote yule anipeleke CASA Motel

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupewa hayo Maelekezo, Maamuzi yako yalikuwa ni nini

Shahidi: Nilienda Kwa Dereva Tax, Nikamwambia Anipeleke CASA Motel, nikaweza Kufika CASA Motel

Wakili wa Serikali: Hicho Kituo Cha Tax Ulicho enda Kutafuta Tax ni Kituo Cha Wapi

Shahidi: Ni Saba Saba Mbele Kidogo Kama Unaenda Kwa Aziz Ally Wilaya Ya Temeke.

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Hiyo Safari yako ya CASA hotel Ilikuwaje

Shahidi: Nili weza Kufika, Nikampigia Simu akapokea, akauliza nimefika Wapi, Nikamwambia Nimeshafika

Wakili wa Serikali: Taratibu Jaji anaandika..

Wakili wa Serikali: endeleaaaa

Shahidi: akanielkeza Pale CASA Motel Kuna Vitu Kama Vimepangwa Kuna watu walikuwa wamekaa Mbali Mbali Ka Wanne hivi, Baada ya Kufika akaniuliza huyu anadai TSh ngapi Nikamwambia TSh 20

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumwambia Ikawaje

Shahidi: Alilipa hiyo Tsh 20.

Wakili wa Serikali: Wakati yoye Haya Unayosema Kuanzia Kupigana Simu Mpaka Unafika CASA Hotel Ilikuwa ni Majira yapi

Shahidi: Ilikuwa Kuanzia Saa Saba Mchana Mpaka Alasiri

Wakili wa Serikali: Pale Mlipoliwa Mmekaa na Kukutana naye, Mwingine nani Mliye kuwa Mmekaa naye

Shahidi: Hapakuwa na Mtu Mwingine zaidi yangu Mimi na Yeye

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Sasa, Nini Mlichozungumza Wakati Mmekutana

Shahidi: Mambo Makubwa matatu, Kutaka Kujua Mimi ni Nani, nafanya kazi gani, Nina Cheo gani?

Wakili wa Serikali: Kwenye Hayo Madodoso wewe Ulimjibu nini

Shahidi: Mimi ni +Rank gami Majibu niliyompa, Nilimwambia Mimi Sina Rank

Wakili wa Serikali: Ulipomueleza Wewe huna Rank Ulikuwa Unamanisha Nini

Shahidi: Nilimwambia Mimi Sina Cheo Chochote.

Wakili wa Serikali: Kwanini Ulimueleza hayo

Shahidi: Kwa sababu aliniuliza Swali

Wakili wa Serikali: Lingine lipi ulilomjibu

Shahidi: Nilimjibu nafanya kazi Mkoani Morogoro, na Nyumbani ni wapi nilimwambia Mimi Nyumbani ni Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Vijijini.

Wakili wa Serikali: Kingine Kipi

Shahidi: Akitaka Kujua Msimamo Wangu dhidi ya Vyama Vya Upinzani

Wakili wa Serikali: Kwenye hilo la Msimamo Wako Majibu yako Yalikuwa ni Yepi

Shahidi: Nilimwambia Kwa Mujibu wa Kazi yangu Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote.

Wakili wa serikali: ukamueleza nini?

Shahidi: Siruhusiwi Kufungamana na Chama Chochote, Ila Kwa Kiongozi aliyepo Madarakani

Wakili wa Serikali: Lingine lipi mililozungumza

Shahidi: Alini uliza Juu ya Makampuni ambayo yangeweza Kufunga Mfumo Wa Mawasiliano Kwenye Ofisi zao, na Kama Jeshini Kuna Makampuni yaliyofunga Mawasiliano Jeshini. Nilipo Muuliza Kwanini anataka Kufanya kazi na Makampuni Yaliyofunga Mawasiliano Jeshini, Akajibu Kuwa anataka Kufuatilia Mawasiliano ya Viongozi Wenzie Wanaotoa Siri Nje ya Chama.

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kuku uliza Juu ya Swala hilo, Majibu yako Yalikuwa ni nini

Shahidi: Nilimshauri aende Kwenye Taasisi za Elimu ya Juu ndiyo atapata Suluhu ya Tatizo lake Wakili wa Serikali Nini Kiliendelea Sasa Baada ya Hapo.

