Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika mapokezi na mkutano wa Tundu Lissu Sumbawanga

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika mapokezi na mkutano wa Tundu Lissu Sumbawanga

"Tundu Lissu akiwa Rukwa - Sumbawanga Mjini kwenye kiwanja cha Ndua.."

Mheshimiwaa Tundu Lissu ameongea na maelfu ya wakazi wa Rukwa hapa Sumbawanga.

Ifuatavyo ni sehemu ya Hotuba yake:

Nawashukuru sana sana watu wa Sumbawanga kwa ukarimu na upendo.

Sasa naomba nianze nahii engua engua ya tume, wanaonyesha ni namna gani wanavyotuogopa. Sasa hata kama wanafanya haya bado Chadema tutashinda kwa Kimbunga na hawataweza kutuibia. Kushinda kwakimbunga kwa kila kata kwa kila jimbo kura za raisi. Hili Tuweze kushinda kwa basi Sumbawanga tukapige kura kwa wingi nakulinda kura, hapo sasa tutakuwa tumeshinda kwa kishindo.

Sasa kama Chadema kwenye uchaguzi huu agenda zetu ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu. Tukisema uhuru wakuwasilisha mawazo, kuhoji, kujisemea na kusema chochote, tumezibwa midomo. Hatupo huru kuendesha shughuli zetu zakiuchumi. Rukwa ni moja ya mkoa wa mpakani ila unakosa fursa zakujiendesha kiuchumi, mmekuwa mkitozwa makodi makubwa na haya yote sababu memkosa uhuru.

Watu wanakosa Haki, huko Tabora kuna kodi ya uzazi, sasa sijui haya mambo yanatoka wapi. Haki ni wajibu kwakila mtu lakini Sasa serikali ya Magufuli inatoza mpaka kodi ya Mimba na Uzazi, alafu anasema zaeni tu kumbe ni deal. Sasa ili haki ipatikane basi uchaguzi huu chagueni Chadema tufanye mapinduzi ya haki katika nchi yetu.

Tukichukua nchi tutaiyang'nya TRA kufilisi wafanyabiashara, tutaweka kodi ya haki. Sababu ukifilisi mfanyabiashara, ukifilisi viwanda watu wanakosa ajira na maisha yanakuwa magumu. Magufuli hajui kufanya biashara ndo maana anakimbiza wawekezaji.

Tutafufua reli toka Kaliua mpaka Mpanda alafu Sumbawanga kwenda Tunduma tuunganishe na Tazara ili kufanya urahisi wa usafirishaji wa mahindi yetu, yafike kipindi bado bei ikiwa nzuri nakupunguza gharama za usafirishaji.

Hizi ndege zilizonunuliwa na Magufuli hazina maana yoyote kwetu, ndio ndege nzuri lakini hazina faida kwa Watanzania.

Maendeleo ya watu, Rukwa ndo mkoa unaolima mahindi mengi kuliko mkoa mwingine wowote lakini ukitazama hali ya wananchi wake hali ni mbaya. Basi maendeleo ya watu pamoja nakuinua hali za maisha.

Napenda nimalizie kuhusu hili swala la viongozi wakidini kupewa mashtaka ya ugaidi na serikali ya Magufuli, Kiukweli kumekuwa na uonevu mkubwa sana na kuwanyanyasa watu wanaoishi maeneo ya mipakani. Sasa Chadema ikichukua nchi vitu vya mwanzo kufanya ni kuwaachilia hawa wafungwa wakisiasa ambao wanateseka pasipo makosa.

Serikali ya Chadema itaheshimu taasisi zakidini, na haitaingilia shughuli zakidini kama katiba yetu ilivyoeleza. Serikali yetu itaheshimu kila tasisi bila kuingilia uhuru wao.

Chadema itarudisha madaraka kwa wananchi ili wajiamulie nini wanataka kufanya kwa maendeleo yao.

Mungu awabariki sana.

#njyeye
View attachment 1572793
View attachment 1572794
View attachment 1572795
View attachment 1572796
Kimbunga lissu 2020 si mchezo
 
Pamoja na kwamba Jiwe atatangazwa ila huku kukubalika kwa Lisu kitapelekea mambo mengi sana kurekebishwa katika hii awamu ya pili. Private sector Jamaa haendi kuziuwa kama alivyofanya sasa.... We SUMA JKT kwa sasa mpaka barabara wanafagia wao wakati hizo ndio kazi za vikundi mitaani ili wajikwamue kwa kipato
Tuombe Mungu Magufuli ashindwe lakini so kwa Muujiza Ni kwakupiga kura tu hata Kama Ni rafiki yako usimpigie
 
Moods ifike kipindi hizi post za chadema zihamishiwe jukwaa la utani/jokes.
Si kwavioja hivi
 
Utafiti nilioufanya kadri siku zinavyozidi kusonga Ndugu Antipas Lissu Nyota yake inazidi kungara kama Nyota za wingu Mungu awe nawe Rais wetu mtarajiwa

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
Ni hivi, kabla ya kampein Mori ilikuwa chini Sana nikiwemo mm Ila kadri siku zinavyoenda Mori inakuwa kubwa mno kwa upande wa Upinzani
Anayebisha na abishe Ila huu ndio ukweli
 
Watanzania wameamka kweli kweli. Hawataki tena upuuzi kwa kweli. Mungu ni Mkubwa mno kuona watu wameamka kiasi hiki.
 
Pamoja na kwamba Jiwe atatangazwa ila huku kukubalika kwa Lisu kitapelekea mambo mengi sana kurekebishwa katika hii awamu ya pili. Private sector Jamaa haendi kuziuwa kama alivyofanya sasa.... We SUMA JKT kwa sasa mpaka barabara wanafagia wao wakati hizo ndio kazi za vikundi mitaani ili wajikwamue kwa kipato
Tuache kutunga marahii hatangazwi tusiwenashaka kurazinakwenda kuheshimiwa ameonywa sanauchahuzi huu huku ni lisu kule ni sef
 
Back
Top Bottom