Yaliyojiri katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA Desemba 18, 2019 katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar

Lete mchanganuo wa matumizi ya mil. 326 kwa mwezi! Mbowe na baba mkwe wanatia kibindoni!
Acha ufala wewe lini mtaacha kuvuta Bangi ghato kwa Le mutuz? Mbona mnatia Aibu sana kwani hujuia kwa saa 24 kila siku CCM wapo busy kuwahujumu chadema njama mbalimbali kuwabambikia kesi kuwadhoofisha kuwapiga risasi kuwafanyia kila ubaya ukiwemo wa kwenda kung’oa Bendera, hivi unajua gharama za kujihami na hujuma za CCM ni kiasi gani? Kesi kuwalipa mawakili kuwalipa mishahara watumishi wa chadema gharama za kuendesha chadema ni kiasi gani? Tambua kuwa hakuna chama kinajiendesha kwa shida kama chadema kwani mda mwingi wanautumia kujihami dhidi ya hujuma za CCM
 
Rekebisha hapo kwenye Mwezi Mkuu ,Mungu awatangulie ktk mnayo kwenda kuyafanya leo yawe na Baraka ili kutoa Matokeo mazuri.
Ndugu Ciril, kuna baraka kwenye dhuluma, dhuluma aliyofanyiwa ndugu yetu anayetokea kwetu sote (HANANG), mungu na waumbe wake wameiona. Na bado tunaendelea kubariki uovu. Tanzania hakuna chama chenye uhalali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno yako hayana chumvi wala pilipili, bali jamejaa asali na ukweli.
Kama Mwambe sio pandikizi wa Mbowe na wanayofanya sio mazingaumbwe, basi uliyasema yatatikea
Hakuna mtu wa kumtoa Mbowe kwenye kiti anachotaka na baada ya Uchaguzi kumalizika, Mwambe atafukuzwa ndani ya CHADEMA!

Yaliyomkuta Zitto mwaka 2014 yanaenda kumpata Cecil Mwambe! Baada ya Uchaguzi wa ndani aanze kutafuta chama kingine mapema!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WanaJF duniani kote,Wasalaam!

Ni asubuhi tulivu kabisa katika jiji la Dar es Salaam huku habari kubwa inayovuma ikiwa ni mkutano mkuu wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA chenye wanachama milioni 6 wenye kadi.

Kama ripota wa JF nipo hapa Mlimani City nimekesha kwa lengo moja tu la kuihabarisha dunia kupitia JF kila kitakachojiri.

Leo ni hitimisho la zoezi refu la uchaguzi ambapo Mkutano mkuu utamchagua Mwenyekiti mpya na Makamu wake wawili.

Hata hivyo kuna dosari kidogo ilmetokea kwenye mkesha wa mkutano mkuu ambapo Polisi wenye magari na silaha walivamia eneo la Mlimani City na kushusha bendera zote za CHADEMA zilizopambwa kuashiria Mkutano Mkuu huu.

Haijajulikana hasa sababu ni nini kwa sababu Chama Cha Mapinduzi kinapofanya Mkutano wake Mkuu jijini Dodoma Mji wote na viunga vyake hupambwa kwa bendera za CCM.

Kwa sasa asubuhi hii tayari maandalizi yote ya ukumbi utakakofanyika mkutano mkuu yamekamilika. Tunatarajia takribani wajumbe 1300 kuhudhuria mkutano mkuu huu.Pia wageni wengi wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo viongozi wa vyama vyote vya siasa,mashiriia ya kimataifa ya ndani na nje, viongozi wa dini nk.

Vyombo vyote vya habari vya ndani na nje vimealikwa vikiwemo CNN na BBC.

Tunatarajia kuwaletea Live updates hapa kwa kila kitakachotokea.

