Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi - 27/09/2021

Si tu hlo , limeibuka lingine kuwa shahidi adamoo alikubali na kusaini kuwa aliachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu, na kwa mujibu wa maelekezo yake aliachishwa kwa sababu ya battle confusion na si utovu wa nidhamu!
Kwa maelezo yake mashitaka yote ya awali aliyakana - alisanishwa na Kingai bila kujua nini kilichomo ndani baada ya mateso makali ya kufungwa ka mshikaki .
 
Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili Kidando: anatambulisha Jopo lake
1. Robert Kidando​
2. Nassoro Katuga​
3. Ignas Mwanuka​
4. Esther Martin​
5. Tulumanywa Majigo​

Wakili Kibatala: anatambulisha Jopo lake
Adv Peter Kibatala​
Adv Sisty Aloyce​
Adv Gaston Garubindi​
Adv Idd Msawanga​
Adv Alex Massaba​
Adv Evaresta Kisanga​
Adv Hadija Aron​
Adv Michael Mwangasa​
Adv Faraji Mangula​
Adv Fredrick Kiwhelo​
Adv Nashon Nkungu​
Adv Jonathan Mndeme​
Adv John Mallya​
Kibatala: Kwa Mshitakiwa wa Kwanza Nashon Nkungu Mshitakiwa wa Pili John malya Mshitakiwa wa tatu Fredrick Kiwhelo Wengine wote ni Kwa mshitakiwa wa Nne

Jaji: Siku ya Ijumaa shahidi( Mshtakiwa wa pili) alikuwa hajakamilisha Utetezi wake

Jaji: arejee kwenye Kizimba tuweze Kuendelea

Shahidianaenda

Jaji: Wakili wa Serikali mpo tayari..?

Jaji: Upande wa Utetezi Mmpo tayari

Wote: wapo tayari

Jaji: Shahidi bado upo chini ya Kiapo kama tulivyokuapisha Siku ya Ijumaa Unaweza kuchagua Kukaa au Kusimama..... Mawakili wa Serikali watakuhoji Maswali na Baadae Upande wa Utetezi hususani Wakili waKo anaweza Kuja Kukuongoza tena Kwa Kukuuliza Maswali.

Shahidi: Nitakaa Mheshimiwa Jaji, nakaa Chini Mahakama Kimya Kidogo, Jaji anaandika

Jaji: bila shaka Wakili wa Serikali Chavula unaendelea

Wakili wa Serikali: Naam Mheshimiwa

Jaji: tafadhali endelea

Wakili wa Serikali: Awali siku ya Ijumaa kabla hatujahairisha nilikuuuliza kuhusiana na wale waliokuvamia maeneo ya Rau hawakupata kujitambulisha,Kweli au Si Kweli

Shahidi: Kweli

WS: wale watu Mlivyotoka pale kwenda Kituo cha Polisi hawakukueleza Majina yao akina nani.? kweli au Si Kweli

Shahidi: Kweli

WS: walivyokutoa Moshi kukuleta Dar es salaam hawakukueleza wao Majina yao ni Akina nani

Shahidi: niliwafahamu kwa wao alipokuwa wanaitana Majina yao na Nikaja kuthibitisha Majina yao hapa Mahakamani walipo Jitambulisha

WS: Wakati wa Kukusafirisha Moshi Kuja Dar es salaam Watu wale walikufunga Kitambaa Usoni

Shahidi: ni Sahihi

WS: ni Jacket,Si Ndiyo

Shahidi: ni Jacket ndiyo

WS: Hukujua ni akina nani unasafiri nao

Shahidi: Kweli

WS: na hata Ulipofika Dar es salaam ukafikishwa Kituo cha Kwanza cha Polisi hukujua upo wapi

Shahidi: kama nilivyoeleza

WS: We Jibu swali langu Kweli au si Kweli

Shahidi: Kweli

WS: Umedai ulipokuwa unasafirishwa Ulikalishwa Chini kwenye gari,Kweli au si kweli

Shahidi: ni kweli

WS: Uliweza Kujua ni sehemu gani ya gari ..?

Shahidi: nilipotoa Upande wa Kulia Kwa Uelewa wangu siyo Kwa Kuona, Nikafahamu nimekaa nyuma ya gari

WS: Ulikaa nyuma ya gari

Shahidi: ndani ya gari,Sehemu ya Nyuma

WS: Bila shaka ilikuwa ni haya Magari Madogo

Shahidi: Siwezi Kujua ni gati gani

WS: unakubaliana na Mimi ukiwa Umefungwa Machoni uwezi Kuona .?

