Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Mkutano Mkuu wa ACT–Wazalendo: Membe apata kura za Ndiyo 410 za Urais Tanzania, Maalim Seif Ndiyo 419 za Zanzibar

Ni kweli kila mwanasisa anapambania tumbo lake
 
Muda huu uchaguzi wa kupata wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano na Urais wa Zanzibar.
 
Kwa kweli nimemsikiliza Shangazi leo kwenye mkutano wa ACT Wazalendo. Shangazi kawapelekea salamu za kutosha CCM na serikali yake. Nimefurahishwa na huyu dada ukizingatia kuwa ni mtoto wa Rais Mstaafu. Huyu kweli ni mpigania haki ... ikiwezekana apewe hata Ugombea mwenza vyama vikiungana. She is real an IRON LADY ......!!
 
Baada ya kuandika na kupitia habari yako... , umeona kwamba imekamilika ? Nadhani cha maana zaidi ya kufurahishwa kwako ungeweka amesema nini....,
 
Napendekeza aolewe na lisu awe first lady mwenye IQ kubwa kama Michelle
 
Ka-sentensi ka mwisho ka hotuba ya Lissu ndiko mhimu. Wahusika wazingatie.
 
waunganishe nguvu ya kuachiana majimbo ili kuunganisha nguvu itakayowapa nguvu wote dhidi ya adui wa taifa.Mfano visiwani na pwani waachiwe ACT. DAR na bara yote waachiwe CDM.Ila jimbo la Kigamboni kwa heshima ya Ndugulile kuwafurahisha watz upinzani wasisimamishe mgombea yeyotewa upinzani ili Ndungulile mzawa apite.
 
Fatuma ni mtu wa tofauti na watu wengine, siyo mnafiki ni mpenda haki, huyu angekuwa Jaji mkuu tungeishi kama tupo Ulaya.
Hiyo pia ni Good idea. Siyo hawa wafuata maelekezo tunaoletewa siku hizi .........!!
 
Tunataka mtu atakaekwenda kutatua shida zetu watz na sio wa kwenda kukimbizana na upinzani,kutoa rushwa makanishani,kuimbiwa sifa,kuabudiwa,kusujudiwa hizo sifa akapate kwa mkeweTunataka mtu anaeuzika kimataifa,mwenye visioni,civilized,mwenye exposure,anayefata utawala wa sheria,atakaelinda watu dhidi ya wasiojulika,asiyebambika watu kesi,asiyewatumia vibaya polisi,asiyetuibia kodi zetu,asiyetusomesha namba
 
Namsikiliza Membe hapa, akihutubia baada ya kushinda uteuzi wa kugombea Urais kupitia ACT
Lakini bado anaonekana Ni kuku mgeni, kwani hata jina la ACT kalichanganya kulitaja kataja ATC,hii sio Mara ya kwanza Kuna kipindi Tena aliita Ngome ya wanawake ya ACT na kuiita UWT

Membe kaongeza boost kubwa Upinzani lakini kakaa muda mfupi Sana kupitishwa awe Rais,
.Tundu Lissu naye yupo too radical kwa Chadema na pengine hili litawaketea matatizo kwenye kampeni

Bado sijaona mgombea Ideal upinzani afadhali
 
Hao wanaandaliwa 2025 huko ndo kutakuwa patashika mav gonga chupi..😂
 
Anaposema atamtoa mtu yule bila kumtaja jina mi nimeshindwa kumuelewa jamani anayeelewa anisaidie
 
Mtaa wa saba wanakunywa panadol...hali si hali...homa inapanda na kushuka

Lissu & Membe & Maalim ndiyo habari ya mjini kwa sasa!!

Hutaki meza viwembe!!
Wafurahisheni mabwana zenu ili waamini kuwa mtashika dola, wazidi kutoa pesa.
Ila siku mmoja lazima watawatapisha hizo pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Mwanakitengo" huwa hastaafu na wana "Vintengo" wetu wengi sio Wazalendo kwa Taifa bali ni Wazalendo wa Chama Chetu Maarufu. Matumaini yangu kwa Upinzani kuchukua nchi yanazidi kufifia, nayaona ya Lowasa yakijirudia. Hakuna ushirikiano wa kweli hapo, Mamluki kibao Wakiongozwa na Membe. Watu watapoteza maisha au mali zao sababu ya Upinzani huu uchwara uliojaa wasaliti kwa wananchi lakini Mungu pekee ndio atakuja kuwalipia wananchi hawa waliodhulimiwa na watakao dhulumiwa mwaka huu. Hakika Mungu yupo na anaona na atawalipia dhidi ya Wasaliti na Watesi wao. Mungu Wabariki Watanzania, Mungu Ibariki Tanzania [emoji1241]
 
Diamond jubilee yameishaje tupatieni taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…