Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa - 28/09/2021

Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa - 28/09/2021

Dah kwa bahati mbaya wanye haki hawajui kujitetea ila wasio haki hujitetea mno.
 
lkn Mbowe kwa nini alifikia kujiingiza kwenye vitendo kama hivyo?

inasikitisha sana mtu mzima kama yeye kudaiwa kujiingiza kwenye vitendo vya kihalifu ni mfano mbaya sana hata kwa familia yake.
 
Watoto wasihukumiwe kwa makosa ya wazazi wao.
Narudia tena kwenu nyie vijana ambao hamjaoa binti wa polisi hata awe pisi kali namna gani msioe ili kuepusha uzao wako na laana.
 
Wakili wa Serikali:
Wewe ni Mohammed Abdilah Ling'wenya

Shahidi:
Ndiyo

Wakili wa Serikali:
wewe ni Komandoo

Shahidi:
Ndiyo

Jaji:
Umeacha Kuwa Komando

Mahakama Kicheko

Wakili wa Serikali:
Ujeshi Ukomandoo haufutiki

Shahidi:
Ndiyo ni sahihi

Wakili wa Serikali:
Ukomandoo na Uanajeshi si unamsharti yake.? yapi ya Kufanya na yapi siyo ya Kufanya

Shahidi:
Rudia swali

Wakili wa Serikali:
Ukomandoo na Uanajeshi si unamasharti yake.? yapi ya Kufanya na yapi siyo ya Kufanya, Miiko inakufunga bado.

Wakili wa Serikali:
Kuna Miiko ya Kijeshi ya hutakiwi Kuongea

Shahidi:
kama Yapi

Wakili wa Serikali:
Wewe ndiyo utuambie

Shahidi:
Wewe ndiyo umeyaleta Ndiyo Utuambie sasa

Wakili wa Serikali:
si Ulikula Kiapo, je nikiapo gani

Shahidi:
Nitalitumikia Jeshi Mpaka Kufa

Wakili wa Serikali:
Ulikuwa unatumikia Jeshi Kwa Mambo gani

Shahidi:
Kulinda Nchi, Kulinda, Silaha, Vifaa na Amani ya Ndani na Nje ya Nchi

Wakili wa Serikali:
Kwa hiyo kule Jeshini si Kuna Miiko hata Ukimaliza Jeshini utakiwi kuyaeleza

Shahidi:
Siyo sahihi

Wakili wa Serikali: Ulipokuwa Jeshini kozi ya Komandoo ulikula Kiapo

Shahidi: Kiapo gani
 
Kwani Mbowe kakamatwa lini? Na ni nani alisema kuwa Mbowe na wenzake wanatumikia kifungo?

Hupaswi kuwa na hasira na mtu mpaka ukashindwa ku reason kawaida tu. Magufuli hayupo. Waliopo warekebishe ambayo aliyakosea.
Tatizo inawezekana hata hujui hii kesi ni ya matukio ya Julai 2020. Sasa niambie nani alikuwa Rais 2020, mama au lile zee?
 
Sijui ka wanaelewa
IMG-20210928-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom