Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 05, 2021: Inspector Mahita Mohamed atoa ushahidi

Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 05, 2021: Inspector Mahita Mohamed atoa ushahidi

Ni kweli kabisa...

Japo ktk mazingira fulani Mungu huruhusu wachache wasio na hatia waumie kwa ajili ya wokovu wa wengi...

Mfano ni Yesu Kristo na upande wa pili Yuda Iskariote akiwa kama facilitator wa mpango bila yeye kujua...

Hapa "maza" ni Yuda Iskariote pasipo kujua akishirikiana na wenzake ana - facilitate hukumu ya watu wasio na hatia...

Yuda Iskariote aliingiwa na pepo (demon) la usaliti lililo facilitate hukumu ya kifo isiyo haki ya Yesu Kristo...

Lilipomaliza zamu yake, likampisha pepo (demon) la mauti/kifo na likaenda kummaliza kwa kujinyonga mwenyewe huku akitamka maneno haya, "OLE WANGUliz MIMI MAANA NIMEISALITI DAMU ISIYO NA HATIA...!!

"Maza" na wenzake vipande 30 vya fedha [Samia na wenzake ni madaraka] yamepofusha fahamu zao]. Hakika kama hawajifunzi kutokana na tukio la Yesu Kristo na Yuda Iskariote na wakaendelea na mpango wao huu muovu, HAKIKA WATAKUFA KIFO KIBAYA NA CHA AIBU KWAO NA VIZAZI VYAO VYOTE....!!!
Kwa leo nilichogundua kwenye hii kesi ni hivi ilindiwa jopo na Sabaya akishirikina na Mwendazake ili kumkomoa Mbowe baada ya kuona hana namna ingine baada ya ile ya kumuua Akwelina kuvumba. Jiulize Sabaya analukuki ya matukio na huyo Jnne ndio alimwekea mzee mstaafu meno ya tembo imaging yule mzee aliongea kwa huzuni sana, hivi leo Mahita kichwa kubwa anaulizwa kama alifahamu au intelijensia ilikuwa na taarifa za uhalifu wa sabaya uliofanyikia katika mkoa wake hajui ila ya mkoa mwingine anajua haya maajabu yako Tanzania tuu.

Na siwezi kujua kwanini mama Samia haioni aibu na kuachia hii kesi tena bila masharti na kumlipa Mbowe muda aliomweka huko magereza hii aibu haitafutika kwenye utawala wake kamwe kamwe,
 
Shahidi namba 7 anaelekezwa na upande wa Jamhuri kuileza mahakama
  1. Kuwepo kwa watu waliokuwa na mpango wa kufanya ugaidi
  2. Kaeleza pia walivyowakamata.
  3. Kuwatambua na kawaonyesha wahusika.




Wakili wa Serikali: Kwenye Briefing Mlielezwa Mambo gani

Shahidi: Afande Kingai alituambia Kuwa amepewa Maelekezo ya Kuunda Kikosi Maalum, na Kikosi Hilo Ndiyo MIMI, ASP Jumanne, Goodluck, Francis, na PC Aziz Kwamba Kuna Kikundi Cha Watu kinataka Kufanya Vitendo Vya kigaidi

Wakili wa Serikali: Vitendo gani hivyo Shahidi: Kuwa Kikundi hicho kinataka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Mikoa Mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya Uhalifu walipokuwa wanataka Kufanya ni KUCHOMA Vituo Vya Mafuta, Kuzuia Barabara, Kukata Miti, kuwadhuru Viongozi Wa Serikali Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Lengai Sabaya Maandamano ambayo haya Ukomo, na Pia alitueleza Washirika ambao wanataka Kufanya Matukio hayo

Wakili wa Serikali: Aliwataja akina nani

Shahidi: Afande Kingai alisema Mpango huo ulikuwa unaratibiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe

Shahidi: alisema Wahalifu Wengine wapo Moshi, Kwa hiyo tuwazuie Twende Mkoani Kilimanjaro Wilaya Ya Moshi Alisema Kuna watuhumiwa 4 ambao walikuwa Moshi

Wakili wa Serikali: Wakina nani

Shahidi: Walikuwa wanakamilisha Mpango wa kwenda Kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya

