Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
- Thread starter
- #41
Kingai ni askari duni sanaJamani leo vipi? Martin alikuwa anatafutwa nadhani imekuwa shida kidogo, let us wait and see
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kingai ni askari duni sanaJamani leo vipi? Martin alikuwa anatafutwa nadhani imekuwa shida kidogo, let us wait and see
Kwa maelezo yake mashitaka yote ya awali aliyakana - alisanishwa na Kingai bila kujua nini kilichomo ndani baada ya mateso makali ya kufungwa ka mshikaki .Si tu hlo , limeibuka lingine kuwa shahidi adamoo alikubali na kusaini kuwa aliachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu, na kwa mujibu wa maelekezo yake aliachishwa kwa sababu ya battle confusion na si utovu wa nidhamu!
Hakuna dada ,Mungu ni wetu sote siyo wa CCM tu.Hata Lema ,Sugu na Mdude Chadema walipigwa mvua kadhaa hatukuwa nacha kufanya.Hata uchaguzi serikali za mitaa tulipigwa na hatukufanya kitu.Hata uchaguzi wa madiwani ,Ubunge na Raia tulipigwa mvua na hatukufanya kitu.MUNGU ATUSAIDIE TU
Kiongozi wetu,mbona updates hakuna nini kimetokea huku?Kingai ni askari duni sana
[emoji28][emoji28]Usiseme tu shahidi, sema yule shahidi kibaka.
updates mbona zipo ! JF haijawahi kushindwaKiongozi wetu,mbona updates hakuna nini kimetokea huku?
Hivi mama anajiskiaje akona haya ambayo ana uhakika ni kusingiziwa. Hata Mtume (SAW) hamuogopi kweli?updates mbona zipo ! JF haijawahi kushindwa
View attachment 1954568View attachment 1954569View attachment 1954570
Unaijua nguvu ya PGO wewe ?Kwann serikali haitaki wananchi tupate mfululizo wa hii kesi wanaogopa nn?
Ni kwa vile ni kesi ya kubumba, uongo ndiyo maana wanasumbua watu wasisikilize...ingelikuwa ukweli wasingelishughulika na upuuzi wa kuwakataza watuKwann serikali haitaki wananchi tupate mfululizo wa hii kesi wanaogopa nn?
ha ha ha haWakili wa Serikali Wewe huwa unatesa watu.?
Shahidi Sijawahi
Wakili wa Serikali Ukiwa umekamata Adui ukamfunga Pingu utakuwa umemtesa
Shahidi Utakuwa hujamtesa,Ndiyo maana umemuita Adui
Hapo ndio wamejichanganya,sababu Mahakama inaweza kuomba taarifa kutoka Jeshini.Si tu hlo , limeibuka lingine kuwa shahidi adamoo alikubali na kusaini kuwa aliachishwa kazi kwa utovu wa nidhamu, na kwa mujibu wa maelekezo yake aliachishwa kwa sababu ya battle confusion na si utovu wa nidhamu!
Unadhani Jeshi wanaweza kupika taarifa?Hapo ndio wamejichanganya,sababu Mahakama inaweza kuomba taarifa kutoka Jeshini.
Sidhani,ndio maana nasema jeshi watatoa taarifa ya ukweli.Unadhani Jeshi wanaweza kupika taarifa?
HawashindwiiUnadhani Jeshi wanaweza kupika taarifa?
Basi itakuwa aibu na fedheha kubwa sana kwa Jeshi kushiriki upuuziHawashindwii
1. Kwanini iwe Jeshi? Kwani aliyekuwa mwajiri wa Adamoo (JWTZ) ambayo ni taasisi ya umma yenye taratibu za kisheria za ku - HIRE, FIRE and SUSPEND ingewezaje kumsimamisha au kumfukuza kazi mwajiriwa/askari wake bila kumtaarifu kwa maandishi na sababu za kufukuzwa kwake..?Sidhani,ndio maana nasema jeshi watatoa taarifa ya ukweli.
Mashaidi wa utetezi (Chadema) wanajigongagonga kweli. Yaani anasema Jaji aandike aliteswa na hakuteswa, vyote kwa pamoja!!! Wahesabu maaumivu kwa ushahidi huuLeo tena kama kawaida tunakuletea moja kwa moja yanayojiri kwenye Mahakama kuu , divisheni ya Uhujumu Uchumi , ambako kesi ya ugaidi unaogharimu kitita cha tsh laki 6 inaendelea.
---
Jaji ameshaingia
Kesi inatajwa
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire, Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili Kidando anatambulisha Jopo lake....
- Robert Kidando
- Nassoro Katuga
- Ignas Mwanuka
- Esther Martin
- Tulumanywa Majigo
Wakili Kibatala anatambulisha Jopo lake
Kwa Mshtakiwa wa Kwanza - Nashon Nkungu
- Adv Peter Kibatala
- Adv Sisty Aloyce
- Adv Gaston Garubindi
- Adv Idd Msawanga
- Adv Alex Massaba
- Adv Evaresta Kisanga
- Adv Hadija Aron
- Adv Michael Mwangasa
- Adv Faraji Mangula
- Adv Fredrick Kiwhelo
- Adv Nashon Nkungu
- Adv Jonathan Mndeme
- Adv John Mallya
Mshitakiwa wa Pili - John Mallya
Mshitakiwa wa tatu - Fredrick Kiwhelo
Mawakili Wengine wote ni Kwa mshitakiwa wa Nne Freeman Mbowe
Jaji: Siku ya Ijumaa shahidi( Mshtakiwa wa pili) alikuwa hajakamilisha Utetezi wake. Arejee kwenye Kizimba tuweze Kuendelea
Shahidi anaenda
Jaji: Wakili wa Serikali mpo tayari..?
Jaji: Upande wa Utetezi mpo tayari?