Shahidi: Baada ya Hapo tuliachana, Akaita Tax akamlipa nikaondoka zangu

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Fedha kiasi gani aliyolipwa

Shahidi: Sijui ni fedha Kiasi gani

Wakili wa Serikali: Baada ya akiwa mmeachana, Mliachana Majira gani.

Shahidi: Majira ya Jioni kati ya Saa 9 Mpaka Saa 11 Jioni

Wakili wa Serikali: Baada ya Wewe Kuachana naye Ulieleka Wapi

Shahidi: Nilirudi Nyumbani

Wakili wa Serikali: Baada ya Kikao Chenu Mawasiliano Yalikuwaje

Shahidi: Yalikuwa Ka Kawaida, anipigia Simu, ananitumia Meseji na anani' Wish Kama ni Sikukuu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya Mwaka 2012, Je ni wakati gani Mwingine Mlikutana ana kwa ana

Shahidi: Ilikuwa ni Mwaka 2020 Mwezi Saba Tarehe za Katikati

Wakili wa Serikali: Hebu elezea Mahakama ni. Mazingira Gani yaliyopelekea Nyinyi Kukutana.

Shahidi: Ilikuwa Kwenye Tarehe 26 Mpaka 30 June Mwaka 2020, Niliacha Simu Kwenye Gari, Nipo rudi Nilikutana Missed Calls Nyingi. Missed Calls zaidi ya Tano Katika Simu

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Unaposema Missed Call zaidi ya Tano.

Shahidi: Ni simu ambazo hazikupokelewa

Wakili wa Serikali: Zilikuwa ni Namba za akina nani?

Shahidi: Hazikuwa Saved, Zilikuwa ni Namba Ngeni Katika Simu yangu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukuta namba Ngeni na Huku pokea, Ulihisi nini

Shahidi: Nili Fikiri ni Familia Yangu, Nilipiga Mwanzo Haku pokea, Nilipiga tena akapokea akasema alikuwa anakutafuta Mwenyekiti Baadae Nilipiga Simu Nyingine, ikapokelewa akasema alikuwa anakutafuta Chairman. Basi sikupiga tena namba Nyingine

Wakili wa Serikali: Hebu elezea Mahakama ni nini Kilitokea

Shahidi: Baadae Ikipigwa Simu na namba Ngeni akasema ni Kaka Yangu wa Dodoma, Nikamwambia Mbona sina Kaka Dodoma, akasema Sikia Mimi ni Freeman Mbowe, Nikamsalimia Shikamoo Mzee.

Wakili wa Serikali: Kasema nini

Shahidi: Akaniambia Kuna Mambo ya Muhimu Sana nataka Tuongee, Nikamwambia Kuwa tunaweza Kuongea tuh kwenye Simu, akasema Ni Jambo Muhimu Sana ni Lazima tuonane, Nikamwambia Kwa sasa Sina Muda.

Wakili wa Serikali: Wakati hayo Yanatokea yalikuwa ni Majira gani

Shahidi: Yalikuwa Majira ya Saa 10 Jioni

Wakili wa Serikali: Wakati hayo Yanatokea wewe Ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa nipo Likizo Morogoro

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kukupa Ombi lake la Kuonana, Nini Kiliendelea

Shahidi: Tulikuwa tunaendelea Kuwasiliana tu. Baada ya Hapo Nilikuja Dar es Salaam Mwezi wa Saba 2020 nilikuja kwa kazi Binafsi, nikafanya Shughuli zangu za Kijeshi, Majira ya Saa 10 nikakummbuka Nilikuwa na appointment, Nimampigia Simu yake Mara Kadhaa hazikupokelewa, Basi Nikawa naenda Station, Kupanda Magari ya Mgulani

Wakili wa Serikali: Nini kitokea

Shahidi: Wakati Nasubiri Gari Kituoni Majira ya Saa 12 alinipigia Simu Kwa namba Nyingine, akaniambia Alikuwa yupo Bussy alishindwa Kupokea simu yangu, Kaniuliza upo wapi? Nikawa Mwambia nipo Station Najiandaa Kwenda Mgulani akaniambia Homeboy hatuwezi Kuonana?

Wakili wa Serikali: Nimesikia Mara Kadhaa unatamla Homeboy, Je Tafsiri yake ni nini

Shahidi: Tafsiri yake Mimi siwezi Kujua, Ila mara Kadhaa alikuwa ananiita Homeboy.