Wakili wa Serikali: Kingai alisema Madhumuni ya Mpango yote ni nini

Shahidi: Kuleta Taharuki, Ili Nchi is iweze Kutawalika Tunapoelekea Kwenye Uchaguzi Akasema tuzuie Matendo hayo, Ili Nchi eindelee Kuwa Salama

Wakili wa Serikali: Mengine

Shahidi: Hayo tu kwenye Briefing


Sioni maswali ya Kibatala na wenzake yakielekea kupangua hayo
Mpaka sasa umeshaona maswali ya KIBATALA (lazima jina liwe herufi kubwa) akipangua au laa au na wewe ndio Jesca wa Sabaya?
 
Halafu anaonekana vitu vingi katika taaluma yake havijui, protocols za kazi hazijui

Amefeli mtihani wa logic, kua kama umeshindwa kujua office mate wako kua ni mhalifu utawezaje kujua uhalifu wa mtu mwingine amnaye yuko mbali?

Unasema waliopanga conspiracy za ugaidi ni makomandoo halafu unawahamisha kutoka kituo cha polisi chenye askari wengi (sehemu yenye uhakika wa usalama) unawapeleka kituo kingine tena mkiwa watatu tu bila securirty escort?
inatakiwa kuwe na aptitude test huko Kufanya recruitment kazi za upolisi atleat, wawe na vi GRE /gmat ZAO ZAO manake sasa hizi ni aibuuu kweli kweli
 
Ukistaajabu ya Musa utauaona ya Friauni wa Tanzania.

Yaani Mbowe apange kufanya Ugaidi mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, DSM, Morogoro na Mbeya na asiwe na uratibu wowote katika mkoa hiyo? Yaani kina Adamoo wao waende tu kwenye hiyo mikoa bila kuandaa watu kwenye hiyo mikoa? Wala hata viongozi waandamizi wa CHADEMA makao makuu wasijue lolote?

Hebu tuondoeni hii aibu tutacheka. Dhambi mbaya ya uongo mnafanya nyie.😄😄
 
Ni wewe ni mtu mpumbavu sana ambaye unaamini kuwa Mbowe hapaswi kupimwa mahakamani, hata hivyo mpaka umauti unamfika huyo jiwe kuu la pembeni Mbowe alikuwepo uraiani.
Ficha upumbavu wako angalao kidogo basi............... huyo unaemwita Jiwe ndio shida ya watanzania inapoanzia mtu alikuwa na roho ya chuki ubinafsi ushamba yaani alikuwa zigo kubwa kwa Tanzania. Ila Mungu hashindwi kamwe
 
Yaani nilizani Uratibu una mpaka wale Suicide Bombers. Ila wakati huo si ndio alikuwa anajiandaa na Kampeni za Ubunge?!!!
 
Kesi hii msingi wake ni kijibu swali kuu Je, kulikuwa na njama za kufanya ugaidi?

Hadi sasa mwenendo wa kesi unahusu kuthibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa kama utaratibu wa kisheria ulitumika.

Tusubiri mashahidi wengine wa Jamhuri kuthibitisha kama hao waliokamatwa, na ni watuhumiwa, walikuwa na njama ya kufanya ugaidi.
 
Nchi imetekwa na upotofu hii.

Wananchi wote tuko ndani ya basi bovu, viti vichafu, kuna joto ndani, dereva mlevi halafu anaendesha kwa kasi sana huku akinena maneno machafu dhidi ya abiria.....The Beautiful Ones Are Not Yet Born
 
Ukistaajabu ya Musa utauaona ya Friauni wa Tanzania.

Yaani Mbowe apange kufanya Ugaidi mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, DSM, Morogoro na Mbeya na asiwe na uratibu wowote katika mkoa hiyo? Yaani kina Adamoo wao waende tu kwenye hiyo mikoa bila kuandaa watu kwenye hiyo mikoa? Wala hata viongozi waandamizi wa CHADEMA makao makuu wasijue lolote?

Hebu tuondoeni hii aibu tutacheka. Dhambi mbaya ya uongo mnafanya nyie.[emoji1][emoji1]
Wanampotezea tu muda mwamba
 
Ukistaajabu ya Musa utauaona ya Friauni wa Tanzania.