Wote wapo tayari
Jaji: Shahidi bado upo chini ya Kiapo kama tulivyokuapisha Siku ya Ijumaa. Mawakili wa Serikali watakuhoji Maswali na Baadae Upande wa Utetezi hususani Wakili wako anaweza kuja kukuongoza tena Kwa Kukuuliza Maswali. Unaweza kuchagua Kukaa au Kusimama
Shahidi: Nitakaa Mheshimiwa Jaji
Jaji: Bila shaka. Wakili wa Serikali Chavula unaendelea. Tafadhali endelea
Wakili wa Serikali: Naam Mheshimiwa
Wakili wa Serikali: Awali siku ya Ijumaa kabla hatujaahirisha, nilikuuuliza kuhusiana na wale waliokuvamia maeneo ya Rau hawakupata kujitambulisha, Kweli au Si Kweli
Shahidi: Kweli
Wakili wa Serikali: Wale watu Mlivyotoka pale kwenda Kituo cha Polisi hawakulueleza Majina yao akina nani.? Kweli au Si Kweli
Shahidi: Kweli
Wakili wa Serikali: Walivyokutoa Moshi kukuleta Dar es salaam hawakukueleza wao Majina yao ni Akina nani. Walipokupeleka Mbweni hawakukueleza Majina yao akina nani?
Shahidi: Kweli hawakunieleza
Wakili wa Serikali: Haukupata Kuwafahamu amajina yao wakati wote?
Shahidi: Niliwafahamu kwa wao alipokuwa wanaitana Majina yao na Nikaja kuthibitisha Majina yao hapa Mahakamani walipojitambulisha
Wakili wa Serikali: Wakati wa Kukusafirisha Moshi Kuja Dar es salaam Watu wale walikufunga Kitambaa Usoni?
Shahidi: ni Sahihi
Wakili wa Serikali: ni Jacket, Si Ndiyo?
Shahidi: ni Jacket ndiyo
Wakili wa Serikali: Hukujua ni akina nani unasafiri nao
Shahidi: Kweli kama nilivyoeleza
Wakili wa Serikali: Na hata Ulipofika Dar es salaam ukafikishwa Kituo cha Kwanza cha Polisi hukujua upo wapi
Wakili wa Serikali: We Jibu swali langu Kweli au si Kweli
Shahidi: Kweli
Wakili wa Serikali: Umedai ulipokuwa unasafirishwa Ulikalishwa Chini kwenye gari,Kweli au si kweli
Shahidi: Ni kweli
Wakili wa Serikali: Uliweza Kujua ni sehemu gani ya gari ..?
Shahidi: Nilipita Upande wa Kulia Kwa Uelewa wangu siyo Kwa Kuona, Nikafahamu nimekaa nyuma ya gari
Wakili wa Serikali: Ulikaa nyuma ya gari
Shahidi: Ndani ya gari,Sehemu ya Nyuma
Shahidi: Siwezi Kujua ni gari gani
Wakili wa Serikali: Unakubaliana na Mimi ukiwa Umefungwa Machoni uwezi Kuona .?
Shahidi: Ndiyo uwezi Kuona, ila ukiwa unatendewa unahisi
Wakili wa Serikali: Ukiwa umefungwa macho uwezi kuona hata kile kifaa wanachokusababishia Maumivu
Shahidi: Ni sahihi
Wakili wa Serikali: Nakurudisha Moshi,umesema walipokuwa wanakutesa Moshi walikuwa wabakuuliza Umekuja Moshi Kufanya nini
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: Wewe Ukajibu umekuja Moshi Kufanya VIP protection ni Sahihi
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: Ulisema ulipofika Dar es salaam kituo cha kwanza cha Polisi walikupa Chakula .?
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: Ni Chakula gani
Shahidi: Ugali na Mboga za Majani
Wakili wa Serikali: na wakati wote ulipokuwa pale hukufanyiwa Mateso
Shahidi: Sahihi
Wakili wa Serikali: na hata ulipokuwa Mbweni hakuna aliyekuja Kukupiga..?
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: Alipokuja Ramadhani Kingai alipolutaka Uthibitishe Marlezo yako na Kutia Sahihi alikupa Vitisho wala hakukupiga.?
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: Ni Lipi Mahakama ichukue kati ya haya Mawili,Ulielezq Mahakama kwamba Wakati unatoa Maelezo hapa Mahakamani,kwamba ulitoa Maelezo kwa sababu ulikuwa unateswa,Sasa unasema kwamba Kingai na wenzake hawakukupatia Mateso isipokuwa Walipa Vitisho tuh
Shahidi: Rudia swali lako
Wakili wa Serikali: Wakati wa Kesi Kubwa Umesema Kuwa Kingai wenzake walichukua Maelezo yangu baada ya Mateso,Leo unasema Alikuja Bwana Kingai kunitishia
Shahidi: Umeuliza wakati wa Kuchukuliwa Maelezo, Mimi wakati wote nilikuwa Chini ya Mateso
Wakili wa Serikali: Aahaaaaaa
Wakili Mallya: OBJECTION. Naomba Shahidi akiwa anatoa Maelezo yake apewe nafasi ya Kumaliza Kujibu Maswali
Wakili wa Serikali: Ulipokuwa Dar es Salaam hukuteswa isipokuwa Bwana Kingai alikutishia.?
Shahidi: Aliniuliza kuhusu Kupigwa siyo Kuhusu mateso,kwa sababu, Mimi nilikuwa Chini yao na Nimefungwa pingu, bado hayo kwangu ni Mateso
Jaji: Shahidi nafikiri ungejibu sasa hilo unalotaka wala hakuna tatizo kwamba uliteswa au lah
Jaji: Naweza kukusomea
Shahidi: Ningependa unisomee Mheshimiwa Jaji
Jaji: Kingai "Hakunipiga tulipokuwa Mbweni, alinipiga na Kunitishia" Sasa tuambie nini kilichokuwa kimetokea
Shahidi: Vyote vichukue
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Mahakama ichukue Vyote
Jaji: Sasa niandike vipi Hukutoa Maelezo na Ulitoa Maelezo ..?