Shahidi: Ndiyo uwezi Kuona,ila ukiwa unatendewa unahisi

WS: ukiwa umefungwa Macho uwezi Kuona hata Kile kifaa wanachokusababishia Maumivu

Shahidi: kweli

WS: nakurudisha Moshi,umesema walipokuwa wanakutesa Moshi walikuwa wabakuuliza Umekuja Moshi Kufanya nini

Shahidi: ni sahihi

WS: Wewe Ukajibu umekuja Moshi Kufanya VIP protection ni Sahihi

Shahidi: ni sahihi

WS: Ulisema ulipofika Dar es salaam kituo cha kwanza cha Polisi walikupa Chakula .?

Shahidi: ni sahihi

WS: Ni Chakula gani

Shahidi: Ugali na Mboga za Majani

WS: na wakati wote ulipokuwa pale hukufanyiwa Mateso

Shahidi: Sahihi

WS: na hata ulipokuwa Mbweni hakuna aliyekuja Kukupiga..?

Shahidi: ni sahihi

WS: Alipokuja Ramadhani Kingai alipokutaka Uthibitishe Maelezo yako na Kutia Sahihi alikupa Vitisho wala hakukupiga.?

Shahidi: ni sahihi

WS: ni Lipi Mahakama ichukue kati ya haya Mawili, Ulieleza Mahakama kwamba Wakati unatoa Maelezo hapa Mahakamani, kwamba ulitoa Maelezo kwa sababu ulikuwa unateswa, Sasa unasema kwamba Kingai na wenzake hawakukupatia Mateso isipokuwa Walipa Vitisho tuh

Shahidi: Rudia swali lako

WS: Wakati wa Kesi Kubwa Umesema Kuwa Kingai wenzake walichukua Maelezo yangu baada ya Mateso,Leo unasema Alikuja Bwana Kingai kunitishia

Shahidi: umeuliza wakati wa Kuchukuliwa Maelezo, Mimi wakati wote nilikuwa Chini ya Mateso

Mallya: OBJECTION Naomba Shahidi akiwa anatoa Maelezo yake apewe nafasi ya Kumaliza Kujibu Maswali

WS: Ulipokuwa Dar es salaam hukuteswa isipokuwa Bwana Kingai alikutishia.?

Shahidi: Wakili anauliza na Kunilisha maneno ambayo mimi Mwanzo sikujibu hivyo.... Aliniuliza kuhusu Kupigwa siyo Kuhusu mateso,kwa sababu, Mimi nilikuwa Chini yao na Nimefungwa pingu, Bado hayo kwangu ni Mateso

Jaji: Shahidi nafikiri ungejibu sasa hilo unalotaka wala hakuna tatizo kwamba uliteswa au lah

Jaji: naweza kukusomea

Shahidi: ningependa unisomee Mheshimiwa Jaji

Jaji: Kingai "Hakunipiga tulipokuwa Mbweni,alinipiga na Kunitishia" Sasa tuambie nini kilichokuwa kimetokea

WS: sasa nafikiri umeelewa, Kwamba Ulitoa Maelezo Yako baada ya Kuteswa na Sasa unasema baada ya kuteswa

Shahidi: miye ananihoji Machaguo ambayo mimi sikuyasema

Jaji: nafikiri Wakili sasa unaweza Kubadirisha swali

Jaji: Mallya tusaidie hapo tafsiri yake ni nini

Mallya: Kupiga ni Kitu Kidogo katika Jambo Kubwa Mateso,Unaweza Usipigwe na Ukawa upo wenye Mateso

Jaji: Mawakili wa pande zote Mbili nisaidieni hapo

WS: Mahakama ichukue kwamba Dar es salaam Hakupigwa

Kibatala: Siyo kwa Nia mbaya lakini wakili Mwenzangu Kakosa mbinu na ulewa

Jaji: Sitaki Muingie Kwenye Malumbano

Jaji: nitamuhoji Shahidi Mwenyewe, Je ungependa tuandike Kuwa Dar es salaam hukupigwa.?

Shahidi: ndiyo Dar es salaam Sikupigwa

WS: shahidi kwahiyo tuchukue kuwa Maelezo ulichukuliwa baada ya Mateso, Chini ya Kingai na Leo unatuambia ulitishwa..?

Shahidi: sijaelewa Swali

Jaji: Maelezo yanayobishaniwa,Maelezo yalichukuliwa Nje ya Muda,Je ulitoa hayo Maelezo lakini kwa mateso.?

Jaji: Picha ninayopata leo hukutoa Maelezo ila ulisaini tuh

Shahidi: sahihi ninazungumzia kuwa niliteswa na Kuning'inizwa kama Popo au Mshikaki

WS: Shahidi ulieza Mahakama Bw Kingai Alikutesa na Kutokana na Mateso hayo ulilazimika Kutoa Maelezo, Sasa unasema Bw Kingai sikutia Maelezo kwake alikuja na karatasi yake akanitaka nisaini na kujaza sehemu ya Kuthibitisha,Kipi unachoeleza sahihi.

