Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 05, 2021: Inspector Mahita Mohamed atoa ushahidi

Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 05, 2021: Inspector Mahita Mohamed atoa ushahidi

Kikubwa leo hii inaonekana upande wa mawakili wa serikali (mashtaka) leo wamepunguza mbwembwe zao za 'kuwaongoza' mashahidi wa upande wa serikali.

Tupo tunafuatilia hapa kijiweni kwetu na washikaji wapo makini.
 
Wafuate @MwananchiNews wapo Twitter. Ukitaka kujua mwenendo wa kesi ya kina Mbowe kama ilivyo bila kuibiwa hisia.

 
Screenshot_20211105-125155.png
kuna vitu vitatu havifichiki daima jua,mwezi na ukweli shahidi wako umemuandaa mwenyewe unakuja kumkana mchana kweupe ogopa sana viapo vya kumtaja Mungu,Mungu anakupa unachoomba.
 
NIMEGUNDUA JAMBO MOJA:

Katika kusema UONGO kamwe hakuna consistency hata kidogo...!!

1. Huyu Afande Mahita UONGO wake ktk ushahidi wa kesi ndogo unagoma kupatana na UONGO wa kesi kubwa kwa maswali yanayofanana na yahusuyo matukio yale yale...!!

##Kumbe walifikaga mpaka Tabora? Halafu tarehe 10 Afande Mahita yuko Tabora kukamata magaidi na tarehe 10 hiyo yuko Arusha anahojiana na shahidi mwenzake Kaaya...!!

This is very interesting at the same time funny..

2. Na leo kwa mara ya kwanza askari Afande Mahita aliyekamata mtuhumiwa na kumhoji na kuchukua mashuhuda wao wanawaita "mashuhuda huru" wakaenda nao Central Police Moshi, anamkana shuhuda huyo kuwa ni MWONGO...!!!

## It's really very funny. Na hawa ndiyo Polisi wetu.
 
Shahidi namba 7 anaelekezwa na upande wa Jamhuri kuileza mahakama
  1. Kuwepo kwa watu waliokuwa na mpango wa kufanya ugaidi
  2. Kaeleza pia walivyowakamata.
  3. Kuwatambua na kawaonyesha wahusika.
Wakili wa Serikali: Kwenye Briefing Mlielezwa Mambo gani

Shahidi: Afande Kingai alituambia Kuwa amepewa Maelekezo ya Kuunda Kikosi Maalum, na Kikosi Hilo Ndiyo MIMI, ASP Jumanne, Goodluck, Francis, na PC Aziz Kwamba Kuna Kikundi Cha Watu kinataka Kufanya Vitendo Vya kigaidi

Wakili wa Serikali: Vitendo gani hivyo Shahidi: Kuwa Kikundi hicho kinataka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Mikoa Mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya Uhalifu walipokuwa wanataka Kufanya ni KUCHOMA Vituo Vya Mafuta, Kuzuia Barabara, Kukata Miti, kuwadhuru Viongozi Wa Serikali Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Lengai Sabaya Maandamano ambayo haya Ukomo, na Pia alitueleza Washirika ambao wanataka Kufanya Matukio hayo

Wakili wa Serikali: Aliwataja akina nani

Shahidi: Afande Kingai alisema Mpango huo ulikuwa unaratibiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe

Shahidi: alisema Wahalifu Wengine wapo Moshi, Kwa hiyo tuwazuie Twende Mkoani Kilimanjaro Wilaya Ya Moshi Alisema Kuna watuhumiwa 4 ambao walikuwa Moshi

Wakili wa Serikali: Wakina nani

Shahidi: Walikuwa wanakamilisha Mpango wa kwenda Kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya

Wakili wa Serikali: Kingai alisema Madhumuni ya Mpango yote ni nini

Shahidi: Kuleta Taharuki, Ili Nchi isiweze Kutawalika Tunapoelekea Kwenye Uchaguzi Akasema tuzuie Matendo hayo, Ili Nchi eindelee Kuwa Salama

Wakili wa Serikali: Mengine

Shahidi: Hayo tu kwenye Briefing

Sioni maswali ya Kibatala na wenzake yakielekea kupangua hayo
 
Back
Top Bottom