Shahidi: Ananiuliza Mambo Mawili tofauti ambayo ajayatenganisha, Mimi nilitoa Maelezo Moshi Chini ya Mateso,nalisaini bila Mateso
Jaji: Nilisaini Maelezo bila Mateso lakini nisaini baada ya Vitisho
Shahidi: ni sahihi Mheshimiwa Jaji
Mahakama Kichekooooooo
Wakili wa Serikali: Kabla ya Kuletwa Dar es salaam tarehe 07,Kabla ya siku hiyo uliwahi Kufika Dar es salaam.?
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Makazi yako yapo Dar es salaam.?
Shahidi: Hapana
Wakili wa Serikali: unafahamu wapi?
Shahidi: Kambi ya Jeshi Twalipo na Maeneo ya Uwanja wa Taifa
Wakili wa Serikali: Ujawahi Kufika Tazara.?
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Ulishawahi Kufika Mbweni
Shahidi: Hapana
Jaji: Kwa hiyo Kabla ya kesi ujawahi kufika Tazara wala Mbweni
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Hakuna Wakati ,unafikishwa Kituo cha Polisi wakakuacha wazi.?
Shahidi sijwahi Kutolewa nje ya kituo cha Polisi
Jaji Mnaeleeana kweli..?
Jaji Kutoka Tazara kwenda Mbweni ulifungwa Jacket.?
Shahidi nilifungwa Jacket Usoni Mheshimiwa
wakili ulimaanisha hivyo.?
Wakili wa Serikali Ndiyo Mheshimiwa
Jaji sasa nitaomba Mnapomtajia Vituo vya Polisi Mtaje na Majina
Wakili wa Serikali Naanza Upya Ulitolewa akitambaa ama Jacket lako ulipofilishwa ndani ya Kituo cha Tazara
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali Mpaka Unaingia Kituo cha Polisi Tazara ulikuwa umefungwa Usoni
Wakili wa Serikali Moshi Mlikamatwa wangapi
Shahidi tulikamatwa wawili
Wakili wa Serikali na nani.?
Shahidi na Mohammed Abdilah Ling'wenya
Wakili wa Serikali wakati wote unasafirishwa hukujua yupo wapi
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali Kingai na Mwenzake Mahita,walieleza Mahakama kwamba waliwasafirisha wewe na Ling'wenya Kwenye gari moja
Shahidi kweli walitoa Ushahidi huo
Wakili wa Serikali Hakuna Mtu aliyewaambia Mashahidi wale kuwa Si kweli Nyie hamkusafirishwa pamoja.?
Shahidi sasaaaaa
Wakili wa Serikali Jibu swali langu
Jaji Je ulisikia au Hukusikia.?
Shahidi Sikusikia
Wakili wa Serikali Kama wakatibwote unasafirishwa Mpaka unafikishwa Kituo cha Polisi Tazara ulikuwa hufahamu Mohammed Abdilah Ling'wenya yupo wapi,Kweli au si Kweli
Shahidi Sahihi
Wakili wa Serikali Ulikuwa peke yako Kwenye mahabusu
Shahidi nilikuwa peke yangu kwenye Chumba Changu,ila Mahabusu wengine walikuwa Kwenye Vyumba vyao
Jaji kwa hiyo ulikuwa Mwenyewe Kwenye Chumba cha Mahabusu..?
Shahidi Ndiyo
Jaji hapakuwa na Mahabusu wengine..?
Walikwepo kwenye Vyumba vyao
Jaji hapa naona tusingeelewana
Mallya Shahidi alitupa Picha Kuwa kuna mahabusu Yenye Vyumba Vidogo Vidogo na yeye alikuwa kwenye kichumba Chake ndani ya mahabusu
Jaji naomba Kusoma "Nilifunguliwa Jacket nikawa naona Sasa,nikajivutq hadi Mlangoni nikaanza akuona Mahabusu wengime wakiwa kwenye Vyumba Vyao" nafikiri ndicho nilicho andika
Jaji sasa tujielekeze Hapo
Wakili wa Serikali Umesema ulikuwa Peke yako Kwenye Chumba
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali Kushoto na Kulia palikuwa na Ukuta
Shahidi ni sahihi Kabisa
Wakili wa Serikali Ulikuwa kwenye tafakari kwanini haya yananiyokea,nimekosa nini.?
washitakiwa 1,2,na 3 walikubali wanafahamianina wa wakiwa wanafanya kazi Ngerengere KJ92
Wahitakiwa 1,2, na 3 Walikuwa wanafahamiana kabla ya Kesi Kuanza
Wakili wa Serikali Hukubisha kwamba kwamba hukuondolewa Jeshini kwa Maswala ya Kinidhamu, na asasa unasema Uliondolewa Jeshini kwa Maswala ya Afya
Shahidi Siwezi kulijibia
wakili wa Serikali Kwanini uwezi Kulijibia
Shahidi Documents zote sijawahi kuzitolea Maelezo, zilikuja na kuletwa na watu walioandaa
Wakili wa Serikali Documents zipi hizi
Shahidi zilioletwa Kufungulia Kesi ya Ugaidi
Wakili wa Serikali Ulisaini hukusoma.?
Shahidi nilisaini
Wakili wa Serikali Na Mahakama ilikusomea.?