View attachment 1296022

View attachment 1296132

View attachment 1296101

Updates No 2
Mkutano Mkuu umeanza rasmi na viongozi wakuu wameshaingia wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Kwa sasa Meya wa DSM Issaya Mwita ameitwa kuwakaribizha wageni kwenye mkutano mkuu huu

Kwa sasa wankaribishwa na kutambuliwa wageni mbalimbali wa vyama vya siasa vikiwemo NCCR, NLD, CUF, CCK, TLP nk

Wageni wengine waliotambuliwa ni kutoka Taasisi mbalimbali kama Mtandao wa jinsia TZ,Repoa,Walemavu nk Pia wapo viongozi wakuu wa dini.Pia yupo Naibu Msajili wa vyama vya siasa Sixty Nyahoza.

Ubalozi wa Marekani umewakilishwa na wajumbe watatu ambao wamekwisha fika mpaka sasa.

Msomi Dr Azaveli Lwaitama ndiye anayetoa salaam katika mkutano mkuu.Anashutumu watu wasiopenda demokrasia.Na amesema yeye ni mwanachama wa Chadema.

Sasa anatoa salaam mbunge kutoka Burundi wa chama cha FNL aliyekuja kuwakilisha Burundi.Anatoa salaam kwa Kiswahili na kuchanganya na kiingereza.Ujumbe wake mkubwa ameomba CDM wasikate tamaa

Viongozi wa dini sasa wanazungumza ambapo Sheikh Salum Kundecha Amir wa Shura ya Maimamu ameongea kwa niaba ya waislam.Kwa upandecwa Wakristo anayezungumza ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya Moravian Tanzania Emmaus Mwamakula.Askofu Mkuu Mwamakula ameelezea kuhusu haki na ustawi katika kuimarisha demokrasia.

Viongozi wa kanda sasa ndiyo wamekaribishwa kutoa salaam kwa niaba ya kanda zao na ameanza Mwenyekiti wa Kanda ya Pemba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini na baada ya hapo Kanda ya Magharibi

Kwa ujumla viongozi wengi waliozungumza hasa wa vyama vya upinzani na viongozi wa dini wamemwagia sifa Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa hotuba yake aliyoitoa Mwanza na kunyoosha mkono wa maridhiano kwa serikali.

Baada ya viongozi wote wa Kanda kuzungumza ameitwa Msanii Mbunge aa Mikumi Prof Jay kutumbuiza na ameshangiliwa sana na wajumbe.

Baada ya burudani wameanza kuitwa viongozi wa Mabaraza na wameanza viongozi wa Bavicha.Mwenyekiti wa Bavicha John Pambalu amelaani kufukuzwa chuo kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi na kusema Bavicha imeshaongea na wanasheria kuona namna ya kuwasaidia.
Chadema ni shida sana,Chadema ni kivuli cha Mungu wa Mbinguni...tunawategemea Chadema mtupeleke Canaan!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hi miaka baada ya Kikwete, Waislamu Tanzania hakuna Chao, wametengwa wizarani , nafasi nyeti na hata kwenye vyama vya siasa, labda ACT kwa sababu ya nguvu ya waislamu wa Pemba.

Kizuri ni kuwa Waislamu nao ni waungwana, hawalalamiki, haliwaumizi na hawana nia ya jupigania haki zao. Sidhani kama watakuwa na msaada wowote kwenye chama chochote, weshaji sideline wenyewe
hiki chama kitachukua muda sana kushika dola mpaka kitakapowashirikisha waislamu nao,

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WanaJF duniani kote,Wasalaam!

Ni asubuhi tulivu kabisa katika jiji la Dar es Salaam huku habari kubwa inayovuma ikiwa ni mkutano mkuu wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA chenye wanachama milioni 6 wenye kadi.

Kama ripota wa JF nipo hapa Mlimani City nimekesha kwa lengo moja tu la kuihabarisha dunia kupitia JF kila kitakachojiri.

Leo ni hitimisho la zoezi refu la uchaguzi ambapo Mkutano mkuu utamchagua Mwenyekiti mpya na Makamu wake wawili.

