ibatala: Hati ya mashtaka inasema hivyo Vitendo vilivyotakiwa kufanywa vinajumuisha MOROGORO, ARUSHA, DAR ES SALAAM na MWANZA... Je ulieleza Kama kuna Mpelelezi alifika Morogoro?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Katika ushahidi wako umeeleza kwenda mwanza Kwa kesi hii
Shahidi: Sikueleza
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji wewe Kama Msaidizi Wa RCO, Ulizungumzia Kuhusu Uwepo wa Njama za Kulipua Vituo Vya Mafuta Arusha... Kwa sisi wenyewe tuligundua kuhusu Arusha Kuna Mipango inaendelea
Shahidi: Ndiyo nimeongea
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Arusha Kituo A na B kilitaka Kulipuliwa
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ARUSHA Kuna Kiongozi A na B walitaka Kudhuriwa
Shahidi: Kimya
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwa Mujibu wa Upelelezi watu tuligundua Maandamano haya yalipangwa Tarehe ngapi na Eneo la Kuanzia
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Unakumbuka Kuzungumzia Chochote Kuhusu Mkoa wa Mbeya
Shahidi: Nilitaja Mkoa wa MBEYA kuwa Upo Miomgoni Mwa eneo linalotakiwa Kufanywa tukio
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kati yenu Kuna Mpelelezi alienda Mbeya
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Vituo Vya Mafuta MBEYA Vilitakiwa Kulipuliwa
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kiongozi gani alipangwa Kudhuriwa
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Morogoro Vituo gani kwamba vinatakiwa Kulipuliwa
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Maandamano yalitakiwa kufanyika Wapi Mkoa wa Morogoro
Shahidi: Si kumwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Sabaya alitakiwa Kudhuliwa tarehe ngapi Mwezi Gani na Mwaka gani
Shahidi: Hapana Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Vituo Vinavyotaka Kulipuliwa Kilimanjaro
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mshitakiwa wa Kwanza alitakiwa anatakiwa kufanya katika Mipango hiyo ya Ugaidi
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je specific Role aliyotakiwa Kufanya ADAM Kasekwa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Specific Role ya Mohammed Ling'wenya Kwamba alitakiwa Kufanya nini
Shahidi: Si kumwambia
Kibatala: Je Specific Role ya Freeman Mbowe katika Kutaka kutenda Ugaidi
Shahidi: Ndiyo nilimwambia
Kibatala: Ulimwambia Nini
Shahidi: Kwamba Ndiye aliyekuwa anaratibu
Kibatala: kuratibu ni suala pana, Nataka Kujua Kazi yake Katika huo Uratibu
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: Je unafahamu katika Maelezo yako Umemtaja ADAM HASSAN na Siyo ADAM HASSAN KASEKWA Maarufu Adamoo
Shahidi: Nimemtaja ADAM HASSAN ila nimemtambua
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Mshitakiwa wetu hapa Mahakamani Anaitwa ADAM HASSAN KASEKWA Maarufu Kama Adamoo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Hwa wote wawili ADAM HASSAN ndiyo ADAM HASSAN KASEKWA
Shahidi: Ndiyo Nimefanya Kwa Kumtambua
Kibatala: Unafahamu Kwamba Sabaya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya amehukumiwa na Mahakama kwa Makosa ya Ujambazi
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Sabaya Amehukumiwa Makosa ya Ujambazi Wakati wewe Ukiwa Afisa wa Polisi Arusha na ACP Kingai
Shahidi: Ndiyo natambua
Kibatala: Wewe Ulifanya Jukumu gani katika Kuzuia uhalifu Wa Sabaya
Shahidi: Siyo lazima Mimi lakini kuna wasaidizi waliopo Chini yangu walizipata
Kibatala: Na Unafahamu Kwamba Matendo Yake yalijirudia rudia
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo wewe na Afande Kingai Kama mlipata Taarifa za Intelijensia kuhusu Uhalifu wa Sabaya
Shahidi: Sikupata Taarifa
Kibatala: lakini unajua Mipango ya Uhalifu wa Wilaya ya Hai Nje ya eneo lako la kazi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwanini tusiseme Kwamba Kesi hii ninyi na Sabaya Mlitengeneza Kesi Kwa ajili ya mambo ya Kisiasa
Shahidi: Siyo Kweli kabisa
Kibatala: Huyu ASP Jumanne Yupo wapi
Shahidi: Yupo Arumeru
Kibatala: Kwamba hufahamu kwamba Jumanne amesimamishwa kazi baada ya kumbambikia Mzee mstaafu kuwekewa meno ya tembo kwenye mzinga wake wa nyuki chini ya usimamizi wa ASP Jumanne ambaye ni shahidi wenu?
Shahidi: Sifahamu najua yupo kazini..
Kibatala: Muda huu tunapo ongea yupo Ofisini?
Shahidi: Sifahamu sababu siwasiliani naye siku nyingi
Kibatala: Unajua tukio lake la kusimamia kumuwekea Mzee wa watu meno ya tembo
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Je ulimfahamisha huyu aliyetaka kudhuriwa Sabaya
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ukimfahamisha Kamati ya Ulinzi ya Wilaya Hai au Mkoa wa kilimanjaro
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: katika Briefing zenu Je Kingai aliwambia kwamba kwamba ametoa Taarifa Kwa Kamati za Ulinzi na Usalama
Shahidi: Hakutuambia
Kibatala: Je katika Briefing Zenu Kingai aliwahi kuwaambia kuwa amemtaarifu Rais ambaye ni Kiongozi wa Nchi
Shahidi: hajatuambia
Kibatala: Labda Kufahamisha watu wa USALAMA WA TAIFA FA
Shahidi: Hapana hakutuambia
Kibatala: katika Maelezo Yako umezungumzia Kuhusu Jumanne Kuweka Sahihi yake Katika Hati ya Uzuiaji Mali
Shahidi: Hapana Sijasema
Kibatala: Statement Yako inasema "Tuliwa chukua watuhumiwa hao na kuwapeleka kituo cha Polisi Central kwa Mahojiano na tuliendelea Kumtafuta Mtuhumiwa Mwingine Moses Lijenje ambaye hatukuweza Kumpata, Je Kuna sehemu umesema Kwamba Mahojiano hayakufanyika
Shahidi: Hapo hakuna ila Ndiyo Maana Nimeelezea
Kibatala: Mheshimiwa Jaji tulikubaliana kuwa na health break, tunge' Break kwa sababu bado ninayo maswali mengi na huyu shahidi.
Wakili wa Serikali: sawa mheshimiwa
Jaji: unategemea muda gani zaidi
Kibatala: Labda nusu saa na zaidi
Jaji: Mpaka saa 8:30 tutarudi kuendelea