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali Unasema Ulikuwa kwenye Misheni Congo
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali Ulikuwa Battalion ya 3
Wakili wa Serikali wewe ulikuwa kikosi cha Mizinga
Shahidi Hapana
Wakili wa Serikali Wewe ulikuwa unafanya nini
Shahidi nilikuwa Special Force
Wakili wa Serikali Huko Special Force ulikuwa unafanya kazi gani
Shahidi Kazi zote
Wakili wa Serikali Zitaje
Shahidi zote kuanzia kupika Mpaka Kwenda Vitani
Wakili wa Serikali Huko Vitani huwa mnajihusisha na Kuteka Watu
Shahidi siyo kazi Yangu kuzungumzia Maswala ya Vita
Wakili wa Serikali lakini Vitani huwa watu wanatekwa
Shahidi Ukingalia kwenye Muvi wanatekwa ila Mimi ya Vitani siwezi kuyaeleza,Kuna watu wake Maalum wa Kuyaeleza
Wakili wa Serikali Moja ya kazi ni Kulinda Lindo,mnalinda dhidi ya nani
Shahidi dhidi ya Adui
Wakili wa Serikali unapoluwa umemkamata Mtu lindo Moja ya jambo ni Kumfunga pingu ili asitoroke
Shahidi Kweli
Wakili wa Serikali kweli kwa sababu Mmeyafanya huko Vitani
Wakili wa Serikali anaongea na Jopo lao
Wakili wa Serikali Wewe huwa unatesa watu.?
Shahidi Sijawahi
Wakili wa Serikali Ukiwa umekamata Adui ukamfunga Pingu utakuwa umemtesa
Shahidi Utakuwa hujamtesa,Ndiyo maana umemuita Adui
Wakili wa Serikali Naomba kuwaachia wenzangu
Jaji nawakumbusha tuna Fakika 20 Kabla hatuja break
Wakili wa Serikali 2 Mheshimiwa mimi ninayo Machache kati ya mengi yaliyoulizwa na Mwenzangu
Jaji labda nimuulize Shahidi Mwenyewe,Unanguvu au tunaweza kuendelea na Maswali
Shahidi Tuendelee Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali 02 Wakati umeanza kuulizwa na Wakili wa Serikali umeongea Ukweli,Tunaomba uendelee kusema Ukwei
Wakili wa Serikali 02 wakati unakamatwa Ling'wenya ,je yeye alikuwa umbali gani
Shahidi alikuwa karibu yangu,Sababu nilikuwa Pembeni naongea na Simu
Wakili wa Serikali 02 Umesema Ling'wenya alishuhudia wakati Unawekewa Madawa ya Kulevya
Shahidi siyo yeye tuh watu wote waliona kwa Sababu Jambo hilo lilifanyika hadharani mbele za watu
Wakili wa Serikali 02 kati yako wewe na Ling'wenya nani Mtaalamu wa Madawa ya Kulevya
Shahidi hakuna,Swala la Madawa walisema wao Wenyewe kuwa "Tumemkuta na Madawa ya kulevya"
Wakili wa Serikali 2 Kwenye ushahidi wako wako ulisema kuwa kuhusiana na Swala la kusaini hati yakukabidhi vitu vyako
Shahidi Siku sema
wakili wa Serikali 02 ulimuonyesha jaji Kuhusu makovu, Je unamakovu Mangapi
Shahidi Mengine yapo kichwani
Wakili wa Serikali 02 Uliiambia Mahakama kuwa makovu haya amengine yatofautishwale na Miguuni
Shahidi Mahakama haikuuliza,Kuwa hayo Mengine yametokana na nini
Wakili wa Serikali 02 amahakama itatofautishaje sasa
Shahidi hiyo ni kazi ya Mahakama siwezi kuifundisha
Wakili wa Serikali 02 Ulipokuwa Mbweni Kuna Askari alikwambai Upo Mbweni Baada ya Kuwaonea Huruma
Shahidi Ndiyo
wakili wa Serikali 02 huyo wa Pili aliyekuwa anasema huyo Askari ni nani.?
Shahidi Mohammed Abdilah Ling'wenya
Wakili wa Serikali 02 kumbe mlikuwa naye na Mkaonana Mbweni
Shahidi Kujua tupo naye nilijua nimesema,Sikuwahi Kumuona kwa macho
Wakili wa Serikali 02 Umeiambia Mahakama aliyekupiga Rungu Moshi ni nani
Shahidi Sikuwa namfahamu
Wakili wa Serikali 02 Maelezo aliyokuletea Bwana Kingai ukayasaini na Kuyathibitisha,Ukiyqona utayakumbuka.?
Shahidi Siwezi Kuyakumbuka,Kwa sababu sikuyasoma,Labda sehemu za sahihi yangu na nilipoandika
Wakili wa Serikali 02 awakati unateswa Moshi uliwajibu Kuwa umeenda kwa VIP PROTECTION ,ukawajibu upo kwenye mazungumzo
Shahidi ni Kweli
Wakili wa Serikali 02 Wakati Wakili Kibatala anakuuliza wakati wa Maelezo ulisema Ungeweza Kumuita Mwajiri wako
Shahidi Muajiri Mtarajiwa
Wakili wa Serikali 02 Kwa hiyo Mahakama iandike ujawahi na kuajiriwa na Mshitakiwa wa nne
Shahidi ni sahihi
Wakili wa Serikali 02 Kwahiyo nisahihi nikosema katika hayo Mazungumzo yenu mliwawahi Kufanyia Aishi Hotel
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali 02 Wakati mnafanya hayo Mazungumzo mlikuwa na Mshitakiwa wa 3.?
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali 02 Wakati Upo Tazara unasema uligudua kwa Vitu Viwili Kwa Honi ya Treni na Kuambiwa hiki ni kituo cha Kuhifadhia Watuhumiwa wa Ugaidi
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali 02 Ulishaiambia Mahakama Kwamba Unatuhumiwa kwa Ugaidi.?
Shahidi Hapana
Jaji Subiri Kidogo
Wakili wa Serikali 02 Ninaswali moja la Mwisho
Jaji sawa endelea
Wakili wa Serikali 02 wakati unachomwa na Bisibisi ushawahi kuiambia Mahakama walikuwa wanataka nini,kama vile Moshi walikuwa wanakuuliza Umefuata nini..?