Yaani Mbowe apange kufanya Ugaidi mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, DSM, Morogoro na Mbeya na asiwe na uratibu wowote katika mkoa hiyo? Yaani kina Adamoo wao waende tu kwenye hiyo mikoa bila kuandaa watu kwenye hiyo mikoa? Wala hata viongozi waandamizi wa CHADEMA makao makuu wasijue lolote?

Hebu tuondoeni hii aibu tutacheka. Dhambi mbaya ya uongo mnafanya nyie.😄😄
Hii kesi Lissu alipaswa awepo
 
NIMEGUNDUA JAMBO MOJA:

Katika kusema UONGO kamwe hakuna consistency hata kidogo...!!

1. Huyu Afande Mahita UONGO wake ktk ushahidi wa kesi ndogo unagoma kupatana na UONGO wa kesi kubwa kwa maswali yanayofanana na yahusuyo matukio yale yale...!!

##Kumbe walifikaga mpaka Tabora? Halafu tarehe 10 Afande Mahita yuko Tabora kukamata magaidi na tarehe 10 hiyo yuko Arusha anahojiana na shahidi mwenzake Kaaya...!!

This is very interesting at the same time funny..

2. Na leo kwa mara ya kwanza askari Afande Mahita aliyekamata mtuhumiwa na kumhoji na kuchukua mashuhuda wao wanawaita "mashuhuda huru" wakaenda nao Central Police Moshi, anamkana shuhuda huyo kuwa ni MWONGO...!!!

## It's really very funny. Na hawa ndiyo Polisi wetu.
Shangaa na wewe. Ila nadhani Mama kuna mtu anamtaka kumchomoa ndio maana kaacha hii sarakasi itembee.
 
Kwa kuendelea kuangalia bila kuchukua hatua (entertain) aina za nyuzi kama hizi, nahisi ni mwanzo wa mwisho au kufa kwa JF. Kwa wale waliokuwepo miaka ile JF ilikuwa msitu wa kujifunza. Lkn sasa, mtu anaweza akaanzisha uzi mpaka unajiuliza... huyu anaota au vp???
 
Kuna wakati hua nasema tupepigwa upofu mahali. Vyombo vyetu vya usalama mnaelewa outcomes za hii kitu? Au hata weledi huko hakuna ni maslahi tu uzalendo umekwisha? Mbowe wa kumfanyia haya kweli?

Kwa upepo navyoenda upepo wa katiba mpya unazidi kukua kuliko hata kabla ya Mbowe kuwekwa ndani.
 
... halafu kwenye hii kesi ya ugaidi ni miongoni mwa mashahidi upande wa jamhuri; sijui atakuja kama polisi au raia!
.....ina maana Sirro IGP alikuwa hajui yote haya?! Mbona mambo ya aibu haya. Sidhani kama Sirro hii kesi anaipenda hata kuisikia na akiona haya yanayoendelea mahakamani anajutia kauli yake. Na bado akina Kibatala watamtaka mahakamani kama shahidi.
 
Magufuli alimtuma sabaya wilaya ya Hai kwa kazi ya kumdhibiti Mbowe!

Kwenye kutengeneza kesi ya ugaidi wakatumika maaskari walewale waliomsaidia na kumlinda sabaya alipokuwa akifanya matukio yake ya ujambazi huko Arusha.

Soon kitaumana!
Na ndiko njia inakoelekea huko...tayari kokoro la Kibala limeanza KUKUSANYA
 
Hivi katika hali ya kawaida kabisa ya namna Polisi waweza kuzuia uhalifu, Mbowe aliachajwe mtaani mpaka baadae hivo wakati ni dhahiri uchunguzi WOTE unaotolewa ushahidi mpaka sasa ukifanyika ndani ya miezi mitatu kuanzia 05.08.2020. Na hata Dennis Urio aliwataarifu hata toka May 2020!!

Halafu shahidi anaulizwa specific matendo ya “uratibu wa Mbowe” anaishia tu kusema aliratibu!!
 
Back
Top Bottom