Wakili wa Serikali: Wewe Sasa Ulimjibu nini Kuhusiana na Ombi lake

Shahidi: Alini taka kama naweza Kufika Mikocheni, Nakamwambia Kuwa Mikocheni sipajui Vizuri, naweza Kupotea Akaniambia huwezi Kupotea, akaniambia Cheki Dereva Tax au Bodaboda Karibu amuelekeze Mahali alipo. Nikampa Bodaboda Simu Pale Stand ya Station akamuelekeza, baada ya hapo nikaondoka na Bodaboda Kuelekea Mikocheni.

Wakili wa Serikali: Hebu tuambie Sasa Hapo Mikocheni Mlienda Hadi sehemu gani

Shahidi: Tulienda Mpaka Kwenye Mgahawa Sipafahamu, Kuna Parking ya Magari, I kabidhi nipigie simu Hakupokea, Wakati Napiga simu, akatokea Kijana Mmoja Nyuma Yangu. Akaniuliza wewe Ndiyo Denis Urio, Nikamwambia Ndiyo Mimi, akatoa Elfu 10 akamlipa Bodaboda akaniambia Mwenyekiti Yupo huku, Tukaenda kwa Nyuma kama VIP, Basi yeye akatoka Nje

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tuambie wakati huo Unafika Pale sasa, Ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi.

Shahidi: Ilikuwa Majira ya Saa Moja Kasoro, Jua lilikuwa Leshazama lakini Bado Kuna Mwanga, Kwa hiyo Kama Saa Moja Kasoro

Wakili wa Serikali: Na Wakati una Mpigia Simu, Na Yeye akakupigia baadae, alikuwa anatumia namba gani?

Shahidi: alikuwa ana tumia namba ambayo siyo ya kwake ni Namba ambayo sihifahamu

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama wakati wewe Umefika pale ulipokutana naye, Ulimpigia Simu Kwa namba ipi?

Shahidi: alikuwa na namba yake ya Airtel na Tigo, Nilipiga Airtel hakupokea na Nilipiga Tigo hakupokea pia

Wakili wa Serikali: Ukiondoa Pale Mlipokutana, Ni nani Mwingine alikuwa pale

Shahidi: Hapakuwa na mtu, Ni Mazingira ya starehe, Tulikuwa wawili tu Mimi na Yeye.

Wakili wa Serikali: Shahidi tuambie Sasa nini Kilichotokea Sasa Pale Mlipokutana

Shahidi: Nilimkuta yupo Pekee yake anakunywa Redbul anamuita Muhudumu anisikilize na mimi nikaagiza Malta

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Tuambie, Ieleze Mahakama Alikueleza au Kukwambia Kitu gani alichokuitia

Shahidi: Kitu cha Kwanza tulisalimiana Salamu za Muda Mrefu, Lakini Baada ya Salamu hizo akaniambia komredi mwaka huu wa 2020 Kuna Uchaguzi Mkuu, Hivyo Chama Changu Kimepanga Kuchukua Dola Kwa namna na Kwa Gharama Yoyote ile. Akaniambia Wewe si Unaona Watu wa wanyonge wa hali ya Chini wanavyoishi Maisha ya Shida Akanielekeza, komredi Tumefahamiana Muda Mrefu, Tunatoka Mkoa Mmoja, pia wewe ni Mchaga Mwenzangu, Tukichukua Dola Unafikiri Wewe Utakosa Cheo Cha Juu Jeshini?

Akaniambia hivyo Jeshini Kuna Watu Waliostaafu au Kufukuzwa Kazi ya Jeshi.. Wale ambao wamefanya Mafunzo Maalum ya Komandoo. Homeboy naomba unitafutie Vijana hao wenye Mafunzo Maalum ya Komando, ambao nitaambatana nao kwenye Harakati za Kuchukua Dola. Najua Watakuwa na Uwezo wa Kunisaidia Kufanya Nchi isitawalike, Kuleta Taharuki na Kusiwe na Amani.. Tutafanya hayo Kwa Kuzua Taharuki Mheshimiwa Freeman Mbowe Alisema yalikuwa ni Kulipua Vituo Vya Mafuta, Kuchoma Moto Masoko na Mikusanyiko Mkubwa Ya watu.