Shahidi Hapana
Jaki sawa tunapumzika kwa Muda tutarejea Baada ya Dakika 20
Jaji ananyanyuka
Mahakama imerejea
Jaji Meingia Leo Mapema sana akuliko watu wengi na Watuhumiwa
Imebidi Jaji asubiri watuhumiwa waletwe
Kesi imetajwaa
Jaji nataka kuanza Utamaduni wa Kuanza Kuzingatia amuda
Nikisema naanza Saa 3 Mtanikuta humu
Nikisema tunaanza saa 3 itakuwa Saa 3 Kamili
Na Nikisema Saa 4 itakuwa Saa 4 Kamili
Itapendeza kama Tutazingatia Muda
Na huo ndiyo Ustaarabu,Ikitokea Mtu anadharula nijulishwe
Haipendezi kesi Ikianza milango inafunguliwa kila Saa
Jaji Upande wa Jamuhuri wapo tayari Kuendele.?
Utetezi.?
Shahidi.?
Wote wapo Tayari
Wakili wa Serikali 03 Wakati tukiendelea na hii Kesi tangu Mwanzoni na kingai,Mawakili wako na Ushahidi wako ulihojiwa Mantle Status ya akili yako,Ni kweli Jambo hili limejitokeza.?
Shahidi Nikweli limejitokeza.?
Wakili wa Serikali 03 kwa usahihi ukaita Battle Confusion.?
Shahidi ni sahihi
Wakili wa Serikali 03 Kama Kweli hali hiyo imejitokeza Moja ya Jambo ambalo litakukumba ni Kupoteza kuona mambo kwa usahihi.?
Shahidi Sijui
Wakili wa Serikali 03 Ujui kwa sababu Hukumbuki wakati Ukiwa na tatizo hilo nini kilikuwa kinakutokea.?
Shahidi Ndiyo
Wakili wa Serikali 03 Umewahi Kupoteza Uwezo wa watu unaowatambua au amaeneo unayoyafahamu.?
Shahidi Sijawahi
Wakili wa Serikali VipibKuhusiana kutambua Muda na Tarehe.? umewahi Kuwa na tatizo la Kuchanganya hivi vitu.?
Shahidi Hapana sijawahi
Wakili wa Serikali 03 Vipibkwenye Kuchukua Maamuzi Sahihi, Kwamba Umempiga Mtu bila Sababu alafu baadae ukaja Kukumbuka
Shahidi Hapana sijawahi Kufanya Maamuzi ya namna hiyo
Wakili wa Serikali 03 kwa sababu ya Jambo la Battle Confusion ujaeleza Kwanini lilikukuta
Shahidi nilieleza Mahakama kuwa tatizo hilo nililipata baada ya Kutoka Vitani
Wakili wa Serikali 03 Sababu ya Battle Confusion zipo Nyingi,utakubaliana na mimi
Shahidi Mimi siyo Mtaalamu
Wakili wa Serikali 03 Moja ya Sababu ya Kupata Battle Confusion ni Matumizi ya amadawa ya kulevya yaliyo Kithiri,Ni sawa.?
Shahidi Sababu zenu hizo siwezi Kuwabishia
Wakili wa Serikali 03 Katika Kipindi cha hili tatizo ulipangiwa kazi..?
Shahidi nilipangiwa kwenda Hospitali
Wakili wa Serikali Ilikuchukua Takribani Miezi 02 baada ya Kurudi Jeshini, kabla ya Kufukuzwa kazi kwa Sababu wewe uliendelea kutumia madawa ya kulevya
Shahidi Sijawahi Kutumia Madawa ya Kulevya
Wakili wa Serikali 03 Post Dramatic Disorder ni Kitu gani.?
Shahidi Sifahamu
Wakili wa Serikali 03 Kama ufahamu kuhusiana na Ugonjwa wa Post Dramatic Disorder limefikaje hapa Mahakamani,Umewahi Kumwambia nani
Shahidi Sijawahi Kumwambia Mtu
Wakili wa Serikali 03 Uataribu baada ya Kurudi kazini ulikuwaje
Shahidi Nilitakiwa Kuendelea kuriport Hospitali
Wakili wa Serikali 03 Kwa hiyo Ugonjwa huu ,umeathiri utimamu wa akili.?
Shahidi Hapana
Wakili wa Serikali Unasema ulienda Moshi Kufanya kazi ya VIP PROTECTION, Kile Kitabu chenye Orodha ya Mashahidi na Ushahidi wote we ulikipata.?
Shahidi Ndiyo ninacho
Wakili wa Serikali 03 Kuna Chochote Mshitakiwa wa nne amesema alikuita wewe na wenzako kwa ajili ya VIP PROTECTION.?
Shahidi Sijakiona
Wakili wa Serikali 03 kwa hiyo hili swala lako la VIP PROTECTION ajalisema,hata alipopewa nafasi ya kusema hakuwahi Kulisema popote
Shahidi Sijui yeyesasa,Miye niliulizwa ndiyo Maana nikajibu
Wakili wa Serikali 03 Ulipoluwa unahojiwa na Mawakili wa Serikali ulikuwa unachukua Muda Sana Kujibu,hata Wakati Mwingine Mheshimiwa Jaji alikuwa akitoa Mwongozo,Nikisema unauwezo Mdogo au Umeathirika kiakili
Shahidi kama wewe ni Daktari siwezi Kukubishia Uchunguzi wako,ila Miye nikikiwa nshindwa akujibu kwa haraka kwa sababu Maswali yanazunguuuuuka hayajanyooka
Wakili wa Serikali 03 Nipo sahihi nikisema hali ya Akili yako ipo sawasawa.?
