Shahidi namba 7 anaelekezwa na upande wa Jamhuri kuileza mahakama
- Kuwepo kwa watu waliokuwa na mpango wa kufanya ugaidi
- Kaeleza pia walivyowakamata.
- Kuwatambua na kawaonyesha wahusika.
Wakili wa Serikali: Kwenye Briefing Mlielezwa Mambo gani
Shahidi: Afande Kingai alituambia Kuwa amepewa Maelekezo ya Kuunda Kikosi Maalum, na Kikosi Hilo Ndiyo MIMI, ASP Jumanne, Goodluck, Francis, na PC Aziz Kwamba Kuna Kikundi Cha Watu kinataka Kufanya Vitendo Vya kigaidi
Wakili wa Serikali: Vitendo gani hivyo Shahidi: Kuwa Kikundi hicho kinataka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Mikoa Mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya Uhalifu walipokuwa wanataka Kufanya ni KUCHOMA Vituo Vya Mafuta, Kuzuia Barabara, Kukata Miti, kuwadhuru Viongozi Wa Serikali Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Lengai Sabaya Maandamano ambayo haya Ukomo, na Pia alitueleza Washirika ambao wanataka Kufanya Matukio hayo
Wakili wa Serikali: Aliwataja akina nani
Shahidi: Afande Kingai alisema Mpango huo ulikuwa unaratibiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe
Shahidi: alisema Wahalifu Wengine wapo Moshi, Kwa hiyo tuwazuie Twende Mkoani Kilimanjaro Wilaya Ya Moshi Alisema Kuna watuhumiwa 4 ambao walikuwa Moshi
Wakili wa Serikali: Wakina nani
Shahidi: Walikuwa wanakamilisha Mpango wa kwenda Kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya
Wakili wa Serikali: Kingai alisema Madhumuni ya Mpango yote ni nini
Shahidi: Kuleta Taharuki, Ili Nchi is iweze Kutawalika Tunapoelekea Kwenye Uchaguzi Akasema tuzuie Matendo hayo, Ili Nchi eindelee Kuwa Salama
Wakili wa Serikali: Mengine
Shahidi: Hayo tu kwenye Briefing
Sioni maswali ya Kibatala na wenzake yakielekea kupangua hayo