Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

Wana JF sisi tuliokatwa kwa sababu ya kutotoa rushwa katika maeneo mengi tumeumia sana kuona vinara wengi wa rushwa ndo wamepenya.

Kwa kuwa nia yetu ilikuwa ni kuwatumikia watanzania tunaomba vyama vya upinzani vitupokee kwa kipindi hiki kifupi.

Kwa wale waliochukua fomu za NEC tunaomba mtuwekee hapa tuanze kuzijaza ili kama kuna makosa tuweze kuzirekebisha mapema. Lengo lingine ni kuandaa viambatanisho vinavyotakiwa kwa mfano background ya picha ya passport nk

Tumebaki na siku 5 zinatosha sana kukamilisha ujazaji wa fomu na kurudisha.

Tunaomba namba za viongozi wa upinzani kwa kila kata au jimbo ambalo vyama vya upinzani hawajateua bado wagombea wao ili sisi watia nia masikini tuweze kuonesha vipawa vyetu vya uongozi huko.

Chonde chonde msitubeze....tupendane

Wajumbe oyee
Tupokelewe[emoji30][emoji30][emoji30][emoji30]
JamiiForums-1236827479.jpg
 
dah hatari sana, futa hii mentality chief tena tupambane kama jamii iliyostaarabika hili lisiwepo kamwe..

Kodi hulipwa na Watanzania wote kwa serikali moja..

Mie sio mnafki. Kwenye ideal society tutasema hivyo na hicho ndicho kilichofanya Kilimanjaro na Arusha wafike mbali, kwakuwa wengine waliona aibu kusema.

Ukweli ni kwamba Mkuu anaipa kanda ya ziwa priority ambayo hii kanda haijawahi kupata. Ni sawa na JK alivyoipaga kanda ya Pwani kipaumbele. Na mkuu amebeba mikoa yote ya kanda hii, sio usukumani tu. Hii ni fursa kwa hii mikoa ambayo licha ya kuongoza kwa rasilimali zinazoingizia pato taifa, ilibaki kuwa na hali mbaya sana.

Huu ni ushauri wangu usiopapasa macho. Rorya watajiamulia wao na watoto wao mwelekeo wao.

Kwa mtazamo wangu, mikoa pekee ambayo inaweza chagua upinzani bila madhara ni mikoa iliendelea kwenye huduma humimu za jamii kama Dar, Arusha na Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom