Wakili wa Serikali:
Wewe ni Mohammed Abdilah Ling'wenya
Shahidi:
Ndiyo
Wakili wa Serikali:
wewe ni Komandoo
Shahidi:
Ndiyo
Jaji:
Umeacha Kuwa Komando
Mahakama Kicheko
Wakili wa Serikali:
Ujeshi Ukomandoo haufutiki
Shahidi:
Ndiyo ni sahihi
Wakili wa Serikali:
Ukomandoo na Uanajeshi si unamsharti yake.? yapi ya Kufanya na yapi siyo ya Kufanya
Shahidi:
Rudia swali
Wakili wa Serikali:
Ukomandoo na Uanajeshi si unamasharti yake.? yapi ya Kufanya na yapi siyo ya Kufanya, Miiko inakufunga bado.
Wakili wa Serikali:
Kuna Miiko ya Kijeshi ya hutakiwi Kuongea
Shahidi:
kama Yapi
Wakili wa Serikali:
Wewe ndiyo utuambie
Shahidi:
Wewe ndiyo umeyaleta Ndiyo Utuambie sasa
Wakili wa Serikali:
si Ulikula Kiapo, je nikiapo gani
Shahidi:
Nitalitumikia Jeshi Mpaka Kufa
Wakili wa Serikali:
Ulikuwa unatumikia Jeshi Kwa Mambo gani
Shahidi:
Kulinda Nchi, Kulinda, Silaha, Vifaa na Amani ya Ndani na Nje ya Nchi
Wakili wa Serikali:
Kwa hiyo kule Jeshini si Kuna Miiko hata Ukimaliza Jeshini utakiwi kuyaeleza
Shahidi:
Siyo sahihi
Wakili wa Serikali: Ulipokuwa Jeshini kozi ya Komandoo ulikula Kiapo
Shahidi: Kiapo gani