Shahidi: Vyote ichukue

WS: Kwa hiyo Mahakama ichukue Vyote

Jaji: sasa niandike Vipi Hukutoa Maelezo na Ulitoa Maelezo .?

Shahidi: Ananiuliza Mambo Mawili tofauti ambayo ajayatenganisha, Mimi nilitoa Maelezo Moshi Chini ya Mateso,nalisaini bila Mateso

Jaji: Nilisaini Maelezo bila Mateso lakini nisaini baada ya Vitisho

WS: ni sahihi Mheshimiwa Jaji

Mahakama Kichekooooooo


WS: Kabla ya Kuletwa Dar es salaam tarehe 07,Kabla ya siku hiyo uliwahi Kufika Dar es salaam.?

Shahidi: ndiyo

WS: Makazi yako yapo Dar es salaam.?

Shahidi: Hapana

WS: unafahamu wapi

Shahidi: Kambi ya Jeshi Twalipo na Maeneo ya Uwanja wa Taifa

WS: Ujawahi Kufika Tazara.?

Shahidi: ndiyo

WS: Ulishawahi Kufika Mbweni

Shahidi: Hapana

Jaji: kwa hiyo Kabla ya kesi hujawahi kufika Tazara wala Mbweni

Shahidi: Ndiyo

WWSS: Hakuna Wakati ,unafikishwa Kituo cha Polisi wakakuacha wazi.?

Shahidi: sijawahi Kutolewa nje ya kituo cha Polisi

Jaji: Mnaeleeana kweli..? Kutoka Tazara kwenda Mbweni ulifungwa Jacket.?

Shahidi: nilifungwa Jacket Usoni Mheshimiwa

Jaji: wakili ulimaanisha hivyo.?

WS: Ndiyo Mheshimiwa

Jaji: sasa nitaomba Mnapomtajia Vituo vya Polisi Mtaje na Majina


WS: Naanza Upya Ulitolewa kitambaa ama Jacket lako ulipofilishwa ndani ya Kituo cha Tazara

Shahidi: Ndiyo

WS: Wakili wa Serikali Mpaka Unaingia Kituo cha Polisi Tazara ulikuwa umefungwa Usoni

Shahidi: Ndiyo

WS: Moshi Mlikamatwa wangapi

Shahidi: tulikamatwa wawili

WS: na nani.?

Shahidi: na Mohammed Abdilah Ling'wenya

WS: wakati wote unasafirishwa hukujua yupo wapi

Shahidi: Ndiyo

WS: Kingai na Mwenzake Mahita,walieleza Mahakama kwamba waliwasafirisha wewe na Ling'wenya Kwenye gari moja

Shahidi: kweli walitoa Ushahidi huo

WS: Hakuna Mtu aliyewaambia Mashahidi wale kuwa Si kweli Nyie hamkusafirishwa pamoja.?

Shahidi: sasaaaaa

WS: Jibu swali langu

Jaji: Je ulisikia au Hukusikia.?

Shahidi: Sikusikia

WS: Kama wakati wote unasafirishwa Mpaka unafikishwa Kituo cha Polisi Tazara ulikuwa hufahamu Mohammed Abdilah Ling'wenya yupo wapi,Kweli au si Kweli

Shahidi: Sahihi

WS: Ulikuwa peke yako Kwenye mahabusu

Shahidi: nilikuwa peke yangu kwenye Chumba Changu,ila Mahabusu wengine walikuwa Kwenye Vyumba vyao

Jaji: kwa hiyo ulikuwa Mwenyewe Kwenye Chumba cha Mahabusu..?

Shahidi: Ndiyo

Jaji: hapakuwa na Mahabusu wengine..?

Shahidi: Walikwepo kwenye Vyumba vyao

Jaji: hapa naona tusingeelewana

Mallya: Shahidi alitupa Picha Kuwa kuna mahabusu Yenye Vyumba Vidogo Vidogo na yeye alikuwa kwenye kichumba Chake ndani ya mahabusu

Jaji: naomba Kusoma "Nilifunguliwa Jacket nikawa naona Sasa,nikajivuta hadi Mlangoni nikaanza kuona Mahabusu wengine wakiwa kwenye Vyumba Vyao" nafikiri ndicho nilicho andika

Jaji: sasa tujielekeze Hapo

WS: Umesema ulikuwa Peke yako Kwenye Chumba

Shahidi: Ndiyo

WS: Kushoto na Kulia palikuwa na Ukuta

Shahidi: ni sahihi Kabisa

WS: Ulikuwa kwenye tafakari kwanini haya yananiyokea,nimekosa nini.?

