Ndugu wanajamvi, nimefuatilia kwa umakini kongamano/mkutano wa viongozi wa dini CHIMWAGA-DODOMA.
KONGAMANO limejaribu kutuweka TANZANIA kuwa nchi ya umoja,amani, na mshikamano. Pia limajaribu kuunga dot za utawala uliopita na wa sasa. PAMOJA na kuwaasa wanasiasa waache kutubagua WATANZANIA. Mimi binafsi naamini kwa MANENO mazuri ''aliyopambwa'' nayo Rais aliyetangulia mbele ya haki basi inatosha kabisa KUMFANYA mtukufu wetu huyo awe PEPONI!
Katika utawala wa uliopita nilitegemea kwamba watumishi wa MUNGU wetu awezaye yote wangekua wazalendo kama walivyoshauri katika hoja zao basi hata wangetuambia mapungufu hata mawili matatu juu ya awamu ile na kutoa muongozo kuhusu nini cha kuendelea nacho na nini cha kuacha katika ngwe hii ya pili baada ya PIGO kubwa tulilopata kama Nchi. Mbona kama watumishi wetu wa Mungu katika nchi nanyi hamtaki kusema ukweli au mnataka nafasi za utawala tuanze kujua mapema?( Mungu anisamehe kama nimesema vibaya). Watumishi wa MUNGU naowajua katika biblia waliweza kuwaambia wafalme juu ya makosa yao.
1 SAMWELI 15(SOMA SURA YOTE). Nilikaa kusubiri huenda BABA ASKOFU mmoja angesema haya mapigo tuliyoyapata ni kutokana na njia zetu kama NCHI kuwa mbaya pengine kutoa MWANGAA!!! juu watawala kutawala kwa UWAZI na HAKI pasipo KUBAGUA kanda ili kuleta utengamano wa KITAIFA. Je ni kweli utawala ule haukuwa na dosari yeyote? je ulikuwa kamilifu? Hakuna haki ya mtu/watu iliyopotea?
Ninasikitika sana juu ya hili ndio maana kuna ndugu nilimwalika kutazama pamoja tukio hili la kihistoria lakina alinijibu hapo kutakuwa na NGONJERA, KWAYA, pamoja na timu nzima ya PRAISE &WORSHIP! Nikasema wacha nijikaze pengine WAKIROHO nao WAMEPEWA ROHO na BWANA kumbe wamepewa SIFA wamsifu, hii ni hatari jamani kama kila jambo ni kusifu tuu HATUTAFIKA.
Imani yangu kwenu MAASKOFU na MAIMAMU naipunguza kutoka 100% hadi 50% mpaka pale MUNGU atakaponiongezea imani tena juu yenu.Mimi nimeona kama vile yote ya nyuma yamebarikiwa na BABA MAASKOFU NA MASHEHE NA MAIMAMU kwa hio wandugu NI JUKUMU LETU TUYAENZI!
Eeeh MUNGU uliye juu uketiye katika kiti chako cha enzi, utusamehe na uwape Watumishi wako UJASIRI kama ule wa MUSA kwenda na kumwambia Farao mfalme, BWANA MUNGU asema uwape watu wangu ruhusa wakanitumikie, usipotii uatapata mapigo, au ule Ujasiri wa Samweli kumwendea Sauli mfalme na kumwambia Umefanya dhambi na MUNGU amekukataa usiwe Mfalme. Utupe akili na maarifa, hekima na ujuzi juu viongozi wenye nia kutudanganya na kutupumbaza ili tussiju kweli maana NENO lako ndiyo KWELI ee BWANA, katika jina la YESU KRISTO- Aaamen!
Jioni njema wanjamvi.