Yaliyojiri Kisutu, Dar: Kesi ya Freeman Mbowe, yaahirishwa hadi 13 Agosti, 2021, Mashtaka yasomwa upya

Yaliyojiri Kisutu, Dar: Kesi ya Freeman Mbowe, yaahirishwa hadi 13 Agosti, 2021, Mashtaka yasomwa upya

Kesi za namna hii si Mara ya Kwanza kubambikizia wapinzani,na Mara zote wanashinda!
Hayo uliyoandika huna ushahidi nayo zaidi ya propaganda mfu!
Kama Mbowe amefanya hayo toka 1980 Basi tumekuwa na serikali za hovyo sana,wewe mlalahoi unajua lakini serikali zote ambazo zimekuwa zikimuwinda zimeshindwa kujua hilo!
Huna jipya!
Wewe ni mtoto wa juzi hujui kitu. Mbowe amechamba sana hadi kakamata kinyesi. Kaa kimya fanya yako
 
Wewe ni mtoto wa juzi hujui kitu. Mbowe amechamba sana hadi kakamata kinyesi. Kaa kimya fanya yako
Mtoto was juzi Ni wewe unayeandika propaganda mfu zisizo na kichwa Wala miguu!
Fyta mkia Kama huna hoja!
 
wewe kwa akili yako timamu unaona siyo ya kubambikiwa? nchi ina mambo ya kipuuzi sana. hayo mapesa yanayotumika kuendesha hii kesi isiyokuwa na kichwa wala miguu si bora ingetumika kununulia madawati kuna watoto 400 wanasoma wakiwa wamekaa chini huko sengerema? stupid!
Sasa mi najuaje Kama sio ya kubambikiwa, na wewe unajuaje Kama Ni ya kubambikwa! Usiniambie 'unajua tu' nipe facts
 
Duh... Kufadhili? Si walisema gaidi? Nilijua kavaa bomu akaenda kwenye mkusanyiko wa watu, kabla hajafyatua fuse akakamatwa! Kumbe kufadhili?

Hamna kesi hapo!
Mkuu kwako kufadhili ugaidi unaona siyo kosa. Akitokea mtu anayefadhili majambazi kwa kuwapatia silaha na fedha za kufanyia ujambazi kwako hilo siyo kosa? Kwa uelewa wako huo nadhani ni bora ubaki huko huko CHADEMA
 
Kama siyo kubambikwa, inakuwaje mtu amefutiwa shitaka la madawa ya kulevya? Unafutaje shitaka la namna hiyo kama ushahidi upo?
 
Hao polisi wamejazana hapo hawana kazi nyingine za kufanya ? hawa ndio wanaokula hela zetu za kodi bure, na wanasababuisha walimu wasilipwe mishahara stahiki na kwa wakati, hii nchi ya hovyo sana, watu wanazurula tu wanalipwa mishahara ya bure
Kuna mwajiriwa wa serikali asiyelipa Kodi?
 
jamani watanzania wenzangu wenye magonjwa kama;
1. KISUKARI
2. UKIMWI
3. SARATANI
4. KIFUA KIKUU
5. CELI MUNDU
Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu lina puputisha balaa, aise.
 
Ijumaa Imefika kukiwa na Baridi asubuhi hii katika jiji la DSM.

Freeman Mbowe aliyebambikwa kesi ya Ugaidi na dola kutokana na vuguvugu la kudai Katiba impya inaendelea Leo baada ya kuahirishwa Jana kutokana na tatizo la kimtandao.

Itakumbukwa mwanzoni mwa wiki hii Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro bila aibu aliitisha Mkutano wa wanahabari bila kujali anaingilia Uhuru wa Mahakama alimshambulia Freeman Mbowe na kumhukumu kwa kesi hii ya kubambikwa. Simon Sirro alienda mbali na kutumia mpaka udini kuhalalisha madai yake ya uongo dhidi ya Mbowe.

Kama ilivyokuwa Jana tunatarajia idadi kubwa ya Wananchi kuhudhuria kesi hii wakiwemo vijana, wanawake na Wazee.

Dunia imesimama na wapigania haki Tanzania na tayari mpaka Jana nchi kadhaa duniani zimetoa matamko ya kufuatilia kesi hii kwa ukaribu ikiwemo Marekani, Canada, Uswiss, Uingereza, European Eunion na Umoja wa Mataifa (UN)

Molemo media tayari tumetinga hapa Kisutu kuripot yanayoendelea mwanzo mwisho.

Updates saa 2.30 Asubuhi
Mpigania haki wa Tanzania Freeman Mbowe amefikishwa Mahakama ya Kisutu chini ya Ulinzi mkali wa Askari wenye silaha.

Mbowe Mara baada ya kushuka amenyoosha ishara ya vidole viwili kusalimia wananchi

=====

UPDATES:

Freeman Mbowe na Watu wengine watatu, Wamesomewa Mashitaka upya. Mbowe ana mashitaka Mawili ambayo ni

1. Kula njama kwa nia ya kutenda kosa(Wote)

2. Kosa la kufadhili Vitendo vya Ugaidi kwa kutoa pesa.(Mbowe)

3.Kukusanya fedha kwa lengo kutekeleza vitendo vya ugaidi

4.Kupatikana na siraha isivyo halali(Mshitakiwa wa tatu)

5.Kupatikana na risasi isivyo halali(Adam)

6.kukutwa na sare za jeshi(Alfan)

Shitaka ambalo limeondolewa ni la dawa za kulevya.