Hata hivyo kuna dosari kidogo ilmetokea kwenye mkesha wa mkutano mkuu ambapo Polisi wenye magari na silaha walivamia eneo la Mlimani City na kushusha bendera zote za CHADEMA zilizopambwa kuashiria Mkutano Mkuu huu.

Haijajulikana hasa sababu ni nini kwa sababu Chama Cha Mapinduzi kinapofanya Mkutano wake Mkuu jijini Dodoma Mji wote na viunga vyake hupambwa kwa bendera za CCM.

Kwa sasa asubuhi hii tayari maandalizi yote ya ukumbi utakakofanyika mkutano mkuu yamekamilika. Tunatarajia takribani wajumbe 1300 kuhudhuria mkutano mkuu huu.Pia wageni wengi wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo viongozi wa vyama vyote vya siasa,mashiriia ya kimataifa ya ndani na nje, viongozi wa dini nk.

Vyombo vyote vya habari vya ndani na nje vimealikwa vikiwemo CNN na BBC.

Tunatarajia kuwaletea Live updates hapa kwa kila kitakachotokea.

View attachment 1296022

View attachment 1296132

View attachment 1296101

Updates No 2
Mkutano Mkuu umeanza rasmi na viongozi wakuu wameshaingia wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Kwa sasa Meya wa DSM Issaya Mwita ameitwa kuwakaribizha wageni kwenye mkutano mkuu huu

Kwa sasa wankaribishwa na kutambuliwa wageni mbalimbali wa vyama vya siasa vikiwemo NCCR, NLD, CUF, CCK, TLP nk

Wageni wengine waliotambuliwa ni kutoka Taasisi mbalimbali kama Mtandao wa jinsia TZ,Repoa,Walemavu nk Pia wapo viongozi wakuu wa dini.Pia yupo Naibu Msajili wa vyama vya siasa Sixty Nyahoza.

Ubalozi wa Marekani umewakilishwa na wajumbe watatu ambao wamekwisha fika mpaka sasa.

Msomi Dr Azaveli Lwaitama ndiye anayetoa salaam katika mkutano mkuu.Anashutumu watu wasiopenda demokrasia.Na amesema yeye ni mwanachama wa Chadema.

Sasa anatoa salaam mbunge kutoka Burundi wa chama cha FNL aliyekuja kuwakilisha Burundi.Anatoa salaam kwa Kiswahili na kuchanganya na kiingereza.Ujumbe wake mkubwa ameomba CDM wasikate tamaa

Viongozi wa dini sasa wanazungumza ambapo Sheikh Salum Kundecha Amir wa Shura ya Maimamu ameongea kwa niaba ya waislam.Kwa upandecwa Wakristo anayezungumza ni Askofu Mkuu wa Makanisa ya Moravian Tanzania Emmaus Mwamakula.Askofu Mkuu Mwamakula ameelezea kuhusu haki na ustawi katika kuimarisha demokrasia.

Viongozi wa kanda sasa ndiyo wamekaribishwa kutoa salaam kwa niaba ya kanda zao na ameanza Mwenyekiti wa Kanda ya Pemba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini na baada ya hapo Kanda ya Magharibi

Kwa ujumla viongozi wengi waliozungumza hasa wa vyama vya upinzani na viongozi wa dini wamemwagia sifa Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa hotuba yake aliyoitoa Mwanza na kunyoosha mkono wa maridhiano kwa serikali.

Baada ya viongozi wote wa Kanda kuzungumza ameitwa Msanii Mbunge aa Mikumi Prof Jay kutumbuiza na ameshangiliwa sana na wajumbe.

Baada ya burudani wameanza kuitwa viongozi wa Mabaraza na wameanza viongozi wa Bavicha.Mwenyekiti wa Bavicha John Pambalu amelaani kufukuzwa chuo kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi na kusema Bavicha imeshaongea na wanasheria kuona namna ya kuwasaidia.

Salaam za pili za mabaraza zimetoka kwa Baraza la Wazee na katika salaam zake Mwenyekiti wa Wazee amelaani hujuma mbalimbali zinazofanywa dhidi ya kukandamiza demokrasia nchini.Ametoa wito kwa Rais Magufuli kuanza mazungumzo ya kuimarisha demokrasia nchini.