Shahidi Upo sahihi
Wakili wa Serikali 03 Ujatueleza Umuhimu wa Kutuleza Utimamu wa kwanini Umeieleza Mahakama Ya tatizo la Akili kwa wakati Fulani
Shahidi nimeeleza Umuhimu, kwa Kufuatia Swali nililoulizwa Mahakamani
Wakili wa Serikali 03 inahusiano gani swala la Ugonjwa wako na Makosa ya Njama za Kutenda Ugaidi
Shahidi Kwangu naona Vinauhusiano kwa Sababu nimeulizwa na Mahakama,Isingekuwa na Umuhimu nisingeulizwa
Wakili wa Serikali 03 Je unajua umuhimu wa kwamba umewahi kupata Battle Confusion ..?
Shahidi Umuhimu unajua Mahakama yenyewe iliyouliza hilo swali
Wakili wa Serikali 03 Mheshimiwa Jaji naomba tukomee Hapa hakuna Swali Lingine
Jaji: Wakili Mallya kama Unamaswali ya marejeo
Malya Mheshimiwa Jaji ninayo Machache
Mallya Swali langu la Kwanza kwamba wewe Ni Komandoo umefundishwa kukaa na Njaa na Kuhimili Mateso, JE uelewa Wako ni nini katika Swali hili
Wakili wa Serikali 03 OBJECTION hilonswalo haliruhusiwi katil Re Examination, Yeye ange recall tuh katika yale aliyojibu katika Examination
Jaji Mallya Unakubaliana na alichosema Wakili wa Serikali
Mallya sababu ya Muda naomba ni Rudie Swali tuh
Jaji Hapana,Je umekubaliana naye
Mallya Sikubaliani naye lakini sababu ya Muda Nirudi swali tuh
Jaji Sasa hapo tulimalize kwanza kabla Ujaenda Mbali,Kuliko kwenda na Mambo ambayo Mtu hajaridhika nayo
Mallya Sijaja ja Swali Jipya napitia Maswali yale yale na majibu yaleyale
Jaji sawa unaweza ukaanza na Swali Mwanzoni
Mallya Swali langu la Kwanza kwamba wewe Ni Komandoo umefundishwa kukaa na Njaa na Kuhimili Mateso, JE uelewa Wako ni nini katika Swali hili
Shahidi Katika Upande wa Mafunzo unakanuni zake na taratibu zake na kwa Uolpande wa ukamataji wa watuhumiwa kuna Kanuni zake na Taratibu zake
Wakili wa Serikali OBJECTION
Jaji Subiri kwanza Shahidi ajibu kwanza tuone kama linahusika na Mnachotaka Kufanya Objection
Wakili wa Serikali Hakuna sehemu tuliyomuuliza kuhusiana na Kuvumilia Njaa
JAJI mliuliza nini Siku hiyo.?
Wakili wa Serikali Chavula,Katika Mafunzo yenu Mnafundishwa Kuvumilia Njaa.?
Jaji Kwanini uliuliza hilo swali,Ulilenga Ku Establish kitu gani
Wakili wa Serikali Nililenga Kuwa ni Mtu ambaye ni Trained na yale ya Kukaa na Njaa si Kitu kigeni kwake
Jaji sawa kaeni Chini nafikiri hakuna Kitu Kigeni kati ya amlichouliza ,kilichoulizwa na Kinachojibiwa
Namruhusu wakili Mallya Kuendelea
Mallya kwa uelewa wako kwanini uliulizwa swali hilo
Shahidi nimeelewa Kuwa akukaa na Njaa ni Haki kwangi,Kupitia Mateso ni Haki yangu na Kwamba Kukamatwa Bila kuzingatia Sheria ni Haki yangu kwa sababu tuh ni Vitu nilivyowahi Kupitia
Mallya Kuna sehemu umesema Ulipigwa na kuna sehemu Uliteswa mgawanyiko wa hili Jambo likoje
Shahidi Kupogwa ni sehemu ya mateso,Kutishiwa ni Sehemu ya mateso,Ndiyo maana nilisema anilipofika Dar es salaam nilikuwa bado nipo Ndani ya Mateso,
Kitendo Cha Kutolewa Kwenye Chumba na akuambiwa Kitakurudia kilichokutokea Moshi ni sehemu ya mateso wakati huo Comfortability yangu Imeshapotewa kwa sababu Nilikuwa nasimamiwa na Bastola
Na Vilevile Kitendo Cha Kushinda na Njaa ni Mateso pia
Kitendo Cha Kutolewa kituo Kimoja kimoja cha Polisi na Kupelekwa Kingime na Kubadirishiwa jina unalotambulika na Ulimwengu,Kwangu iliniathiri na Nikaona bado Nipo Chini ya mateso
Mallya Umeulizwa kumjua au Kumuona Mahabusu ya Tazara na Mbweni,ulipokuwa unasema Ulijua yupo ila sikumuona
Shahidi nilikuwa nakimaanisha alipokuwa Mahabusu Nyingine tuliweza kusalimiana hata kwa sauti ya Juu,Lakini siyo Kuonana Kwa face to face
Mallya Nia ya Kuonyesha Makovu ilikuwa ni nini.?
Shahidi Kwa sababu kuonyesha Kuwa baada Matendo yale yaliacha Alama za kuumia, ndiyo maana nikaonyesha Makovu
Mallya umeulizwa Pia Kuhusiana na Kupigwa ukiwa moshi na Kuwaona waliokutesa moshi kama uliwatambua au hukuwatambua
Shahidi Kwenye kile chumba nilichokuwa nateswa palikuwa na watu wengi,Wengine nilikuja kuwatambua mbele ya Mahakama na Mtu Mwingine sikuweza Kumfahamu
Mallya Uliulizwa kuhusiana Kutobolewa na Bisibisi Kwenye Makalio,.........