Kukata Miti Mikubwa iliyoota pembezoni Mwa Barabara zote, Hasa Kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro hasa Mjinwa Moshi na Barabara Kuu ya Morogoro - Iringa, Kwa Kufanya Vitendo hivyo Vitatu Kutapelekea watu Kuwa na Taharuki na Kuandamana Nchi Nzima.

Mikoa Mingine Iliyobakia Itasapoti Mikoa hii niliyo highlight.. Point Nyingine ya Mwisho ni Kuwadhuru Viongozi Wengine Wa Serikali, Ni Viongozi ambao ni Vikwazo Kwa Vyama Vya Upinzani.. Hivyo Homeboy nisaidie Kuwapata hao watu Nina Haraka nao sana, MWISHO WA MAELEZO YAKE FREEMAN.

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama alipokueleza yeye Hayo Makusudi yake wewe Ulifanya Jambo Gani

Shahidi: Nilitafakari nikamkubalia

Wakili wa Serikali: Shahidi hebu tueleze Wewe alipokueleza hayo Maneno, Ni Kipi kilikupelekea ukamkubalia

Shahidi: Kwa Experience yangu Kuna kitu kinaitwa Tactical appreciation

Wakili wa Serikali: Experience yako Kwenye Nini

Shahidi: Kwenye Ulinzi

Wakili wa Serikali: Tactical appreciation ni Kitu gani hicho

Shahidi: Kuna Binadamu, Kuna Mimi na Tanzania, lakini Mimi si kitu Kuliko Tanzania, Freeman Ni Ndugu yangu, Tayari Alishakuja na Ile Nia, Kwamba Unataka nimkatalie, lakini Mimi huenda ni Plan B au C. Je Nikimkatalia atachukua hatua gani? Je, nitakuwa ni solution matatizo yasitokee, Naweza Kumkatalia lakini kumbe ana Backup plan nitakuwa sija solve tatizo.

Wakili wa Serikali: Sasa hiyo Tactical Appreciation Uliyotumia Ulitumia Kufanya nini

Shahidi: Ikaniongoza Kwamba Nimkubalie, Kwamba Nipe Muda Nikutafute hao watu

Wakili wa Serikali: Sasa Shahidi Tuambie, yeye alikwambia anataka Wangapi

Shahidi: Hakuna Kikomo cha Watu, Ni wale Watakaopatikana.

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Baada ya kukueleza Maneno yale nini Kilitokea

Shahidi: alimuita Kijana wake, Akaita Tax nikarudishwa nilipotolewa

Wakili wa Serikali: Wakati huo unamaliza na Wewe unarudi Mgulani ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi

Shahidi: Saa Mbili hadi Saa Tatu, Kwa sababu Taarifa ya Habari Ilikuwa imeshaanza

Wakili wa Serikali: Na Huyo Dereva Tax alikuwa amelipwa TSh ngapi

Shahidi: Sijui alikuwa amelipwa TSh ngapi

Wakili wa Serikali: Shahidi Umerudi Mgulani, Nini Sasa Ulichofanya au Hatua ulizo chukua Juu ya Ujumbe Uliopewa

Shahidi: Nilishindwa Kulimeza

Wakili wa Serikali: Kushindwa Kulimeza ndiyo nini

Shahidi: Nilishindwa kukaa nalo.

Wakili wa Serikali: Kwanini Ushindwe Kukaa na Taarifa Ya siri

Shahidi: Nature ya Taarifa

Wakili wa Serikali: Taarifa Ipi

Shahidi: Ya Kuleta Taharuki

Wakili wa Serikali: Baada ya Kushindwa Kueleza Ulifanya nini

Shahidi: Nilichukua Hatua Ya akimpigia DCI Afande Boazi Majura ya Saa 3 Usiku

Wakili wa Serikali: DCI ni Kitu gani?

Shahidi: Director of Criminal intelligence, Mkurugenzi Wa Makosa ya Jinai.

Wakili wa Serikali: ulipo Mpigia nini Kilitokea

Shahidi: Nilimpa Taarifa amilizopewa na Freeman Mbowe, Juu ya Uvunjifu wa Amani, Kwamba ameniambia nitafutie Watu wa Kukata Miti Barabarani na Kuchoma Masoko wakati naendelea Kusema hivyo akasema Subiri, Unaweza Kuja Kesho Ofisini Kwangu Asubuhi.