Upelelezi umekamilika wanasubiri jalada kutoka kwa DPP. Kesi imeahirishwa hadi 13|08|2021

Zaidi soma: Thread 'Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua' News Alert: - Kisutu: Kesi ya Freeman Mbowe yaahirishwa hadi Kesho 06/08/2021, Mtandao umesumbua

Thread 'Hati ya Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe iliyotumiwa Julai 26, 2021' Hati ya Mashtaka dhidi ya Freeman Mbowe iliyotumiwa Julai 26, 2021

Kuna wadada fulani nimewaona pale Mahakamani wakikumbatiana na Mbowe, mbona wewe hizo picha hukuziweka kama hizo ulizoweka, au hukuziona au umezingatia uadilifu na weledi wa kazi humu JF!?
 
Nguvu waliyotumia kujaza mapolisi mahakamani wangekuwa wanaitumia kupeleka maji vijijini huko ambapo watu hunywa maji ya kisima kimoja na mifugo ingekuwa heri !
 
Wapenda amani kote nchini na wazalendo wa nchi popote pale walipo kamwe tusikubali hawa wahuni wachache wanao jifanya wanadai haki kwa kuvunja sheria watuharibie Amani ya nchi yetu.

tuchukue hatua za kuwafichua na kuwa ripoti popote pale walipo. sio wafuasi wote wa chadema wanafurahia uhuni huu bali wapo wahuni wachache wenye chembe chembe za Ugaidi/uhalifu/ujanbazi/wizi ndio wanafanya vitendo hivi vya kihuni ili wapate sababu.
images.jpeg
Unawakumbuka hawa vibaka wa UVCCM waliomfanyia Mbowe fujo hai?

Walichukuliwa hatua gani zaidi ya kulipwa buku 7 na kisha kwenda kulewa pombe za kienyeji zinazowazeesha mapema
 
View attachment 1883003Unawakumbuka hawa vibaka wa UVCCM waliomfanyia Mbowe fujo hai?

Walichukuliwa hatua gani zaidi ya kulipwa buku 7 na kisha kwenda kulewa pombe za kienyeji zinazowazeesha mapema
kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa jingine.
jambo la msingi kwa watanzania wenzangu tujifunze kuheshimu utawala wa sheria, haswa pale watu wenye wadhifa ktk siasa au uongozi wanapo chukuliwa hatua, tusiwe wanafiki.
kwa mfano;
1. alipo kamatwa aliye kuwa DC wa Hai Sabaya na kisha kushitakiwa Mahakamani watu wengi wakiwamo wafuasi wa Cjadema pamoja na James Mbatia walipongeza jeshi kwa kuchukua hatua na akasema huo ndio utawala wa sheria, cha kushangaza Mbatia huyo huyo mara baada ya Mbowe kukamatwa amebadilika nakuanza ohh kabambikowa ohhh suluhu ipatikane!! unamshangaa kabisa mtu kama Mbatia ana kuwa na ndimi mbili tena bila aibu anazungumza mbele ya vyombo vya habari.!!!
 
Mkuu kwako kufadhili ugaidi unaona siyo kosa. Akitokea mtu anayefadhili majambazi kwa kuwapatia silaha na fedha za kufanyia ujambazi kwako hilo siyo kosa? Kwa uelewa wako huo nadhani ni bora ubaki huko huko CHADEMA
Sawa Bwana Genious.
 
kosa moja haliwezi kuhalalisha kosa jingine.
jambo la msingi kwa watanzania wenzangu tujifunze kuheshimu utawala wa sheria, haswa pale watu wenye wadhifa ktk siasa au uongozi wanapo chukuliwa hatua, tusiwe wanafiki.
kwa mfano;
1. alipo kamatwa aliye kuwa DC wa Hai Sabaya na kisha kushitakiwa Mahakamani watu wengi wakiwamo wafuasi wa Cjadema pamoja na James Mbatia walipongeza jeshi kwa kuchukua hatua na akasema huo ndio utawala wa sheria, cha kushangaza Mbatia huyo huyo mara baada ya Mbowe kukamatwa amebadilika nakuanza ohh kabambikowa ohhh suluhu ipatikane!! unamshangaa kabisa mtu kama Mbatia ana kuwa na ndimi mbili tena bila aibu anazungumza mbele ya vyombo vya habari.!!!
Thibitisha Mbowe alitaka kuua kiomgozi gani?

Maana kama ulinzi tu wa mahakama wamejaza hao polisi huyo kiongozi aliyepanga kuuliwa ni nani?

Unaweza kunitajia waliotaka kumuua Lissu yapata miaka 4 sasa hawajajulikana na kesi haizungumzwi je Lissu hakua kiongozi?

Lissu alishambuliwa katika compound ya viongozi mchana kweupe achilia mbali hizo shutuma za Mbowe za kupanga na hapajatokea kitu..

Ifike mahali CCM mjue watanzia wa miaka ya 90 sio hawa wa sasa..
 
Back
Top Bottom