Wakili wa Serikali OBJECTION aulize Yaliyojitokeza kwenye Examination ,Hii kwamba elezea hiyo,Ni Mswali ambayo hayaruhiwi
Jaji Wakili Mallya
Mallya Re examination wajibu wake ni Kufanya Explanation
Jaji Nafikiri Wakili wa Serikali yupo sahihi,Unachouliza Unaacha ywanja Mpana wa Shahidi Kueleza Jambo Jipya badala Kuziba Mwanya wa Kilichoulizwa
Mallya Wale waliokuwa wanakuchoma Bisibisi, Walikuwa wanataka nini
Shahidi Ilikuwa ni sehemu ya Mateso
walikuwa wanasema Nyinyi si mmejifanya kutisaliti,Sasa Mtaona
Jaji Nafikiri sasa tunafungu Box kwa kile nilichokuwa naeleza
Mallya Mawakili wa Serikali alikuuliza Swali kwamba waliokuwa wanakuchoma bisibisi walitaka Kujua nini.?
Jaji Naona Mawakilibwa serikali wanataka mshauriane hapo,Inaruhusiwa
Mallya nitarudi baadae kwenye swali hilo,Je hapa Kwa ufahamu wako kinachoendelea Mahakamani ni Jambo gani
Shahidi ni Shauri dogo katika Shauri Kubwa
Jaji lile swali lako umeuliza kweli
Mallya nimeliweka Akiba nitalirejea
Mallya anaenda Kushauriana na Jopo lake
Mallya wakati wanakuchoma walikuwa wanataka nini
Shahidi Muendelezo wa Mateso
Mallya nafikiri nimemaliza
Shahidi (Mshitakiwa wa pili) Anatoka Kizimbani
JAJI wakili Malya endelea Uwanja ni Wako
Mallya tunae shahidi Mwingine
Mallya Mohammed Abdilah Ling'wenya
Jaji Jitambulishe
Shahidi Mohammed Abdilah Ling'wenya
Dini Muislamu
ajibThibitisha Wallah Billah taalah Natihibitisha mbele ya Mahakama hii Ushahidi nitakaotoa utakuwa ni Kweli tupu,Eeh Mwenyezi Mungu Nisaidie
Jaji tutapisha Hadhana alafu tutaendelea
Hadhana Inaendeleeeee
Jaji Wakili Kibatala Ulitaka Kuzingumza
Kibatala naomba nimtambulishe Wakili Dickson Matata kwa ajili ya Mshitakiwa watatu
Jaji sawa nakushukuru
Jaji Hapa Kuna Maelezo
Jaji kuna Shida Kumuita Msjitakiwa watatu kuwa Shahidi ,Serikali.?
Jaji Kiwhelo Kuna tatizo kwa Mshitakiwa wako kuwa Shahidi
Wakili Kiwhelo Hapana
Mallya Makazi yako kwa sasa hivi Kimara King'ong'o
Jaji Makazi yako kwa sasa hivi
Shahidi Natolea Gereza la Ukonga
Kabla ya Kukamatwa ulikuwa wapi
Shahidi Mtwara kampuni DOT kampuni ya kusaga Kokoto
Mallya Kabla ya hapo..?
Shahidi nilikuwa Ngorongoro
Mallya Unamfahamu Mshitakiwa wa 2
Shahidi Ndiyo
Mallya umemfahamu wapi.?
Jeshini KJ 92 JWTZ Ngerengere
Mallya Umeanza Lini
Shahidi Mwaka 2008 Mpaka 2017
Mallya Kazi gani ulikuwa unafanya .?
Shahidi Komandoo,Special Force
Mallya Unamfahamu Vipi Mshtakiwa wa Pili
Shahidi nilikuwa nipo Mtwara nikapigiwa Simu na Askari Mwenzangu ambaye nilikuwa nipo naye Jeshini anaitwa Dennis Urio
Kwamba Kuna kazi ya kwenda kumlinda Mtu bila kunitajia huyo Mtu ni nani
Nikamwambia asubiri nikifika Nyumbani aongee na Baba akikubali sawa
Nilipofika Nyumbani akapiga simu nikampa akaongea na Baba
Baba akauliza si unamfahamu,nikasema Ndiyo akaniambia nakuombea Dua nenda
Mallya Siku ya tarehe 05 Mwezi 08 2021 Maeneo ya Rau Madukani kulitokea kitugani
Shahidi Nilikuwa kwa Dada yangu Mmoja anaitwa Asma,akiwa Dukani kwake mimi na Adamoo tukawa tunasubiria Chakula
Mallya kilichokupeleka Rau Moshi ni kitu gani
Shahidi Tulikuwa tunaenda kukutana na Mwajiri wetu ilikuwe kukubaliana naye
Mallya Mshitakiwa wa pili alikuwa anafanya kitu gani
Shahidi Wakati nipo Dykani Kwenye Upenyo Coridor nikasikia Kelele sana,Nikatika niende Kuona
Nikakuta Adamoo ameshanyanyuliwa na Kukabwa
Nikauliza Tatizo ni nini.?
Nikashikwa Mkono wakaniuliza wewe Unamfahamu huyu
Mallya Ulipata Kujua ni akina nani.?
Shahidi Niliwaona kwa mara ya kwanza
Wakaniuliza unamfahamu huyu.?
Akatoka mwingine akasema anapistol anapistol anapistol
Alinyofoa Kutoka amwilini Kwa Adamoo Upande wa Kulia akasema anapistol anapistol akasema na madawa ya Kulevya anayo
Mallya eleza sasa Pistol anatoa wapi.?
Wakili wa Serikali OBJECTION anamfeed Majibu
Mallya baada ya kumkuta Adamoo amenyanyuliwa Juu kitu gani kiliendelea
ukisema alimtolea unataka Mahakama ipate apicha gani
Shahidi Baada ya Kuona Wanamfanyia Adamoo yale na Adamoo na Mfahamu na nilikuwa naye muda mrefu,Nikauvuta Mkono wangu kwa aliyekuwa amenishika
Nikawaambia Kuwa adamoo hakuwa na hivyo Vitu,nikatoa Simu na wallet nikaweza Kibarazani
Jaji Ulitoa simu na nini
Shahidi Simu na wallet
Mallya Kusema walimuwekea unamanisha nini.?