Wakili wa Serikali: alikwambia nini

Shahidi: Kama naweza Kufika Ofisini Kwake Kesho Asubuhi

Wakili wa Serikali: Na shahidi Unaweza Kukumbuka namba ya Simu ya Robert Boazi (DCI) Uliyompigia

Shahidi: Sijaikariri Kichwani.

Wakili wa Serikali: alikwambia Uende Ofisini Kwake wapi

Shahidi: Makao Makuu ya Polisi, Jijini Dar es Salaam Mtaa wa Ohio

Wakili wa Serikali: Iambie Mahakama Alikutaka Uende Ofisini Kwake Saa ngapi

Shahidi: Majira ya Asubuhi

Shahidi: Nilifika Makao Makuu ya Jeshi Polisi, nikajitambulisha Getini Kuwa Nina Appointment na Afande DCI, Nikaenda Pia nikamkuta Polisi nilajitambulisha Kuwa mimi ni Afande Mwenzao Nina appointment na Afande DCI, wakaniruhusu Nikaenda Ghorofa ya Saba

Wakili wa Serikali: Wewe Ulikuwa unapanda Juu Kuelekea Wapi

Shahidi: Nilikuwa napanda Juu Ofisi ya DCI Ghorofa Ya Saba

Wakili wa Serikali: kabla Ya Siku hiyo Kwemda Kwa DCI ni lini tena Ulienda Ofisi hiyo

Shahidi: Nilishafika Mara Mbili Mwaka 2017 na Mwaka 2014

Wakili wa Serikali: Hebu ieleze Mahakama Kipi kililufahamisha Ofisi za DCI zipo Ghorofa ya Saba

Shahidi: Nilishafika Awali, ila baada ya Kufika Reception Nili Confirm kwa wale askari

Wakili wa Serikali: Ulienda Vipi Ghorofa ya saba

Shahidi: Kuna Njia Mbili Kuna Lift na Kuna Ngazi, Lift ilikuwa haifanyi kazi, nikapanda ngazi.

Shahidi: Inapofika Ghorofa ya Saba Kwa Kupanda Ngazi, Pembeni yake Kuna Mlango, Nilipo Fungua Mlango Nikakuta Kuna Askari Mwanamke ambaye ni PS wake, Nikajitambulisha Kwamba Naitwa Luteni Denis Leo Urio Askari Wa Jeshi la Jeshi la Wananchi.

Wakili wa Serikali: Baada ya Kujitambulisha, Ulimwambia nini huyo PS

Shahidi: Nilimwambia Nina appointment na Afande DCI

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kumueleza hayo

Shahidi: Palikuwa na Kochi pembeni akaniambia Nikae pale pembeni afanye Mawasiliano naye. Baada ya Kufanya Mawasiliano naye, Nikaambiwa Ingia, Nikakuta tena kuna Makochi na Kuna msaidizi Wake akasema Subiri utaitwa

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukaa hapo Nini Kiliendelea.

Shahidi: Baada ya Muda PS Wake akaja akaniambia Fungua Mlango Niingie Kwa DCI

Wakili wa Serikali: Ulikutana na Kitu gani

Shahidi: Nilimkuta Afande DCI yupo Pekee yake, Nikamsalimia, Nikajitambulisha, Nikamkumbusha

Wakili wa Serikali: Ukajitambulishaje

Shahidi: Mimi naitwa Luten Denis Urio, Miliyekupigia simu Jana Usiku

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Samahani Sasa ni saa Saba Kasoro Dakika Nne, Na Mimi bado Nina Maswali mengi sana, Naomba Tupate Break Kidogo

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Basi tunahairisha Kwa Muda Kupata Health Break, Kwa hiyo tutarudi Saa Saba na Dakika 45

- Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Jaji..

- Jaji anatoka


Jaji ametoa mapumziko ya dakika 45 itaendelea...
- Jaji ameingia Mahakamani

- Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa.


Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile kama awali tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia Upande wa Utetezi Quorum yetu haijabadirika Shahidi aliingia Mahakamani aliongozana Wakili Wa Serikali Ignasi Mwinuka
Huyu jamaa si ndiye Adamoo alikiri alichukua kipondo cha nguvu kutoka kwa mahita.,?! Yajayo yanafurahisha
 
Aiseeeee! Amazing! Flabbergasting, even! Ushahidi wa watuhumiwa ni wa kweli, ila wa Luteni ni wa uongo! Ujiniasi wako ni wa Planet Mars!
If you are speaking about a civil case your word against an others is 50% to 50%, you must get 51% usually by presenting some type of evidence, witness, video, letters, emails, recorded audio etc. Further the judge or jury can also look at the credibility of both parties especially in a criminal trial etc.
 
