Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Maselle muhongaji sana yule. Ila Katambi nae atapata tabu sana kutoboa mbele ya Chadema. Shy town Chadema wapo vizuri.
CCM hawashindwi kuiba hapo Shytown,tangu DED alipomtangaza Masele badala ya marehemu Sherembi aliyeshinda mwaka 2010 na kisha huyo DED akakimbia kituo cha kazi na baadae usikia kuwa amepata uhamisho mimi naona CCM hawashindwi kitu hapo Shy,labda ingekuwa Arusha
 
.
IMG_20200723_224635.jpg
 
Hizi haraka za nini?
Nipo seat No.8 nawatazama nasubiria majina. Jimbo maarufu linalo subiriwa na wengi ni Kigamboni au sio taifa
Baada ya kikao cha halmashauri kuu kuketi asubuhi, Katibu mkuu mwenezi wa CCM anaongelea yaliyojiri.
=======

Polepole: Vikao vyote cha jana na leo vilikuwa chini ya mwenyekiti wa CCM. Kikao cha halmashauri kuu kilikuwa na lengo moja na limekamilika. Lengo lilikuwa kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagomea wa majombi na viti maalum. Napenda kuleta taarifa hiyo kwenu kwa maana hawa walioteuliwa leo kwa majimbo na viti maalum.

Walijitokeza 10,367 nafasi za majimbo 264, chama chetu kimeandika rekodi na historia ya kukubalika. Upande wa uwakilishi leo haukufanyika uteuzi kwa sababu ya muingiliano wa ratiba ya NEC. Wagombea 33,094 waliomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye udiwani ilhali nafasi zipo kama elfu nne na kitu na kufanya jumla ya watu 43,461 waliiomba kukiwakilisha chama cha mapinduzi kwenye nafasi mbalimbali.

Wajumbe wa halmashauri kuu wametimiza wajibu wao na kikao kimeeleza wajibu wao wa kusimamia serikali mpaka tumefika hapa, uamuzi walioufanya leo umezingatia watu wabobevu kusimamia maslahi ya watu wetu watakaofanya kazi sambamba na serikali ya chama cha Mapinduzi ambayo tunaenda kuiombea kura.

Kwa kauli moja wajumbe wamefanya uteuzi baada ya kupokea majina kwa watakaokuwa wagombea wa CCM kwa nafasi ya ubunge. Vilikuwepo vingezo na sifa ambazo tumezitumia ikiwemo wanaCCM wanaojitoa kwa chama, tumetafuta yule ambae atatuleta pamoja, wenye mahusiano mazuri na wananchi na wanakubalika na jamii.

Watu ambao wameteuliwa leo wanatakiwa wanatakiwa wafanye maandalizi ya msingi.

Kwenye majimbo wanaCCM ni nidhamu tuendelee kuwa watulivu, wagombea ni wengi hatuwezi kupata wote lakini nawahakikishia kwamba, chama chetu ni kikubwa na fursa zake ni nyingi tuendelee kuwa wanyenyekevu na watulivu, chama kina taarifa zenu.

ARUSHA
Arusha mijini- Mrisho Mashaka Gambo

Arumeru Magharibi- Noah Lebrus Molel

Arumeru Mashariki- John Palangyo

Karatu- Daniel Tlemai

Longido- Stephen Kirusya

Monduli- Fred Lowassa

Ngorongoro- Ole Nasha

DAR
Ubungo- Prof Kitila Kitila

Kibamba- Issa Jumanne Mtemvu

Kinondoni- Abass Tarimba

Kawe- Askofu Josephat Gwajima

Kigamboni- Dr. Faustine Ndugulile

Ilala- Mussa Zungu

Segerea- Bonna Kamoli

Ukonga- Jerry Slaa

Temeke- Doroth Kilave

Mbagala- Abdallah Chaurembo

DODOMA
Bahi- Keneth Nolo

Chamwino- Deo Dejembi

Mvumi- Livingstone Lusinde

Chemba- Mohammed Moni

Dodoma Mjini- Anthony Mavunde

Kongwa- Job Ndugai

Kondoa mji- Ally Juma Makoa

Kondoa Vijijini- Dr. Ashatu Kijaji

Kibakwe- George Simbachawene

Mpwapwa- George Nataly Malima

GEITA
Busanda- Tumaini Magesa

Geita Mjini- Consatantine Kanyasu

Geita vijijini- Joseph Kasheku(Musukuma)

Bukombe- Dotto Bisheko

Chato- Medard Kalemani

Mbogwe- Nicodemas Maganga

Nyang'alwe- Hussein Amar

IRINGA
Iringa Mjini- Jesca Msavatambangu

Kalenga- Jackson Kiswaga

Isimani- William Lukuvi

Kilolo- Lazaro Nyamoga

Mafinga mji- Cosato Chumi

Mufindi Kaskazini- Exaud Kigahe

Mufindi Kusini- David Kihenzile

KAGERA
Bukoba mjini- Stephen Byabato

Bukoba vijijini- Jackson Rweikiza

Nkenge- Frolent Kyombo

Karagwe- Innocent Bashungwa

Kyerwa- Innocent Bilakwate

Ngara- Ndaisaba Luhoro

Bihalamuro- Ezra Chiwelesa

Muleba Kaskazini- Charls Mwijage

Muleba Kusini- Oscar Kikoyo

KATAVI
Mlele- Isack Kamwele

Kavuu- Geophrei Mizengo Pinda

Mpanda Mjini- Sebastian Kapufi

Nsimbo- Anna Lupembe

Mpanda Vijijini- Moshi Kakoso

KIGOMA
Vv
 
Sio tu suala la dini. Gwajima Kawe hakubaliki, Kawe ni jimbo la wasomi na watu wenye uwezo kifedha, uchafu wa Gwajima kuanzia kimaadili mf video zake za ngono na ule upotoshaji wake mf suala la corona sijui amphiphilo labda angegombania majimbo ya watu wengi wasio la elimu pamoja na uwezo. Sio Jimbo la Kawe!!
Nikweli kabisa, lakini mimi sintomchagua Gwajima sio sababu ya dini yake lkn nikulingana na udini wake.
 
Halima Mdee Kawe hawamtaki kabisa, na kilichomponza ni kwamba hajihusishi na Jimbo kabisa, yeye kila siku Mahakamani, kukimbizana na Askari wetu na kulia lia hovyo , yoyote yule atambwaga Halima Mdee, ...
Waislam hatuwezi mchagua gwajima aliyetutukana waziwazi
 
Back
Top Bottom