Mwisho limeitwa Baraza la Wanawake Bawacha na Mwenyekiti wake Halima Mdee ambaye ametoa wito wanawake waendelee kuheshimiwa ndani ya Chadema kwani wameonyesha uwezo mkubwa katika kuongoza Chadema na kusema chama kwa ujumla kimeamua kuwekeza kwa wanawake

Baada ya Salaam za mabaraza sasa inafuata burudani kutoka kwa Mbunge Joseph Mbilinyi ikiwa nu kuwaweka watu sawa kwa ajili ya kumkaribisha Mwenyekiti Freeman Mbowe kuhutubia.

Kabla Mwenyekiti kuhutubia Lazaro Nyalandu na Esther Bulaya wameitwa kwa dakika chache kuzungumza na wajumbe.Nyalandu amesema aliamua kuhamia Chadema baada ya kuona CCM ya sasa imeacha njia aliyoasisi baba wa Taifa Mwl Nyerere.Nyalandu amelaani dola kupokonya mamlaka ya Bunge na Mahakama na ndiyo sababu kubwa ya kuachana na chama hicho na kujiunga Chadema.Amesema anasimama katika mkutano mkuu kama Nabii Ezekiel wa Biblia kwa kuiambia CCM anguko lao limefika.Nyalandu amekula kiapo mbele ya mkutano mkuu atasimama na Chadema mpaka mwisho wa Uhai wake na atailinda Chadema mpaka mwusho wake.

Vipi mabalozi wa nchi mbalimbali mbona umewasahau kuwataja na salami zao walizotoa?
 
Ndugu Ciril, kuna baraka kwenye dhuluma, dhuluma aliyofanyiwa ndugu yetu anayetokea kwetu sote (HANANG), mungu na waumbe wake wameiona. Na bado tunaendelea kubariki uovu. Tanzania hakuna chama chenye uhalali

Sent using Jamii Forums mobile app
dhuluma gani ,si alipigiwa kura! ingekuwa dhuluma wasingemsimaisha peke yake!😀😁😆😆😅😂 simu haionjwi!
 
Hivi TBC kwa nini hawako mubashara maana kodi za wananchi zinaiendeshe

Sent using Jamii Forums mobile app
Walipa kodi wengi siyo CCM lakini TBC hawataki kurusha live mkutano wa chadema, cha ajabu wanarusha live mikutano ya CCM kwa kodi za wananchi ambao wengi ni wapinzani ni matumizi mabaya ya kodi
 
Maguful ana mbinu gani?

Kununua wapinzani?

Kuwaambia wasimamizi wa uchaguzi wasitoe form kwa wagombea wa upinzani?

Kuwaambia wasimamiz wa uchaguzi wasipokee form za wagombea wa upinzani pindi warejeshapo kwa wale waliobahatoka kuchukua?

Kuwaambia wasimamiz wa uchaguzi kuongeza maneno na tiki kwenye maeneo ambayo wagombea wa upinzani hawakuweka ili waonekane walikosea kwa wale wachache waliobahatika kurejesha?

Kuwaambia wasimamiz wa uchaguzi wakimbie ofisi?
Mpaka sasa Chadema umepoteza mwelekeo, haina uhakika hata na kiti kimoja cha udiwani. Anahutajika mtu wa kuivusha Chadema, Mbowe hana jipya, mbinu za Magufuli haziwezi kabisaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mtu wa kumtoa Mbowe kwenye kiti anachotaka na baada ya Uchaguzi kumalizika, Mwambe atafukuzwa ndani ya CHADEMA!

Yaliyomkuta Zitto mwaka 2014 yanaenda kumpata Cecil Mwambe! Baada ya Uchaguzi wa ndani aanze kutafuta chama kingine mapema!
Mwambe ni kama Pamba tu,wala hakuna atakayemfukuza,atajichuja mwenyewe tu

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom