Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

Nauliza tu kama viongozi wa chama tawala yaani CCM na wale wa chama kikuu cha upinzani Chadema wamepata mwaliko wa mkutano mkuu wa ACT wazalendo.

Maana safari ya ushirikiano wa Chadema na ACT wazalendo ilianzishwa jana pale Mlimani city .

Maendeleo hayana vyama!
 
CDM mbona hawajatokea? Ilhali wenzao walikwenda kwenye mkutano wao mkuu?

Labda wamechelewa
 
Nje ya topic kidogo; naomba kuuliza, hivi dada Fatuma Karume kaolewa? I mean is she Mrs. somebody au bado yupo single? Nimeanza kumuelewa elewa hivi.

Mkuu tuheshimiane, huyo ni shemeji yako. Watu tumewekeza hapo.
 
Hivi vijamaa kidogo viko serious naona hapa wajumbe wanapewa barakoa zenye nembo ya ACT. Hongereni watani
 
"Ndugu Wajumbe naomba tufanye kazi nzuri ili tupate wagombea ambao wanauzika. Sawasawa?"

Maalim Seif
Mwenyekiti wa Chama
 
Maalim Seif anasema safari hii CCM wasidhani kuwa Iwapo atashinda uchaguzi Zanzibar halafu CCM wakaleta figisu basi atafunga mikono, Safari hii anasema haki lazima iheshimiwe!
 
Back
Top Bottom