Naomba mmpatie ^health breaks^ za kutosha iwapo akizihitaji, ili isitokee dharura yoyote ya kiafya; tunataka mwendelezo wa hii the so-called sinema.
Joto la Dar halafu wanaomba kwenda haja ndogo,wawe wanaomba kwenda kupunga upepo!
 
Kama kamondoo mwenye cheo Cha Luten anafanya utoto huu nchi yetu haipo salama, yaani mtu unaambiwa Jambo kubwa Kama hili la kuvuruga Amani, unaamua kucheza mchezo wa kua undercover kwenye kikundi kinachopanga kuleta vurugu, then wewe unaenda kufanya recruitment ya watu ambao wameachichwa jeshi kwa utovu wa nidhamu ili wakawe sehemu ya kundi, then kabla ya ushahidi wa kutosha kuhusu hizo habari unaenda kuwakamatisha watu ambao wewe ndo umewashawishi kujiunga. Je, alishindwa vipi kutafuta askari ambao bado ni waadilifu wakawa undercover ili wakaendelee kuufuatilia mtandao mkubwa wa Mbowe ambayo hata yeye alihisi kua anaweza kua ana backup ndio maana akaamua kumkubalia. That is nonsense! Kama kweli hizi njama zilikuwepo hafai kua Luten wa jeshi, Ila Kama game yao unaendelea kuchezwa tuendelee kufuatilia
Your logic is LOGICAL!

Possibly alikuwa anataka kuridhisha pande zote mbili--upande wa ^sirikali^ na upande wa FM. Don't forget kwamba politicians wana ushawishi mkubwa sana, si kwa jeshi wala kwa raia wa kawaida.

Inaonekana mazungumzo yao yalikuwa marefu sana. Imagine watu wawili wazungumze kuanzia around saa saba hadi saa tisa! Almost two hours! Then, kuna hii kwamba walikuwa wanaendelea kuwasiliana hata baada ya hapo.

Bado kuna [SQUARE BRACKETS] nyingi sana zinazohitaji kujazwa punje halali za ngano!
 
Kwenye Cross examination sasa;
Kibatala: Umesema wewe ni Mwajiriwa wa Jeshi la wananchi Tanzania,
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Umemuonesha Mh. Kitambulisho chochote cha kuthitisha wewe ni Mwajiriwa kweli wa JWTZ na sio shahidi wa Mchongo
Shahidi: Hapana
Kibatala: umemwonesha Mh. Jaji Barua yoyote ya ruhusa inayotoka kwa mwajiri wako wa 92 KJ Ngerengere
Shahidi: Hapana
Kibatala: Katika mazungumzo yenu na Mteja wangu Mh. Mbowe lipo eneo ambalo alizungumzia ugaidi?
Shahdi; hapana Ila ............
Kibatala: Hakuna ila hapa, ushajibu
Acha ikae hivyo
 
Sauti alizorekodiwa wakati wanakutana zitawasilishwa.
Maana FM alikataa mazungumzo ya kwenye simu akasahau Kuna voice recorder.
Yajayo yanahuzunisha.
Hizo ndo zinaweza kua Uthibitisho wa anachokisema, ngoja tusubiri. Sauti inaweza inatengenezwa hivyo bado watahitaji uhalisia wa hiyo sauti. Ko ngoma bado mbechi, tuendelee kufuatilia Ila Urio amelitia aibu jeshi letu kwa mbinu yake aliyoitumia kumkamata Mbowe na kuwakamata watu ambao yeye mwenye aliwashawishi kujiunga na Mbowe. Afu una wakamatisha kabla hata kazi hawajaanza. Hivi police walimwacha vipi anayewashawishi watu wakafanye ugaidi?
 
Shahidi: Afande Boazi alinitambulisha Kuwa Yule Mtu anaitwa ACP Ramadhan Kingai

Wakili wa Serikali: Baada ya Utambulisho huo

Shahidi: DCI akanitaka tena nianze tena Upya Kusimulia
... muda wa saa 2 kuelekea saa 3 usiku umefika nyumbani kwako kutoka kuonana na Mbowe (Mikocheni huko). Baada ya kutafakari, "likakushinda kumeza" ukaamua kumpigia DCI. DCI akakuelekeza uende ofisini kwake kesho (Dar es Salaam nadhani; hajahamia Dodoma tarehe hizo? Itakuwa Dar maana Dodoma jengo la Polisi halina ghorofa 7).