Shahidi Kwa Sababu nilianza Safari ya kwenda moshi na Adamoo Kuanzia Chalinze,Nafahamu hakuwa na Vitu hivyo
Nikasema huyu Mtu kwakuwa mmemuwekea na Mimi ngoja nitoe Vitu vyangu
Mallya: wakati huo Adamoo Yupo wapi
Shahidi: Wameshusha Chini ila wanampiga pale pale chini
Mallya: uliweka vitu vyako wapi,.?
Shahidi: waliochukua walikuwa ni Polisi
Mallya Kwenye wallet Kulikuwa na nini.?
Shahidi Palikuwa na Pesa.?
Mallya Kiasi gani.?
Shahidi Laki tatu
Mallya Zipo wapi
Shahidi Haoana sielewi
Mallya Waru waliomvamia Adamoo Unaweza Kujua walikuwa ni watu wangapi.?
Shahidi Walikuwa Zaidi ya watano
Mallya baada ya Kupanda gari Mmlielekea Wapi.?
Shahidi Central Moshi
Mallya Kichofuata nini.?
Shahidi Waliotuleta wakatoka,baada ya kutuacha
Walitutenganisha,Nakumbuka Mmoja alikuwa Askari Bonge nilimueleza Kuwa Mimi nilikuwa mwanajeshi
Wakauliza Kama nawajua Komba na msellemu.?
Jaji Komba ni Mtu Mwingine na Msellemu Mtu Mwingine
Mallya nini ulishihudia Kinacho muhusu Adamoo
Shahidi nilishihudia akiwa yeye ni wa Kwanza kuinginzwa Cello yake na Mimi nikawekwa Cello Nyingine
Mallya Walipomtoa Cello Ulionaje.?
Shahidi Cello ya Kwanza Ya Kwangu na Yapili,Wakati wanamuingiza Cello yake sikumuona ila wakati wanamtoa alikuja Mtu kwenye Cello yangu akaita Ling'wenya Nyuma yake wakampitisha amtu wamemuinamisha ,
Mallya Ulimtambuaje..?
Shahidi alikuwa na Jinsi Nyeusi na Shati la amaua Maua
Mallya nini Kilifuata
Shahidi nilisikia akilio Huko alipopelekwa Kwa Sababu haikuwa mbali na Cello yangu,Nilisikia kilio akilia na nilimtambua kwa Sauti sababu namuitaga sauti ya zege
Mallya ulitambua sauti ni ya nani.?
Shahidi nilitambua ni Sauti ya Adamoo
Mallya Ilikuwa ni Sauti ya namna gani.?
Shahidi ya amtu anayepigwa ,alikuwa analia Eeeehiii Ehiiiiiii Ehiiiiiiiiiiiiiiii ya amtu anayeteswa
Mallya ilidumu kwa Muda gani
Shahidi Sina uhakika ila ni Kama Nusu saa
Mallya Umesikia Sauti ya zege analia kwa Nusu saa,Nini Kilifuata
Shahidi Baada ya amuda amfupi Kupita akapitishwa Mtu yuleyuke aliye Vaa Jinsi Nyeusi na ashati la maua akiwa awezi akutembea alishikwa huku Kushoto na kulia na kwamba wakamburuza hadi Cello inayofuata baada ya kwangu
Mallya nini Kilifuata
Shahidi nikajua anayefuata ni mimi
Mallya baada ya akujia Unayefuata ni wewe,kilifuata nini
Shahidi walinichukua Mimi wakanipeleka huko,Nikaenda anikakuta watu wamekaa na wanasimu zao wananirekodi
Wakasema taja majina Matatu
Nikawatajia
Wakaniuliza Unafanya kazi gani
nikawatajia nimetoka Mtwara
Wakanipiga Buti wakasema wanajua mimi nimefuata nini Moshi
Mallya Mahita yupi unayemzungumzia.?
Shahidi Mara ya Mwisho nilimuona hapa mahakamani akitoa Ushahidi
Mallya hapo Mlikuwa sehemu gani
Shahidi Ni ndaninya Central Police palepale,nilitolewa Cello nikapalekwa kwenye Kijumba Kidogo
Palikuwa na Bomba refu,nikiwa nimefungwa Mikono na miguu,Mimi kwa ufahamu wangu inaitwa killing zone
Mallya Killing zone ni Kitu gani
Shahidi Unakuwa Unaning'inizwa Miguu Juu Kichwa chini,
Mallya kilifuata kitu gani..?
Anilipigwa Sana kwenye Unyayo kwa sababu Zilikuwa zimekaaa Juu
Mallya wakati wanakupiga wanasemaje
Shahidi aliyenipiga ni Mahita tuh
Mallya walikuwa wanahitaji kitu gani
Shahidi niliwaambia nimekuja kwa kazi ya VIP PROTECTION Kwa Kumlinda Mwenyekiti wa Chadema
Wakasema Utasema tuh
Mallya Ilichukua Muda gani
Shahidi kama Nusu saa
Mallya ikawaje
Shahidi alikuja Mtu Mtu aliyevaa akiraia akatoa Amri "Mwacheni sasa msimpige
Wakawa wameniweka nimekaa Chini nikiwa na Pingu na Mguuni nimefungwa kamba
Jaji Miguuni Ulifungwa nini
Shahidi Miguuni nilifungwa kamba
Mallya baada ya hapo Ulipelekwa wapi
Akaniambia huku Hoi na yeye akaniambia Mimi Mwenyewe Huku Hoi
Jaji Ukisema Mimi Huku hoi unamaanisha nini.?
Shahidi yani nimeumiabsana na kuchoka sana
Mallya Mahita alikuwa anakupiga na Kitu gani
Shahidi Sijakishika Vizuri lakini kama Shaba Nzito
Mallya nini Kilifuata?