Hili jopo la Wanasheria wa Serikali wanne wanamtetea nani au wanamuwakilisha nani?
 
Hiyo Mahakama, bado tu haijapata fundisho kwa Kesi ya ugaidi ya akina Mbowe?

Tumechoka kusikia visingizio vya mashahidi wa Jamhuri kuomba ruhusa ya mara kwa mara, kwenda jisaidia🥺
 
Mahakama za kimichongo zinatoa hukumu za kimchongo, ndio maana tunahitaji katiba mpya ambao hawa senior CEOs wote Watanabe hizi kazi na kuhojiwa na kamati za bunge, na watawajibika kwa bunge sio mpangaji mkuu wa pale magogoni, it's shame kesi ipo mahakamani msamaha unaombwa ikulu
 
Kuna kitu nakiona hapa .... mama SSH anataka kuwatoa hawa covid-19 bungeni kwa kutumia mgongo wa mahakama ili isionekane ni shinikizo ... watch this pace
 
Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
... nimeilewa sana hiyo observation; wanataka kuwa wabunge wa kutokea hewani? Nikajua la muhimu ilikuwa kwanza kupigania uanachama ili ku-justify ubunge! Ndio mnasema Mdee ni mwanasheria? Kweli ulikuwa ubunge wa Ndugai na Magufuli!
 
Kitabala ni balaa
 
mbona kama wameshtukiza!?
hizi mahakama za michongo hizi..!?
Chadema hawakupewa taarifa ya kusikilizwa hii kesi leo mahakama kuu.

Kama Chadema wasingetokea kwa kuvizia [ baada ya kutuma makachero wao] hapo mahakamani, shauri hili lilipangwa liamuliwe upande mmoja, huku tayari kina Mdee wakienda mahakamani kwa kujificha, CCM na vyote vilivyomo ni najisi kwa hili taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…