Kesho yake unaenda kwa DCI mkiwa kwenye mazungumzo anaingia mtu mwingine ambaye ulikuja kugundua ni ACP Ramadhan Kingai (ambaye kituo chake cha kazi ni Arusha)!!!!!!! Bagosha! Jifunzeni kutengeneza igizo lenye mashiko basi! Soon mtaenda kujua kwamba hamjui!

Cc: Bome-e, Frank Wanjiru, cool d, et. al. tieni neno hapa. Huyu naye akaribie hapa comte
 
Hizo ndo zinaweza kua Uthibitisho wa anachokisema, ngoja tusubiri. Sauti inaweza inatengenezwa hivyo bado watahitaji uhalisia wa hiyo sauti. Ko ngoma bado mbechi, tuendelee kufuatilia Ila Urio amelitia aibu jeshi letu kwa mbinu yake aliyoitumia kumkamata Mbowe na kuwakamata watu ambao yeye mwenye aliwashawishi kujiunga na Mbowe. Afu una wakamatisha kabla hata kazi hawajaanza. Hivi police walimwacha vipi anayewashawishi watu wakafanye ugaidi?

Urio kachezea kelbu (vitasa) sana kule Mbweni, ili tu akubali kuongea hayo aliyoongea.
 
Naona Luten Urio katuletea kitu kimya kumbe Akina Adamo nao walikua Informer lakini wenzie wameshtakiwa kwa ugaidi yeye informer mkuu anakuja kuwazamishia huko shimoni yeye akiendelea kula bata

Screenshot_20220126-150226.png
 
... muda wa saa 2 kuelekea saa 3 usiku umefika nyumbani kwako kutoka kuonana na Mbowe (Mikocheni huko). Baada ya kutafakari, "likakushinda kumeza" ukaamua kumpigia DCI. DCI akakuelekeza uende ofisini kwake kesho (Dar es Salaam nadhani; hajahamia Dodoma tarehe hizo? Itakuwa Dar maana Dodoma jengo la Polisi halina ghorofa 7).

Kesho yake unaenda kwa DCI mkiwa kwenye mazungumzo anaingia mtu mwingine ambaye ulikuja kugundua ni ACP Ramadhan Kingai (ambaye kituo chake cha kazi ni Arusha)!!!!!!! Bagosha! Jifunzeni kutengeneza igizo lenye mashiko basi! Soon mtaenda kujua kwamba hamjui!

Cc: Bome-e, Frank Wanjiru, cool d, et. al. tieni neno hapa. Huyu naye akaribie hapa comte
Nilikuwa sijanotice hii kitu,nadhani mawakili wa utetezi watakuwa wameliona hili!Kingai alifika lini Arusha?
 
Urio kachezea kelbu (vitasa) sana kule Mbweni, ili tu akubali kuongea hayo aliyoongea.
Mahita alimla marungu akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu akalia kama mbusi ya kichaga! meeeeee! nitakubali nitasema eeeehhh mmeeee!
Mahita: hili ni agizo la mwenyenchi JPM kwani mbowe mmezaliwa pamoja! Haya ongea na rais live hapa!! JPM:-- We urio shimboni shafyo-- usiposema hapo unaishia kutupwa kwenye mto wenye mamba unasikia Mimi ndiye Lahisi. Umesikia? Kibano====Meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeemhhhhhhhhhh keleuwiii-----
General Mabeyo unaliaibisha Jeshi kwa mtindo huu!!
 
Kwenye hii kesi shahidi anaandaliwa kama anaenda kufanya NECTA wakati hujui Kibatala atatoa maswali kwenye topic ya Geometry? Algebra? hujui akiomba kielelezo namba fulani swali linalofuata shahidi anachanganyikiwa kwamba atumie calculator au four figure table, shahidi akienda kwenye desa/kibuti anatoa majibu ya swali la kwanza kumbe aliulizwa swali la tatu........
The young people think the old people are fools -- but the old people know the young people are fools"
— Agatha Christie
 
Back
Top Bottom