Shahidi: ni Ukweli

WS: Ulikuwa unaugulia Maumivu huku ukitafakari,Kweli au si kweli

Shahidi: Kweli

WS: Nikujeresha Moshi,Unasema walikuning'iniza Kama Mishikaki Kwenye Bomba

Shahidi: Kweli

WS: Ulikuwa unaeleaelea ukiwa Juu

Shahidi: Kweli

WS: Walikuwa wanakupiga Maeneo gani ya Mwili wako

Shahidi: Kwenye Magoti na Kwenye Unyayo

WS: Mara ngapi.?

Shahidi: Mara nyingi

WS: alikuwa anatumia Nguvu kubwa sana

Shahidi: kweli

WS: Walikuwa wanakupiga kwa Kutumia nini.?

Shahidi: Rungu la Chuma

WS: walikuvunjavunja magoti.?

Shahidi: hapana

WS: Eeenhee wewe si Komandooo Bwana awawezi Kukuvunja,Umefuzu sana Bwana

Jaji:Naomba Mawakili kama kuna lolote msinong'one tufuate utamaduni wetu Jaji nafikiri Wakili wa Serikali Umeelewa swala la wakili Mwenzako

WS: ni swali tuh Mheshimiwa Jaji

Jaji: ulikuwa uulizi Swali ulikuwa unaweka Maoni yako

WS: sawa Mheshimiwa Jaji

WS: Kutokuvunjika kwako ni kwa sababu umefuzu Mafunzo ya Ukomando

Shahidi: Sahihi

WS: kutokana na Ukomandoo wako na Kufuzu kwako hukuona haja ya kwenda Hospitali

Shahidi: siyo sahihi

WS: Umeeleza walikuwa wanakupiga kwa kutumia nini

Shahidi: nishaeleza ni Rungu la Chuma

WS: alikupiga mara ngapi

Shahidi: Sikumbuki

WS: Zaidi ya amara 10

Shahidi: Ndiyo

WS: Walikutesa kwa muda gani

Shahidi: sikumbuki,maana walikuwa wananipiga na Kuniacha wakipumzika wanarudi tena

WS: nyayo zilivunjika.?

Shahidi: Hapana

WS: Baada ya Kukupofa kwenye Nyayo ulimba

Shahidi: Ndiyo

WS: ulipatwa na lengelenge

Shahidi: lengelenge na Kuvilia ni Kitu gani

WS: yote ni hayohayo, Ulipofika Tazara uliweza kutembea..?

Shahidi: Kwa tabu sana

WS: anawafuata wenzie wananong'ona

WS: ulieleza Mahakama kuna Ugonjwa uliupata Ulipokuwa Jeshini,ni Ugonjwa gani

Shahidi: Battle Confusion

WS: Ulisema ulitibiwa Lugalo ukapata nafuu

Shahidi: kiasi chake

WS: Walikupa Dawa za Kuwa unameza

Shahidi: nilikuwa napewa nilipokuwa pale

WS: uliporuhusiwa ulirudi Moja kwa moja kwenye kituo chako cha Kazi

Shahidi: ni sahihi

WS: Ulirudi kwa Muda gani

Shahidi: Kwa amuda wa Miezi Miwili

Jaji: Miezi miwili ya nini​
 
Si tu hlo , limeibuka lingine kuwa shahidi adamoo alikubali na kusaini kuwa aliachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu, na kwa mujibu wa maelekezo yake aliachishwa kwa sababu ya battle confusion na si utovu wa nidhamu!
Hapo ndio wamejichanganya,sababu Mahakama inaweza kuomba taarifa kutoka Jeshini.
 
Sidhani,ndio maana nasema jeshi watatoa taarifa ya ukweli.
1. Kwanini iwe Jeshi? Kwani aliyekuwa mwajiri wa Adamoo (JWTZ) ambayo ni taasisi ya umma yenye taratibu za kisheria za ku - HIRE, FIRE and SUSPEND ingewezaje kumsimamisha au kumfukuza kazi mwajiriwa/askari wake bila kumtaarifu kwa maandishi na sababu za kufukuzwa kwake..?

2. That means, lazima lazima Adamoo ana barua ya kuachichwa kwake kazi ya uaskari jeshini. Kwa hiyo haihitajiki hata kuomba taarifa kwa CDF kwa sbb evidence kwamba Adamoo aliachichwa kazi kwa sababu yoyote anayo yeye anayejitetea...

Kama JWTZ lilimwachisha kazi Adamoo kwa sababu yoyote ile bila ya kumwandikia suspension/dismissal letter inayoeleza sababu ya kuachichishwa kwake kazi ya uaskari, basi hilo ni tatizo jingine kabisa na tena ni kubwa linaloweza kuathiri kesi yote hii na kuipa sura nyingine kabisa...!!!
 
Mashaidi wa utetezi (Chadema) wanajigongagonga kweli. Yaani anasema Jaji aandike aliteswa na hakuteswa, vyote kwa pamoja!!! Wahesabu maaumivu kwa ushahidi huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…